Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Zanzibar wapewe nafasi ya kuchagua je? muungano wanautaka au la!! wakikataa Wazanzibar wote walio bara wanaamua kuchagua kuishi bara ama warudi,vivyohivyo wabara nao wawape kuchagua wawe wazanzibar ama wabara.

Harafu jina la nchi kunakua hakuna haja ya kulimun'gonyoa wabara wana asume ni Tanzania bila matatizo na Zanzibar inakua hivyo.

Ila huko zanzibar nadhani kutokua hapatoshi kati ya pemba na unguja.
 
Mbona hamuidai Tanganyika na mmeng'ang'ania Muungano ? Yupo wapi Mtikila ? Ipo wapi G-55 ? Sababu gani zinamfanya Mtikila na Kundi la G-55 kuidai Utaifa wa Tanganyika ? Je hao ni au walikuwa wajinga ? Wasioitakia mema Tanzania ?


..tanganyika ikirudi hakutakuwa na zanzibar, kutakuwa na unguja na pemba.

..mtakuwa kama visiwa vya comoro. in fact zanzibar itabidi itawaliwe. kwasababu kutakuwa na civil war isiyoisha.
 
...Naye Naibu Spika wa Bunge, Bibi Anne Makinda alipoulizwa kuhusu kanuni za Bunge zinasemaje kuhusu shinikizo anazopewa Dkt. Mwakyembe, alimtaka mwandishi azitafute ili ajionee mwenyewe... Umeona ustadi wa kukwepa suala ,huyu Bibi Anne ameshaona tatizo linalomnyemelea Mwakiyembe.


Ama kweli Tanzania tuna Viongozi...

Ushauri wa bure kwa Mwakiyembe ,awaombe radhi ikiwa anajiona ana kosa au hana kosa na atakuwa amefunga mjadala kiustaarabu kabisa. Mwakiyembe afahamu kuwa yeye ni mbunge na natumai anaifahamu CCM ilivyo ,Mwakiyembe amegusa sega ,sega ambalo linawanufaisha magogo wa CCM bara , natumai mtaiona factor na hatari inayoplay kwa Mwakiyembe.


KWELI MKUU MWIBA UNATAKA DR MWAKYEMBE NA ELIMU YAKE YOTE AWAOMBE HAWA WATU WASIOJUA KATIBA WALA MAANA YA MUUNGANO MSAMAHA. HII NITHAMU YA WOGA IMEPITWA NA WAKATI, JK ANATAKIWA ATOE ONYO KALI KWA KARUME KUWA AWAFUNDISHE NITHAMU VIONGOZI WA VISIWANI LA SIVYO AWAATHIBU YEYE KWA NGUVU ALIZONAZO KAMA KIONGOZI WA JAMHURI.

HIZI KAULI HUWA ZINACHIMBA MASHIMO AMBAYO KUYAFUKIA SIO RAHISI.
 
Mwiba naanza kama kukupata unakoelekea! nakubaliana na wewe kimsingi kwamba inawezekana hasira ya wazanzibari inatokana na kuona kwamba hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na serikali ya muungano kuhusiana na kashfa zote zilizoikumba nchi hususani hii ya EPA ambayo wao wana-stake inawafanya wapandishe hasira na kujifanya wao ni nchi. Na wanaanza kuzungumzia mafuta yao kwasababu wanaona watanganyika bila kumoffend yoyote hapa ndiko kunakozalishwa mafisadi angalau hao wanaotajwa kuhusika na kashfa zote kubwa katika nchi hii.Wanahisi ufisadi huo utafika kwenye mafuta yao na hivyo wao kama nchi hawatafaidika chochote! Hakuna ubishi kwamba kila kauli zinazotolewa zanzibar japo hazitoki katika ikulu ya zanzibar kwa maana ya rais Karume lakini zinaonekana kuwa na baraka zote za mkuu wa SMZ.
 
..tanganyika ikirudi hakutakuwa na zanzibar, kutakuwa na unguja na pemba.

..mtakuwa kama visiwa vya comoro. in fact zanzibar itabidi itawaliwe. kwasababu kutakuwa na civil war isiyoisha.

Mkuu DAR si LAMU,

Naona umegeuka Yahaya, unajua yatakayotokea Zanzibat wakitengana na Tanganyika?

Mimi sioni kabisa hapa hata tunajadili nini, kama Zanzibar wanajiona ni nchi sawa, waandike hata vitabu kwamba wao ni nchi na hakuna kitakachobadilika, bano UN, hawatakuwa na mwakilishi, bado Olympic wataendelea kuwakilishwa na team ya Tanzania nk.

Hata wakijitenga sioni ubaya wowote, tumeona nchi kibao zinajitenga hapa duniani lakini bado matatizo yao hayakutatauliwa kwa kujitenga. Wazanzibar kama wataamua kwa kura huru kwamba wanajitenga, wajitenge tu. Tena mimi ningelikuwa rais wa TZ, ningewapa na champain ya kusherehekea huo uhuru wao.

Muda wa mabavu kwenye hii dunia umepita kabisa. Ukiona mambo yameshindikana ni bora kuachana kuliko kudundana mangumi.
 
Lol hakuna mafisadi kwa sababu hakuna cha kuiba.


Hata kuiba kura ni ufisadi tena mkubwa.Ni bora mtu akuibie pesa kuliko kumyang'anya mtu haki na demokrasia yake yake.
Hivi cuf wanamtambua Karume??

Viongozi waliposema JK ametumwa na Mungu si lazima atumwe kuja kubadirisha uchumi tu bali hata hiyo wanayomchokoza muchokoza ametulia anawalia timing 2010 ili awatose na hatimaye CUF kupata haki yao ya msingi.
 
Hawa jamaa wanatangaza secession na Rais wa Muungano anabaki kucheka cheka tu!!

Mwanakijiji, unachokisema kina kweli ndani yake. Inabidi sasa Rais atoke huko alikojificha na kutoa statement kuhusu hili suala. We muache tu achekecheke na hawa wapemba aone kama hawata secessed toka kwenye muungano!

NB: As a matter of fact, kwani tunafaidika nini hasa na muungano?
 
Kauli ya SMZ inatoa picha hii moja kubwa ama SMZ haitambui Katiba ya Jamhuri ya Muungano au SMZ ina wajinga wasiojuwa wajibu wao au kuifahamu Katiba.

Katiba ya Jamhuri inazungumza Waziri Mkuu kama nafasi ya tatu kutoka Rais na makamu wa Rais.

Waziri mkuu huteuliwa na Rais na kisha hidhinishwa kwa kura za Wabunge ambao ni kutoka pande zote za Muungano.

Maamuzi ya bunge la Muungano ni ya Tanzania si ya Tanganyika (Tanzania bara).

Sasa kama Waziri Mkuu anapewa kura ya kuhalalishwa na Wabunge kutoka Zanzibar, je hicho kitendo maana yake ni nini?

Je SMZ leo inawakana wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Muungano? Je SMZ inaikana Katiba ya Jamhuri wa Muungano? Je huo si Uhaini?
 
Katiba inasema hivi kuhusu madaraka na majukumu ya Waziri mkuu

52​
.-(l) The Prime Minister shall have authority over the
control, supervision and execution of the day to-day functions and
affairs of the Government of the United Republic.
(2) The Prime Minister shall be the Leader of Government
Business in the National Assembly.
(3) In the exercise of his authority, the Prime Minister shall
perform or cause to be performed any matter or matters which the
President directs to be done.

53.​
-(1) Subject to the provisions of this Constitution, the Prime
Minister shall be accountable to the President for the exercise of his
authority.
(2) The Executive of the United Republic, under the
authority of the President, shall be the organ having the power to
determine the policy of the Government in general, and Ministers
under the leadership of the Prime Minister, shall be collectively
responsible in the National Assembly for the execution of the affairs
of the Government of the United Republic.

 
Narudia tena, wanachokifanya Zanzibar ni kutangaza secession by default:

Kama: Wana Rais, Kama wana Baraza la wawakilishi, kama wana "vyombo vya ulinzi", kama wana maamuzi yao wenyewe, na kama wao ni nchi kamili (siyo sehemu ya nchi iliyoungana) kimsingi wanachosema ni kuwa Zanzibar ni nchi huru nje ya Muungano na hivyo itambulike hivyo i.e not part of the Union and hence by default declaring itself an Independent Country.

Kama tukilinganisha walichoadiwa kufanya CUF na kile walichodaiwa kufanya wazee wa Pemba, kinachofanywa na CCM Zanzibar is by law treasonous.
 
Narudia tena, wanachokifanya Zanzibar ni kutangaza secession by default:

Kama: Wana Rais, Kama wana Baraza la wawakilishi, kama wana "vyombo vya ulinzi", kama wana maamuzi yao wenyewe, na kama wao ni nchi kamili (siyo sehemu ya nchi iliyoungana) kimsingi wanachosema ni kuwa Zanzibar ni nchi huru nje ya Muungano na hivyo itambulike hivyo i.e not part of the Union and hence by default declaring itself an Independent Country.

Kama tukilinganisha walichoadiwa kufanya CUF na kile walichodaiwa kufanya wazee wa Pemba, kinachofanywa na CCM Zanzibar is by law treasonous.

Mzee Mwanakijiji,

nimekupata vizuri ndio maana nauliza je kauli yao kumdharau Waziri mkuu walifanya kwa makusudi au kijinga ionekane makusudi!

Angalia utata wa Muungano wetu kwenye hiki kipengele;-


64.-​
(1) Legislative power in relation to all Union Matters
and also in relation to all other matters concerning Mainland
Tanzania is hereby vested in Parliament
(2) Legislative power in Tanzania Zanzibar over all
matters which are not Union Matters is hereby vested in the
House of Representatives.
(3) Where any law enacted by the House of
Representatives concerns any matter in Tanzania Zanzibar
which is within the legislative jurisdiction of Parliament, that
law shall be null and void, and likewise if any law enacted by
Parliament concerns any matter which is within the legislative
jurisdiction of the House of Representatives that law shall be
null and void.
(4) Any law enacted by Parliament concerning any matter
shall not apply to Tanzania Zanzibar save in accordance with
the following provisions:
(a) such law shall have expressly stated that it shall
apply to Mainland Tanzania as well as to
Tanzania Zanzibar or it replaces, amends or
repeals a law which is in operation in Tanzania
Zanzibar;
(b) such law replaces, or amends or repeals a law
which was previously in operation in Mainland
Tanzania and also in operation in Tanzania
Zanzibar pursuant to the Articles of the Union of
Tanganyika and Zanzibar, or
pursuant to any law which expressly stated that it
apply to Mainland Tanzania as Tanzania Zanzibar;
or
(c) such law relates to Union Matters; and whenever
reference is made to the term ‘Tanzania” in any law
it is hereby declared that such law shall apply in the
United Republic accordance with the interpretation
contained in the provisions of this Article.
(5) Without prejudice to the application of the Constitution
of Zanzibar in accordance with this Constitution concerning all
matters pertaining to Tanzania Zanzibar which are not Union
Matters, this Constitution shall have the force of law in the whole
of the Republic, and in the event any other law conflicts with the
provisions contained in this Constitution, the Constitution shall
prevail and that other law, to the extent of the inconsistency with
the Constitution, shall be void.

 
Wakuu tusichanganye mambo hapa, straight to the point Zanzibari ni Mkoa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa maneno mengine ni only a State kama Rukwa na Manyara kama kuna asiyetaka dawa ni kubadili katiba ili Zanzibar iwe Nchi ndani ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Zanzibar ni RC, kama ma-RC wengine wa Rukwa na Manyara, kama sio Mtwara, rais anapokuwa hayupo katiba iko very clear anakaimiwa na Makamu wa Rais Shein, na yeye akiwa hayupo nafasi ya Rais inakaimiwa na Waziri Mkuu, na yeye akiwa hayupo inakaimiwa na Spika wa bunge,

Rais wa Zanzibar is no where in the picture, sasa kama sio RC wa mkoa ni nani huyu? Kama wa-Zanzibari wana tatizo hapo basi waende kwenye katiba, tumechoka sana na nonesense! no solution so far wanaonekana kuamua kuwa part of the problem, badala ya kuwa part of the solution sasa sisi Bara hatuwezi kuwasaidia kwa hili, ni uamuzi wao kusuka au kunyoa!


Sisi Bara tunaondoka!
 
KWA TAARIFA HIYO: SERIKALI YA ZANZIBAR IMEJIMALIZA YENYEWE
Wakuu nimekuwa consistent toka juzi kuwa hoja alizozi"raise" Dk. Mwakyembe ni zamsingi mno ukiziangalia kwa makini. Angalia sasa statement kutoka Serikali ya Zanzibar:
(a) kwamba PM hana authority over Zanzibar, mwenye authority ni huyo Chief Minister wao! PM na Chief Minister ni level moja!
(b)hawawajibiki kwa Bunge wala Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(c)ina vikosi vya majeshi!
Hii ni nini kama si uasi! PM anapigiwa kura kwenye Bunge na wabunge wanaochaguliwa na Wazanzibari na Watanzania BARA. Ana direct authority Zanzibar kwenye masuala yote ya Muungano ambayo ni mengi: mambo ya nchi za nje, ulinzi na usalama, polisi, emergency matters, citizenship, immigration, loans and foreign trade, income tax, customs, bandari, usafiri wa anga, posta, simu, sarafu (fedha), leseni za viwanda, takwimu, elimu ya juu, mafuta, gesi asilia, mitihani ya taifa, utafiti, utabiri wa halio ya hewa, mahakama ya rufaa, vymana vya siasa n.k. (Ibara ya 4 ya Katiba ya Muungano na Nyongeza ya kwanza ya Katiba) Sasa hiyo "sovereign" state ya Zanzibar imebaki na nini cha msingi kutukoromea kila kukicha na kudai wimbo wao wa taifa na bendera?
Kwa hiyo Kikwete ni Rais wa wabara tu? Makubwa!

Serikali ya Zanzibar leo inadiriki kutamka kuwa ina majeshi ya kwake? Mbona wanainajisi Katiba? Ibara ya 147 inasema ini marufuku yeyote yule kuunda au kuweka jeshi la aina yeyote isipokuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Ndiyo maana Shamhuna alitamka kuwa "kipindi cha kutishana kimepita", kwa maana ya kwamba sasa wamejizatiti, Bara tukileta ujinga watatudhibiti hata kijeshi!
Nimeisoma taarifa ya Serikali ya Zanzibar mara sita, ni hoja za kitoto zinazokwepa hoja ya msingi aliyoi"rasie" Mbunge Mwakyembe: Shamhuna ana mamlaka gani kum"criticise" na kumpinga PM, bosi wake, na kuacha kutumia vyombo vya kiserikali vya ku"handle" misuguano ya kimuungano, kaka huo si utovu wa nidhamu? Sasa kuna haja gani kuwa na Makamu wa Rais (Mzanzibari)na Waziri specifically for Muungano ambao kwanza ni Wazanzibari na ni kiungo kikuu cha kikatiba cha Serikali ya Muungano na Zanzibar?
Nilicheka sana juzi wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Bw. Hamza Hassan Juma, alipoongea na waandishi wa habari na kukataa kujibu maswali ya ziada. Mwandishi mmoja wa Zanzibar (jina silisemi sasa) akanieleza: "angejibu nini mtu mwenyewe hata taarifa yenyewe alikuwa hajaielewa, alikuwa anasoma tu kama kasuku. Unawajua mawaziri wa Karume - huyo jamaa ni darasa la saba na profession yake fundi cherehani". Sijui kama ni kweli, lakini washikaji you are free to cross-check. lakini hawa ndo waobeba hatma ya maisha yetu!
 
Wakuu tusichanganye mambo hapa, straight to the point Zanzibari ni Mkoa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa maneno mengine ni only a State kama Rukwa na Manyara kama kuna asiyetaka dawa ni kubadili katiba ili Zanzibar iwe Nchi ndani ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Zanzibar ni RC, kama ma-RC wengine wa Rukwa na Manyara, kama sio Mtwara, rais anapokuwa hayupo katiba iko very clear anakaimiwa na Makamu wa Rais Shein, na yeye akiwa hayupo nafasi ya Rais inakaimiwa na Waziri Mkuu, na yeye akiwa hayupo inakaimiwa na Spika wa bunge,

Rais wa Zanzibar is no where in the picture, sasa kama sio RC wa mkoa ni nani huyu? Kama wa-Zanzibari wana tatizo hapo basi waende kwenye katiba, tumechoka sana na nonesense! no solution so far wanaonekana kuamua kuwa part of the problem, badala ya kuwa part of the solution sasa sisi Bara hatuwezi kuwasaidia kwa hili, ni uamuzi wao kusuka au kunyoa!

Sisi Bara tunaondoka!

Mkuu Field Marshall ES.

Nakuongezea... President wa Zanzibar... ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Muungano.

Ingawa sikumbuki ... kwamba mwenyekiti wa baraza la mawaziri ni nani... Rais au Waziri Mkuu....

Ni wakati muafaka wa kupima competence za mwanasheria mkuu wa serikali... anawajibika kumshauri vizuri mheshimiwa Rais.
 
nadhani kuwa swala hili liamuliwe tena na jaji mkuu ambaye bahati nzuri ni mzanzibari. katika moja ya hukumu zake kwenye swala linalofanana na hili aliwahi kutamka kuwa zanzibar siyo sovereign state kiasi kuwa haiwezi kuwa na kesi ya uhaini (treason). sijui akipelekewa hili la sasa atasemaje safari hii.
 
Back
Top Bottom