Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Wewe hujui unafikiri kitu gani na unachokiandika sicho ulichokipanga inaonyesha una mgongano wa mawazo na huna coordinasheni ,

Sasa hebu nipe majibu.
1 ) Zanzibar ni kitu gani ? Mkoa ,wilaya,tarafa kata ,jimbo au sehemu ?
2 ) Nani aliwapa nguvu waasisi hao kuunganisha Nchi bila ya ridhaa zaW/nchi?
3 ) Hakuna Muungano kama Nchi zinazoungana hazipo ,ndio ukaona ili kuwepo na Muungano basi inahitajika serikali ya Tanganyika ,huu ni Muungano feki uliojaa mazabe .
4 ) Hakuna mZanzibari anaetaka Zanzibar iwe Nchi kwani haijawahi kutokuwa si Nchi.
5 ) Zanzibar ina maamuzi yake ,Raisi ,Mawaziri ,mahakama na Baraza la wawakilishi.
6 ) Suala unalolizungumza halipo kwani halijatolewa kauli na kuthibitishwa rasmi.ni waZiri Mkuu ambae anakurupuka kwa tiketi ya CCM na sio kama Waziri Mkuu maana tumesikia anapozungumza kama Waziri mkuu huwa analikwepa suala hilo ,huzungumza kama CCM ili kuwatosa wahafidhina si unafahamu wana matatizo tokea walipopigwa na chini kule Butiama.
7 ) Damu itamwagika naona umekwenda mbali hivi kitu gani na nani atamwaga damu kwa ajili ya nini ?
8 0 Mjadala huu upo kwa lengo la kisiasa ,unafahamu tokea wahafizina wamchafulie Kikwete kule Butiama na kumwambia awarudishie ASP yao hadi leo mambo hayajakaa sawa na katika gazeti moja la juzi Wahafidhina wa Zanzibar walisema wanahisia za wenzao wa bara kuwawekea ngumu kwa matatizo yale yaliotokea Butiama ,sijui kama uliliona hilo.

Hapa hakuna kundi wala kikundi ila kuna Muungwana na akina kaka kazi wake wa Butiama na kikundi cha Karume ambavyo vimo katika mapambano ya vita vya maneno na kila mmoja anataka kujionyesha kuwa yeye ndio Superior kuliko mwengine ,nani atapwaya ,hatujui ila muda ndio utakaotuwekea mambo waziii.

Naombeni mnisaidie, hv United States of America ilikuwaje kuwaje..?? Au uliundwaje..!!..?? Na pia, ni nchi ziliungana au ni majimbo au ni kata..??

Second, hv kama ile mipango ya kina Nyerere na Kwame Nkurumah ya kuleta United States of Africa ingekuja, na kukachaguliwa rais mmoja then Tanzania ingeitwaje..?? Jimbo au Nchi..??

Third, hv United Kingdom i.e. London ilianzaje..??

Mimi naomba majibu then ndio nitoe comments..!! As bado niko na maswali haya kichwani mwangu...!!
 
Swali la nyongeza, kwenye orodha ya nchi za dunia, nimejaribu kutafuta kila mahali kama kuna nchi zinazoitwa Tanzania ama Tanganyika ama Zanzibar, nikakutana na nchi inaitwa "United Republic of Tanzania". Kuna mtu amekutana na nchi ya Zanzibar..!!! If yupo anisaidie plse..!! Ninapenda kujua zaidi...!!!..Kabla sijatoa msimamo wangu...!!..!!
 
Wana JF, nimesearch kwenye google nimekutana na hiki kitu:-

For other uses, see Zanzibar (disambiguation).
Zanzibar

Flag
Seal


Map of Zanzibar's main island

Zanzibar is part of Tanzania
Coordinates: 6°8′S 39°19′E / -6.133, 39.317
Country Tanzania
Islands Unguja and Pemba
Capital Zanzibar City
Settled AD 1000
Government
- Type semi-autonomous part of Tanzania
- President Amani Abeid Karume
Area
- Total 1,651 km² (637 sq mi)
Population (2004)
- Total 1,070,000
Zanzibar (pronounced /ˈzænzɨbɑr/) is part of the East African republic of Tanzania. It consists of the Zanzibar Archipelago in the Indian Ocean, 25–50 km (15–30 mi) off the coast off the mainland. There are numerous small islands and two large ones: Unguja (the main island, informally referred to as "Zanzibar"), and Pemba. Zanzibar was once a separate state with a long trading history within the Arab world; it united with Tanganyika to form Tanzania, and still enjoys a high degree of autonomy within the union. The capital of Zanzibar, located on the island of Unguja, is Zanzibar City, and its old quarter, known as Stone Town, is a World Heritage Site.

Zanzibar's main industries are spices, raffia, and tourism. It is still sometimes referred to as the Spice Islands, a term also associated with the Maluku Islands in Indonesia, because of the significance of its production of cloves, of which it is the world leader, and also nutmeg, cinnamon and pepper. The ecology is of note for being the home of the endemic Zanzibar Red Colobus and the elusive Zanzibar Leopard. The word "Zanzibar" probably derives from the Persian زنگبار, Zangi-bar ("coast of the blacks"); it is known as Zanji-bar (زنجبا&#1585😉 in Arabic.
 
Marekani nchi zake zipo na zinaitwa kwa majina yake na kama kuna baazi ya miaka nafikiri Chicago au Texas ilitaka kujitenga kutokana na matatizo ya gawio ila watu walikaa sawa na kusawazisha ila hapa kwetu hakuna kukaa sawa kunaundwa kamati halafu ripoti inatiwa kwenye mashubaka au madroo ndio husikii tena inabaki kumbukumbu tu ,maana baada ya kamati kunahitajika utekelezaji wa kasoro au matatizo yaliogunduliwa na kamati ambayo wakati mwengine kamati huwa inakuja na suluhisho ,lakini huoni kufanyiwa kazi utasikia tu kamati imemaliza na imeshapeleka ripoti kunakohusika ,inakuwa ndio basi imepita.
Kama Kamati au tume ya Nyalali maagizo yake yangefanyiwa kazi na kutekelezwa leo hii kusingekuwepo na manung'uniko , tukubali tu kuwa Tanzania inaongozwa na mafisadi wamegundulika wameundiwa kamati ,uchunguzi umetoka ,kamati ikaundiwa kamati kamati ndani ya kamati maamuzi yametoka lakini hadi leo hakuna utekelezaji zaidi ya uzinguaji ndio kama ulivyosikia Waziri Mkuu kumbe ni goigoi mbali ya vyombo vya habari kumpamba mara utasikia anaanza kuonyesha kucha mara utasikia kavaa njuga ,mara utasikia aanza kuonyesha makeke ,ila kauli zake za hivi karibuni zinaonyesha wazi kuwa tumepata Waziri Goigoi labda atanikamata mimi kwa kusema kuwa ni goigoi.
 
mambo yanayotokea sasa yamenifanya nione kuwa tunaelekea mwisho wa mfumo wa Muungano ambao tunao sasa. Awali, kuzungumzia Muungano hadharani ilikuwa kama taboo, hata miongoni mwa wananchi wa kawaida katika mijadala rasmi. Kutokana na hali hiyo, wananchi waliogopa kuzungumzia Muungano, achilia mbali viongozi.
Lakini mambo yamebadilika sana. Kwanza walianza wananchi wa kawaida kuhoji. Walihoji mambo mengi kuhusu Muungano kiasi cha viongozi kulazimika kuukubali ukweli kuwa kuna matatizo mengi katika Muungano.
Hivi sasa, viongozi na taasisi wanauzungumzia Muungano hadharani na mjadala umekuwa mpana zaidi. kama tungekuwa tunaogelea hapo tu, nisingekuwa na wasiwasi.
Lakini tumekwenda mbali zaidi. Imefikia hatua sasa mihimili mikuu ya utawala (namely Mabaraza ya kutunga sheria na serikali) si yanajadili, bali yanabishana hadharani kuhusiana na Muungano. Viongozi na wanachama wa mihimili hii wa pande mbili zilizounda Muungano wamefikia hatua ya kurushiana maneno huku kila mmoja ukimshutumu mwenzake kwa kupotosha ukweli wa mambo kuhusu Muungano.
Haya yananifanya niamini kabisa kuwa huko tuendandako, si muda mrefu kuanzia sasa, aidha tunaweza kugawana kila mmoja akaelekea upande wake, au tukabadili muundo wa Muungano na kuwa na kitu kipya. Ninaamini haya yatatokea kwa sababu hakuna tena mtu kama Mwalimu Nyerere, ambaye alikwua anatumia ubabe wa kidiplomasia kunyamazisha hoja kama hizi. Lakini hata kama angekuwepo, siku hizi 'wananchi si mabwege tena.'
Naomba kuwasilisha
 
Kuna tatizo hapa,Waziri Mkuu inaonyesha amechanganyikiwa na hili si yeye peke yake hata Kikwete ,uongozi wanauchanganya na uanachama, ni kweli kuwa wao ni wanachama wa CCM lakini unaposhika madaraka ya Inchi na kuwa Raisi au Waziri Mkuu au waziri wa aina yeyote ile inatakiwa uwe na tahadhari kubwa ya kuchanganya mambo la si hivyo utakuwa unafanya mambo kama mwenyekiti wa Chama chako au Katibu ,aliposema Tambwe sikuwa na la kusema kwani alikuwa anakisemea Chama chake au alikuwa anawakilisha Chama chake kama alivyo ni mkuu wa uongo wa kisiasa katika CCM,lakini Pinda anaposema tena ndani ya Bunge Tukufu kuwa anaiwachia CCM kuamua au kutoa tafasiri , Pinda kama Waziri mkuu labda angelisema suala hilo anamuachia Waziri wa mambo ya ndani na nje au anawaachia wanasheria wa Serikali zote mbili na angewapa miezi sita ili warudi na jibu.Kusema anawawachia CCM ni kosa la jinai.
Suala la Zanzibar au Tanganyika kuwa Nchi au si Nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano hilo kwa ukweli ulio wazi si suala la kuhusisha Serikali ya Muungano au Serikali ya Zanzibar ,seuze chama cha siasa ambacho kimejaa mafisadi na uongozi unaohujumu Taifa au chama kingine chochote ,labda pengine naweza kusema Bunge la Jamhahuri na Baraza la wawakilishi kwa upande wa Zanzibar wanaweza kwa kiasi fulani kulijadili suala hili na sio kulihitimisha ,bali maamuzi ya mwisho warudi kwa wananchi na kulijadili na ukiangakia ,hakuna cha kujadiliana ila kuna kupanga upya namna ya Muungano lakini sio kusema Zanzibar sio Nchi au Tanganyika sio Nchi ,sidhani kama kuna Mtanganyika anekubali kuambiwa au kusema Tanganyika sio Nchi na wale wanaosema Tanganyika ilipotea kwa kuanzishwa Muungano hao ni maadui wa waTanganyika inafaa wamulikwe ni dizaini za akina Tambwe ambao hawaoni tabu kupoteza uzalendo wao kwa ajili ya maslahi, huku wakiangamiza wengi kwa tamaa zao.
Kweli tupu!
 
Jana nilimuona na kumsikia PM wetu akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni na alipokuwa akijibu maswali ya Mheshimiwa Mnyaa na mbunge mwingine, alisema kitu ambacho kilinishitua kidogo aliposema kuwa masuala ya uamuzi wa au Zanzibar ni nchi au la; anaiachia CCM kuamua.
Kitu kimoja sijakielewa na nahitaji ufafanuzi kwa kweli kutoka hapa jf ni ile kauli kwamba suala zima la Zanzibar kuwa nchi au la analiacha mikononi mwa CCM.
Je CCM ni nani katika kuamua mstakabali wa nchi yetu? najua kuwa hili ni jambo la kikatiba wala si la katiba ya CCM ila katiba ya nchi ambayo wote tuna maslahi ndani yake. Yaani tusio na vyama vya siasa na wao wenye vyama na maslahi katika vyama vyao. Je ni halali CCM kutuamulia mustakabali wa kikatiba?
Nisaidieni nielewe jamani!
 
Kishazi umekimbiya ?

197006.1010.A.jpg
 
Mmemsikia Sghamhuna leo? Amesema abadani hakuna anayeweza kuondoa unchi wa Zanzibar. Anasema Zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa hivyo daima milele. Ametumia baadhi ya vifungu vya Katiba ya Zanzibar kusisitiza hoja yake.
 
Unajua Tumepata Waziri Mkuu Goigoi yaani ukisikia majuto ni mjukuu basi ndio haya yaliotuganda ,hatujui WaTz tufanye nini naona tupo njia panda, huyu jamaa ni mmoja kati ya kakakazi wa Kikwete ,wanawazamisha wahafizina na Mkuu wao Karume maana kila siku akina kakakazi wa Kikwete wanakanyaga tu na kuwawacha wahafizina na Karume wao wakilia .
Maana kusema mambo ya Zanzibar ni nchi au si nchi anawaachia CCM ni kuzidi kuwafanyia ukorofi wahafizina ,yaani akina kakakazi wamekazana kujibu mapigo ya Butiama na kuwaangalia ASP watajipapatua vipi ,maana kakakazi Pinda akishawachia bomu basi waZanzinbari wanawasakama wahafizina kwa masuali yasiojibika hivyo kuwa na wakati mgumu wa kulinda maslahi ya CCM-Zanzibar upande wa wahafizina ,yaani kama mimi ni Waziri Mkuu kwa kulikwepa suala hilo ningewaambia kuwa siku hizi mtandao kila sehemu hivyo angewapa changamoto waende kugoogle halafu warudi na majibu.Lakini Waziri Pinda anajibu mapigo waliyoyapata Butiama ,kubwa lijalo.
 
wa wapi huyu sipendi kuona anatupeleka anapofikiria (dhambi mbaya ya ubaguzi na utengano)
 
Tatizo sio waziri mkuu ila tatizo ni mfumo wetu wa sheria na katiba mbovu.

Kwani PM anaposema kuwa Znz sio nchi hii ni kwa mujibu wa katiba ,sasa hili linapokuwa ni issue ujue kuwa kuna kitu .

Wazanzibar wamegundua udhaifu uliopo kwa Rais Kikwete na haswa baada ya kumkwamisha kuhusu muafaka kule Butiama sasa wanaua ajenda ya Muafaka na kulifanya taifa na haswa wazanzibar kuanza kuona kuwa adui wao ni bara na sio Karume na wahafidhina wenzake huko visiwani wasiopenda mabadiliko.

This is a test kwa Rais wa nchi hii ambaye pamoja na mjadala mkali kiasi hiki hajajitokeza hadharani kuweka msimamo wa serikali yake ,ingekuwa leo mwalimu yupo angeshaweka msimamo wake dhabiti na sio kama huyu JK .
 
Mmemsikia Sghamhuna leo? Amesema abadani hakuna anayeweza kuondoa unchi wa Zanzibar. Anasema Zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa hivyo daima milele. Ametumia baadhi ya vifungu vya Katiba ya Zanzibar kusisitiza hoja yake.
Haya hiyo ni kutoka Genge la wahafizina liongozwalo na karume likijibu mapigo kutoka KisiwaNdui ,tusubiri akina Kakakazi wa Kkwete nao wakiweka msumari mwengine kutoka Azimio la Butiama sms ambazo zimepangwa kutokana na hasira za Kikwete baada ya juhudi zake ambazo zingempandisha chati kupigwa na chini juu ya muafaka na masuko wa Zanzibar.
 
Ni kufuru kwa Watanzania kuujadili Muungano kama vile ilivyo kufuru kumjadili Mungu na kuuliza maswali kuhusu Muumba!!! Hawa watu ni vichekesho kweli kweli!!! Wanataka kufukia kila kitu na kupretend kama mambo ni shwari kumbe yanafukuta chini kwa chini!!!


Sitta also bans debate on Zanzibar status

2008-07-25 10:19:32
By Bilal Abdul-Aziz, Dodoma


National Assembly Speaker Samwel Sitta issued a directive here yesterday effectively barring Members of Parliament from any further discussion on whether Zanzibar is legally a state.

Sitta, whose intervention came as MPs shot direct questions at Prime Minister Mizengo Pinda under a recently introduced weekly procedure, invoked Rule 53 (8) of the House Standing Orders to cut off the questions and end the session.

``Rule 53 (8) of the House Standing Orders disallows any MP from reverting to any issue that has already been discussed and decided upon? Therefore, my ruling is that we shall not discuss this issue any further,`` he declared.

The Speaker explained that the Prime Minister elaborated comprehensively enough on the issue inside the House last week, including recommending that the Union and Zanzibar attorney generals pursue it jointly to its logical conclusion.

``The issue has already been handed over to the two attorney generals?and when the Prime Minister made the announcement to that effect last week, honourable MPs clapped as a sign that they concurred with him,`` he said.

He stood by his ruling amid a wave of questions on what the Union Constitution said about the status of the Isles from the opposition camp, led by Zanzibar legislators Mohamed Habib Mnyaa (Mkanyageni - CUF) and Dr Ali Tarab Ali (Konde - CUF) .

Mnyaa had demanded explanation from the Prime Minister on whether it was the Articles of Union that formed the United Republic of Tanzania or the Union Constitution that reigned supreme.

``I think Hon Mnyaa is not wishing me any good?I didn?t want to comment on this issue at length?I have learned from the media that there was a demo planned against me in Zanzibar,`` noted Pinda, before responding.

He then said the matter had already been left in the hands of the two attorney generals in the hope that they would make a thorough study of the Constitution and see where there were problems and how best to deal with them.

He added that he believed time had come for the ruling CCM to take up the matter and issue a conclusive statement on it ``after which I think we will be in a position to get a definitive answer``.

But the Konde MP found the response unsatisfactory and stood up to throw a supplementary question opposing the idea of leaving the matter in the hands of the two attorney generals and the ruling party.

``Since the Union belongs to all Tanzanians, the issue is not the responsibility of only the government but of all the people,`` argued the legislator, his favourite option being the initiation of a public dialogue ?so that the people can decide``.

It was at that juncture that Speaker Sitta intervened, issuing the ``stop order``, just as Zanzibar House of Representatives Speaker Pandu Ameir Kificho did only days ago..

Responding to MPs` questions in the National Assembly last week, the Prime Minister was emphatic that there was no way Zanzibar could become a sovereign state within another sovereign state (the United Republic of Tanzania) because doing that would automatically break the April 26, 1964 Union between Tanganyika and Zanzibar.

Pinda, a lawyer, explained that Zanzibar was not a sovereign state because it lost the status when it became part of a new sovereign state known as the United Republic of Tanzania.

He said he saw no way during his prime ministerial tenure in which he would be party to a political experience or process that would lead to the collapse of ``the precious and exemplary Union between Tanganyika and Zanzibar``.

SOURCE: Guardian
 
Na bora iwe hivyo Watanganyika wengi tutafurahia kuutua huu mzigi tuliobeba kwa miaka 44 sasa. Kuna matatizo mengi kuhusu muungano lakini hawataki tuyajadili sasa ni wakati muafaka kabisa wa kuvunja huu muungano wa pwagu na pwaguzi maana wenzetu kidogo kidogo wameanza kuonyesha makucha yao kwa kuwa na bendera yao, wimbo wao wa Taifa na si ajabu watakuwa na pesa na passport zao hivi karibuni, Wadanganyika bado tunang'aa macho tu!
 
Kwa uelewa wangu ni kwamba Zanzibar si nchi. Hii ni kutokana na muungano ulifanywa na waasisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kusema Zanzibar ni nchi ina maana muungano usiwepo. Na hii itamaanisha Zanzibar iwe na maamuzi yake yenyewe bila kuishirikisha Tanzania Bara.

Wazanzibar wanataka Zanzibar iwe nchi. Hapa inabidi busara itumike ya hali ya juu kutatua suala hilo. Kinyume chake damu itamwagika. Lengo la mjadala huu upo chini ya suala la kisiasa. Inaonekana kuna kikundi au kundi la watu wanaotaka kuiyumbisha serikali ya muungano.

Suala hilo ninashauri iachiwe mahakama. Na mahakama inabidi kutoa maamuzi yatakayokubalika na pande zote mbili, zinazotaka Zanzibar kuwa nchi na Zanzibar kuwa sehemu ya Jamhuri ya Tanzania.

Kama Wazanzibar wanataka Zanzibar iwe nchi kwa nini wasiachiwe wajitoe kwenye muungano?
 
Folk,
Muungano haufi leo, amini usiamini kinachotokea hapa ni CCM Zanzibar kutikisa kiberiti wao wanajua A to Z mpini wa CCM Zanzibar kutawala hivyo visiwa umeshikwa na CCM bara. Watapiga kelele lakini Kikwete akiamua kuondoa uvivu wake wote hawa watanyamazishwa, mnakumbuka Dr.Salmini alivyosumbua, mwishoe Mkapa akachoka na alimfokea kama mtoto mdogo kwenye mkutano Dodoma. Kama CCM Zanzibar wangekuwa na upeo wa kuona mbali wangekuwa wamekataa mgombea uraisi wa CCM Zanzibar apitishe na halmashauri ya CCM wakati kuna wajumbe hata hawajui Zanzibar ni nchi au wilaya. Lakini wao walidhia hiyo kwa matakwa binafsi. Na hiki kiburi chote ni kufikiri kuwa wana mafuta na bara itawabembeleza. Huyu Raza, yeye aombe Kikwete asiamue kuwavulia uvivu, ni CCM bara ndo itawaamulia nani awe raisi anayekuja watake wasitake.
 
Back
Top Bottom