Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
Ingawa nina malalamiko mengi na muungano wa sasa, lakini bado sidhani kama ni wazo zuri kuvunja muungano. Hii mipaka mingi iliwekwa na wakoloni. Waafrika kabla ya wakoloni wa kiarabu na kizungu, tulikuwa tukiishi pamoja.
Kutengana sio suluhisho katika mgogoro wa sasa!
Nakubali 100%. Tena tukianzisha 'Jamhuri ya Afrika' ni poa zaidi Mwafrika wa Kike. (Japo ni ndoto, ukifikiria nani atakuwa nani kati ya Mugabe, na Ghadafi na Kibaki. Na Dafur, na Comoro, na Congo. Na Chenge na Billal na Mkapa na Mkono na Karamagi na Rostam).
Swali langu dogo sana. Mkataba wa Muungano uko wapi? Siombei usiwepo. Na sisemi haupo. Na hata kama haupo haimaanishi hatujaungana. Na kama tumeungana na mkataba haupo sidhani tuuvunje!
Najifunza historia tu. Mkataba uko wapi?