Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
M-bongo na Mahegema.
Sema, Zanzibar- Tanzania (ukitaka kumaanisha visiwa vya Unguja na Pemba) Ukisema Tanzania Visiwani (hivyo ni Ukerewe , Mafia na nyenginevyo). Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni sahihi katika kipengele chake kinachosema Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano. Na katiba ya Zanzibar ni sahihi katika kipengele chake kinachosema Zanzibar ni Nchi (ya kidemokrasia). Unapochambua hizo Katiba unatakiwa uende nazo sambamba. Don't take them in isolation-Ndio maana mnapata taabu sasa kuthibitisha ni Nchi au si Nchi.
 
Mwiba,
In a Government administration yule Waziri wa Zanzibar ni "bomu" kweli kweli; hajui miiko yake ya kazi! Harrison kama mbunge kaongea ukweli mtupu! It is time for presidents to appoint people who are capable as learders than such a crap like this Zanzibar fellow!

Sielewi kipi kimekufanya upelekee attack kwa Harrison! Different stories!

Yule Waziri wa Zanzibar kaongea kwa usahihi kabisa kwani kwa msiojua yule ni msaidizi wa mkuu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi. Kama alivyofanya Pinda aliposema kwa sauti ya kinanda kuwa ZAnzibar si nchi bila kutafakari nini alichokuwa akikisema nae shamuhuna alifanya hivyo akijiamini nini alichokuwa akikisema.
Hivyo huyu Mwakyembe pamoja nanyi mnaomsaidia hamuelewi kuwa Pinda si Bosi wa Shamuhuna? Kwani hiyo katiba kandamizi inasema nini kuhusu Waziri Mkuu na anawakilisha sehemu gani ya Muungano na Katiba hiyo hiyo inasemaje kuhusu kuwepo kwa Serikali mbili kwenye Muungano?
Kukurupuka tu hasa kwa mwanasheria kama mwakyembe kunamuanika aina ya mtu alivyo.
 
Jee Zanzibar ni Nchi au hapana? tumeshuhudia malumbano ya upande wote wa muungano huu.. wengi wa upande wa Tanganyika wamesisitiza si nchi na ni uhaini kuzungumza suala hili...upande wa Zanzib wengi wameonesha hisia zao kwamba ni nchi.wanaokatta Zanzibar si nchi wanasisistiza katiba ndio inasema hivo... katiba ni sheria...mama ya kila nchi..lakini katiba ina badilika...NCHI... Haibadiliki....ZAnzibar ilipoungana naTanganyika bado imebaki kuwa nchi kamili ijapokua haina madaraka kamili kutokana na Muungano hivo baadhi ya mambo yakahamishiwa ndani ya Muungano.. lakini imebaki kuwa nchi....ni makubaliano tu.. kwamba tutakuwa na kiti kimoja U.N ... HIVIO Zanzibar haijuilkani huko sababu sio ... mwanachama...ni makubaliano tu ....na Muungano sio SACRED Au ..sio kitu kitakatifu....kama nchii mbili hizi Mmoja wapo akiona hakuna maslahi...ya kuendea na Muungano.. basi ...anayo haki ya kujitoa...walifanya hivyo..nchi zote zilizokua za USSR...Wamefanya hivo.. Yugoslavia,...Checkoslovakia , nk...
Hapa suali kubwa kwanini kila siku huu Muungano haishi Manungunuko... na KILA siku manunguniko hayo yanatoka..upande wa Zanzibar pekee yake????..na mara Zote Wa Zanzibari wamepoteza uhai na hadhi zao..kwa kuhoji muungani...walianza kina Kassim Hanga..Othman Sharif,...Aboud Jumbe....SEif Sharif..na orodha ni ndefu...Hata Salmin pia hakusalimika alipata kejeli baada kuonesha dalili tu za kutetea maslahijapo kidogo ya Zanzibar.....SUALI NI JEEE HUU MUUNGANO UNA FAIDA NA MASLAHI NA MUSTAKABALI WA KIUCHUMI NA WATU WAKE KWA UPANDE WA ZANZIBAR????/.
Mara Nyingi utasikia wapemba wana Biashara na Majumba kariakoo so ndio faida ya muungano ....khaaa...hizi ni faida ..za maslahi binafsi..ZANZIBAR kama NCHI haifaidiki na kuwepo majumba kama yale yaliopo opposite na Sea cliff ambayo ni ya Fatma Karume....hizi ni faida ambazo hazina tija yoyote na Zanzibar...ni faida ya kibinafsi tu..hata kenya wako wa Zanzibar ..wako UK...WAKO ARABUNI..WAKO..USA..WAKO Dunia nzima wamejenga na hakuna Muungano...hilo halina mshiko.....
Muungano huu ni kama wa kulazimishwa...inaonesha wazi KARUME alilazimishwa na Nyerere kuungana..kwani Tangia mwanzo Alisaidiwa kuwekwa madarakani na Tanganyika...lakini hakujua kama atakuja ku pay high price ya kupoteza uhai na uhuru wa nchi yake.. hakuona mbali...lengo lilikua tangia zamani kuitia mkononi Zanzibar......hio muungano huu sio wa hiari yasemwe ya kusemwa lakini huu haukuwa wa hiari ...
Ili Zanzibar iendelee kiuchumi na elimu basi ni lazima ijitoe...
UCHUMI
Leo Zanzibar inaendesha uchumi wake yenyewe lakini nchi haina BANK KUU YAKE hivyo inashindwa kupanga mambo yake ya kiuchumi..sawa sawa
Zanzibar inatumia sarafu moja ..shillings ambayo haina udhibiti nayo...hata wakifanya vipi kiuchumi..export yao ikiongezeka..haina ATHARI yoyote katika uchumi wa Zanzibar...thamani ya sarafu...inflation..vyote vinaamuliwa na na BOT...KUTEGEMEA hali ya uchumi upande wa Tanganyika...export ...ya Tanganyika ikiporomoka...utalii ukiporomaka..Tax collection yaKE IKIPOROMOKA na kusababisha thamani ya vitu kupanda Masikini Zanzibar nao wanabebeshwa mzigo...ingawa wao wana bajeti yao..wanakusanya ushuru wao...lakini UKWELI hawawezi ku COTROLL ukuaji wala mfumuko wa bei....wao ni wakuumia tu....
Na hata kama utalii utakua Upande wa Zanzibar...karafuu zivunje rekodi...bado mapato hayo hayatakua na athari yoyote Zanzibar....mfumuko wa bei hauwezi kupungua....
wakati Tanzania Bara ilipokubali masharti ya Kufufua uchumi..ya IMF...Upande wa Zanzibar haukufikiriwa...athari zake ...ni...kubwa....wakati Tanganyika imekubali kupunguza thamani ya sarafu yake.....haikuangalia upande wa pili wa muungano...wao walipata missada mingi ya kufufua uchumi wao...wakawaacha Zanzibar na madonda ya kushuka kwa thamani..ya fedha....bila msaada wowwote.....hapa ndipo Zanzibar ilipoanguka...na mpaka leo....ni mahatuti....misaada ile ilikua ni kwa ajili ya Tanzania bara tu....
ITAENDELEA...............................................
[/LIST]

 
Nashindwa kukusoma mkuu, unaonekana bado una mengi ya kusema kuhusu Mwakyembe, maliza yote tuendelee na mjadala.Kufananisha kamati ya bunge kumsema Lowasa na huyo kiongozi wa Zanzibar ni vitu viwili tofauti kabisa!

Tena jamaa inaonekana hamuogopi mtu yeyote yule anazungumza ukweli kabisa.anazungumzia kanuni za baraza la mawaziri.umechanganya vitu tofauti kabisa kaka.Are you senior???

Big up Dr.; mwiba ukuchome wenyewe!!!!!

Waberoya
''Dot let school interfere with your education''

Kanuni za Baraza la Mawaziri? Mbona hueleweki ? Mwakyembe ni Mbunge anazungumzia Baraza la Wawakilishi hapa kuna uhusiano gani? Hii ni sawa sawa na Mwakyembe aseme JF iathibiwe kwani inampinga Waziri Mkuu au SIo?
Barza la wawakilishi ni chombo cha Serikali ya Zanzibar iliyopo kikatiba na Bunge ni Chombo kincho mamlaka kwa Serikali ya Tanganyika(oops! Ya Muungano) Sasa Mwakyembe anawakilisha jimbo gani kule Zanzibar na jee Uspika wa Kule Zanzibar unapokezana kati ya Sitta na Kificho?

Mbona tunashindwa kutofautisha mamlaka au hii ndiyo ile ile kuwa Upande mmoja unahozi kila kitu hata cha upande mwengine juu ya makubaliano?
 
Of course, this Shamuhuna guy anastahili kuadhibiwa. Hili ni suala la kikatiba ndugu Mwiba na halina uhusiano kabisa na makosa ya kiutendaji yaliyofanywa na Lowassa.

Nadhani unachuki binafasi na Mwakyembe mkuu. Otherwise, it looks like you must be experiencing some serious pyschological problems; and I strongly suggest that you find some good professional counseling before things get even worse.

Aadhibiwe kwa kumpinga Pinda au aadhibiwe kwa kukaidi Katiba. Nafikiri wewe una chuki binafsi na Shamuhuna. Shamuhuna kumpinga Pinda ni haki yake kikatiba na Shamuhuna kuipinga Katiba hana kosa kwani hata yeye Pinda mwenyewe ameomba ufafanuzi wa katiba hiyohiyo kwa Wanasheria wa pande mbili. Sasa anachotaka mwakywembe ni nini? Alimuondowa Lowassa pengine alikenda kinyume na watu wake lakini Shamuhuna hajaenda kinyume ha Wazanzibari hivyo KIMASOMASO!!!!!!!!!
 
Nafikiri nakubaliana nawe Ngekewa. Wengi tunaojadili hii mada muhimu tunajichanganya kama anavyojichanganya Mbunge Msomi wa masuala ya Katiba Mheshimiwa Mwakyembe. Sishangai ndio maana hata hatuwezi kusoma "between the lines" wakati Wenzetu Wazanzibari wanapohoji. Jee yao ni Nchi au si nchi ndani ya Muungano huu. Watu wanawasikia lakini wanawakariri ki- Kasuku.
 
Habari Ndugu zaku watanganyika, tatizo lililoko mbele yetu ni kwmba viongozi wa juu wa kisiasa nchi hii hasa wale wa CCM hawataki kusema ukweli, Zanzibar siyo nchi, hii maada haina mjadala, na la kusema kuwa kwa sababu wamegudua mafuta ndiyo tuenedelee na huu muungano feki mimi sikubaliani nayo hata kidogo.

Hakuna kitu tunachokipata sisi watanganyika kwa kuwa chini ya kivuli cha Muungano, kila kitu tunacho katika ardhi hii ya watanganyika, jamani huweji kulinganisha mafufa ya Pembe na utajili huu tulionao, nini hatuna watanganyika, kila kitu Mugu ametupa ila tuu, Viongozi tunaowachangua kwa sifa za mwonekano wa sura zao na mengineyo mengi ndiyo umetufikisha hapa.
Watanganyika tuna tatizo la kuchangua watu kwa sura, hivi leo hii Mheshimiwa raisi anaweza kusimama mbele ya kadamnasi na kuseme ulemsemo wake wa danganya toto "Nguvu mpya na kasi mpya" nadhani kwa upande wangu watanganyika watakaomsikia akisema hivyo mbele yao watampiga mawe ka si kumzomea.
Umefikia wakati ndugu zangu watanganyika tukaacha kuchagua watu kwa kuaangalia vyama bali kwa kuangali Mtu vs utendaji kazi wake na uhalisia wake kiudani zaidi.

Kwa upande wangu nataka MUUNGANO UVUNJIKE HATA SASA HIVI.
 
Hey East AFrica, Zanzibar is not sovereign.

...the thing which is happening here is that, the zanzibaris want to depart from Tanzania mainland because they think they are sufficient of themselves because of discovery of oil in Pemba, so wanataka wayafaidi yale mafuta with exclusion of watz mainland. Na kweli kuna mafuta mengi sana kule na kama zanzibar wakiamua kujitenga na tz wakayachimba, kila raia wao atakuwa tajiri sana kwasababu utajiri wao utakuwa mkubwa kuliko uwingi wa watu. zanzibar is below 1 mil. population. it is not easy for them to be independent from Tanzania unless the constitution of the United Rep.of tz is amended to exclude it.

Mbeba Maono,

If this is the motive of their separation from TZ mainland, I think they are buying a dangerous idea due to the fact that; if they succeed to quit from mainland will be just the beginning of the show.

The second show will be that, people from Pemba where there is the discovery will never accept to share the fortune with people from Unguja.

Is this not the start of oil's curse syndrome? Wait and see!

Our brothers and sisters in island should think twice.

Njimba
 
Wana JF tunatakiwa kuwa makini na watu wanaopost comment kama "MWIBA", watu kama hawa ambao wanashindwa kuchambua na kuelewa ukweli na pumba hatuwataki.
Mheshimiwa Mwakyembe amesema kweli tupu na kama tutapata watanganyika kama hao 50 ndani ya bunge letu mambo yengukuwa tofauti leo hii, nadhani hata Mheshimiwa rais angesema kwa sauti kubwa ZANZIBAR SIYO NCHI.
Huyu waziri wa zenji anakesi ya kujibu mbele ya watanganyika.
Mwiba: kama unachuki binafsi na Mwakyembe sema ili wana JF wakusaidie, tupo tayari kukurekibisha ili uende kwenye mstari.
 
Pole sana MWIBA lakini siku zote kweli itakuwa nzito na ndio maana magunia ya Pumba yanakuwa makubwa ili yafikishe uzito wa kiroba kidogo cha mchele.
Inasikitisha kuona JF ikiwa na watu mahiri na waliosoma wanashindwa kuona mwanga wa uliyoyaeleza na kwa wingi wao wanakuvamia kwa kuonyesha sura halisi ya yule wanaofikiri wao kuwa ni shujaa. Hata shujaa ni binaadamu na hukosea na anapofanya hivyo basi tumsahihishe ili arudi kwenye njia iliyo sahihi.
JF mnashindwa kuelewa kuwa Muungano huu ni wa sehemu mbili na tunahitaji kuheshimiana. Pinda kama Waziri Mkuu na kofia mbili ,Mtanganyika na Mkuu wa mambo ya upande wa Tanganyika ndani ya Muungano huu aliwakosea Wadau wa upande mwengine na walipomweleza kuwa kwao wao neno alilolitamka ni baya kwao aliwajibika kuwa muungwana na kukubali kuwa nimekosea lakini kusisitiza kuwa kile kibaya kwa upande mmoja ni sahihi kwake kulikwisha muondolea heshima kwa Wazanzibari na ndio maana Wazanzibri waliamua kumpinga. Sasa wana JF ni sahihi kunyamaza kwa kitu unachokiamini kuwa ni sahihi? Kosa liko wapi kupinga kauli ya Pinda?
Nini nafasi ya serikali ya Zanzibar kwenye Katiba ya Muungano? Sio kushughulikia masuala ya Zanzibar? na Shamuhuna Ameisemea Zanzibar kwenye chombo halali cha serikali inayotambuliwa kikatiba. Hili lote JF hamlitambuwi? Sasa mbona tunachanganya mambo , huyu Mwakyembe anaposema wathibitiwe Wawakilishi wa Zanzibar anasema kwa ajili ya Wazanzibari au nani?
JF mnamvamia MWIBA kwa kumsema Mwakyembe na double Standard mnasahau kuwa Lowassa alikuwa Waziri Mkuu na kwa mujibu wa kauli ya Mwakyembe anayotupa sasa ni DHAMBI kumpinga Waziri Mkuu, jee nyie JF ni sahihi hii ? Jee wabunge waliposimama na kuupinga utetezi wake walikuwa wakiifanya hiyo Dhambi.? Tusiseme kuwa hizi ni isse tofauti kwani mtiririko mzima wa shughuli za bunge ndio unaojenga matukio.
 
Nilishasema na ninarudia tena ushauri wangu wa kuuvunja mfumo mzima wa utawala wa zanzibara ili tuunde mikoa miwili yaani mkoa wa kwanza uwe 'Unguja' nzima na mkoa wa pili uwe 'Pemba' yote. Vinginevo tuvunje muungano, tumechoshwa na madai yao yasiyokuwa na tija kwetu! Wasitubabaishe na hayo mafuta yao yanayochimbika na kuisha muda wowote! Na sisi tutachimba ya kwetu! Hivi wanafikiri sisi hatuna mafuta?!! Ngoja wajitenge halafu wayaone matokeo yake!
 
Binafsi ninaheshimu sana watu ambao wana msimamo na kile ambacho wanakiamini na hawaogopi kusema hivyo mbele ya mtu yoyote bila kujali ni Rais au Polisi (hata kama mimi sikubaliani nacho). Sidhani kama PM kusema kuwa 'Zanzibar si nchi' alafu ikatokea mtu yeyote mwingine akasema 'Zanzibar ni nchi' basi mtu huyo anastahili kuitwa mtovu wa nidhamu. Woga wetu kwa viongozi wa juu wa serekali wa kuongea yale ambayo tunaamini ni kweli (hata kama si kweli) umetutia matatizoni kwenye masuala mengi, enzi za 'hewala bwana' zimeshapita!

.....lets assume ulichoandika hapo juu ni sahihi.........sasa wewe kwa hiyo hoja je unakubaliana na justification ya kulinganisha anayoifanya Nudgu Mwiba kuwa Dr Mwakyembe..........kamchafua Lowassa na eti kwa kuwa Kamati yake haikuyasema maovu yote then anastahili kuadhibiwa?

.....where do we draw the line between the two here.......? where is the correlation....?

......Mkuu Mwiba nahisi kuna mtu kaiba password yako.....ama?
 
Mwakyembe is very right. I would expect these strong words to have been uttered by the president and the issue of Zanzibar would have come into the end. Leaving this issue of whether Zanzibar is a sovereign state or not into the hands of Sitta and people like Shamhuna it gives much worries if proper answer/solution can be obtained.


Well said Taffu.

These strong words were supposed to be uttered by the president! It could be the end of discussion!
 
Ndugu yangu Mwiba, wakati mwingine huwa unanichekesha sana unapoamua kumwaga pumba kavu kavu.
 
Kura za hapa JF zinaonyesha Muungano hauna faida na unahitaji kuvunjwa haraka.
zaidi ya silimia 90 wanasema haufai uvunjwe na 40 za mafisadi wanasema ulindwe . Haya tanganyika inakuja mafisadi tafuteni pa kukimbilia.
 
.....lets assume ulichoandika hapo juu ni sahihi.........sasa wewe kwa hiyo hoja je unakubaliana na justification ya kulinganisha anayoifanya Nudgu Mwiba kuwa Dr Mwakyembe..........kamchafua Lowassa na eti kwa kuwa Kamati yake haikuyasema maovu yote then anastahili kuadhibiwa?

.....where do we draw the line between the two here.......? where is the correlation....?

......Mkuu Mwiba nahisi kuna mtu kaiba password yako.....ama?

Tatizo la ufahamu bado mnalo na inaonyesha mna view ya karibu na mnasahau mlipotoka,habari niliyoiandika niliianzia mbali sana mambo ya mafisadi ambayo yameanza kutoweka na haikutokana na kauli zilizotamkwa na Mwakiyembe bali nilijaribu kuingilia tabia ya mwakiyembe ni mtu aneonyesha ana kigeugeu hayupo katika kuiona haki inatendeka na inatumika ipasavyo ,mMwakiyembe kitabia anaonekana ni mtu wa maji kujaa na kupwa au anafuata mshindo au anafuata upepo na yupo tayari kukuzamisha ili aonekane ni mkweli mwenye kufuata maadili,sasa watu wanaosahau sahau wataona Mwakiyembe yupo na msimamo lakini msimamo wake ukiupima na kurudi kwenye baadhi ya mambo utaona hana tofauti na akina Mwinyi,Kisumo na Tambwe Hiza ,watu wa maslahi na ndivyo walivyo ndugu zetu wa CCM japo baadhi yao maana wengine wanaonyesha wasafi au wanang'ara kama mwanga lakini tabia zao utaziona wakati wanapotoa sauti.
 
Mwiba.

Ukitaka kumkosoa Waziri mkuu au kukosoa msimamo wowote wa serikali, tema kwanza ulaji wako kama waziri ndipo uanze kulonga.
Huwezi anzakata tawi la mti ulo kalia.
Waziri ukipinga usemi wa Waziri mkuu kweli ni utovu wa nidhamu kiutendaji; hii haina uhusiano na utovu wa nidhamu wa kushindwa kumwamkia mkubwa huko mtaani.

Mwiba?

Ile sentensi yako ya Mtu kuruka kama mwanamke aliye shikwa mbavu inanifanya nikuweke kwenye kundi fulani.
Kuna njemba kibao pengine ikiwa ni pamoja na wewe zikishikwa mbavu zinaruka kama farasi alopagawa,sasa ni vipi mwenzetu uwataje wanawake tu???
 
Vijana

Kama nilivyoandika hapo awali ni mfumo wa utawala wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) ambao unawabaisha hata mawaziri wa Zanzibar pamoja na wazanzibari wenyewe.
Hili ndilo tatizo la muungano wetu mwaka huu wa 2008. Waziri Mkuu Pinda amabaye yeye mwenyewe ni mwanasheria na alikuwa ni msaidizi wa hayati Nyerere aliposema bagu bagu bila kuficha kwamba Zanzibar sio sovereingn state bali ni serikali ndani ya serikali ya muungano wa Tanzania basi kumezuka ubishani.

Swala ni kwamba Zanzibar ina mabalozi wake n’gambo ama inawakilishwa na mabalozi wetu wa Tanzania?

Tusidanganywe wala msidanganywe hata tone la mafuta hawana. Miamba hiyo na majabali hayo ambayo tunayaita “sedimentary rocks” bado kamwe hayaonyeshi dalili za petroleum.
Bali tusisumbuwane ila tuufunje huu muungano ili tuondowe kero la hawa wanzanzibari amabo hawana fadhili.
 
Wana JF tunatakiwa kuwa makini na watu wanaopost comment kama "MWIBA", watu kama hawa ambao wanashindwa kuchambua na kuelewa ukweli na pumba hatuwataki.
Mheshimiwa Mwakyembe amesema kweli tupu na kama tutapata watanganyika kama hao 50 ndani ya bunge letu mambo yengukuwa tofauti leo hii, nadhani hata Mheshimiwa rais angesema kwa sauti kubwa ZANZIBAR SIYO NCHI.
Huyu waziri wa zenji anakesi ya kujibu mbele ya watanganyika.
Mwiba: kama unachuki binafsi na Mwakyembe sema ili wana JF wakusaidie, tupo tayari kukurekibisha ili uende kwenye mstari.
Ana kesi ya kujibu mbele ya WaTanganyika iweje waTanganyika ? na Sio WaTanzania hivi unaelewa ya kwamba Tanganyika imezirai na Zanzibar bado inatuta ? Unaweza kukariri mstari ambao wewe unauona kuwa ni kweli tupu,halafu tuone kama Mwakyembe hakuvunja Katiba kwa kuzuia haki na kutaka Shamhuna asulubiwe ,maana ndivyo ilivyozoeleka ndani ya CCM ukisema ukweli unaitwa mhaini,unaitwa mpinzani unaonekana si mwenzetu ,unaekewa kikao na wafuata upepo wote wanakuzamisha kwa kuwa tu umepinga kauli,jamani mambo ya Ndio Mkuu yamepitwa na wakati wakuu wenyewe sasa hawajui hata dira ya Tanzania ilipoekea wanahitaji msaada wa hali ya juu na sio kila wanakotuongoza tuseme ndio huko huko mbele kwa mbele ,huu ni wakati wa kuekana sawa awe Raisi,Waziri Mkuu,au Waziri yeyote au kiongozi yeyote yule Jeshi au Polisi si wakati wa kunyamaziana na anapopingwa mtu wengine wakaruka na kusema unakosa adabu ,huna nidhamu ,kila mtu tapewa heshima yake na kuheshimiwa lakini linapokuja suala la kujadiliana hapo hapatakiwi usawa nani Mkuu nani mtawala nani mtawaliwa panatakiwa hoja kujadiliwa kupingwa kukosolewa isiwe akipingwa mtu aseme fulani inafaa adhibitiwe,inafaa achuliwe hatua ,inafaa aadhibiwe, ukisikia mtu anasema hivyo basi huyo ni adui wa haki tena ni mtu ambae inaonyesha ubaya wake upo ndani kwa ndani.
Shamhuna hana uhusiano na serikali ya Muungano wala CCM kama sikosei,ni kiongozi katika serikali ya Zanzibar ,hivyo alikuwa anawajibika kusema lolote iwe amesema alivyosema Pinda ni sahihi au alivyosema Pinda si sahihi ,natumai anayo haki hiyo ,sasa kilichowatonesha akina Mwakiyembe ni kwa nini Shamhuna amesema au ameipinga kauli ya Pinda hata kama kauli hiyo ilikwishatolewa maelezo lakini ifahamike ni wapi ilipotolewa maelezo ni Bungeni kwenye chombo cha Muungano na Shamhuna nae ametolea maelezo kwenye Baraza la wawakilishi Chombo chao huko Zanzibar ,kosa lipo wapi ? Bahati mbaya Shamhuna amesimamia Uzalendo wa Taifa lake na Katiba ya Zanzibar ambayo inatamka wazi Zanzibar ni nchi ,na yeye yupo sahihi zaidi kuliko Pinda kwani hakuna sehemu katika Katiba ya Muungano palipoandikwa Zanzibar si Nchi.
Jaribuni mnaposoma na kutoa hoja msiwe na jazba aidha kama wewe ni CCM hapo nitakuwa sina la kukufanya ,vilevile ukiwa ni Mtanganyika pia nitakuwa nakuangalia tu.Ila Kama unajihesabu ni Mtanzania basi itabidi uwe katika njia inayotakiwa kuwepo ,japo upo na Chama usijaribu kukilinda chama kinapokosea ni lazima ukiulize,ukihoji ili kupata maelezo na kama yanahitajika kupingwa basi usisite kupinga ,kuliko kuogopa kuambiwa unadharau au huna adabu ni aibu kwa DR>Mwakiyembe kusema maneno alisema ya fulani adhibitiwe au sijui atiwe adabu na wengine mnarukia na kumuona ni shujaa sijui kwa kigezo kipi.
 
Back
Top Bottom