KWA TAARIFA HIYO: SERIKALI YA ZANZIBAR IMEJIMALIZA YENYEWE
Wakuu nimekuwa consistent toka juzi kuwa hoja alizozi"raise" Dk. Mwakyembe ni zamsingi mno ukiziangalia kwa makini. Angalia sasa statement kutoka Serikali ya Zanzibar:
(a) kwamba PM hana authority over Zanzibar, mwenye authority ni huyo Chief Minister wao! PM na Chief Minister ni level moja!
(b)hawawajibiki kwa Bunge wala Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(c)ina vikosi vya majeshi!
Hii ni nini kama si uasi! PM anapigiwa kura kwenye Bunge na wabunge wanaochaguliwa na Wazanzibari na Watanzania BARA. Ana direct authority Zanzibar kwenye masuala yote ya Muungano ambayo ni mengi: mambo ya nchi za nje, ulinzi na usalama, polisi, emergency matters, citizenship, immigration, loans and foreign trade, income tax, customs, bandari, usafiri wa anga, posta, simu, sarafu (fedha), leseni za viwanda, takwimu, elimu ya juu, mafuta, gesi asilia, mitihani ya taifa, utafiti, utabiri wa halio ya hewa, mahakama ya rufaa, vymana vya siasa n.k. (Ibara ya 4 ya Katiba ya Muungano na Nyongeza ya kwanza ya Katiba) Sasa hiyo "sovereign" state ya Zanzibar imebaki na nini cha msingi kutukoromea kila kukicha na kudai wimbo wao wa taifa na bendera?
Kwa hiyo Kikwete ni Rais wa wabara tu? Makubwa!
Serikali ya Zanzibar leo inadiriki kutamka kuwa ina majeshi ya kwake? Mbona wanainajisi Katiba? Ibara ya 147 inasema ini marufuku yeyote yule kuunda au kuweka jeshi la aina yeyote isipokuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Ndiyo maana Shamhuna alitamka kuwa "kipindi cha kutishana kimepita", kwa maana ya kwamba sasa wamejizatiti, Bara tukileta ujinga watatudhibiti hata kijeshi!
Nimeisoma taarifa ya Serikali ya Zanzibar mara sita, ni hoja za kitoto zinazokwepa hoja ya msingi aliyoi"rasie" Mbunge Mwakyembe: Shamhuna ana mamlaka gani kum"criticise" na kumpinga PM, bosi wake, na kuacha kutumia vyombo vya kiserikali vya ku"handle" misuguano ya kimuungano, kaka huo si utovu wa nidhamu? Sasa kuna haja gani kuwa na Makamu wa Rais (Mzanzibari)na Waziri specifically for Muungano ambao kwanza ni Wazanzibari na ni kiungo kikuu cha kikatiba cha Serikali ya Muungano na Zanzibar?
Nilicheka sana juzi wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Bw. Hamza Hassan Juma, alipoongea na waandishi wa habari na kukataa kujibu maswali ya ziada. Mwandishi mmoja wa Zanzibar (jina silisemi sasa) akanieleza: "angejibu nini mtu mwenyewe hata taarifa yenyewe alikuwa hajaielewa, alikuwa anasoma tu kama kasuku. Unawajua mawaziri wa Karume - huyo jamaa ni darasa la saba na profession yake fundi cherehani". Sijui kama ni kweli, lakini washikaji you are free to cross-check. lakini hawa ndo waobeba hatma ya maisha yetu!