hiki kitabu niliwahi kukisoma zamani lakini naona kwangu sasa hakifunguki sijui tatizo ni nini lakini ni moja ya kitabu ambacho kina majibu mengi ya hili tunalolizungumza na wakati huo huo kuibua mijadala mingi.
nnategemea tutajitahidi kwa sote kuutafuta ukweli juu ya yote yaliojiri
http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html
UKWELI NI HUU (KUUSUTA UWONGO)
Aman Thani Fairooz
Dibaji
Kitabu Hichi
Ukweli Ni Huu (Kuusuta Uwongo)
Utukufu Na Neema Ya Zanzibar
Zanzibar Na Ubaguzi Kabla Ya Mavamizi
Ubaguzi Umeanzishwa Zanzibar Wakati Wa Serikali Yenye Kujiita Ya "Mapinduzi"
Elimu Na Matibabu Bure!
Taalimu
Matibabu
Hali Za Maisha
Neema Zilikuwepo
Kuanza Harakati Za Siasa
Sheikh Ali Muhsin Kwenda Nchi Za Ulaya Ikiwemo Na Uingereza Kupigania Uchaguzi Wa "Common Roll" (Mtu Mmoja Kura Moja).
Kuasisiwa Hizbul-Wattan (Zanzibar Nationalist Party)
Wakoloni Dhidi Ya Hizbu, Uhuru Na Umoja Wa Zanzibar
Makao Makuu Ya Hizbu
Hizbu Kumleta Zanzibar Seyyid Abdul-Rahman (Babu)
Natija Ya Safari Ya Sheikh Ali Muhsin
Wakoloni Na Nyerere Ndio Waasisi Wa Afro-Shirazi
Uchaguzi Wa Mwanzo Juni 1957
Kwanini Sheikh Ali Muhsin Aliamua Kusimama N'gambo Badala Ya Majumba Ya Mawe?
Kwenye Shari Huzaliwa Kheri
Kukuwa Kwa Harakati Za Siasa
Ati Husemwa Kuwa Hizbu Imefeli!
Kugawanyika Kwa Afro-Shirazi
Kuasisiwa Kwa Zanzibar And Pemba Peoples' Party (ZPPP)
Tume Ya Sir Hillary Blood
Uchaguzi Wa Pili, Januari 1961
Uchaguzi Wa Tatu Juni 1961
Ushirikiano Wa ZNP/ZPPP
Kutokufaulu Mazungumzo Ya Mwanzo Ya Katiba Ya Uhuru
Afro-Shirazi Iliandaa Machafuko Siku Ya Uchaguzi
Muungano Wa ZNP/ZPPP, Waunda Serikali
Kutokufaulu Mazungumzo Ya Mwanzo Ya Katiba Ya Uhuru
Babu Kutoka Katika Hizbu
Dhamiri Za Babu
Kufungwa Gerezani Kwa Seyyid Abdul-Rahman Babu
Kutolewa Gerezani Babu
Babu Na Fisadi Yake Ya Mwisho
Kipi Kilicho Mpelekea Babu Kuchukua Khatua Kama Hizo
Uchaguzi Wa Julai 1963
Nyerere Anasema Wakoloni Walipendelea Kuiacha Serikali Ya Zanzibar Mikononi Mwa Hizbu
Mkutano Wa Katiba Ya Uhuru.
Uhuru Wa Zanzibar
Sherehe Za Uhuru
Yaitwayo "Mapinduzi"
Kuuliwa Kwa Muhsin, Suleiman Na Ahmed
Kifo Cha Ali Mzee Mbalia
"Skolashipu" Za Misri
Yaliyo Nifika Nafsi Yangu Na Hayo Yenye Kuitwa "Mapinduzi"
Maafa Ya Gerezani
Kufungwa Kifungo Cha Miaka 10 Gerezani
Kiasi Cha Kazi Alichokuwa Akifanyishwa Mfungwa
Maovu Waliyotendewa "Wafungwa Wa Kisiasa"
Kutolewa Gerezani
Nakimbilia Dar-Es-Salaam
Mahabusi Wadhulumiwa Wa Mwalimu Nyerere
Mateso Ya "Kwa Ba Mkwe"
Maisha Ya Gereza Langoni
Nyakati Za Kufanyishwa Kazi "Wafungwa Wa Sisasa"
Ufungwa Wa Karume Ni Zaidi Ya Utumwa
Kurejeshewa Uhuru Wetu
Kuuliwa Wananchi Msikitini
Kuuliwa Kwa Wananchi Wengine
Namna Walivyo Uliwa
Wafungwa Waliyokufa Gerezani
(1) Mzee Mohammed Mbaba
(2) Maalim Harun Ustadh
(3) Idi Hassan
(4) Ramadhan Ibrahim Saadalla
Wameuliwa Vifungoni
Wafungwa Wengine Wauliwa
"Wafungwa Wa Siasa" Bado Waendelea Kuuliwa
Aliyonizungumziya Twala
Yalomfika Othman Shariff
Kuteswa Na Kuuliwa Othman Shariff
Kufungwa Na Kuuliwa Saleh Saadalla
Karume Kuanza Kumbadilikia Twala
Mwisho Wa Twala
Makomred Wamechangia Maafa Yaliopo Nchini
Kwanini Mwalimu Nyerere Alikataa Kuwapeleka Zanzibar Watuhumiwa Wa Kesi Ya Ukhaini?
Siri Hii Ni Kubwa Sana!!
Serikali Ya Mavamizi Ya Zanzibar Bado Imo Na Ubaguzi Wake
Nilitakiwa Nitoke Nchini
Namna Nilivyoondoka Kuukimbia Wattani Wangu
Kuleta Ahli Zangu Dubai
Mengineyo Kwa Ufupi
Mwalimu Na Uislamu
Mwalimu Na Utumwa
Porojo La Mitaani
Demokrasi Ya Vyama Vingi (Multi-Party Democracy)
Vipi Kuifikilia Demokrasi
Shukrani
DIBAJI
Namshukuru Mwenye Enzi Mungu Mwenye Wingi wa Rehema Kubwa na Ndogo kuniwezesha kuandika kijitabu hiki ambacho nimejaribu kiasi nilichoweza kuyaeleza yale yaliyotokea katika Nchi yetu, Zanzibar. Na yaliyonitokelea mimi mwenyewe na yaliyowatokelea Wananchi wenzangu kutokana na hayo yenye kuitwa, "Mapinduzi" yaliyofanyika katika Visiwa vyetu mnamo taarikh 12 Januari, 1964. Haya ninayoyaandika ni kiasi ya hayo niyajuayo mimi tu; hapana shaka yapo mengi ambayo sikupata kuyajuwa. Bali nataraji watatokea wenzangu nao, wakayaeleza waliyotendewa au waliyoyaona yakitendwa.
Nafanya haya si kwa makusudio yoyote mengine zaidi ya kutaka kueleza ukweli wa yaliyotendeka katika Nchi yetu ili Wananchi wenzangu (na ndugu zetu wa Tanganyika, bali na ulimwengu, pia) na khasa wale waliokuwa wadogo, na wale ambao hawajaja duniani wakati huo waweze kuyafahamu japo kwa uchache yaliyotendeka katika Nchi yao kwa hayo yenyekuitwa "Mapinduzi". Ikiwa katika kuyaelezea haya, kutahitajia kumtaja mtu au watu kwa njia yoyote, itakuwa nafanya hivyo kwa kutokana na maudhui ninayo izungumza wala si kwa ajili ya kusengenya au kukejeli au kudharau au kwa kutia illa za namna fulani, hashaa! Bali kwa vile dhamiri ya kukiandika kijitabu hiki ni kuelezea ukweli wa mambo yalivyokuwa, basi sitochelea kulieleza lolote madhali kwa kufanya hivyo ndio itakuwa natimiliza lengo nililolikusudia, nalo ni kuueleza ukweli. Kutokana na hayo, nachukuwa nafsi yangu mas-uliya yote yatayotokea katika maandishi haya.
Muhimu, nawaomba wasomaji wangu wajishughulishe zaidi na hayo niliyokusudia kuyaeleza, kwani hayo hayana shaka yoyote, ni kweli tupu. Na nawaomba wasijishughulishe na makosa madogo madogo, kama vile ya upigaji chapa, makosa ya lugha au juu ya utaratibu wa uwandishi.
Ikiwa litatokea suala lolote, au ikiwa lolote halitafahamika, basi wakurejelewa ni mimi. Inshallah, nitajaribu kama nitavyoweza kutanzua kila lililotanzika na ikiwa nitashindwa, basi sitoona taabu kutaka msamaha. Mwenye kukamilika kwa yote ni Mwenye Enzi Mungu.
Tunamuomba Mwenye Enzi Mungu ajaaliye haya tunayoyaeleza yapate kusomwa, kuzingatiwa na kufahamika na ipatikane faida ndani yake kwa kutumiwa kwa kheri. Kubwa ya kheri hizo ni kusahihisha palipo haribika, kuiondosha haramu, kuomba toba na kutenda mema, kwani mema huondowa mabaya. Mwenye Enzi Mungu atupe taufiq, Amin.
Aman Thani Fairooz
P.O. Box 10836
Telephone 04-850802
Dubai United Arab Emirates
Januari, 1995
KITABU HICHI
Kidogo-basi, Chungu-tamu.
Kwa hakika Kitabu hichi ni kidogo basi. Lakini, kama alivyosema muandishi kuwa kaandika kwa ufupi, bali ufupi wa kutosheleza faida yake. Yoyote atakaye kisoma kitabu hichi kwa kutaka kufahamu na bila ya mawazo yake kudhibitiwa na kupenda au kuchukiya, basi hapana shaka atapata faida. Atafahamu jinsi wananchi wa Zanzibar walivyokuwa katika harakati zao za kuwania uhuru wa nchi yao kutokana na ukoloni wa Muingereza. Harakati ambazo zalianza kabla ya miaka ya 1940. Pia ataweza kufahamu ni nani walioanzisha harakati hizo, namna zilivyopata kuungwa mkono na wananchi na namna zilivyokuwa zikiendeleya. Pia atapata kufahamu jinsi ya pingamizi zilivyokuwa. Atafahamu pingamizi hizo zilivyoanzia, nani aliyezianzisha na kuzipalilia na kuzikuza.
Atafahamu natija yake! Pia atafahamu vipi wananchi chini ya uwongozi wa vyama vyao ZNP/ZPPP walivyokuwa wakizikabili pingamizi hizo. Na zaidi atafahamu juhudi za waongozi wa ZNP/ZPPP katika kutaka mafahamiano na ushirikiano na wananchi wenziao - ASP - na nini ulikuwa muelekeo wa waongozi wa ASP, muelekeo ambao mara nyingi ulikuwa ukiathirika kwa uwongozi na fikra zilizokuwa zikipangwa na kuletwa kutoka nje ya nchi. Chungu-tamu. Kweli ni chungu! Lakini ni wajibu isemwe na kubainishwa. Uchungu uliyomo ndani ya kitabu hichi ni kuona jinsi wananchi walivyohangaika kwa jasho, mali na hata damu zao kwa kuwania uhuru wao kutokana na ukoloni wa Muingereza, lakini kwa sababu ya husda, chuki na ufisadi uhuru huo haukuachiwa kuishi zaidi ya siku thalathini! Isitoshe, sio kuwa uhuru huo ulipotezwa kwa kutumiliwa njiya za usalama, sivyo, bali kwa fujo! Fujo ambalo natija yake ni kupotezwa Dola ya Zanzibar, roho za wananchi, heshima ya binaadamu, mali za watu na mwisho kuwachwa wananchi kuishi ndani ya haramu.
Utamu - japo kwa hakika sio utamu - ni kwa vile kuweza wananchi kupata kuufahamu UKWELI ambao kwa muda wa zaidi ya miaka thalathini umekuwa ukifunikwa kwa UWONGO. Lakini, kama yalivyo maumbile, kweli daima huibuka.
Tunamshukuru Mwenye Enzi Mungu kwa kudhihiri kitabu hichi na kuweza kuufahamisha umma, bali na ulimwengu, maafa yaliofikishiwa Zanzibar, Nchi na Wananchi.
Msomaji, na pengine hata asimuliwaye haya, huenda akasema, yaaleiti yalielezwa haya kiasi cha miaka ishirini liyopita, au kabla ya hapo. Hivyo ni kweli! Lakini kila kitu kwa majaaliwa, na kuchelewa kwengine kuna kheri zake kama kwengine kunavyo shari zake. Kheri katika kuchelewa kudhihiri kitabu hichi ni kuwa vijana waliokuwa wadogo wakati wa maafa ya Zanzibar leo ni watu wazima, wenye uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda. Kwa hivyo wanahitajia kuujuwa Ukweli.
Wao si kwa ajili ya Kuusuta Uwongo, hashaa!! Bali ni kwa ajili ya kuujuwa ukweli, kisha iwe ni mafunzo kutokana na yaliotendeka. Watasoma, na Inshallah watayafahamu na kuyatumia. Na haya ndio khasa makusudio na faida ya kitabu hichi. Kutumia kwao huko kwanza iwe ni kwa kuepusha yasitendeke tena maafa yaliyotendwa, kufuatilia hilo - au yote mawili sambamba - ni kwa kufanyakazi katika kujenga palipo bomolewa. Kubomowa daima ni rahisi kuliko kujenga, kujenga kunataka umoja na ushirikano wa kila mmoja wetu. Kwa hivyo ni waajibu wa kila mmoja wetu kushirikiana, bega kwa bega, kwa nia na nguvu moja kufanyakazi kuirejesha Zanzibar. Kwanza, kuirejesha katika ramani ya ulimwengu ili iwe na jina na pahala pake kuwa ni Dola kaamili na iliyo huru. Kisha, bali ndio la muhimu, kuirejesha katika neema zake.
Hichi ni kitabu cha kusomwa na kila Mzanzibari, bali na ndugu zetu wa Tanganyika, pia.
Abdulla Ali (Baba)
UKWELI NI HUU (KUUSUTA UWONGO)
Nimelichagua jina hili la UKWELI NI HUU KUUSUTA UWONGO, baada ya kuyasikia na kuyasoma me ngi ya uwongo na hata yakafika kusomeshwa watoto wetu katika maskuli ya Zanzibar kukhusu hayo yenye kuitwa "MAPINDUZI" yaliyofanyika katika visiwa vyetu vya Zanzibar mnamo taarikh 12 Januari 1964.
Kabla ya kuingia katika hayo, ningependa ku-waambia wasomaji wangu wote kuwa mimi si mjuzi hata kidogo wa fani hii ya uandishi; tena ni mbovu sana katika "spellings" na ka-tika "nahau" za Kiswahili cha kisasa. Pia nawaomba radhi kwa Kiswahili changu cha kizamani
Bali, kutokana na huo uzushi na kupotezwa kwa makusudi ukweli wa hayo yaliofanyika kukhusu hayo yenye kuitwa "mapinduzi" nimeo-na sina budi illa ni kujitolea hivyo hivyo juu ya upungufu wangu katika fani hii ya uandishi. Lakini ukweli lazima niudhihirishe ili vichipukizi vyetu viweze kuyaelewa vilivyo yaliyotendeka katika nchi yao. Kwani wengi walikuwa wadogo na wengine walikuwa hata hawajazaliwa katika wakati huo.
Ilivyokuwa Kiswahili ni lugha yangu ya kuzaliwa, basi ninaiandika kama ni-navyoisema. Si shughuliki na "kua au kuwa, aliniambia au aliniambiya, ameuawa au ameuw-awa kenda au kaenda, amekwenda au ameenda". Hayo kwa wataalamu wa lugha ni mambo muhimu lakini kwa mimi nakutakeni msamaha juu ya hayo. Muhimu ya kuyaangaliya na kuyazingatiya ni yale nikusudiayo kuyaeleza, kwani hayo ndio muhimu na ndio ya kweli tupu isi-yokuwa na dosari hata chembe.
La mwanzo nitakalo kuombeni mlifahamu uzuri ni ile hakika ku-wa hayo yaliyofanyika katika visiwa vyetu taarikh 12 Januari 1964, hayakuwa "MAPINDUZI" wala hayafai hata kidogo kuitwa 'mapinduzi' kwa maana asili ya neno. Bali kwa maana zote yalikuwa khasa ni "MAVAMIZI", yaani kwa Kiingereza - "INVASION".
Mapinduzi lazima yapangwe, yaongozwe na yatekelezwe na wananchi wenyewe kwa maslaha ya nchi na wananchi wake. Sasa tukiangalia hayo yaliotendeka Zanzibar, yali-pangwa, yaliongozwa na yalitekelezwa na WAGENI kutoka nchi za nje za jirani zetu. (Ni wao wala si wananchi ndio waliochukua ngawira kubwa kubwa).
Haya yanathibitika zaidi kwa vile kuwa huyo jamadari aliyeyaongoza hayo 'mavamizi' ni John Okello na wa chini yake waliku-wa Injini na Mfaranyaki. Nani kati ya hao aliyeku-wa kitovu chake kimezikwa visiwani? Okello amezaliwa na amekulia kwao Uganda, Injini amezaliwa na amekuliya kwao Kenya na Mfaranyaki amezaliwa na amekuliya kwao Tanganyika. Wote hao walikuja Zanzibar wakiwa watu wazima na shughuli zao, wamekuja kutafuta kibarua na kukimbia kodi za kichwa katika nchi zao.
Liangalie hilo waliloliita "Baraza la Mapinduzi". Utaona sehemu kubwa ya wanachama wa Baraza hilo walikuwa si Wazanzibari, laa kwa kuzaliwa wala kwa kuchukua Tajnisi (Kuandikisha Uraia). John Okello, Khamis Darweshi, Seif Bakari, Said Natepe, Said Washoto, Muhammed Mfaume, Edington Kisasi, Mohammed Abdalla Kaujore. Ukiwaacha wengineo ambao nao vile vile walikuwa si wananchi wa Zanzibar kwa kuzaliwa, bali wao walikuja Zanzibar wakiwa katika migongo ya wazee wao na waliendelea kuishi humo visiwani kwa maisha yao yote. Na wakachukuliwa kama ni Wazanzibari.