Jembajemba,
Very interesting ulivyoweza kuiweka historia ya Hizbu kwani nina hakika umeitoa kama vile mwandishi mfuasi wa Hizbu!.,... badala ya kuzungumzia zaidi ukweli ambao hauchukui pande moja. Nina hakika ukiulizwa kusema jinsi ASP ilivyoanzishwa lazima utaanza kuponda na kusingizia watu wa kuja badala ya kuwa kubali hawa ASP kama ni chama cha Wazanzibar walioungana.
Labda hufahamu ya kwamba ni Arab Association kilichotanguliza madai yote uliyoyaweka hapo juu na huyu Ali Muhsin Barwani alikuwa mwanachama wa chama hiki. Na sii kweli Hizbu ndio walidai non racial election isipokuwa huyu mjomba Ali Muhsin Barwan na Abraham Babu, tena basi tunavyozungumza hapa huyu Muhsin Yuko zake Oman ni raia na anaishi hukooo!.
JembaJemba,
Historia ya Zanzibar imepotoshwa sana na watu kwa sababu ya uhasama wa hizi tabaka za Rangi ambazo zilikuwepo toka enzi na kukorezwa na Muingereza. Wakati huo kulikuwepo na chama cha weusi (African Association), washiraz na Shiraz Association na hata wahindi na chama chao cha Muslim Association kabla kabisa ya kuwepo Hizbu ama ASP. Trust me, kila mmoja wa vyama hivi anaweza kudai kwamba chama chao kilisimamia maslahi ya Wazanzibar wote! Lakini Uadui ulikuwepo kati ya wanasiasa wa pande zote kiasi kwamba inategemea wewe ulikuwa upande gani. Kisha basi kumbuka ya kwamba Nuingereza alikuwa hawezi kutoa Uhuru wa nchi nzima kwa vikundi vya watu na ndio maana wasomi hao waliotangulia walijua kwamba hakuna ujanja isipokuwa kudai haki za Wazanzibar wote. Hata Bara huku Bara na Africa nzima mchezo ulikuwa ni huohuo ni lazima chama kiwakilishe taifa zima ili kiweze kupewa Uhuru wa nchi hiyo.
Sasa basi pamoja na yote hayo unaweza kunambiakifo cha Arab Association?.. mbona chama hiki hakionekani tena ktk historia ya zanzibar baada ya kuzindsuliwa ZNP.
Umeuliza pia, kama kweli Hizbu kilikuwa chama cha waarabu basi wasingeshinda uchaguzi wa 'one on one' mwaka 1957!...Mjomba sii kweli hata kidogo kwani ASP ndio walishinda kwa viti 5 kati ya 6 , tena basi hicho cha 6 kilichukuliwa na Muslim Association. ZNP hawakupata hata kiti kimoja kati ya majimbo hayo.
Karume alimshinda Ali Muhsin kwa kura 3,328 dhidi ya kura 918 lakini Muhsin alikuja pewa Uwaziri pamoja na kwamba chama chake cha ZNP kilishindwa.
Umeulizia pia upatikanaji wa hizi kura 918 kama ni dalili ya kuonyesha Hizbu hakikuwa chama cha waarabu!.. mjomba vipi yaani unataka kusema upigaji kura huwa unaendeshwa kwa population ya watu? Ama ni watu wangapi waliosajiri kupiga kura!... Je wewe unaamini kabisa kuwa kama Hizbu kingekuwa ni chama cha waarabu basi kisingeweza pata hata kura 900 kwa sababu ya population yao!... you must be kidding.
Sikiliza ndugu yangu ni kwamba hivi vyama viwili ZNP na ASP walikuwa na uhasama toka zamani na haya maswala ya rangi unayojaribu kuyatumia hapa ni propaganda za kisiasa ambazo tumezizoea. Wanachama wa ZNP wakikuwa hadi koo za hao Ma - Sultan kama vile chama cha Ian Smith na walijaribu kwa kila hila kukivunja chama cha ASP vile vile. Hata kuondoka kwa Sheikh Mohammed Shamte, Sheikh Ameir Tajo na Sheikh Ali Shariff Mussa ASP ilikuwa ni njama za kukivunja chama hicho. Hawa waliitwa wasaliti kama vile Abraham Babu alivyochukiwa na ZNP kwa kuondoka chama hicho.
Ebu nikuulize tena kama kweli ZNP kilikuwa chama kinachopigania Umoja na Muungano wa Wa - Zanzibar wote imekuwaje ktk uchaguzi wa kwanza kabisa wamekosa hata kiti kimoja!...