Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Jembajemba,

Very interesting ulivyoweza kuiweka historia ya Hizbu kwani nina hakika umeitoa kama vile mwandishi mfuasi wa Hizbu!.,... badala ya kuzungumzia zaidi ukweli ambao hauchukui pande moja. Nina hakika ukiulizwa kusema jinsi ASP ilivyoanzishwa lazima utaanza kuponda na kusingizia watu wa kuja badala ya kuwa kubali hawa ASP kama ni chama cha Wazanzibar walioungana.
Labda hufahamu ya kwamba ni Arab Association kilichotanguliza madai yote uliyoyaweka hapo juu na huyu Ali Muhsin Barwani alikuwa mwanachama wa chama hiki. Na sii kweli Hizbu ndio walidai non racial election isipokuwa huyu mjomba Ali Muhsin Barwan na Abraham Babu, tena basi tunavyozungumza hapa huyu Muhsin Yuko zake Oman ni raia na anaishi hukooo!.

JembaJemba,
Historia ya Zanzibar imepotoshwa sana na watu kwa sababu ya uhasama wa hizi tabaka za Rangi ambazo zilikuwepo toka enzi na kukorezwa na Muingereza. Wakati huo kulikuwepo na chama cha weusi (African Association), washiraz na Shiraz Association na hata wahindi na chama chao cha Muslim Association kabla kabisa ya kuwepo Hizbu ama ASP. Trust me, kila mmoja wa vyama hivi anaweza kudai kwamba chama chao kilisimamia maslahi ya Wazanzibar wote! Lakini Uadui ulikuwepo kati ya wanasiasa wa pande zote kiasi kwamba inategemea wewe ulikuwa upande gani. Kisha basi kumbuka ya kwamba Nuingereza alikuwa hawezi kutoa Uhuru wa nchi nzima kwa vikundi vya watu na ndio maana wasomi hao waliotangulia walijua kwamba hakuna ujanja isipokuwa kudai haki za Wazanzibar wote. Hata Bara huku Bara na Africa nzima mchezo ulikuwa ni huohuo ni lazima chama kiwakilishe taifa zima ili kiweze kupewa Uhuru wa nchi hiyo.
Sasa basi pamoja na yote hayo unaweza kunambiakifo cha Arab Association?.. mbona chama hiki hakionekani tena ktk historia ya zanzibar baada ya kuzindsuliwa ZNP.

Umeuliza pia, kama kweli Hizbu kilikuwa chama cha waarabu basi wasingeshinda uchaguzi wa 'one on one' mwaka 1957!...Mjomba sii kweli hata kidogo kwani ASP ndio walishinda kwa viti 5 kati ya 6 , tena basi hicho cha 6 kilichukuliwa na Muslim Association. ZNP hawakupata hata kiti kimoja kati ya majimbo hayo.
Karume alimshinda Ali Muhsin kwa kura 3,328 dhidi ya kura 918 lakini Muhsin alikuja pewa Uwaziri pamoja na kwamba chama chake cha ZNP kilishindwa.
Umeulizia pia upatikanaji wa hizi kura 918 kama ni dalili ya kuonyesha Hizbu hakikuwa chama cha waarabu!.. mjomba vipi yaani unataka kusema upigaji kura huwa unaendeshwa kwa population ya watu? Ama ni watu wangapi waliosajiri kupiga kura!... Je wewe unaamini kabisa kuwa kama Hizbu kingekuwa ni chama cha waarabu basi kisingeweza pata hata kura 900 kwa sababu ya population yao!... you must be kidding.

Sikiliza ndugu yangu ni kwamba hivi vyama viwili ZNP na ASP walikuwa na uhasama toka zamani na haya maswala ya rangi unayojaribu kuyatumia hapa ni propaganda za kisiasa ambazo tumezizoea. Wanachama wa ZNP wakikuwa hadi koo za hao Ma - Sultan kama vile chama cha Ian Smith na walijaribu kwa kila hila kukivunja chama cha ASP vile vile. Hata kuondoka kwa Sheikh Mohammed Shamte, Sheikh Ameir Tajo na Sheikh Ali Shariff Mussa ASP ilikuwa ni njama za kukivunja chama hicho. Hawa waliitwa wasaliti kama vile Abraham Babu alivyochukiwa na ZNP kwa kuondoka chama hicho.
Ebu nikuulize tena kama kweli ZNP kilikuwa chama kinachopigania Umoja na Muungano wa Wa - Zanzibar wote imekuwaje ktk uchaguzi wa kwanza kabisa wamekosa hata kiti kimoja!...
 
Mkandara kama historia ya HIZBU niliyokupa ilikuwa ya upande mmoja tupe hiyo yako ya pande zote mbili.

Sasa ulitaka nikupe jina la Mtu mweusi aliyemuoa mwanamke wa kiarabu kweli ungeliamini? wakati hiyo historia niliyokupa huiyamini - Mkandara kuwa mkweli

Halafu unasema Muhsin yupo Oman anaishi huachi wewe? mbona huyu Mtu kesha jifia (Mungu amrehemu) unaonekana haupo updated na hayo maelezo yako unayoyatoa yamebase upande mmoja tu (ASP) na yamejaa uongo.
 
JembaJemba,
Kama Muhsin amesha kufa hilo jingine lakini alikuwa akiishi Oman na ni raia wa Oman hii naifahamu vizuri sana hukuna haja ya kubishana unless wewe unafahamu alipokuwa akiishi hapo Unguja ama Pemba kabla ya kifo chake, naomba data hizo. Kwa kurahisisha habari hii nambie hayo niliyoandika hapo ju ni UONGO! na ukweli ni upi kwani nimedondoa kila sehemu niliyoiona umepotosha.

Pili, Nimesema hii historia ya Hizbu ni ya Upande mmoja nikwa na maana zote nilizoandika hapo juu. Kwanza waliotaka Uhuru wa Zanzibar ni Arab Association ambao ndio walio initialize non - racial election kwa sababu nchi yoyote iliyotawaliwa haiwezi kupata Uhuru wake kwa kuwakilisha kundi la watu. Muhsin na Arab Association ndio shina la historia ya Hizbu hata kama kulikuwepo watu wengine waliotunga shanga.

Mbona sisi Bara tunakubali kuwa shina la TAA,TANU na leo hii CCM ni waislaam wakazi wa Dar akina Abdul Wahid?..Kuna ubaya gani kusema kwamba chimbuko la siasa Tanzania Bara limeanzishwa na waislaam ati kwa sababu tu kulikuwepo akina Nyerere ambao historia ya leo ndiyo imewatambua zaidi.
Tofauti ya Hizbu, TANU walimleta Nyerere kuongoza chama hicho kwa mtihani ule ule mliokuwa nao Visiwani ya kwamba chama ni lazima kiwakilishe nchi nzima na sio kundi la watu. Sasa mbinu zote zilizotumika kuwaingiza wakristu ili kupata kura za wananchi haiwezi kufuta historia ya kwamba TAA kilikuwa chama kilichotakana na waislaam kutafuta Uhuru wa Bara.
Maelezo uliyonipa hapo juu sio historia bali majina ya watu kuonyesha kwamba chama hicho hakikuanzishwa na waarabu kama vile naweza mimi kukupa majina ya waasisi wa TANU kuficha historia ya wauislaam na TAA.
Kuna mengi nimejaribu kuyapinga hapo juu na kama kweli wewe waijua historia ya Hizbu nambie ni wapi pasipo kuwa na Ukweli. Mshikaji mimi nafahamu siasa za Zanzibar toka wakati ule hadi leo hii, ni siasa zilizojaa chuki kama ilivyo kati ya CCM na CUF. Nitakuwa najidanganya kabisa kama nitaamini kuna ushirikiano mkubwa kati ya CCM na CUF ama kuweka lawama zangu upande mmoja. Jaribuni sana kuondoa chuki zenu kwa maslahi ya Zanzibar kwanza na kukataa kwenu kuwa Hizbu haikutokana na Arab Association ni uongo mkubwa!
Haiwezekani kabisa chama kama ASP kishinde uchaguzi kwa viti 10 kisha baada ya uchaguzi vyama viungane kuunda jumla ya viti vyao kuwa 13, kuondoa ushindi wa mtu kisha ukategemea hicho chama kitaachia Utawala kirahisi. Huyo Shamte mwenyewe alikuwa muasi wa ASP na aliondoka kwa chuki ASP kwa hiyo kubebeshwa kwake kombe la Uongozi ilikuwa kuwatia ASP vidole vya macho!.Hii ndiyo fact na chuki iliyokuwepo Zanzibar kati ya vyama vya siasa.
Mjomba hiii ni Afrika yetu, tunafahamu majungu yetu wenyewe kwa mapana yake. Kamwe hatuwezi ku-solve kitu ikiwa sisi wenyewe tutakataa ukweli kwa sababu ya chuki na unazi wa chama. Maelezo yako yamejaa unazi wa ZNP ..I can tell that!
Siwapendi CCM hata kidogo kwa yote wanayoyafanya na nadhani umeniona kila sehemu nikisema ovyo kuhusu Watawala wetu. Sijamwacha mtu hata kidogo awe wa bara ama visiwani kama sikubaliani na mawazo yake ama Uongozi wake.
Na kama ungelijua kwamba chaguo langu la kiongozi alikuwa Salim A Salim nadhani usingeweza kuamini kwani mawazo yako ni kwamba nawachukia Wazanzibar ama Hizbu. That was history kwangu na ndio maana nataka kuamini kulikuwepo na mwanzo mpya Zanzibar!
As a fact kiongozi kama Shein ni mmoja kati ya watu ninao waheshimu..lakini nina hakika kubwa kwamba ni hesabu ndogo sana ya Wazanzibar ambao wanaweza kumtaja kiongozi wanayefikiria kuwa bora toka Bara!..
 
Ansbert Ngurumo wa Tanzania Daima said:
Wazanzibari wanajua historia yao. Walau tukianzia uchaguzi wa Juni 1957, utaona kwamba ASP kilifanyiwa dhuluma nyingi na watawala, kikawa kinashinda na kunyimwa madaraka. Juni 1957 kilishinda kwa asilimia 61.14 dhidi ya 21 za Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na asilimia 16.89 za Muslim Association (MA). Watawala wakasema ‘mtashinda nyie, tutatawala sisi.'

Kikavuta subira na kurejea ulingoni Januari 1961. Kikashinda tena; zamu hii kwa asilimia 43.19 dhidi ya asilimia 38.52 za ZNP na 18.29 za Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP).

Wakasema tena ‘shindeni nyie, tutatawala sisi.' Ukazuka mgogoro hadi kukalazimika kufanyika uchaguzi mwingine Juni 1961. ASP kikashinda tena kwa asilimia 49.39 kikiwa na viti 13 kati ya 23. ZNP kikapata asilimia 35.50 ya kura zote, na viti 10; ZPPP kikapata asilimia 13.89 ya kura zote, na viti 3. Bado ASP ikafanyiwa mizengwe na kushindwa kutawala kwa sababu ZNP iliungana na ZPPP kuunda serikali ya mseto ili kukinyima fursa ASP.

Hali hiyo ilijirudia Julai 1963 ambapo ASP kilishinda viti 13, dhidi ya 12 vya ZNP na sita (6) vya ZPPP, lakini kikanyimwa tena fursa ya kuunda serikali kwa ujanja ule ule. Ndipo kikagundua kwamba kwa staili hii ya kuingia kwenye uchaguzi, kushinda na kunyimwa fursa, kisingeweza kutawala kamwe.

Hiki ndicho kiini cha mapinduzi ya Zanzibar dhidi ya Sultani Jamshid ibn Abdullah.

Kipande hiki kinazidi kutufumbua macho kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Matangazo unalipia?

Noma hiyo

PIPO: DO NOT KLIK ON ZE LINKS PROVAIDED BY DHIS GUY 🙁
 
G. THOMAS BURGESS
Assistant Professor of History, US Naval Academy
gburgess@usna.edu

Education: Ph.D, History, Indiana University (IU), 2001
Dissertation: "Youth and the Revolution: Mobility and Discipline
in Zanzibar, 1950-1980"
M.A., African Studies, IU, 1992
B.A., History and English, Brigham Young University (BYU), 1990


Lectures:
September 2006 “The History of Youth in East Africa: A Retrospective,” British East Africa Institute Conference on Youth in East Africa, Nyeri, Kenya, July 2006

“Memory and Language in Postcolonial Zanzibar” St. Cross College, Oxford University, June 2006

“The Visual Power of African Nationalist Spectacles: Halaiki in Zanzibar,” School for Oriental and African Studies, University of London,June 2006

“The Revolution vs. People’s Power in Zanzibar,” United States Department of State, September 2005.

“Discipline in the African Nationalist Imagination,” Texas Southern University,April 2003.

“Culture, Connections, and the Longue Duree on the Swahili Coast,” Rice University, April 2003.

“Kujenga Taifa: Youth, Nation Building, and Discipline in Zanzibar,” Northwestern University, May 2002.

Selected Presentations:
“Youth Labor Camps in Revolutionary Zanzibar,” British East Africa Institute Conference on Youth in East Africa, Nyeri Kenya, July 2006.

“A Field of Dreams: Revolutionary Festivals in Zanzibar,” Annual Conference of the African Studies Association, November 2005.

“Mao in Zanzibar: The Construction of Knowledge in a Cosmopolitan Island Society,” Empires and Cultures Workshop, “Rethinking Afro-Asian Connections During the Twentieth Century,” Stanford University, May 2005.

“A Vanguard Generation: Ali Sultan Issa and the Paradise Imperative,” Annual Conference of the African Studies Association, November 2003.

“Imagined Generations: Constructing Youth in Revolutionary
Zanzibar,”
International Conference on Youth and Politics in Africa, University of Leiden, Netherlands, April 2003.

“Morality and Violence: Memory Narratives of the Zanzibari Revolution,” Annual Conference of the American Anthropological Association, November 2001.

“African Youth and the Colonial State,” Conference of the Historical Association of Tanzania, University of Dar es Salaam, Tanzania, June 2001.

“Bell Bottoms, Miniskirts, and Big Hair: Assaults on the Revolutionary Order in Tanzania,” Annual Conference of the African Studies Association, November 2000.


Books: Zanzibari Voices: Race, Revolution, and the Struggle for Human Rights in Tanzania, forthcoming, James Currey Press/Ohio University Press, 2007.

Youth and Citizenship in East Africa, Africa Today, 51, 3 (April 2005 guest-edited theme issue).World Societies since 1500, Tapestry Press, 2001.


Articles: “The Young Pioneers and the Rituals of Citizenship in Revolutionary Zanzibar,” Africa Today, 51, 3 (April 2005).

“Introduction: Youth and Citizenship in East Africa,” Africa Today, 51, 3 (April 2005).

“Cinema, Bell Bottoms, and Miniskirts: Struggles Over Youth
and Citizenship in Revolutionary Zanzibar,”
International Journal of African Historical Studies, 35, 2 (2002).

“Remembering Youth: Generation in Revolutionary Zanzibar," Africa Today, 46, 2 (1999).

Chapters: “Mobility and Discipline: Colonial Age Discourse in Tanzania,” in Rethinking Age in Africa: Colonial, Post-colonial and Contemporary Interpretations of Cultural Representations, ed. by Mario Aguilar, Trenton: Africa World Press,
2006.

“A Socialist Diaspora: Ali Sultan Issa, the Soviet Union, and the Zanzibari Revolution,” in Africa in Russia, Russia in Africa: 300 Years of Encounters, ed. by Maxim Matusevich. Trenton: Africa World Press, 2006. “

“An Imagined Generation: Umma Youth in Nationalist Zanzibar,” in In Search of a Nation: Histories of Authority and Dissidence From Tanzania: Essays in Honor of I.M. Kimambo, eds. Gregory Maddox, James Giblin, Y.Q. Lawi. London: James Currey Publishers, 2005.

“Imagined Generations: Constructing Youth in Revolutionary Zanzibar,” in Vanguards or Vandals: Youth, Politics and Conflict in Africa, ed. by Jon Abbink and Ineke van Kessel. Leiden: Brill Academic Publishers, 2004.


“Mao in Zanzibar: Discipline, Development, and African Nationalists’ Search for a Usable Future,” in Bandung and Beyond, ed. by Christopher Lee. Columbus: Ohio University Press, forthcoming.


Manuscripts “Islands of Discipline: Youth, Revolution, and Power in Zanzibar” In Preparation:A revision of my dissertation.
 
Ubaguzi wa rangi umerudi maradufu kule zanzibar na mbaya zaidi huuu ubaguzi ambao mzee KARUME aliukemea haufanyiwi lolote na hii inapelekea hata hali ya kiuchumi nayo unaiona. Unajua kuna wale wanzaibari weusi kama akina BI KIDUDE huwa wana ile ngoma yao MAARUFU NA KULE HUONI WALE RANGI RANGI au maarufu kama MACHOTARA ambao hujiona wao wako civilized zaidi

Tazama hata wale waliosafiri utaona ni wale rangi rangi mpaka mtu unajiuliza wale WEUSI WAKO WAPI?


sasa kurekebisha hii hali mnasemaje? irudishwe ile Amri ya kuwaoa kwa lazima hawa wanaojiita waarabu au mnasemaje?
 
Umetoka kwenye udini unaenda kwenye ukabila! na sasa umefikia hadi kwenye urangi.. mweh! mtu mbaguzi hajifichi.
 
Samvulachole,
Hebu tupe mifano zaidi! Maanake naona Wabunge Wawakilishi na Muungano wapo wengine weusi na weupe!
Sasa mtakuja sema warefu ndo wanapendelewa na wafupi wanabaguliwa na kunyimwa vyeo!
Na mimi mwembamba je na elimu yangu pia watanibagua wawachukue mwanene?
 
Haya mambo najua yalikuwepo lakini kama yamerudi tena basi nawatakia maisha mema.
 
Ubaguzi wa rangi umerudi maradufu kule zanzibar na mbaya zaidi huuu ubaguzi ambao mzee KARUME aliukemea haufanyiwi lolote na hii inapelekea hata hali ya kiuchumi nayo unaiona. Unajua kuna wale wanzaibari weusi kama akina BI KIDUDE huwa wana ile ngoma yao MAARUFU NA KULE HUONI WALE RANGI RANGI au maarufu kama MACHOTARA ambao hujiona wao wako civilized zaidi

Tazama hata wale waliosafiri utaona ni wale rangi rangi mpaka mtu unajiuliza wale WEUSI WAKO WAPI?


sasa kurekebisha hii hali mnasemaje? irudishwe ile Amri ya kuwaoa kwa lazima hawa wanaojiita waarabu au mnasemaje?
tutalirekebisha ukilithibitisha, kwasasa hujathibitisha kitu,umeporoja tu, ni sawa na kusema dar-es-alam wamewabagua mikoani kwa kuwa dar kuna majumba marefu mikoani hakuna.nakubali zanzibar upo ubaguzi ,lakini sio huo uliouzungumza wewe na wala hauko hivyo ulivyoueleza wewe.pia namna ulivyomalizia hicho kifungio chako unaonekana kwamba huna nia ya kurekebisha bali una hamu hali iwe hiyo uliyoiainisha.kwa nguvu za mungu hatutarudi tulikotoka.
 
mola atatuvua na kila hasada na beluwa

mtu wa BEACH.....

amin ya rabal alamin..........watatuona hivi hivi

SAMVALUCOLE......

hizo data umeziona wapi wewe?wacha chokochoko zenu CHADEMA.
 
Ubaguzi wa rangi umerudi maradufu kule zanzibar na mbaya zaidi huuu ubaguzi ambao mzee KARUME aliukemea haufanyiwi lolote na hii inapelekea hata hali ya kiuchumi nayo unaiona. Unajua kuna wale wanzaibari weusi kama akina BI KIDUDE huwa wana ile ngoma yao MAARUFU NA KULE HUONI WALE RANGI RANGI au maarufu kama MACHOTARA ambao hujiona wao wako civilized zaidi

Tazama hata wale waliosafiri utaona ni wale rangi rangi mpaka mtu unajiuliza wale WEUSI WAKO WAPI?


sasa kurekebisha hii hali mnasemaje? irudishwe ile Amri ya kuwaoa kwa lazima hawa wanaojiita waarabu au mnasemaje?


duh wewe sasa unataka kuleta ufyokonyoko na ufisadi?

huo ubaguzi wa rangi umeuona wapi wewe ?

kama alivyosema Bi Senti 50 umetoka kwenye ukabila sasa unakwenda kwenye urangi - inaonyesha wewe ndie mbaguzi mkubwa

sasa mbona umeangalia kwenye unyago tu ? hujaangalia kwenye taarabu ?
 
Sasa kuangalia unyago tu unaconclude kuwa zanzibar kuna ubaguzi wa rangi au unalako jambo wewe?

kama unataka kuoa mwaarabu sema tu tutakutafutia tena utaowa bila ya kutumia nguvu yoyote, hoja pesa yako tu - siku hizi hakuna mambo ya uarabu na uweusi, pesa yako ndio inayosema - kabila lolote unalotaka kuoa wewe utaoa zanzibar. Lakini kusema kuna ubaguzi wa rangi zanzibar huo ni uongo usiohitaji tochi
 
kama ubaguziwa rangi huo uliouzungumzia wewe basi hata bara upo kwani kwenye ngoma ya sindimba hao watu wa rangi rangi (machotara) mimi sijawaona so Tanganyika nako kuna ubaguzi wa rangi?
 
rekodi ambayo haijavunjwa tangu 27 August 1896


AngloZanzibarWar.jpg



habari zaidi HAPA:

http://en.wikipedia.org/wiki/Anglo-Zanzibar_War
 
Marekani kusimamia muafaka CCM, CUF


Habari Zinazoshabihiana
• CUF waandamana, wawafungia mlango Lipumba, Seif 16.06.2007 [Soma]
• CUF yanawa mikono muafaka Zanzibar 08.08.2007 [Soma]
• Askofu anayedaiwa kutapeli kwa kutumia jina la Nyerere apandwa presha kizimbani 03.10.2006 [Soma]

Na Hassan Issa, Zanzibar

SERIKALI ya Marekani imeeleza kuwa daima itasimama katika imani yake ya kuhamasisha muafaka wa kisiasa Zanzibar.

Balozi wa Marekani nchini anayemaliza muda wake, Bw. Michael Retzer, amesema Serikali ya nchi yake imekuwa tangu zamani ikipigania kufikiwa kwa muafaka wa kweli wa kisiasa Zanzibar baina ya CCM na CUF.

Alisema juzi mjini hapa, kuwa Serikali ya Marekani kama ilivyotangulia na juhudi zake za awali za kutafuta muafaka huo, ingependa pia kuwapo na imani ya kweli ya kujenga umoja wa kitaifa kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

“Wiki zijazo tutakuwa pia na kazi ya kukutana na kufanya mazungumzo na CUF na CCM katika kujenga imani ya kweli ya kuufikia muafaka huo,” alisema.

Balozi Retzer alitetea msimamo huo akisema kuwa Marekani haina unafiki katika kupigania muafaka huo kwani ni muhimu katika kuweka hali ya amani na utulivu na maridhiano kwa Taifa zima.

“Unajua hapa hakuna unafiki na sisi tumekuwa na imani ya kuendeleza muafaka tangu mwanzoni mwa mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar ingawa katika hili, kunahitajika uvumilivu,” alisema.

Aidha, Balozi alisema mara kadhaa amekutana na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, ili kutafuta njia za kufikia muafaka wa kweli.

“Marekani inaamini kuwa azma ya pande zote ni njema na itaendelea kufuatilia juhudi za kuendelea na mazungumzo ya muafaka wa kisiasa wa Zanzibar,” alisema.

Balozi aliahidi kuwa hilo ni miongoni mwa majukumu yatakayoendelea kusimamiwa kikamilifu na mrithi wake, yaani Balozi mpya wa Marekani ajaye Tanzania hivi karibuni, Bw. Mark Green.

Balozi Retzer alisema kama alivyofanya Dar es Salaam, kuwaaga Waislamu wa Tanzania na wananchi wengine kupitia Radio Quran, ameonelea pia kutumia ziara hii kuwapa mkono wa kwaheri Waislamu na wananchi wote wa Zanzibar kazi ambayo aliifanya kupitia Radio Adhana ya mjini hapa.

Alisema anaelewa kuwa baadhi ya taasisi za kidini nchini zilikuwa na majibizano ya hapa na pale na nchi yake, lakini anaamini hilo ni muhimu katika kufikia maelewano na maendeleo maishani.

Alisema migogoro na tofauti za watu zisiwe sababu za kuleta machafuko ulimwenguni, bali ieleweke kuwa ni sehemu ya kufikia maendeleo na hasa baada ya kujirekebisha na kuelewa matakwa ya kila upande.

Balozi Retzer alisema anachoweza kumhadithia kila mtu katika safari yake ni ukarimu na ustaarabu mzuri wa Watanzania wote, na hilo ameshalieleza kwa mrithi wake.

Alisema Tanzania ni nchi ya jamii mjumuisho, yenye watu wa kila namna, lakini wanaoweza kuishi pamoja kwa amani na utulivu na kwamba ataendelea kulisifia hilo.

Balozi Retzer ambaye aliwaaga Watanzania kwa staili hiyo ya aina yake, alisisitiza kuwa kuaga kwake ni pamoja na kauli yake na ya nchi yake kuwa muafaka ni lazima na idumu amani ya Watanzania.

source : http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=3597
 
Mtu wa pwani wewe unataka mwafaka uwepo ama usiwepo?
 
Back
Top Bottom