Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Pinda ameshavurugia wahafidhina mambu yao,sasa wanaemda kumsakama ,tuone Butiama V/s Unguja. Sijui nani anaenda kumuomba razi nani ?
Na vikao kama hivi mara nyingi huizamisha CCM haswa kwa siasa za Zanzibar ambazo wananchi wake huwaga wananunua ubishi.Lolote litakaloamuliwa na CCM huko basi halikubaliki kwenye vichwa vya waZanzibari kama wasivyokubalika jinsi mafisadi wanavyorudisha feza.
Mwaka huu wananchi wa pande zote mbili za Muungano wako macho ,wacha mafisadi wavuke ,mito maziwa na bahari lakini mambu ya kuiba na kula hazina ya Taifa imefikia mwisho ingawa mafisadi wamekodolea macho mafuta ya Zanzibar lakini hila na njama zinajulikana kwani mafisadi wanajipanga kikao cha mkao wa kugawana.
Tatizo mafisadi wa Unguja hawakupata kumega vyanzo vya feza huku Tanganyika sasa wamekuwa wakali kuona mafisadi kutoka bara wananyatia vyanzo bikira huko Zenji.
Hapa hakuna tatizo la Muungano wala Zanizibar ni nchi au si nchi ,naomba tusizinguane ,lipo jambo kwani ukiangalia utaona mabishano hayakuanza kwa CCM na CUF bali ni huko huko upande wa CCM baina ya mafisadi na Wahafidhina ila CUF alijibanza kati na kusema aliyosema akijua sivyo inavyotakiwa lakini ndio siasa zilivyo.
 
Mainland sizani kama ilikua na inalengo zuri; ukitizama huko nyuma wakati wote kabla na baada ya vita vya Idd Amin; Kila ambapo uchumi wa mainland ukididimia ulikua unaivuta znz bila ya hata kuweko na sababu.

Hii ni kwa sababu visiwa vyenu hivyo ni sehemu ya Tanzania. Zanzibar imekuwa na matatizo yake ya kiuchumi mengi tu ila nisingependa kukuchambulia hapa.Kiufupi ni kwamba Bara kwa sababu ndio sehemu kubwa na yenye nguvu kubwa ya kiuchumi katika Muungano huu, ikipatwa na matatizo yoyote ya kiuchumi ni vigumu sana kwa "mwenza" wake kutoathirika pia.

Na yote haya alikua Nyerere ndio fundi mkuu; alipomuona Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi anafanya vizuri ZNZ - akaona hawafai wazanzibari - akamuweka tanganyika.

Sijui kama unatania au la.Hata hivyo hayo maneno si ya kweli na ni ya kusikitisha kama kweli ndio fikra zako hizo.

Siyo hilo tu, uporomokaji wa Shilingi ambao umeiathiri znz kwakiasi kikubwa - huko mwanzo znz ilikua ina fanya biashara vizuri sana kupitia nazi na karafuu - znz serikali ilikua inaumia pale ilipokua inatakiwa ifidie malipo kila ambapo shilingi inaporomoka - hatujasikia lolote kutoka serikali ya muungano kuangalia hili - zaidi bank of Tanzania ambao ndio wamekua kama IMF wa zanzibar kwenye Tanganyika kuinyonya na kuiua Zanzibar (ukoloni Mamboleo wa Tanganyika).

Shilingi ni fedha ya Tanzania nzima na si bara, kuanguka kwa shilingi sio sababu ya kuanguka kwa kilimo cha Zanzibar. Jaribu kuangalia uzalishaji wenu kwanza.Kuanguka kwa shilingi tena kungewafaidisha wazalishaji wenu maana bidhaa zenu zingekuwa rahisi kuuzika nje.
Kuhusiana na BoT nyie si mlikuwa na bado mnayo benki yenu ya watu wa Zanzibar? Iwaje haikufanya kazi yake?

Leo hii wameshaona Zanzibar inaweza kujikomboa kupitiza mafuta - wao wanasema na hichi kiwe chini ya muungano! Kwa hilo tu bora usikuwepo huo muungano - sioni faida yake kwa zanzibar.

Unazidi kunisikitisha, hivi hii leo wananchi wa Shinyanga, Mwanza, Manyara na kwingineo wakianza kuwa na fikra kama zako tutafika kweli?

Uzalendo kwanza!

Muungano upo tu kwakuikandamiza Zanzibar; kama wanahisi uwepo ( hao mainland) kutahitajika kulipa fidia kwa yote tuliopoteza kwa zaidi ya miaka 40!

Wewe ni wakuombewa tu maana inaelekea una matatizo ya hali ya juu!
 
CHAMA ni VIKAO. Waulizeni kina DP, UDP, TLP, UMD,TADEA, ... Bado navyo ni vyama?
 
Na yanayojadiliwa katika vikao huweza kukijenga au kukibomoa chama. Kwa mwelekeo wa hili, CCM ipo katika hali gani? Wazanzibariw amechanganywa na kauli ya tambwe jana kuwa Zanzibar si nchi
 
Ni NCHI MBILI zilizoungana tukapata TZ. Ukisema Zanzibar ni NCHI, maana yake TZ haipo.
 
SIdhani kama tunapoongea Muungano tunamaanisha nini? Nikionacho mimi tena kwa macho ayngu ni kwamba kuna muungano wa ASP na TANU = CCM. Lakini kusema kuna Tanganyika + Zanzibar = Tanzania ni uongo mkubwa. Ni kwa nini kuna Zanzibar hali kuwa hakuna Tanganyika? Hayo ni mazingaombwe tu.

Lakini nashangaa kuona watu wanagombea vitu vilivyoko kwenye magazeti. Kama wazanzibar hawaelewi nini maana ya mafuta waje hata kwangu niwafafanulie. Ni kwa nini mnalumbana kwa kitu kisichokuwepo?
Watu walimwaga damu Burundi baada ya kusikia kuna dalili za mafuta karibu ziwa Tanganyika, kule Sudan Al-Bashir na ze Garang wanaumizana kwa kuwa kuna dalili za mafuta.

The presence of FF indicators does not signify its presence. Therefore, my people, don't hurry in hate while you own nothing.
 
TANGANYIKA + ZANZIBAR = TANZANIA

Therefore,

ZANZIBAR = TANZANIA - TANGANYIKA

But, TANGANYIKA = nil

It follows that: Zanzibar ni nchi kama ilivyo Tanzania!
 
Mkuu leo ni dola $ 129 kwa debe! the lowest in the last three months! Kula yangu inategemea haya mafuta ndio maana niko on top of it kila siku mkuu sio kuwa nakurupuka on this ya mafuta, maana kila yanavyobadilika ndio na kula yangu inabadilika!

Mkuu FMES nimeuswa na hiyo data ya $129, ila cha kushangaza bongo bado ni mwendo wa dizeli buku mbili hata kama itasimama hapo kwa miezi sita.

Others: sorry kidogo kwa kutoka nje ya mada
 
Kuna haja ya viongozi wetu kujifunza kutoka kwa Joseph Kabila na Vladimir Putin, hawa wakubwa huongea maneno machache sana tena kwa tahadhari kubwa. Ukweli kauli ya mh.Pinda imeleta mtafaruku mkubwa zanzibar, kauli hiyo ilipaswa kutamkwa na jk au ak.
 
Ni kweli kabisa. Huwezi kusema una mafuta wakati hujachimba kisima. Fikira duni za kizanzibari zinakera kweli...hawa watu wanalilia Zanzibar iwe nchi kamili ili wafaidi mafuta, wasaidiwe na OIC.....kweli fikra duni. Zanzibar ikijitenga itakufa kifo kibaya jamani...nini kinazalishwa zanzibar? Ingekuwa mimi uwezo wangu ningewaruhusu wawe watakavyo uone kazi...wapemba waingie Bongo kwa visa..mmmh yakheeeee..waua ati.
Wandugu Zanzibar mafuta yapo tena mengi sana,kuna mkutano fulani ilielezwa histori ya mafuta na nafikiri alikuwa huyuhuyu Maalim seif wakati wa kugombea yeye na Dr Salmin Amuri ,alielezea historia ya mafuta na kumega kuwa utafiti na data zipo ,sio hizi za jana na juzi ,zipo za tokea wakati wa utawala wa Sultani na Muingereza na visima vya majaribio viliwahi kuchimbwa na ndipo hapo wingi wake ulipojulikana ,ila wakati huo mafuta hayakuwa tabu na shida kama ilivyo sasa na Mfalme akaamua kutoa amri ya visima hivyo vizibwe na kuwa ni akiba ya baadae kwa vizazi vijavyo vya Zanzibar kwani karafuu ilikuwa tosha na bei yake ni kubwa kuliko ya mafuta ,na iliweza kuiendesha Zanzibar na hata kufikia Zanzibar kutoa misaada kwa nchi za Kizungu akina Norway na Denmark na baazi ya nchi za ukanda huo kutokana na urafikifi waliokuwa nao watu hao wa zamani ni wapi ukiitaja Zanzibar ilikuwa hawaijui kwa ufupi hakuna ,ila usije ukawauliza vijana wa leo ,waulize wale vikongwe vizee vilivyokuwa hoi bin taaban vitamaka na kuitamka Zanzibar kwamba hata wewe unaijua,yaani vitaonekana kama vinakushangaa.
Hivyo Zanzibar imezunguukwa na mafuta msitie shaka juu ya jambo hilo ,kwani mafisadi wasingesimama kidete kuyatafutia washauri ambao eti watapanga mgao wa faida ,wameshafumaniana kwenye zahabu na almasi sasa wengine wanaanza kuelekeza majeshi Zanzibar.
Mafisadi hawachimbi mafuta wakavuna mbona kutageuka Nigeria makandarasi wataondoka viuno juu.
 
Kwanini kusiwe na kipya? Wazanzibari wametunisha misuli na hivyo itabidi walainishwe na kwa upande wa Bara watatakiwa kuacha mchezo wa kuwadharaulisha SMZ mbele ya wananchi.
Hata hivyo kiburi cha CCM Bara kimeshaiponza CCM Zanzibar kwani 2010 mikakati ya mizengwe huenda Wazanzibari wengi wasikubaliane nayo safari hii na mshindi wa kweli wa uchaguzi kupatikana ili suala hili la Muungano lipate utatuzi. Kwa Wazanzibari Uzanzibari kwanza na vyama vitafuata.
Mpaka pale tatizo hili litapopatiwa usuluhishi wa kutowa madaraka zaidi kwa Zanzibar nachelea CCM ina wakati mgumu,
 
nafikiri ajenda kuu itakuwa ni kufahamishana vizuri kama zanzibar si taifa ila ni nchi au vyenginevyo....

muungano una lega lega kwa kuwa wazanzibari hawataki serikali moja na wanataka lazima identity yao isipotee.
 
Nani Atakuwa Sauti Ya Kuwanyamazisha Upande Wa Pili?maana Naona Nchi Haina Mwenyewe Hii......................si Mwenyekiti Wala Amri Jeshi .....hakuna Kitu Hapo......jamaa Ni Soft Kupitiliza Hana Jipya Na Hana Lolote.....nchi Ina Serikali 3 Tofauti....(mafisadi,jk Na Ya Zbar)hamtaki???
 
Hapo umesema na nakubaliana na wewe kuwa Pinda alikuwa na maana kuwa wenye akili zao sawa sawa hawawezi kuwa kwenye haki na namna ya Muungano wetu,
 
hili ni tatizo la kuwa na muungano ambao haupo clear.

huwezi kusema gas ya muungano, zanzibar haiwezi kupewa fungu kama special na itapewa fungu kama mkoa mwengine tu wa tanzania.....kwa sababu zanzibar si mkoa tu mwengine wa tanzania.

na ndio maana zanzibar inapopata mafuta imekuwa na uwezo wa kusema hatutayatoa kugawana kwa sababu mali ya bara zanzibar haifiki.

muungano ukiandikwa sawa sawa, nafikiri matatizo kama hayo yataondoka
 
Mkuu Gaijin, ukweli hakuna sababu ya kupoteza identity ya wazanzibar, tuuwache wenyewe waamue kumaintain au la, kwa Pinda kuwatamkia haikuwa sawa hata kidogo. Kauli hiyo ingetamkwa na waziri kiongozi ingeleta maana. Hata hivyo kuna ubaya gani wakaingia EAC kama state kama ilivyo burundi na rwanda.
 
The oil in Tanzania's coastal belt was discovered in the 1960s but it is only recently, with western governments searching for alternative sources to the Middle East, that these paradise isles are being taken seriously as drilling sites. With negotiations on Zanzibar bogged down between the island and the mainland over which should benefit (semi- autonomous Zanzibar is unhappy with a proposed 60:40 split of profits),
Hapo mafisadi na Wahafidhina ndipo wanaposhikana mashati si mmesikia wamekutana leo huko Unguja.
 
Nikiwa nasoma nimekutana na comment hii pahala, "kwa hivyo mzozo mkubwa unaoleta uhasama na kupatilizana kati ya pande mbili za muungano unatokana na jinsi ya muungano huu unavyoendeshwa,ambapo hatamu za dola ya jamhuri ya muungano zinamilikiwa na Tanganyika na kwamba zanzibar ni wabembezi tu.Maana waziri wa kilimo wa tanganyika huzungumza na nchi za nje kama kwamba yeye ni waziri wa muungano wakati ukweli yeye siye,kama alivyo siye yule waziri wa kilimo wa zanzibar".

Tafakari maneno haya utaona nini kinaweza kutokea huko mbeleni kama viongozi wasipokuwa tayari kufanya kazi nzito na ngumu juu ya kuunusuru huu muungano.
 
Back
Top Bottom