Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mimi nadhani ni vizuri waendelee kuambiwa kuwa kuna mafuta ili hatimaye waamue kuvunja muungano halafu miaka michache tunaanza kuchimba ya kule Mkuranga!
 
Mwenzenu kuna siku nilitaka kupigwa na rafiki mmoja mwenye asili ya Pemba. Yeye alikuwa anadai Zanzibar ( specifically) Pemba kuna mafuta mie nam-bishia na kumwambia nijuavyo kuna "potential" ya mafuta akaja na hoja hizo hizo za tafiti za miaka 1950 still hizo sites kuzifungua kakuta neno "potential" lakini wapi hatimae almunusra tushikane mashati.

Back to the article kweli siasa SI_HASA sasa baina ya hao "wawakilishi" na Mr Raeding sijui nani ni mtaalam.

Kazi kweli kweli
 
Swali la kujiuliza ni kwa nini Baraza la Wawakilishi linamhoji huyo mshauri Reading wakati linajua habari za mafuta zaidi yake au ndiyo usanii wa kizenj?
 
wapumbavu hawa wanapenda kuambiwa uwongo ndiyo wafurahi. Mtaalamu kasema uwezekano wa kuwepo mafuta ni mdogo lakini hamkubali sasa mlimwita mtaalamu wa nini kama majibu ya maswali yenu mlikuwa nayo?
 
Mzee Mwanakijiji umenikuna! Hawa Wazanzibari wanaota ndoto za mchana za utajiri, sasa wameipata. Ooh Mafuta ya Zanzibar ni ya Zanzibar; mara Ooh zama za kutishana zimeisha, Ooh mafuta ya Zanzibar hayaendi bara mpaka dhahabu ya Mwanza igawiwe Zanzibar! Hawa wala tende wana matatizo kweli kweli! Wanasema hayo huku bara tukilipia starehe zao zote kwa fedha itokanayo na pamba, mpunga, chai n.k. Zama za kuwabeba Wazanzibari zimekwisha - tuwaachie Zanzibar yao ndogo kama wilaya ya Pangani lakini yenye Rais, Waziri Kiongozi, Naibu WK, mawaziri na manaibu wao 40, wakurugenzi na makatibu wakuu zaidi ya 100, viongozi wa siasa zaidi ya 5,000! Kisiwa cha viongozi! Kalagha bhao!
 
wapumbavu hawa wanapenda kuambiwa uwongo ndiyo wafurahi. Mtaalamu kasema uwezekano wa kuwepo mafuta ni mdogo lakini hamkubali sasa mlimwita mtaalamu wa nini kama majibu ya maswali yenu mlikuwa nayo?

Huyu Bwana Reading angewaambia kuwa Zanzibar mafuta ni mengi sana kuliko nchi yoyote duniani, halafu awaombe wampe contract ya kutathmini gharama za uchimbaji wake. najua kuwa hiyo contact ingepita bila kupingwa na kwa gharama yoyote ile. Sasa baada ya kuwala hela, ndipo angekuja awaambie kuwa mafuta ya Zanzibar yako chini ya mwamba mgumu kuliko yote duniani, na hivyo uchimbaji wake utachukua takribani miaka sabini usiku na mchana kabla ya kuyafikia. Full stop.
 
Hii imekaa kifisadi zaidi...
 
Nafikiri hapa kwa hali ya sasa tatizo lilopo ni wanasiasa wa bara (Tanzania Bara) kwani utaona kabisa wazanzibar including Karume hawataki muungano, sasa kwa nini tunawang'ang'ania? mtu hataki kuishi na wewe tatizo ni nini? kama mafuta wanayo si basi na sisi tutaendelea kuishi bila shida. Vikao vikubwa vya chama hawa jamaa wanatishia kuvunja muungano, kule Butiama swala la muafaka kati ya CCM-Zanzibar na Cuf, Karume kaongea kwa jaziba mpaka analia anamwambia coton man (Muungwana) kama anataka muafaka basi yeye anarudi Zanzibar na nchi yake. Sasa kweli hapo kuna muungano? na wajumbe wote wa Zanzibar wakawa wanafoka kama nguruwe kapigwa mkuki. It's time tufanye referendum Zanzibar, kama wanataka kuwa nasi au lah
 
Huyu Bwana Reading angewaambia kuwa Zanzibar mafuta ni mengi sana kuliko nchi yoyote duniani, halafu awaombe wampe contract ya kutathmini gharama za uchimbaji wake. najua kuwa hiyo contact ingepita bila kupingwa na kwa gharama yoyote ile. Sasa baada ya kuwala hela, ndipo angekuja awaambie kuwa mafuta ya Zanzibar yako chini ya mwamba mgumu kuliko yote duniani, na hivyo uchimbaji wake utachukua takribani miaka sabini usiku na mchana kabla ya kuyafikia. Full stop.

Could'nt put better than this.....
 
Mimi binafsi siwalaumu wazanzibar angalu wameamka kupigania wanalohisi kuwa ni haki zao wakati sisi huku Tanganyika tumekuwa tunasukumwa kama vile mikokoteni na ndio pale jirani zetu wakenya wakasema kuwa waTZ wote akili sao ni zakawaida akiwa waziri profesa msukuma mkokoteni wote zinalingana na hili nikweli kwanini basi ni ile siasa ya ujamaa imetufanya tuwe hivi tukumbuke kuwa kuna wakati Mwalimu aliwahi kusema hataki Tanganyika pawe na TV kwa sababu watu wataiga mambo ya maharibi aliyekuwa Rais wa zanzibar Akasema yeye ataweka zanzibar na alifanya hivyo Tanganyika bado sisi tumekuwa na mjivuno mengi hivi na vile na ndio mpaka sasabado tupo malimbukeni wa maisha hilo hatutaki kulikubali lakini ndiohali halisi
 
Enzi zile nchi yetu ikiwa na viongozi wenye vision!

Immediately ingetafutwa kampuni la wazungu na waarabu lingine... lije lidhibitishe kwamba Zanzibar sorry Pemba hakuna mafuta... maana hawa lazima uwahakikishie tena kwa kudhibitishwa na watu wengi kwamba hiyo kitu ilikuwa hadithi tamu za wakati huo.

You know what?

Muafaka ungepatikana haraka sana... maana kiburi cha wapemba na chokochoko zao pia ni hiyo hadithi kwamba kuna mafuta Pemba.

Wakati wananchi wa Comoro wanatamani wangekuwa sehemu ya Jamhuri ya Tanzania, wenzetu wao wanatamani kuwa na Jamhuri yao.

Mungu ibariki Tanzania
 
Masikini Reading!
Namuonea huruma sana mtaalamu huyu, kwamba anabishana na watu wasio na utaalamu wa mafuta, bali siasa. Alikuwa hajui kwamba anabishana na watu ambao lengo lao ni kuwakomoa watu wa bara kwa kumiliki na kupigia kelele 'mafuta hewa' ambayo kwayo, wanataka kuuvunja muungano.
Nakumbuka vema jinsi Shamsi Vuai Nahodha na Ali Juma Shamhuna walivyowachamba wabara, kwamba mafuta ya visiwani ni kwa ajili ya watu wa visiwani na wala wasiingiliwe kabisa.
Kumbe 'mafuta' yenyewe ndio hayo anayojaribu kuwaelewesha mtaalamu Reading, nampa pole sana mtaalamu huyu.
Sasa hawa ndugu zetu wa visiwani wanataka mgao wa dhahabu na gesi asilia, hivi pesa hizi haziingii katika hazina ya serikali kuu na kugawanywa katika wizara mbali mbali kwa maendeleo?
Naomba kueleweshwa!
 
Nilipojiunga elimu ya Upili pale Dabanga Camp (kwa wanaoijua) miaka ya 1980 mwishoni nilipokelewa na SWALI hili
" Kuna utumwa na utumwa; kuna utumwa wa mwili na utumwa wa akili: Kuna utumwa wa kutumwa na utumwa wa kujituma. Mradi kuna utumwa na utumwa. Jadili.

Swali hilo sikuwahi kulielewa hadi yalipoanza mambo haya mara UFISADI mara ZENJ ni nchi mara;mara; mara.
Ila yote ni ubatili na kujilisha upepo kwa wazenj; wanachokitaka wakiseme na kukitekeleza upesi
 
wapumbavu hawa wanapenda kuambiwa uwongo ndiyo wafurahi. Mtaalamu kasema uwezekano wa kuwepo mafuta ni mdogo lakini hamkubali sasa mlimwita mtaalamu wa nini kama majibu ya maswali yenu mlikuwa nayo?
Nafikiri aliye mpumbavu ni wewe. La msingi ni kuwa kwa nini nyinyi wa Bara mshikilie hili la mafuta tu. Kama kweli ni watu mnaojali haki na usawa.-Na ujadiliwe Muungano sasa na kurekebisha mapungufu yote (tena mengi tu yaliyopo) Siyo kugawana mafuta tu. Tafadhali Bwana msiwafanye Wazanzibari ni mazuzu sikuzote. Hao waliotoa maoni ni Wawakilishi waliochaguliwa na Wazanzibari majimboni mwao. Hayo ni maoni ya Wazanzibari. Kama unayabeza, nafikiri ni wewe wa kubezwa na kuambiwa zuzu. Fahantum?
 
Mkuu Pakacha punguza munkari.
Kubishana na mtaalam hakuonyeshi ukomavu wa hao wawakilishi. Unless wangekuja na ripoti ya kitaalam kupinga utafiti wa bwana reading. Hakuna mbara anayeshikilia la mafuta tu, suala la mafuta limekuwa ni kete ya wazanizbrai, ndilo wanalolitumia kila siku. Ukisoma bandiko la mwanzo kabisa utaona wawakilishi wameonyesha mawazo yao kuhusu suala la mafuta.
Kujadiliwa Muungano! Mbona hilo linafanyika, tatizo baadhi wanaujadili kwa jazba kwa kupenyeza mambo mengine yasiyokuwepo ili kukwepesha hoja kuu-kama wanavyotaka kulifanya suala la mafuta lionekane kuwa nalo ni tatizo.
 
Wengi wao hapa wanabishana kama nani zaidi, bara au visiwani

Mmeshindwa kujadili kitu cha msingi.

Siku nyingi sisi wabara tunasema Zanzibar inatubebesha mzigo mkubwa kwenye muungano, lakini hapo hapo kama hata ni wazo la mzanzibari mmoja akisema hatuutaki muungano basi habari kwenye magazeti itakua kwa herufi kubwa.

Mtikila amesema mara ngapi?

Huwa najiuliza kuna nini huko visiwani mpaka tukung'ang'ania hivi? Nchi yetu Tanganyika ina kila kitu lakini tukisikia tu visiwani wana uwezo wa kuwa na kitu hiki basi hata kulala macho hatulali.

Tumekua kama watoto wadogo ambao tumepewa kila aina ya toys lakini kesho tukimuona mtoto mwingine ana toy moja tu ambayo hatuna tutawalilia wazazi ili tununuliwe.
 
Back
Top Bottom