Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Nakubalina nawe dada angu kuwa wao wanajikaza tu lakini wanawategemea nyinyi kwa kila kitu. Pengine ingekuwa vizuri ukaeleza kiasi na kwa namna gani wanawategemea nyinyi.
Tulielezwa hapo nyuma na SMZ kuwa serikali ya Muungano au Tanganyika haisaidii chochote kwenye bajeti ya Zanzibar. Mengine kama umeme,maharage,mbatata ni biashara hamtowi msaada kwa Wazanzibri. Mlishindwa hata kuwakumbuka kwa misaada ya chakula wakati wa EL NINO na pale mwaka 2006 mliposaidia mikoa iliyopata janga la njaa hamkuuliza Wazanzibari waliponea nini. Nafikiri suala hapa si utegemezi bali ni ubanaji wa kuwafanya Wazanzibari wasipate maendeleo.

Hivi kwa nini serikali ya Muungano ichangie bajeti ya Zanzibar? Lakini si kuna mambo ambayo yanasimamiwa na serikali ya Muungano huko Zanzibar? Kwangu mimi swali la muhimu ni mchango wa Zanzibar kwenye bajeti ya Muungano? Mbona mara nyingi tu nimesikia serikali ya Muungano ikiisaidia serikali ya Zanzibar? Kuna wakati iliwalipia mishahara na deni la umeme! Haya yote wenzetu hamyaoni?
 
Hivi kwa nini serikali ya Muungano ichangie bajeti ya Zanzibar? Lakini si kuna mambo ambayo yanasimamiwa na serikali ya Muungano huko Zanzibar? Kwangu mimi swali la muhimu ni mchango wa Zanzibar kwenye bajeti ya Muungano? Mbona mara nyingi tu nimesikia serikali ya Muungano ikiisaidia serikali ya Zanzibar? Kuna wakati iliwalipia mishahara na deni la umeme! Haya yote wenzetu hamyaoni?

Swadakta. Tusisahau pia kuwa Muungano ni ujumla na pale TRA, Civil aviation, leseni za uvuvi wa bahari kuu na nyenginezo zinapotiwa kwenye mfuko wa Muungano inafika wakati tugawane na hapo ndipo unapoona kuwa Zanzibar wanapewa chao.
By the way hapa tukizungumzia utegemezi total wa Zanzibar kwa Tanganyika na sio Muungano kama alivyodai dada yetu niliyemnukuu kabla.
 
Hivi kwa nini serikali ya Muungano ichangie bajeti ya Zanzibar? Lakini si kuna mambo ambayo yanasimamiwa na serikali ya Muungano huko Zanzibar? Kwangu mimi swali la muhimu ni mchango wa Zanzibar kwenye bajeti ya Muungano? Mbona mara nyingi tu nimesikia serikali ya Muungano ikiisaidia serikali ya Zanzibar? Kuna wakati iliwalipia mishahara na deni la umeme! Haya yote wenzetu hamyaoni?
Sasa na wewe nawe ndio unauliza suala gani hilo ? Hivi wafadhili hawasaidii bajeti ya Cocktail (Tanganyika ndani ya Tanzania ) ,Zanzibar ilepeleka majeshi Uganda tena ndio waliokuwa mstari wa mbele au hilo hulijui na ndio walioanza kumkurupusha adui ,hebu mtafute mkweli akupe hadithi za Majeshi kutoka Zanzibar yalichokifanya Uganda ,maana hawa wanaotoka Tanganyika wao walikuwa wanavamia maduka na kuondoka na vijisenti na maredio na Matv wakati wa kurudi wakubwa waliowazidi ujanja wakawambia vitu vyote mlivyopora viwekeni pale vitarudishwa huko huko mliko viiba ,ila kati ya hao mmoja alikuwa bamdogo ambae ndie alienipa mkasa huo ,yeye akasimama kidete na kumwambia mkubwa huyo kuwa kama anataka vita vizuke ndani ya Tanzania basi ajaribu kuwapokonya zana walizokwapua huko Uganda ,mkubwa akasinyaa na kuona jamaa bado wanavumbi vumbi .
Zanzibar imebaki kuwa Nchi ndani ya Tanzania tofauti na mlivyokuwa mnatomeza kama mnawinda, sasa sijui WaTanganyika masikini za Mungu hawajui wako wapi wanabaki kuing'ang'ania nchi ya kubuni.
 
JK agonga mwamba.
Maandamano ya kumuunga mkono yavunjwa

na Mwandishi Wetu
SASA ni dhahiri kuwa kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete kuhusu hadhi ya Zanzibar katika Muungano haijawaridhisha Wazanzibari.
Taarifa kutoka visiwani humo zinaeleza kuwa imeibuka misuguano ya chini kwa chini baina ya viongozi wa serikali visiwani humo na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), yakiibuka makundi miongoni mwao ambao bado hawajaridhika na kile kilichosemwa na Rais Kikwete katika hotuba yake ya kihistoria bungeni wiki iliyopita.

Kwa upande mwingine, msimamo wa Chama cha Wananchi (CUF), ambacho ni chama kikuu cha upinzani visiwani humo, wa kuipinga hotuba ya Kikwete katika kipengele cha hadhi ya Zanzibar, umezidi kuleta mfarakano baina ya viongozi wa CCM na SMZ.

Kilele cha kugonga mwamba kwa kauli ya Kikwete, kilijidhihirisha baada ya maandamano yaliyoandaliwa kuiunga mkono hotuba yake hiyo, na kupata baraka za Jeshi la Polisi juzi, kuvunjwa jana katika mazingira ya kutatanisha.

Maandamano hayo yalikuwa yameandaliwa na CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar na yalipangwa kufanyika leo.

Maandamano hayo yalikuwa yaanzie katika viwanja vya Komba Wapya hadi Msikiti wa Ngamia, Amani mjini Zanzibar, na mgeni rasmi alipangwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz.

Kwa kuonyesha kuwa suala hilo linahusisha mgogoro mzito, viongozi kadhaa wa CCM Mjini Magharibi, waliohojiwa na gazeti hili kutaka kujua sababu ya kuahirisha maandamano hayo, walikataa kulizungumzia suala hilo na wengine wakitoa kauli za kutaka kujiweka mbali na mgogoro huo.

Alipohojiwa jana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, Yussuf Mohammed, alisema hafahamu sababu ya kuahirishwa kwa maandamano hayo, kwa vile wasaidizi wake walikuwa bado hawajampa taarifa yoyote.

"Ni kweli nimesikia yameahirishwa, lakini sifahamu hadi sasa sababu ya kuahirishwa kwake, kwa vile wasaidizi wangu bado hawajanipa taarifa juu ya sababu ya msingi ya kuahirishwa maandamano hayo," alisema mwenyekiti huyo wa mkoa, ambaye kimsingi ndiye alipaswa kuwa na taarifa zote kuhusiana na maandamano hayo.

Hata hivyo, alisema kwamba azima ya kufanyika maandamano hayo na mkutano wa hadhara, bado ipo na ratiba ya kufanyika kwake inatarajiwa kupangwa tena kwa vile muda bado upo.

Taarifa ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi kupitia kituo cha televisheni cha serikali (TVZ) juzi usiku, ilisema kuwa, maandamano hayo yameahirishwa hadi itakapotolewa taarifa nyingine.

Maandamano hayo yamevunjwa siku chache tangu kufanyika kwa maandamano kama hayo kisiwani Pemba na kuwashirikisha wanachama wa CCM kutoka mikoa miwili ya kisiwa hicho.

Taarifa zaidi zilizopatikana jana zilieleza kuwa, kumejitokeza mvutano kutokana na baadhi ya viongozi wa CCM Zanzibar kutaka yafanyike na wengine kupinga.

Haikueleweka wazi kwa nini baadhi ya viongozi wa CCM Zanzibar wanapinga maandamano hayo, lakini habari zaidi zimesema kuna viongozi ambao hadi sasa hawajaridhishwa na ufafanuzi wa Rais Kikwete juu ya hadhi ya Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano, alioutoa alipohutubia Bunge hivi karibuni.

Aidha, kitendo cha CCM kisiwani Pemba kuandaa na kufanya maandamano hayo, nacho kimeanza kulalamikiwa na baadhi ya viongozi wa CCM Unguja.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz, ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi, naye alisema hafahamu sababu ya kuahirishwa maandamano hayo, kwa vile hayakuandaliwa na CCM taifa.

"Naomba watafuteni watu wa mkoa ndio walioandaa maandamano hayo, wao watakuwa wanafahamu zaidi sababu za kuahirishwa kwake," alisema.

Maandamano hayo yameahirishwa yakiwa tayari yamepatiwa kibali na Jeshi la Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mapema juzi, Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi ilipiga marufuku maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na kikundi cha Wazanzibari, yaliyokuwa yamelenga kuunga mkono tamko la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuwa Zanzibar ni nchi.

Polisi katika taarifa yao walisema kwamba walilazimika kuzuia kufanyika kwa maandamano hayo kwa vile tayari kulikuwa na maombi ya wananchi wengine kufanya mkusanyiko kwa siku hiyo, na hivyo ulinzi wa polisi ungeelekezwa huko.

Hayo ni maandamano ya tano kukwama kufanyika katika Kisiwa cha Unguja tangu kuibuka suala la hadhi ya Zanzibar katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Inaonekana kuwa hotuba hiyo ya Kikwete kuhusu hadhi ya Zanzibar, imewagawa Wazanzibari hata ndani ya CCM yenyewe.

Dalili kwamba maandamano hayo yalikuwa katika hatihati zilianza kuonekana juzi, siku moja kabla ya kufanyika kwake. Kwa kawaida, CCM inapoandaa maandamano, kunakuwa na shamrashamra siku moja kabla katika maskani zote za chama hicho.

Lakini hali ilikuwa tofauti juzi ambapo hakukuonekana shamrashamra zozote katika maskani za CCM.

Tayari wanachama wa CCM katika mikoa kadhaa nchini wameshafanya maandamano kama hayo. Waliongozwa na wanachama wa CCM wa mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya, ambao waliandamana mapema wiki hii, kumpongeza rais kwa hotuba yake makini na nzuri bungeni.

Mjini Dar es Salaam, mamia ya wanachama hao wa CCM waliandamana kutoka ofisi ndogo za chama hicho Mtaa wa Lumumba hadi katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Huko Mbeya, mamia ya wanachama wa CCM nao waliandamana mapema wiki hii kuanzia kwenye eneo la Mafiati jijini humo na kutembea umbali wa kilomita moja na nusu hadi katika ofisi za CCM mkoa, wakiwa wamebeba mabango ya kuwapongeza wafanyakazi kwa kuunga mkono hotuba ya rais na kusitisha mgomo.

Akihutubia baada ya kupokea maandamano hayo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Nawab Mulla, alisema hotuba ya rais imejibu maswali mengi yaliyokuwa yanawatatiza wananchi, likiwamo suala la EPA na suala la Muungano, ambalo lilizua mjadala mkubwa katika siku za karibuni.
----------------------------
Ukiandamana kuunga mambo ya CCM ni sawa na kuwaunga mkono mafisadi.Hayo ya Pemba sijui wamechomekea maana sikuona kuandikwa wala sikuwahi kuyasikia ,fahamu kuwa Pemba ni anga za CUF kama kungelifanyika maandamano basi magazeti yangeandika kwenye ukarasa wa mbele au front line ,kuna mtu yeyote aliona au waliohudhuria ni mgeni rasmi na meza na kiti chake.
Wacheni kuikumbatia CCM.
 
Kimataifa Tanzania ni nchi moja, ndani ya nchi je ni nchi ngapi?

Nukuu kutoka maneno ya Mohamed Seif Khatib!

Kuhusu suala la Muungano, Bw. Khatib, alisema wanaunga mkono hotuba hiyo ya Rais Kikwete kwamba kimataifa (nje) Tanzania ni nchi moja na kwamba sera ya CCM ni mfumo wa serikali mbili na kuwaonya Watanzania kutovunja muungano huo na endapo watafanya hivyo, watajutia jambo hilo baadaye.
 
Sasa na wewe nawe ndio unauliza suala gani hilo ? Hivi wafadhili hawasaidii bajeti ya Cocktail (Tanganyika ndani ya Tanzania ) ,Zanzibar ilepeleka majeshi Uganda tena ndio waliokuwa mstari wa mbele au hilo hulijui na ndio walioanza kumkurupusha adui ,hebu mtafute mkweli akupe hadithi za Majeshi kutoka Zanzibar yalichokifanya Uganda ,maana hawa wanaotoka Tanganyika wao walikuwa wanavamia maduka na kuondoka na vijisenti na maredio na Matv wakati wa kurudi wakubwa waliowazidi ujanja wakawambia vitu vyote mlivyopora viwekeni pale vitarudishwa huko huko mliko viiba ,ila kati ya hao mmoja alikuwa bamdogo ambae ndie alienipa mkasa huo ,yeye akasimama kidete na kumwambia mkubwa huyo kuwa kama anataka vita vizuke ndani ya Tanzania basi ajaribu kuwapokonya zana walizokwapua huko Uganda ,mkubwa akasinyaa na kuona jamaa bado wanavumbi vumbi .
Zanzibar imebaki kuwa Nchi ndani ya Tanzania tofauti na mlivyokuwa mnatomeza kama mnawinda, sasa sijui WaTanganyika masikini za Mungu hawajui wako wapi wanabaki kuing'ang'ania nchi ya kubuni.

Sihitaji kuambiwa au kusimuliwa. Nilikuwa huko! Hao unaowazungumzia hawakuwepo bali walikuwepo watanzania waliotoka Zanzibar, Kilimanjaro, Kigoma, Singida na sehemu zingine za nchi yao. Sikuona jeshi la Zanzibar huko. Na sikuona makaburi ya wanajeshi wazanzibar pale Kaboya! Sikuona majeruhi wa jeshi la Zanzibar Simba Bure na kwingine. Niliona watanzania tu.

Huyo baba yako mdogo mnyang'anyi alitokea wapi? Bara?

Uongo kama huu ndiyo unaowaharibia.
 
Sihitaji kuambiwa au kusimuliwa. Nilikuwa huko! Hao unaowazungumzia hawakuwepo bali walikuwepo watanzania waliotoka Zanzibar, Kilimanjaro, Kigoma, Singida na sehemu zingine za nchi yao. Sikuona jeshi la Zanzibar huko. Na sikuona makaburi ya wanajeshi wazanzibar pale Kaboya! Sikuona majeruhi wa jeshi la Zanzibar Simba Bure na kwingine. Niliona watanzania tu.

Huyo baba yako mdogo mnyang'anyi alitokea wapi? Bara?

Uongo kama huu ndiyo unaowaharibia.
Nafikiri unaeleza yaliyo sahihi Bwana Fundi. Achana na huyo. Huyo ni Mchupiaji tu na Mdandiaji.
 
Sihitaji kuambiwa au kusimuliwa. Nilikuwa huko! Hao unaowazungumzia hawakuwepo bali walikuwepo watanzania waliotoka Zanzibar, Kilimanjaro, Kigoma, Singida na sehemu zingine za nchi yao. Sikuona jeshi la Zanzibar huko. Na sikuona makaburi ya wanajeshi wazanzibar pale Kaboya! Sikuona majeruhi wa jeshi la Zanzibar Simba Bure na kwingine. Niliona watanzania tu.

Huyo baba yako mdogo mnyang'anyi alitokea wapi? Bara?

Uongo kama huu ndiyo unaowaharibia.
Hata Jeshi la Marekani wapo wachina,vietnamese ,wafilipino na juzi tumeona waTz ila wote wanavaa ngozi ya kondoo.
Anatokea Ntwala ni Mzanzibari mwenye asili ya Kimakonde,halafu ni maarufu pale mjini Ntwala ,ila na yeye utafikiri amekunywa maji ya bendera ya CCM yaani unaweza kuikandamiza CCM kihoja basi yeye atatokea na jawabu la kichama ,eti haelewi unazungumzia kitu gani au hujamuelewa.
Si unawajua CCM kwa kubabaisha.
 
US official advocates tolerance, respect in Union structure debate

2008-09-02 11:28:30
By Guardian Reporter


A US official in Dar es Salaam has said that mutual respect and tolerance are needed in finding a standing solution to the ongoing debate on Tanzania`s union structure.

Larry E Andre, Jr., Charge d`Affaires of the US embassy, made the remarks over the weekend when introducing the embassy\'s Zanzibar Affairs Officer David Scott.

``Tanzania is clearly a free society. In our view, it is healthy for such debate to be moderated by mutual respect and tolerance,`` he said.

He said the US respects Zanzibar`s history, its cultural achievements and its unique union with mainland Tanzania.
``I note that Tanzanians have often debated particular aspects of the union agreement, and continue to do so today.

Lively debate about fundamental issues characterises free societies. This is a challenge for politicians worldwide, including in my own country,`` said Andre.

He reminded the gathering that the U.S Ambassador to Tanzania , Mark Green often reminds Americans that they serve the United States Mission to Tanzania and not the US mission to Dar es Salaam [MAFISADI].

``We work with people throughout Tanzania,`` he said.
``In the case of Zanzibar, we recognise its historical role as a principal source of the Swahili culture and it`s a peaceful, well governed, healthy and prosperous island that can greatly influence the entire region for the better,`` he said.

The official said the job of the Zanzibar Affairs Officer would be to be helpful to US support to the island.

``The idea is to support the efforts made by the government of Zanzibar and its people,`` he said, adding that the US had established the Zanzibar Affairs Officer position as one way of strengthening the existing historic ties.

He said the US had directly funded the efforts of various groups of Zanzibaris who were endeavouring to better their communities in many different ways.

He said all the initiatives were undertaken by the official US mission in Tanzania, adding that the United States-Zanzibar partnership extended beyond government-funded efforts.

``Many private American individuals and groups are also working in the island to promote the progress of people in Zanzibar,`` Andre stressed.

``David will help the mission to deepen our relationships with the people and leaders of Zanzibar and to promote all the elements of our partnership,`` he said.
 
Suluhu ya namna gani wanataka wakati mpaka leo bado wabara hawaruhusu ata kuendesha biashara uko visiwani? Kwa lugha fupi huu ni UBAGUZI!!!!

D.12 Short-term domestic travel is not restricted, and there are no entry controls whatsoever for Zanzibar-born Tanzanians onto the mainland. Zanzibaris may travel to live and work freely on the mainland, subject to the same laws that apply to mainlanders, and there is no requirement for mainlanders to show identification to travel to Zanzibar. Mainlanders are allowed to work in the islands but not allowed to own land there. Zanzibaris own property, work and run businesses on the mainland. The "Kazi Nguvu" laws, which date back to the colonial period, and the Human Resources Development Act 1983 were intended to prevent migration to the cities from agricultural areas, and to support the 'Ujamaa' (community) policies of Nyerere to resist urbanisation. They stipulate that persons who are unemployed must return to their home region. These laws are however practically never used, with the exception of removing professional beggars from city streets. Tanzanian citizens can return to Tanzania without difficulty.
 
tuungane na kenya pale kuna ndugu zetu, kwa nini tukaungane na nchi iliyoko kwenye bara lingine kama zanzibar
 
S Mainlanders are allowed to work in the islands but not allowed to own land there. Zanzibaris own property, work and run businesses on the mainland.
Wapo wafanyabiashara wengi tu sasa toka Bara wakiendesha biashara mbalimbali visiwani humo. Zaidi hata hao wazenj hawana haki ya kumiliki ardhi kwani ardhi yote ya Zanzibar ni mali ya Serikali(SMZ), kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1985.
 
Ismail Jussa: Zanzibar tukilala hatutakuwa tofauti na Ukerewe

Mwandishi Wetu Septemba 10, 2008

Hivi karibuni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi na Msaidizi Maalum wa Katibu Mkuu wa CUF kuhusu Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Ismail Jussa Ladhu alifanya mahojiano na kituo cha Redio cha Zenj FM cha Zanzibar, kuhusiana na kauli kwamba Zanzibar si nchi. Katika kipindi hicho, “Nyota Njema: Harakati za Kisiasa,” Jussa, ambaye pia ni mwanasheria, anaelezea msimamo wake na CUF kwa ujumla, kuhusu kauli hiyo kama alivyonukuliwa na redio hiyo na RAIA MWEMA kupata nukuu zake.

Swali: Tuangalie katiba zetu na mapungufu yake. Hebu tuanzie hapo. Kwenye Katiba kuna mapungufu, Ismail Jussa, hali ikoje?

Jussa: Kwanza nashukuru kupata nafasi hii ya kuja tena Zenj FM. Tunathamini sana nafasi kama hizi za kuja kutoa mawazo yetu na kubadilishana mawazo na wananchi. Pili, naam kuna mapungufu katika katiba zote mbili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Katiba ya Zanzibar.

Lakini zaidi, naweza kuthubutu kusema kwamba, ni katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuliko katika Katiba ya Zanzibar. Na nadhani ni mapungufu haya makubwa ndiyo yaliyozua hii mitafaruku isiyokwisha, kuhusiana na tafsiri za mambo mbalimbali ya kikatiba na kisheria.

Hivi karibuni tulipokuwa katika mazungumzo ya Muafaka kabla hayajavunjika, tulikuwa tukifanya rejea katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano kujaribu kuona wenzetu wanafanya vipi mambo mengine. Utashangaa kuona kwamba Katiba ya Zanzibar iko mbali zaidi katika kuweka mambo sawa kuliko Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Ina mapungufu na makosa mengi sana ambayo yanahitaji kurekebishwa.

Swali: Baada ya kuona kuna mapungufu hayo, sasa kwa upande wako na kwa upande wa Chama cha Wananchi, CUF, mnaitafsiri vipi Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Jussa: Nadhani suala wala si chama cha CUF. Haya ni mambo ya kisheria. Suala ni: zinasimama vipi kisheria katiba zote mbili? Hapo ndipo penye tatizo kubwa lililojitokeza kutokana na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda bungeni. Kwa sababu, inaonekana – na wala si suala la Pinda kwa hakika – inaonekana kumekuwa na msimamo wa muda mrefu sana kwa upande wa wanasiasa, na mara nyingine hata wasomi, kutoka upande wa Tanganyika, wanaojaribu kuleta sura kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano iko juu ya Katiba ya Zanzibar. Na hata kauli yake, Pinda, anasema vivyo hivyo, kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano ndio Katiba Mama.

Sasa hapo ndipo penye matatizo, kwa sababu katiba zote hizi mbili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Katiba ya Zanzibar, ni katiba sawa sawa. Hakuna iliyoko juu ya mwenzake. Unaweza kusema kwamba itapokuja tofauti ya tafsiri katika baadhi ya mambo yanayohusu mambo ya Muungano tu, ndipo Katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na nguvu kuliko Katiba ya Zanzibar.

Lakini hata katika hilo, kipimo cha mwisho na cha juu kabisa ni Mkataba wa Muungano. Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili, ambazo zilikuwa dola kamili zenye uhuru wake na uwezo wake kamili, ambazo ziliamua kuungana Aprili 26, 1964, kupitia marais wa nchi mbili hizi.

Sasa Mkataba ule, kwa mujibu wa sheria, ni Mkataba wa Kimataifa, it’s an international treaty, na ndio unaoongoza mahusiano yetu kati ya Tanganyika na Zanzibar na ndio uliozaa Jamhuri ya Muungano. Sasa maana yake nini? Maana yake, Katiba, ambayo ni sheria kama zilivyo sheria nyingine, zote zinapaswa zitafsiri yale mapatano au makubaliano yaliyofikiwa kati ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, zilipoungana kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hapo ndipo penye tatizo.

Sasa wenzetu wamekuwa wakifanya kwa makusudi ili kuendeleza dhamira yao, kwa sababu bahati mbaya wakati Zanzibar tumeingia katika Muungano huu kwa dhamira njema kabisa ya kujaribu kuleta umoja wa Kiafrika, kushirikiana, wenzetu wana dhamira na fikra za ukoloni, kwamba wao wanaona kama vile wameiteka Zanzibar au wanaitawala Zanzibar.

Kwa hiyo, wanapenda wasahau na isahaulike kwamba kulikuwa na Mapatano ya Muungano, ambayo ndiyo yangepaswa kuongoza mahusiano haya na wanajaribu kuyazima. Ndiyo maana hata Mapatano haya sasa huyaoni katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Wanachojaribu kuonyesha ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano ati ndio sheria kuu. Lakini kwa mwanasheria yeyote ungemuuliza, angekwambia kuwa sheria kuu, sheria mama, katika Muungano wetu ilipaswa kuwa ni Hati za Muungano, Mkataba wa Muungano, ambao ni Mkataba wa Kimataifa, na Katiba ya Jamhuri ya Muungano na hata Katiba ya Zanzibar zinapaswa zitafsiri kivitendo. Hapo ndipo penye tatizo kwenye masuala haya yaliyojitokeza.

Swali: Inawezekana kabisa kuwa baadhi ya wananchi hawajui Katiba ya Zanzibar au Katiba ya Jamhuri ya Muungano kule Tanzania Bara, lakini lengo ni kutoa ufahamu. Kama ninyi mlifahamu hivyo, kwamba hizi katiba mbili zina mapungufu, iweje sasa baada kauli ile ya Waziri Mkuu, Pinda, Dodoma, ndipo ianze kuzuka mijadala namna hiyo? Kama mliliona tangu mwanzo, kwa nini hamukuibua hizi hoja tangu hapo ili kuhakikisha kuwa Katiba inarekebishwa isije ikatokea migongano ya namna hii baadaye?

Jussa: Hapana. Kwa hakika wala si chama cha CUF wala si wanasiasa tu. Wananchi wenyewe wamekuwa wakizungumza, mara nyingi kutoka pande zote mbili, kuzungumzia mapungufu ya katiba zetu na mfumo mzima huu wa Muungano namna unavyoendeshwa.

Tatizo ni kuwa tuna Serikali zisizosikia: Serikali ambazo zimetia pamba masikioni, hasa upande wa Jamhuri ya Muungano, kwa sababu kama nilivyosema wenzetu inaonekana dhamira yao ni nyingine dhidi ya Zanzibar. Kwa hiyo wamekuwa wakikataa kuleta mjadala wowote wa maana kuhusiana na masuala haya ya kikatiba na kisheria.

Karibuni kabisa, kama miezi mitatu iliyopita, kwa wanaofuatilia maendeleo katika nchi yetu, watakuwa wanakumbuka kuwa mwanasheria anayeongoza katika masuala ya katiba nchini Tanzania, Profesa Issa Shivji, amezindua kitabu chake kinachoitwa Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika – Zanzibar Union.

Ni kitabu safi kabisa kilichochambua kwa kina masuala ya Muungano. Katika kitabu kile, moja ya dosari kubwa alizozitaja ni kutoshirikishwa kwa wananchi. Kwamba ni mara chache sana wananchi walioshirikishwa katika kutoa maoni yao kuhusu masuala ya Katiba.

Anasema katika historia ya Muungano huu, ni mara moja tu ndipo wananchi walipopata nafasi, mwaka 1983/84, wakati wa mjadala wa Mabadiliko ya Katiba. Lakini na pale, baada ya wananchi kupewa fursa ya kutoa maoni yao, ilipoonekana maoni yaliyotolewa si yanayotakiwa na watawala–na wakati ule hasa, si yaliyokuwa yanatakiwa na Mwalimu Julius Nyerere, basi mjadala ule ukazimwa na Zanzibar kukaambiwa kumechafuka hali ya hewa ya kisiasa.

Nini cha kuitwa kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa? Halikuwa jambo lolote, bali ilikuwa ni dhana iliyobuniwa ili kuja kuhalalisha kuzima mjadala ule ili kuifanya sauti ya wananchi isisikike.

Kwa hiyo, si kweli. Katika kila forum, katika kila jukwaa, katika kila nafasi iliyopatikana, iwe katika Bunge au katika Baraza la Wawakilishi, katika semina, katika mikutano ya hadhara, tumekuwa tukizungumzia haja ya kufanya mapitio ya Katiba zetu ili zitafsiri, kwa njia iliyo sahihi na safi kabisa, Makubaliano na Dhamira za Msingi walizokuwa nazo Mzee Karume na Mwalimu Nyerere wakati wanaunganisha nchi zetu za Tanganyika na Zanzibar kuunda Jamhuri ya Muungano mwaka 1964.

Swali: Historia ni ndefu sana, na ina mambo mengi ambayo yamehusisha waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini kuna tofauti gani kati ya makosa ya kimatamshi na hali halisi ya Katiba yenyewe ilivyo, maana halisi ya Katiba?

Jussa: Sijakuelewa, samahani.

Swali: Yaani, kwenye Katiba yenyewe, kuna tofauti gani kati ya matamshi na maana halisi ya neno lenyewe? Kwa mfano, tunaambiwa Zanzibar si nchi lakini baadaye tukasikia huenda ikawa ni makosa ya kimatamshi, lakini maana halisi ni ipi? Tuanzie hapo. Zanzibar ni nchi au si nchi?

Jussa: Mimi nadhani, suala muhimu hapa na la msingi ni kuzijua dhana, yaani kwa maana ya Kiingereza tunazungumzia concepts ndizo zilizokuwa zinahusika. Na bahati mbaya sana, tunaligeuza suala hili kama vile mchezo wa taarab. Twatafuta lugha gani, neno gani litaleta kibwagizo kizuri.

Hapana, haya ni masuala ya kisheria. Na, nimesikia mwanasiasa mmoja akisema kwamba Kiswahili hakijitoshelezi katika istilahi zake, katika kuyayafanua na kuyachambua maneno ya Kiingereza ya kisheria. Si kweli, maneno matatu ndiyo yanayozungumzwa hapa ya Kiingereza: ni country, nation na state, na yote haya matatu yana tafsiri zake katika Kiswahili.

Country ni nchi, nation ni taifa na state ni dola. Sasa, unaposema Kiswahili hakijitoshelezi na mtu akasema Zanzibar si nchi, ndipo ninapojiuliza amekusudia nini? Na kama alivyosema mwenyewe Pinda – mimi nasema kwamba si mawazo ya Pinda, ndiyo mawazo ya watawala wa Tanganyika kwa upande wa Zanzibar. Amesema hakuteleza ulimi, kakusudia hasa kusema kwamba Zanzibar si nchi.

Haya ni makosa. Ni makosa kwa mujibu wa Mapatano ya Muungano, ni makosa kwa mujibu wa Katiba zetu mbili. Yeye ametumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayosema katika Kifungu cha 1, kwamba Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano, lakini kama nilivyosema Katiba ya Muungano ina mapungufu mengi.

Ukiangalia Katiba ya Zanzibar – kama nilivyosema zote mbili ziko sawa sawa – kwanza katika Utangulizi wa Katiba, ile wataalamu wanayoita Preamble, ambayo ndiyo inayoweka dhamira ya wananchi, inasema wazi wazi, katika miongoni mwa vifungu vyake – na naomba niisome hapa – inasema: “Na kwa kuwa sisi, wananchi wa Zanzibar, tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya haki, udugu na amani…” halafu inamalizia kwa kusema kuwa: “…tumeunda Katiba hii.”

Sasa, inazungumzia dhamira ya wananchi wa Zanzibar kujenga katika nchi yetu. Nchi yetu ni ipi? Ni Zanzibar. Hilo ni moja limo katika utangulizi.

Lakini vile vile katika kifungu cha 9 katika Katiba ya Zanzibar, katika sura ya pili inayozungumzia malengo na maamuru muhimu ya sera ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kinasema wazi wazi: “Zanzibar itakuwa ni nchi ya kidemokrasia na haki za kijamii.”

Kwa hiyo, ninachosema, Katiba iko wazi. Tatizo ni ile dhana ya kikoloni ya utawala, iliyojengeka miongoni mwa baadhi ya watu, hasa watawala upande wa Tanganyika, kwamba hii Katiba ya Zanzibar kwao si chochote si lolote na ati kwamba Katiba ya Muungano ndiyo inapaswa kuwa juu ya Katiba ya Zanzibar.

Kama ni suala la kuzipima katiba zote mbili, tuzipime kwa kupitia Mapatano ya Muungano. Na Mapatano ya Muungano, ambayo ninayo nakala yake hapa, hakuna pahala popote yanaposema kwamba, kwanza, yamefuta nchi za Tanganyika na Zanzibar, hakuna pahala popote yanaposema kwamba yamefuta utaifa.

Yanachosema ni kwamba: “Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika zimeunganishwa kuwa Jamhuri moja.” Na jamhuri kwa Kiingereza ni republic. Kuwa na jamhuri moja hakuna maana ya kufuta nchi, wala hakuna maana ya kufuta utaifa wa watu.

Swali: Tuangalie upande mwingine sasa, Zanzibar ni nchi au si nchi?

Jussa: Zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa ni nchi na itabakia kuwa ni nchi hadi mwisho wa dunia hii.

Swali: Na nilisikia kwa upande wenu, Chama cha Wananchi, CUF, muliunga mkono kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ni kweli Zanzibar si nchi kutokana na mapungufu ya Katiba, ambayo yameonekana. Imekuwaje tena mnakubali kwamba ni nchi?

Jussa: Hapana. Chama cha CUF kimeweka wazi wazi msimamo wake kupitia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano alipozungumza Hamad Rashid, ambaye ni mmoja kati ya watu waliyemtaka Waziri Mkuu Pinda atoe maelezo.

Akamwambia ikiwa kuna tafauti ya tafsiri, suala hili kwa nini lisipelekwe katika Mahakama Maalum ya Katiba ambayo imewekwa kutanzua tofauti kama hizi.

Lakini zaidi, juzi tu pale Mtoni, tulifanya mkutano mkubwa wa hadhara na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Juma Duni Haji, alisema wazi wazi kwamba Zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa nchi.

Na nasema, hili si suala ambalo tunapaswa kubishania kisiasa. Hili ni suala linalohusu maslahi ya Zanzibar na watu wake, kama nchi, kama taifa. Ni suala ambalo tunapaswa kuweka pembeni tofauti zetu za kiitikadi, tofauti zetu za kisiasa, na sote kwa pamoja kusimama kwa dhati kusimamia haki hii. Siku tukiipoteza haki hii ya kuwa Zanzibar ni nchi, siku tukikubaliana na malengo haya ya wanasiasa wa upande wa pili wa bahari, ambao wana dhamira ya kuvifuta kabisa visiwa hivi, basi tujue sote tutakuwa tumezama.

Mwalimu Nyerere, mwaka 1959, katika kitabu maarufu kilichoandikwa na William Edger Smith, ambacho kilikuwa kinamuelezea siasa zake katika mahojiano yake, alisema kwamba: “Ningekuwa na uwezo, ningevikokota visiwa vya Zanzibar nikavitupa mbali katika Bahari ya Hindi.” Dhamira hii haikutimia, maana uwezo huo aliokuwa nao ni Mwenyezi Mungu, lakini inaonekana wenzetu baada ya kukosa nguvu na uwezo wa kuvitupa visiwa hivi katikati ya Bahari ya Hindi, basi wameona angalau labda wavifute katika ramani ya dunia kwa kusema kwamba hivi si nchi.

Kwa hiyo, nasema hili ni suala zito. Bahati mbaya kuna watu wanasema kwamba watu wasiingize jazba. Huwezi kukwepa kuingiza hamasa katika suala hili, kwa sababu masuala ya utambulisho wa nchi, masuala ya utaifa, ndio kipimo kikuu cha uzalendo wa nchi.

Nchi zimeingia katika mapambano kulinda utaifa wake na hadhi yake. Kwa hiyo, nasema ni masuala ambayo watu wanapaswa wawe makini sana katika kauli zao, kwa sababu ni kauli zinazoweza kuchochea hasira za wananchi wa Zanzibar na hata kupelekea kuhatarisha Muungao huu, kwa sababu wananchi wa Zanzibar wakifika pahala – kama tulivyoona katika statements (kauli) zilizotolewa katika Baraza la Wawakilishi na hata katika gazeti la serikali la Zanzibar Leo – ukifikisha pahala, wananchi wa Zanzibar wakaona pana hatari ya kupoteza nchi yao, wanaweza kusema basi Muungano huu uwe basi. Hatukuungana ili tupoteze hadhi yetu ya kama nchi na taifa katika jamii ya kimataifa.

Swali: Na hebu tupate tafsiri sahihi ya kuwa Zanzibar ni nchi. Kuna vigezo gani, maana wengine tumekuwa tukisikiliza mawazo tu ya watu. Hatujui kwa nini Zanzibar ni nchi? Ili nchi iitwe nchi ama taifa, kuna vitu gani ndani yake, kuna vigezo gani?

Jussa: Mwanzo pale nilizungumzia kwamba kuna dhana hizi tatu: kuna nchi, kuna taifa na kuna dola. Na yote haya yana tafsiri zake katika sheria. Nchi ni eneo ambalo mipaka yake inafahamika, kwa Kiingereza wangeliita geographical area, ambayo ina wananchi wanaofahamika, population, na ina serikali ambayo inafanya kazi, yaani yenye madaraka – tunazungumzia hapa a functioning government. Hiyo ndiyo nchi.

Taifa, wala si dhana kubwa ya kisiasa kwa hakika. Taifa au nation, wanazungumzia uwe na eneo lenye mipaka inayotambulika, lenye watu wanaofahamika, na ambao wana utamaduni na historia inayowaunganisha. Dola ni ile ile ya mwanzo ya nchi. Inatakiwa iwe na eneo la mipaka inayofahamika, iwe na wananchi wake wanaofahamika, iwe na serikali inayofanya kazi na – na hili muhimu sana – la nne, iwe na uwezo wa kuingia katika mahusiano na nchi nyingine za kigeni.

Sasa Zanzibar si dola kwa sababu imepoteza hili la mwisho. Kwa hiyo, tunaweza kuzungumza, tukatofautiana, lakini pengine watakaosema kwamba Zanzibar si dola, wanaweza kuwa na hoja kubwa hapa. Lakini kusema kwamba Zanzibar si nchi, si taifa, si sahihi; kwa sababu kama ni taifa, Zanzibar ina eneo lake linalofahamika, Zanzibar ina watu wake, ambao ni Wazanzibari, wanafahamika, na watu hao Wazanzibari wana-share, au wana kitu kinachowaunganisha, ambacho ni historia na utamaduni wao.

Na Zanzibar ni nchi, kwa sababu mbali ya kuwa na mipaka na mbali ya kuwa na watu wanaofahamika, ambao ni Wazanzibari, lakini pia ina serikali inayofanya kazi. Kwa hiyo, tunasema kuwa hakuna mjadala kwamba Zanzibar ni nchi ama si taifa. Na pengine, ingefaa tukawauliza wale wanaosema kwamba Zanzibar si nchi: Eneo lolote ambalo lina namna fulani ya utawala lazima ulipe jina. Sasa kama Zanzibar si nchi katika Jamhuri ya Muungano, je, Zanzibar ni mkoa, Zanzibar ni wilaya, Zanzibar ni kitongoji, Zanzibar ni shehia? Watuambie sisi wanaotuambia hii si nchi, ni nini hii Zanzibar?

Swali: Mipaka ya Zanzibar, au mipaka ya visiwa hivi na Tanzania Bara, ni ipi?

Jussa: Katika hili, kama nilivyosema, turudi katika Katiba. Mimi kwangu, kwa sababu ni Mzanzibari na tunazungumzia nafasi ya Zanzibar, kwangu mimi Katiba ya msingi zaidi ni Katiba ya Zanzibar.

Ibara ya 2, kifungu kidogo cha 1 inasema: “Eneo la Zanzibar ni eneo lote la visiwa vyote vya Unguja na Pemba na visiwa vidogo vidogo vilivyovizunguka na bahari yake, ambayo kabla ya Muungano ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.”

Kwa hiyo, Katiba ya Zanzibar imefafanua wazi wazi eneo la ardhi na hata mipaka ya bahari, territorial waters. Imefafanua wazi wazi nini mipaka ya Zanzibar. Na bahati mbaya katika hili, kwa mara nyingine, Katiba ya Jamhuri ya Muungano – kwa dhamira ile ile niliyosema, makusudio ambayo yamepangwa kwa muda mrefu – inajaribu kupotosha.

Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Kifungu cha 2, kifungu kidogo cha 1, inasema: “Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania imepakana nayo.” Hili ni kosa.

Jamhuri ya Muungano ni Muungano wa nchi mbili. Ilipasa iseme hapa kwamba eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanganyika ambayo kabla ya Muungano ikiitwa Jamhuri ya Tanganyika na eneo lote la Zanzibar ambayo kabla ya Muungano ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kwa sababu msingi wa Muungano wetu huu ni kuunganishwa hizi jamhuri mbili. Huwezi ukataka kuifuta historia hiyo.

Sasa, tatizo la hawa wenzetu upande wa pili, kama nilivyosema, kila wakati wanajaribu kuifuta historia hii, kwa sababu lengo ni hatimaye kuwa na serikali moja. Na hili si siri.

Mwaka 1993 wakati wa mjadala mzito wa kundi la G55, au wabunge 55 waliokuwa wakidai Serikali ya Tanganyika, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wakati ule na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mzee Ali Hassan Mwinyi, alisema wazi wazi kwamba lengo la Muungano wetu ni serikali mbili kuelekea serikali moja. Katibu Mkuu wa CCM wakati fulani, Phillip Mangula, alisema wazi wazi kwamba sera ya CCM ni serikali mbili kuelekea moja. Mtu ambaye ndiye aliyeubuni Muungano huu na ambaye ndiye hasa aliyekuwa akiujua madhumuni na malengo yake, Julius Nyerere, katika kitabu chake cha mashairi kiitwacho Tanzania Tanzania, alikemea wazi wazi watu wanaodai serikali tatu, akisema ni kurudi nyuma. Alisema lengo ni serikali mbili kuelekea moja.

Kama mnakumbuka Gibons Mwaikambo alipokuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, alikuja kuhutubia mkutano mmoja wa CCM pale Kisonge, akasema hivyo hivyo kwamba lengo la Muungano huu ni serikali mbili kuelekea moja.

Sasa nasema wenzetu wanajua nini wanachokitafuta, nini wanachokitaka. Kwa hiyo, mara zote malengo yao, matamshi yao, nyaraka zao na hata huu utaratibu wa kuandika Katiba, umefanywa kidogo kidogo kuondosha kila siku yale mambo yanayoashiria kwamba hii ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili na kutuelekeza kwa nguvu kwamba hii ni nchi moja.

Suala la mipaka Katiba ya Muungano ndiyo yenye makosa. Haikuweka tafsiri safi ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano kwamba inatokana na maeneo ya nchi mbili hizi: iliyokuwa Jamhuri ya Tangayika na iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Lakini, tofauti na Katiba ya Muungano, Katiba ya Zanzibar inaeleza kwa usahihi kabisa, kwa lugha safi kabisa, kwamba eneo la Zanzibar ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba na visiwa vidogo vidogo vilivyovizunguka na bahari yake.

Katika mkoa huwezi kutafsiri neno bahari, hapa panazungumzwa nchi ndiyo maana panazungumzwa territorial waters, ambayo kabla ya Muungano ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Kwa hiyo, hii ndiyo mipaka ya Zanzibar.

Swali: Ukisema bahari yake hapo tunazungumzia maeneo gani ukiacha ndani ya Visiwa hivi? Kwa sababu tunaona bahari imepita maeneo mengi, kwa hiyo tunataka tujue hapa upi sahihi mpaka wa kibahari, ama vipimo gani vinatumika hapa kupima huu mpaka wa kibahari na kipimo gani ambacho ni sahihi?

Jussa: Kama nilivyosema, kwa mwananchi wa kawaida anaweza asielewe, lakini haya ni mambo ya kisheria na yote yamewekwa na taratibu za kisheria zinazoongoza mahusiano ya kimataifa na mahusiano ya nchi na nchi. Zote zimekubaliana kupitia international law, sheria ya kimataifa, nini mipaka ya bahari ya nchi.

Nchi yoyote ambayo inapakana na bahari, eneo lake linakuwa ni maili 20 kutoka nchi kavu. Hizo wanazoita nacotic miles, si hata hizi maili za kawaida. Kwa hiyo, inafahamika kabisa kwa sababu hata kabla ya Muungano, Zanzibar ilikuwa na mipaka yake.

Kwa hiyo, kuna eneo la bahari, ambalo linakuwa ni mamlaka au ni sehemu ya nchi ambayo imepakana na bahari ile, ambazo ni hizo maili 20, lakini zaidi ya hapo ni ile ambayo tunaiita international sea, bahari ya kimataifa. Hii haina mwenyewe, ni ambayo jamii yote ya binadamu ulimwenguni ina haki ya kuitumia. Na ni eneo hili la bahari, kwa mfano, ambalo tunapaswa kulinda haki zetu.

Hata kama ni bahati mbaya tumeiacha nchi yetu kama haina mwenyewe, hawezi mtu kuingia katika eneo hili la bahari bila ya ruhusa ya wenye nchi. Hawezi tu mtu kuja akavua katika eneo hili, kama kuna rasilimali ni mali yetu tunayomiliki katika eneo hili la bahari.

Kwa hiyo, ndiyo kusema kwamba kama tuna mafuta leo Zanzibar, na mafuta hayo kwa mfano, yako kwenye eneo la bahari la ndani ya maili hizo 20, basi hiyo itakuwa ni mali, ni rasilimali, ni utajiri wa wananchi wa Zanzibar.

Swali: Sasa baada ya kuona mapungufu haya katika katiba hizi mbili – Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Katiba ya Zanzibar – kuna makosa ambayo lazima yarekebishwe haraka iwezekanavyo. Mamlaka ya Zanzibar katika maamuzi yake muhimu yako wapi?

Jussa: Mamlaka ya Zanzibar ni chombo cha kutunga sheria cha Zanzibar, ambacho ni Baraza la Wawakilishi. Ni bahati mbaya sana kwamba hatukitumii chombo hiki inavyopaswa. Na kwa Zanzibar, ambako kuna mitafaruku mikubwa ya kisiasa baina ya kambi mbili zinazovutana, ni bahati njema kwamba chombo pekee ambacho kinatukutanisha sote – hakuna taasisi Zanzibar yoyote ya kiutawala, ya kisiasa inayowakutanisha CCM na CUF, inayozikutanisha pande mbili zinazovutana – isipokuwa Baraza la Wawakilishi.

Kwa hiyo, chombo kikuu cha maamuzi, cha kisiasa, cha kiutawala, na cha kisheria kwa upande wa Zanzibar ni Baraza la Wawakilishi. Inasikitisha sana–majuzi tulizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mtoni pale – kwamba tulitarajia kwamba Serikali ya Zanzibar ingeweka tofauti hizi upande, na sasa hivi ingepeleka katika Baraza la Wawakilishi – na bado hatujachelewa – ingepeleka hoja inayotaka kuwa na azimio la Baraza la Wawakilishi: kwanza mjadala mpana si kuhusu suala la hoja ya Pinda tu kwamba Zanzibar ni nchi, kwa sababu tunasema kwamba haya ni matokeo tu.

Msingi wake ni katiba ambazo zimeachwa kuwa na mapungufu, hasa kwa upande wa Jamhuri ya Muungano.

Kwa hiyo, nadhani imefika wakati, ili kuondoa dharau, inda, jeuri, kebehi, umefika wakati Baraza la Wawakilishi lifanye mjadala wa wazi kuhusu hatima ya Zanzibar katika Muungano huu, halafu kutoa azimio linalowakilisha sauti ya Wazanzibari, ambalo ndilo litakalotumika kwenda kuzungumza na upande wa pili wa Muungano kupata muungano wa kweli, muungano wa dhati, unaozingatia haki sawa na fursa sawa baina ya nchi mbili hizi zilizoungana.

Kwa hiyo, Zanzibar inacho chombo chake ambacho ni Baraza la Wawakilishi. Tukitumie kama kweli tuna nia ya dhati ya kuibakisha nchi hii kwa faida ya vizazi vyetu vinavyokuja.

Swali: Turudi kwenye Mambo ya Muungano sasa. Haya Mambo ya Muungano ambayo tunayasikia sikia tu wengine, hatuyajui, pengine tunataka kuelekezwa zaidi. Yalikuwa mangapi?

Jussa: Mambo ya Muungano kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano ni 11 na yameorodheshwa katika Mkataba wa Muungano wenyewe. Haya ni Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, la pili Mambo ya Nje, la tatu Ulinzi, la nne Polisi, la tano Uwezo wa Kutangaza Hali ya Hatari, la sita Uraia, la saba Uhamiaji, la nane ni Biashara ya Nje na Mikopo, la tisa ni Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, la kumi ni Kodi ya Mapato, kodi ya Biashara, Mambo ya Ushuru wa Forodha na la mwisho ni Bandari, Usafiri wa Anga, Posta na Simu.

Swali: Na hivi sasa yako mangapi?

Jussa: Sasa hivi yameongezwa na yamefikia, kwa mujibu wa orodha na ukisoma kwa nambari, ni 22. Lakini ukiyachambua – kwa sababu kama nilivyosoma hapo umeona, kuna kifungu kimoja kinasema ni Bandari, Usafiri wa Anga, Posta na Simu – haya ni mambo manne, lakini yamewekwa kwamba ni kifungu kimoja.

Sasa yamewekwa 22, lakini kwa hakika ukiyachambua, basi unaweza ukafikia mambo 40. Na nasema, hili ni vizuri umeliuliza kwa sababu, kama nilivyosema Muungano huu – na pengine tutarudi pale pale kwenye mjadala wetu kwamba Zanzibar ni nchi au si nchi – Muungano huu haukuziunganisha serikali hizi mbili kwa mambo yote. Kwa hiyo, haukufuta nchi hizi mbili, haukufuta serikali za nchi hizi mbili. Muungano huu ni kwa mambo maalum yaliyokubaliwa, ambayo ni hayo 11 ambayo nimeyasoma.

Ndiyo kusema, hata Serikali ya Jamhuri ya Muungano mamlaka yake juu ya Tanganyika na juu ya Zanzibar ni kwa mambo hayo tu 11 yaliyokubaliwa katika Mkataba wa Muungano. Na yaliyobakia yote, ukiangalia mkataba huo huo wa Muungano, kifungu cha 3, kifungu kidogo cha A, kinasema vizuri kabisa, kwamba mambo yatakayozingatiwa ni pamoja na kuwepo, kwa Kiingereza wanasema, a separate legislature and executive in and for Zanzibar from time to time constituted in accordance with existing laws of Zanzibar and having – na hapa ndio muhimu – and having exclusive authority within Zanzibar for matters other than those reserved to the parliament and executive of the Republic.

Yaani kuwa na serikali ya Zanzibar na Baraza lake la kutunga sheria, ambapo vyombo hivi viwili vitakuwapo kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar na vitakuwa na mamlaka kamili ndani ya Zanzibar kwa mambo yote yasiyo mambo ya Muungano.

Kwa hivyo, hata suala la sovereignty tunayoita, yaani udola, basi Zanzibar ina mamlaka yake kamili kwa mambo yote yasiyokuwa Mambo ya Muungano. Lakini tumefikaje hapa? Kama nilivyosema, tangu mwanzo, dhamira ya wenzetu wa upande wa pili, Tanganyika, ni hatimaye kuleta serikali moja kuifuta Zanzibar.

Kwa sababu ukisoma dhamira ya CCM, mwaka 1983, wakati wa mjadala ambao hatimaye ulipelekea Wazanzibar kuondoshewa Rais wao wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe, ambaye walimchagua wenyewe Zanzibar, bila kushauriwa akaondoshwa Dodoma, katika wakati ule ulipoletwa waraka ule, ambao ulikuwa unawaongoza wananchi katika mabadiliko ya katiba.

Ilisemwa mule kwamba: Kuimarisha Muungano maana yake ni kuyaangalia mambo yote yasiyo ya Muungano na kuona vipi yanaweza kufanywa mambo ya Muungano na yakifanywa mambo ya Muungano yataimarisha Muungano.

Maana yake kwa tafsiri ya wenzetu, au kwa tafsiri ya CCM, kuimarisha Muungano ni kuchukua kila siku madaraka ya Zanzibar na kuyahamishia katika Serikali ya Muungano. Hii haiwezi kuwa tafsiri sahihi. Hii haiwezi kuwa nia njema katika nchi mbili zilizoungana.

Kuimarisha Muungano kungekuwa kuna dhamira njema, kungekuwa pia kujumuishe kupitia yale Mambo ya Muungano, ambayo utekelezaji wake umeleta matatizo, kwa hivyo bora yaondoshwe katika Mambo ya Muungano yarejeshwe katika Mamlaka zinazohusika.

Lakini waraka wa mwongozo wa CCM wa mwaka 1983 haukusema hivyo. Waraka wao, na imekuwa ndio sera yao siku zote, ni jinsi gani kila siku kuondosha mambo ya Zanzibar kuyahamishia Dodoma. Na hili ndilo tatizo ambalo tunalipata hivi sasa.

Yameongezeka mambo haya kuwa 22 kutoka 11 ya asili, ambayo kama nilivyosema ukiyachambua moja moja yanafika 40. Na tukilala Wazanzibari, hatimaye tutakuwa si nchi, tutaondoshewa mamlaka yetu. Tutakuwa hatuna tofauti na Kisarawe au pengine Ukerewe.

Swali: Nikwite mwanasheria labda. Tuangalie, haya marekebisho ambayo yamefanywa na ambayo tumeona yako mengi, kama ulivyosema, na kwa jinsi yalivyojigawa katika makundi tofauti, yameathiri chochote mpaka hivi sasa?

Jussa: Bila shaka.

Swali: Yameathiri nini?

Jussa: Nasema kwa hakika. Unajua kuna watu wanaojaribu labda kuyaona haya labda ni mambo ya kisiasa tu. Hapana. Siasa ni njia ya kufikia maendeleo ya watu. Unapoleta mambo yanayoathiri utawala na siasa katika nchi, unaathiri maendeleo ya watu.

Swali: Yameathiri nini?

Jussa: Leo katika Zanzibar, uchumi wetu ni mbovu. Mbali ya matatizo yetu ya ndani – sikatai kwamba yote yamesababishwa na Muungano. Yako matatizo yetu ya ndani wenyewe: Serikali isiyojali wananchi, Serikali ambayo ina watu wake hawazingatii uwezo na vipaji vya watu – yako haya mambo yamechangia – na wizi, rushwa unaofanyika Zanzibar.

Lakini kwa kiasi kikubwa, uchumi wa Zanzibar umedorora, umefikia hapa ulipo, ni kwa sababu ya jinsi Muungano huu unavyoendeshwa.

Kwa sababu gani nasema hivyo? Kwa sababu utakuta katika kuchukua madaraka haya, kila siku kuongeza mambo ya Muungano, mambo mengi ambayo yangeipa Zanzibar uhuru wake wa kujiamulia sera zake za kujiendeleza kiuchumi na kimaendeleo na kijamii yamehamishwa hapa.

Sasa, wajibu wa kuiletea maendelea Zanzibar na watu wake ni wajibu wa Serikali ya Zanzibar. Masuala ya maendeleo si mambo ya Muungano, na ndiyo maana tuna wizara zetu hapa zinazoshughulika na elimu, afya, serikali za mitaa, ardhi, ujenzi, mawasiliano na uchukuzi. Lakini zile sera za kuamua mambo ya kodi, mambo ya uchumi, zote zimehamishiwa upande wa Bara.

Ndiyo utakuta matokeo yake Serikali ya Zanzibar inajikuta haina madaraka. Wakati fulani tulikuwa na dhamira ya kutangaza bandari huru, kwa sababu Zanzibar ni Visiwa; uchumi wake unategemea biashara. Tukanyimwa madaraka hayo. Zanzibar ilikuwa inategemea biashara ya mpito hapa, masuala ya madaraka yote yanayohusu uwekaji wa kodi na ushuru yakaondolewa.

Masuala ya leseni za viwanda, masuala ya utafiti, masuala ya elimu ya juu – masuala ambayo yangelikuwa ndiyo nyenzo ya Zanzibar kuweza kujitungia sera zitakazoweza kuinua maisha ya watu, ambalo ni jukumu lake kwa upande wa serikali ya Zanzibar – yamehamishwa.

Kwa hiyo, nasema, mambo haya kwa kweli yametuathiri sana Zanzibar na kama nilivyosema wakati umefika Wazanzibari waamke, waungane pamoja bila kujali tofauti zao za kiitikadi ili kwa pamoja kuitetea Zanzibar na kutetea haki zetu ndani ya Muungano huu.

Swali: Nafasi yenu kama upinzani, CUF, kiko wapi sasa katika kunusuru hili, katika kuwaunganisha, katika kuyaibua ama kuyaweka sawa, au kuyarekebisha hayo yote ambayo tunaona sasa muda unavyokwenda mbele yanazidi kuibuka?

Jussa: Sisi wajibu wetu mkubwa ni kusema, kwa sababu sisi hatuna hatamu za utawala. Lakini tumetumia vyombo hivi viwili: wabunge wetu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiongozwa na kiongozi wetu, Hamad Rashid Mohammed, na hata wajumbe wetu wa Baraza la Wawakilishi wamesimama kidete kutaka suala hili lisimalizwe hivi hivi.

Na Hamad Rashid amemwambia hata Waziri Mkuu kwamba, ikiwa kuna tofauti ya tafsiri kwamba Zanzibar ni nchi au si nchi, kwa hivyo maana yake ni tafsiri ya Katiba kwenye sheria zetu, basi pahala pa kupatiwa ufumbuzi wa suala hili ni katika Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ambayo imewekwa kwa mujibu wa Kifungu cha 125 cha Katiba ya Muungano. Kwamba ametaka suala hili liwekwe.

Lakini Waziri Mkuu anasema kwamba anawataka wanasheria wawili wakuu wakae. Hakuna pahala popote katika Katiba zetu panapowapa wanasheria wakuu wawili mamlaka, kwamba watakutana kuamua hatima ya nchi zetu. Ni Mahakama Maalum ya Katiba itakayoundwa na pande hizi mbili ndiyo itakayoamua.

Tumesema majuzi katika mkutano wa Mtoni na hata kuwaalika Wazanzibari wote kuja katika uwanja wa Kibandamaiti. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amelichambua suala hili na kuweka msimamo wa CUF wazi na vile vile kuzungumza kwa niaba ya Wazanzibari wote: wawe CCM, wawe CUF, wawe hawana chama, kuzungumza kwa niaba yao wote, nini unapaswa kuwa msimamo na mwelekeo wa Wazanzibari katika kulikabili suala hili.

Swali: Unazungumziaje, kwa ufupi tu, hili suala la kuondolewa Rais wa Zanzibar katika nafasi ya Makamu wa Rais?

Jussa: Kama ulivyoniuliza kwamba tumeathirika vipi. Moja katika ubabe wa hali ya juu uliofanyika katika kuburuza Zanzibar na kuufanya Muungano huu utazame misingi ya upande mmoja tu, ni kumuondolea Rais wa Zanzibar nafasi yake ya kuwa moja kwa moja mmoja kati ya makamu wawili wa Rais katika Jamhuri ya Muungano.

Suala hili ni matakwa ya Mkataba wa Muungano katika kifungu cha 3, kifungu kidogo cha B, kinachosema kutakuwa na makamu wawili wa rais na mmojawapo atakuwa ni Rais wa Zanzibar au kiongozi wa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sasa imetuathiri vipi? Kama tulivyosema, pale tulipokuwa tukichambua kuhusu nchi, taifa na dola, dola ni nchi yenye uwezo wa kuingia mahusiano ya nchi za nje.

Sasa Zanzibar imepoteza kwa sababu katika Mambo ya Muungano ni pamoja kukabidhi masuala ya mambo ya nje katika Jamhuri ya Muungano. Lakini pamoja na kupoteza lile, kwa sababu tuna serikali yetu ndani na ambayo ina madaraka yote isipokuwa kwa mambo ya Muungano, na bado tutahitajika kujitafutia misaada na ushirikiano na wenzetu, kwa hiyo Rais wa Zanzibar, kwa kutumia nafasi yake ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, alikuwa ana uwezo wa kutumia fursa zile za Mambo ya Muungano, ikiwamo masuala ya mahusiano ya kimataifa, ikiwamo masuala ya mambo ya nje anapokwenda nje kutambulika kimataifa na akatumia nafasi ile kutafuta mambo yanayogusa maslahi ya Zanzibar.

Kuikosa nafasi ile, Zanzibar imekosa utambulisho, Rais wa Zanzibar amekuwa hatambuliki. Leo amefika hadi Rais wa Zanzibar kuambiwa ni mjumbe tu wa Baraza la Mawaziri katika Serikali ya Muungano. Ni kumdhalilisha kwa mwisho kabisa. Na ndiyo tumeona, karibuni Amani Karume, alipokwenda Marekani, anapokewa na meya.

Hapa ndipo nafasi ya Rais wa Zanzibar kuondoshewa u-Makamu wa Rais ilipotufikisha. Mtu ambaye alipasa kupokewa kama si na Makamo wa Rais mwenzake au pengine Waziri wa hadhi ya juu katika nchi, leo anapokelewa na meya wa mji, kwamba yeye ndiye sawa sawa yake.

Haya ndiyo matokeo ya kuyadharau Makubaliano ya Muungano na kuyapondaponda. Tunaweza kuimarisha Muungano huu ikiwa tu tutarudi katika Mapatano ya Muungano, tukaheshimu dhamira na malengo yaliyokuwamo mule kama yalivyowekwa na waasisi, Mzee Abeid Karume na Julius Nyerere.

Source: Raia Mwema



 
Zanzibar
Zanzibar was declared a British Protectorate in 1890 as part of the European 'scramble for Africa'. The British politically and economically favoured the Arab minority (the second largest ruling minority in Africa after South Africa's whites) placing the Sultan and his Arab government in power at independence.
Thirty-three days later the Zanzibar Revolution occurred. This brought to power the Afro-Shirazi Party (ASP) led by Sheikh Abeid Amani Karume. In the pre-independence elections the ASP had won 54.21 per cent of the popular vote. But, as a result of constitutional gerrymandering by the British and Arabs, it won only 13 of the 31 elected seats.
The union between Tanganyika and Zanzibar followed three-and-a-half months later on 26 April 1964 with the unified sovereign states now known as Tanzania.'Under the articles of union both countries retained a degree of sovereignty with their own Presidents, goverments and responsibility for specified domestic affairs. Other areas such as foreign affairs, defense and security became union subjects. Nyerere was elected as President of Tanzania, Karume the First Vice-President and Kawawa the Second Vice-President. In February 1977, TANU and the ASP merged to form the Chama Cha Mapinduzi (Revolutionary Party) with Nyerere as its chairman.
 
Suluhu ya namna gani wanataka wakati mpaka leo bado wabara hawaruhusu ata kuendesha biashara uko visiwani? Kwa lugha fupi huu ni UBAGUZI!!!!

D.12 Short-term domestic travel is not restricted, and there are no entry controls whatsoever for Zanzibar-born Tanzanians onto the mainland. Zanzibaris may travel to live and work freely on the mainland, subject to the same laws that apply to mainlanders, and there is no requirement for mainlanders to show identification to travel to Zanzibar. Mainlanders are allowed to work in the islands but not allowed to own land there. Zanzibaris own property, work and run businesses on the mainland. The "Kazi Nguvu" laws, which date back to the colonial period, and the Human Resources Development Act 1983 were intended to prevent migration to the cities from agricultural areas, and to support the 'Ujamaa' (community) policies of Nyerere to resist urbanisation. They stipulate that persons who are unemployed must return to their home region. These laws are however practically never used, with the exception of removing professional beggars from city streets. Tanzanian citizens can return to Tanzania without difficulty.

Babu uongo huu umeuopowa wapi na kweli unauamini? Labda nikuulize ni mara ngapi umeshafika huko Zanzibar?
 
Salma Said, Zanzibar
KAULI ya Mtaalamu kutoka Scotland, David Reading, kwamba kuna uwezekano mdogo wa kupata mafuta na gesi asilia katika visiwa vya Unguja na Pemba imewakera mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na kumta aifute.

Lakini mtaalamu huyo alisisitiza kwamba yeye akiwa mshauri ni lazima awaeleze ukweli wa mambo, kwani hata makampuni yaliofanya utafiti siku za nyuma kuhusu mafuta walitoa ripoti ambayo haikueleza uhakika wa kuwepo kwa nishati hiyo.

Reading pia alisema kuwa gharama za utafutaji wa mafuta hayo ambayo hayana uhakika ni kubwa mno.

Mtaalamu huyo alikuwa akizungumza katika semina ya siku moja kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyofanyika jana mjini Ugunja.

Reading alisema katika sehemu nyingi zilizogunduliwa mafuta au kuwepo kwa fununu za kuwapo kwa nishati hiyo, gharama yake ilikuwa ni kubwa ambapo ililazimu makampuni kusitisha kazi kwa sababu hiyo.

Matamshi hayo yalionekana kuwachukiza zaidi wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambapo walimtaka mtaalamu huyo kufuta matamshi yake kwa maelezo kuwa tafiti nyingi zilizofanywa katika miaka ya mwanzoni mwa 1950 zilionesha kuwa yapo mafuta ya kutosha ya kibiashara Zanzibar.

Hoja hiyo iliibua hisia za wajumbe hao za siku nyingi na waalipopata nafasi ya kuchangia, walisema kuwa mafuta ya Zanzibar ni kwa Wazanzibari na kamwe yasifanywe kuwa ya Muungano na kusisitiza msimamo wa kutaka kuondolewa kwa sheria inayoelezea kuwa mafuta na gesi asilia kuwamo katika orodha ya mambo ya Muungano.

Wajumbe hao walisema kuwa huenda suala hilo la mafuta linaweza kusababisha machafuko visiwani, kwani uozefu unaonyesha kwamba nchi nyingi zenye mafuta kuzuka mapigano, hivyo wakashauri suala hilo lisiwe chanzo cha machafuko kwa Wazanzibari.

Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan, alionekana kushangazwa na taarifa za Mshauri Mwelekezi na kuhoji: "Kama uwezekano wa kupatikana mafuta Zanzibar ni mdogo kwa nini serikali ya Muungano ilikataa wazo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwenye kamati ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi katika kugawana mapato ya mafuta?"

Hata hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, aliwataka wananchi kuipuuza kauli hiyo ya Mshauri Mwelekezi na kuongeza kuwa ikiwa mafuta hayataondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano hatajutia kuona Muungano unayumba.

"Kuna msemo wa kihindi…ipasuke ngoma au ichanike lakini tujue moja kuwa mafuta ya Zanzibar ni kwa Wazanzibari na sio ya Muungano," alisisitiza waziri huyo.

Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari kama walivyo wajumbe wengine waliochangia alisema mafuta yasiwe mambo ya Muungano kwani hata kuingizwa kwake haukufuatwa utaratibu unaofaa.

Mwakilishi wa Jimbo la Gando, Said Ali Mbarouk alisema kwamba Wazanzibari wamezoea kukosa, hivyo haitokuwa jambo la kushangaza ikiwa hakutakuwa na mafuta wakati jambo hilo litakapoondolewa katika orodha ya Muungano, kwani hivi sasa hainufaiki na lolote katika suala la gesi asilia.

Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha akifungua semina hiyo aliwasihi wajumbe hao kutumia busara katika kumpa ushauri mtaalamu huyo ili aweze kupata maoni mwafaka na aweze kuzishauri serikali mbili namna bora ya kugawana mapato yatokanayo na utafutaji na ushimbaji wa mafuta.

Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Ali Mzee Ali alisema Wazanzibari wanapochangia kwa ajili ya kutetea nchi yao wasionekane kama ni wasaliti au wana nia ya kugombea urais bali wanatelekeza ahadi yao kwa wananchi ya kuwatetea katika baraza hilo.

Akifunga semina hiyo Waziri wa Maji, Ujenzi Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid aliungana na wajumbe wengine wote kwa kutaka kuwa mafuta yaondolewe katika orodha ya Muungano kwani tokea asili hayakuwa hivyo.
======================================================

My take;
Mimi nadhani zanzibar ikikosa mafuta kero za muungano na mambo ya kudai nchi yataisha.


Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom