Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Kutakuwa na kikao maalum kesho Zanzibar. Kikao hicho kitahudhuriwa na viongozi wa CCM Bara na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kikao hicho kina muelekeo wa kuzungumzia masuala ya muungano.

Je, tutarajie chochote kipya?

Wazanzibari "wataburutwa" tuu .... Bara haiwezi kuvunja Muungano na kuwaachia mafuta.
 
Hapa wanania ya kuwanyamazisha wanaodai nchi yao, unaweza sikia akina Maalimu ni wahujumu wa nchi au wahaini! Cha maana wangetuwekea mezani tujue tunafaidika vipi na huu muungano.
 
Nadhani usitarajie chochote.... kumbe tumesahau tu, jambo lenyewe lilikuwa limeshafikishwa na kukamilishwa kwenye mahakama ya rufaa... ambacho nadhani ni chombo cha mwisho kabisa....

Alisema maadui hao wanaitumia fursa hiyo kuendeleza chuki dhidi ya muungano ambazo walikuwa nazo siku nyingi bila kujali maswali na hoja wanazozitoa sasa zilishawahi kujadiliwa siku za nyuma na kutolewa majibu.

Alihoji kwa nini wanaohoji leo Zanzibar ni nchi na wanataka Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume atangaze mgogoro wa Katiba hawakukata rufaa miaka ya nyuma wakati Mahakama ilipotangaza kuwa Zanzibar si nchi.

Mwaka 2000 Machano Khamis Ali na wenzake 18 walishitakiwa kwa kosa la uhaini la kutaka kuipindua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na kupitia mawakili wao walijenga hoja kuwa Zanzibar si nchi hivyo wasingeweza kuipindua.


Habari kamili
 
Kwani si wapo wale wale Makamba kingunge na wenzake?.....hakuna jipya wamekwenda kwenye tamasha la Ziff
 
Mkuu leo ni dola $ 129 kwa debe! the lowest in the last three months! Kula yangu inategemea haya mafuta ndio maana niko on top of it kila siku mkuu sio kuwa nakurupuka on this ya mafuta, maana kila yanavyobadilika ndio na kula yangu inabadilika!
 
This is the best time for whatever is there (oil and/or gas) to be economical .... oil is selling at $140/barrel

......Je ukikuta gharama za uzalishaji ni equivalently $300/barrel.....bado utachimba?............utafiti ni kitu muhimu kabla ya kukurupuka
 
Mkuu leo ni dola $ 129 kwa debe! the lowest in the last three months! Kula yangu inategemea haya mafuta ndio maana niko on top of it kila siku mkuu sio kuwa nakurupuka on this ya mafuta, maana kila yanavyobadilika ndio na kula yangu inabadilika!

Mkuu, sijacheki bei wiki nzima hii ... kumbe yameshuka hivyo; lakini still this is the best time kwa TZ ku-take advantage .... hizi bei za over $110/barrel bado ni nzuri sana kwa exploration companies .... sasa hivi ni wakati muafaka kwa TPDC kujipanga upya na kuandaa bidding round kwa offshore blocks (including zile za Zanzibar) na hata onshore (Mbarali basin na kule Ruvuma basin) ... kuna makampuni mengi yako tayari kuwekeza; lakini TPDC inabidi wajifunze toka Angola (Sonangol) ... hawa jamaa kila block wanakula at least 20%, mtaji wao ni ardhi.
 
......Je ukikuta gharama za uzalishaji ni equivalently $300/barrel.....bado utachimba?............utafiti ni kitu muhimu kabla ya kukurupuka

Mkuu, haiendi hivyo .... huku ninakofanya kazi gharama ya uzalishaji pipa moja ni less than $35; na huku ni Marekani ... offshore Gulf of Mexico ... na hiyo $35/barrel ni kwa kisima cha urefu wa zaidi ya 18,000 feet! .... Tanzania labour charges ni cheap, na isitoshe nimeona seismic images za baadhi ya maeneo ya Bongo ... looks like visima vyake havitazidi 12,000 feet ... so it will be even cheaper!
 
Mkuu, haiendi hivyo .... huku ninakofanya kazi gharama ya uzalishaji pipa moja ni less than $35; na huku ni Marekani ... offshore Gulf of Mexico ... na hiyo $35/barrel ni kwa kisima cha urefu wa zaidi ya 18,000 feet! .... Tanzania labour charges ni cheap, na isitoshe nimeona seismic images za baadhi ya maeneo ya Bongo ... looks like visima vyake havitazidi 12,000 feet ... so it will be even cheaper!

It is still uneconomical. Kuna factors nyingi. Lazima wafanye research, mbona mbishi wewee? Lazima pia wajue kuna kiasi gani, na kisima kitakuwa na umri gani. Waangalie na cost za decomissioning (kama wanajali).

Kwasasa hivi kampuni haliwezi kutoka Canada kichwakichwa au marekani wakati kwao wanachimba kiulaini. Mafuta yapo ya kumwaga huko kwao, unachokonoa tu.

Incase huja notice, makampuni yanayopata blocks Tanzania ni makampuni yasiyokuwa na stakes kubwa duniani, wala hayajawahi kusikika dunia hii (this alone should tell you alot about Tanzania as a country). We unaweza kuniambia kwanini BP waliondoka Tanzania? Unajua wanafanya biashara gani Tanzania? What will happen, yakipiga jackpot, makampuni makubwa zaidi yatayanunua haya makampuni. Kuna vikampuni vingene vimenunuliwa kwasababu cost za kusearch wanapoteza hela. wamepewa blocks wakaingia kichwakichwa.

Sasa wewe inabidi utulie ungalie mchezo unachezwa vipi. Ila mafuta yapo, but its uneconomical so far. Wazanzibari wanajua wanataka nini.

P.s Makampuni makubwa TZ ni mawili tu. Wabrazil na kuna la wamarekani.
 
Huu Muungano sasa hivi umeshakuwa ni kichekesho. Watanganyika wengi wanaanza kugundua kwamba hauna manufaa yoyote na Wazanzibar wengi hawautaki tangu zamani. Wanaoupigia debe ni wanasiasa hasa wa Tanganyika sijui kwa sababu zipi hasa. Z'bar wana deni la TANESCO la shilingi bilioni 22 hawataki kulipa kwa sababu wanadai hayo ni mambo ya Muungano na hawastahili kulipa hata senti tano. Wakati huo huo sasa hawako tayari kushare mafuta kama yakipatikana huko kwa sababu mafuta ni ya Z'bar na siyo ya muungano!!!! Huu ni undumilakuwili wa hali ya juu. Chako chetu, changu changu!!!

Wakati huo huo Z'bar sasa hivi ni nchi ina Rais wake, ina bendera yake, ina mwimbo wake wa Taifa na siajabu siku za karibuni wakawa na sarafu yao na passport zao na pia mabalozi wao katika nchi za nje ili kukamilisha matakwa yao ya kuwa nchi. Lakini siye Wadanganyika bado tunadanganywa tu!!! eti tuna muungano wakati wenzetu katika miaka michache iliyopita wamefanya juhudi kubwa za kuonekana kwamba wao ni nchi kwa Wananchi wao na jumuiya ya kimataifa!!!

Z'bar hawana rasilimali zozote zao lao la kibiashara ambalo lilikuwa likiwapatia maparo ya kigeni mengi sasa hivi linalimwa na nchi nyingi duniani hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa mapato yao ya kigeni na mazao ya chakula wanayolima ni madogo mno ambayo hayawatoshelezi hata wao wenyewe. Kwa kifupi mapato yao mengi ya kuendesha serikali yanatoka katika serikali ya 'muungano' pamoja na hili bado hawaoni umuhimu wa kushare mapato yao ya mafuta pindi yakipatikana. Muungano huu hautufai Tanganyika una hasara zaidi kuliko faida lakini kamwe wanasiasa hawatatwambia hilo wataendeleza usanii wao wa kutuambia mashairi amzuri kuhusu muungano.
 

... Wanaoupigia debe ni wanasiasa hasa wa Tanganyika sijui kwa sababu zipi hasa.

Bubu, we have to solve that conundrum. That's the holy grail right there.

Wazanzibari hawautaki. Watanganyika nao ni vigumu mno kukutana na anaeutaka. Aliyekuwa amebaki ni marehemu.

Sasa, hawa Watanganyika, hao Wanasiasa wao wa Bara, ambao wanawang'ang'ania Wazanzibar ni kina nani?

Na kwanini?

Think about it, kama ni CCM establishment, wao CCM hakuna kinachowatishia maisha kama CUF. Na CUF stronghold yao iko Zanzibar. So you would presume that CCM would be done a big favor were the Zanzibar politics be axed off the Tanganyika/Tanzania politics. Kwa sababu siasa za Zanzibar ndio nemesis ya CCM tokea NCCR ya Mrema ife. Tabaka tawala la CCM sidhani linafaidika hapa.

Sasa Watanganyika wanaotetea Muungano wana nini humo?

We have to work out that question.
 
Kutakuwa na kikao maalum kesho Zanzibar. Kikao hicho kitahudhuriwa na viongozi wa CCM Bara na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kikao hicho kina muelekeo wa kuzungumzia masuala ya muungano.

Je, tutarajie chochote kipya?

Hakuna kipya chochote toka chama cha mafisadi. Nadhani unakumbuka kikao chao kule Butiama ambacho kilijaa usanii wa hali ya juu pamoja na nchi kugubikwa na habari nzito kuhusu mafisadi hakukuwa na chochote kipya, na huko Z'bar hali itakuwa ni hiyo hiyo maana badala ya kuweka maslahi ya nchi mbele wao wameweka mbele maslahi ya chama chao cha mafisadi
 
Just another "social gathering" mainly for a cup of tea on our cost ofcourse!
 
Duh kwanza ilikuwa Butiama, ikawa Dodoma, sasa Zanzibar, kweli bila safari uongozi bongo ni bure, lazima kuwa na perdiem by anymeans necessary!
 
Wanakutana Bwawani hoteli kwa kikao cha dharura na moja ya jambo kubwa ambalo watalizungumza ni juu ya hatima ya Muungano, hiki ni kikao cha NEC maalumu ambacho kitahusisha wajumbe wote wa NEC kutoka ZNZ, wakijumuika na viongozi wa juu wa CCM pamoja na wajumbe wa kamati kuu.

Kuna tatizo juu ya hatima ya muungano .....
 
Muungano unayumba mojawapo ya tatizo ni ufisadi ambapo kunaonekana Tanzania bara ndiyo yenye mafisadi wa kutosha. Hivyo naona kuna kila dalili kwamba wanajihami
 
Tunataraji walio chunguni watatujuvya kinachoendelea. MK ushafika Unguja?
 
Back
Top Bottom