Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
muafaka nnautaka, ila jee unawezekana ukawa muafaka wa kweli au just babaisha, maana .....
 
Zanzibar haitapatiwa muafaka mpaka CCM watakapo amua kuacha ujambazi wao.
 
Baaaab Kubwa... Zaidi kuna rekodi kadha wa kadha katika visiwa hivyo!
 
Au siku Jebu Bush atakapoamua kukamata mafisadi wote duniani.
 
mtu wa pwani......

taratibu kaka,huogopi kwenda KULALA CHUO CHA MAFUNZO WEWE?tumeshakujua SHAURI yako....FIRST WARNING!!!!!!!!
 
Huu muafaka sasa tuweze kufika mahali na kuhakikisha kuwa wananchi wanashirikishwa kila hatua ambayo imefikiwa kama cuf na ccm wanaona kuwa huu ni muafaka wa viongozi wasijidanganye kwani kuna siku wataulizwa na sisi wenyenchi yetu yaani watanzania.

Marekani inataka uwepo kwani nimeisoma sehemu fulani ripoti ya benk yao moja iliyopo hapa nchini kuwa kuzorota kwa siasa za zanzibar ni hatari kwa iashara zao hapa nchini.
 
Waziri ‘ashitakiwa’ na raia Zanzibar

na Mohammed Abdulrahman

WANANCHI wa Zanzibar, wameanza kuwasilisha malalamiko yao Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, na miongoni mwa watu wa mwanzo kulalamikiwa ni Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid.

Waziri Mansour amefunguliwa malalamiko hayo mbele ya tume hiyo, akituhumiwa kuvamia eneo la ardhi la Abdallah Ahmed Sharif (80), liliopo kando kando ya bahari ya Hindi, huko Buyu Wilaya ya Magharibi, Unguja.

Kamishna Mkaazi wa tume hiyo Zanzibar, Safia Masoud, alithibitisha kupokea malalamiko hayo na tayari tume hiyo imeanza kufanya uchambuzi na itahakikisha inawasiliana na waliolalamikiwa ili nao wasikilizwe kabla ya kutolewa maamuzi.

Katika barua ya malalamiko, ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, mzee Sharif anasema amesikitishwa na kitendo cha Waziri Mansour kuvamia eneo lake la ekari 10 bila ya kuzingatia sheria za umiliki wa ardhi.

Alieleza kwamba kitendo hicho kimefanyika huku viongozi wengine ambao wametakiwa kuondoka kwa amri ya mahakama katika eneo hilo, wakiwa hawajatekeleza amri hiyo kwa zaidi ya miaka 17 tangu maamuzi hayo kutolewa na Mahakama ya Rufaa Tanzania, katika kesi iliyofunguliwa 1989.

“Njama hii ya kuingilia haki yangu kikatiba inaendelezwa na Mheshimiwa Mansour Yussuf Himid kuchukua sehemu ya pwani ya shamba hili,” alilalamika mzee Sharif.

Alisema kwamba baada ya kupokea taarifa ya shamba lake kuvamiwa na Waziri wa Ardhi, alikwenda kuthibitisha katika eneo hilo na kuchukua hatua ya kukutana naye ili kujua nani aliyemruhusu kuchukua eneo lake bila ya ridhaa yake.

“Nilipoenda kuonana naye ofisini, aliniarifu kuwa yeye amethibitishiwa na uongozi wa wizara yake na wa CCM eneo la Shakani, hususan Khatib Abdallah Makame na Sheha wa eneo hilo, Yahya Matar na uongozi wa wilaya kuwa, sehemu hiyo ni ya serikali,” alisema.

Sharif alisema kwamba kitendo hicho kinamvunja moyo kwa vile Waziri wa Ardhi alitakiwa kusimamia haki yake.

Katika shamba hilo, mbali na Waziri Mansour, pia viongozi kadhaa wameamriwa na mahakama waondolewe, na nyumba zao kubomolewa baada ya kushindwa katika kesi Mahakama ya Mkoa, Mahakama Kuu Zanzibar na baadaye Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Baadhi ya viongozi walioamriwa kuondoka na nyumba zao kubomolewa ni Mshauri wa Rais Karume Mambo ya Mazingira, Abdallah Rashid, aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa Zanzibar, Mohammed Hija, mfanyabiashara maarufu Zanzibar, Edward Kissasi na aliyekuwa Meneja wa hoteli ya kitalii ya Reef.
source : http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/9/21/habari5.php#

muda mrefu zanzibar kumekuwa na ukiukwaji wa haki za binaadam, na viongozi kujioa wao wako juu ya kila kitu na kufanya walitakalo. sasa jee huu ni mwanzo wa kuthaminiwa haki za raia? au ni ubabaishaji tu?
 
Kwa Wazanzibar nawaaminia, wana msimamo thabiti hawako tayali kuyumbishwa, naamini haki yao itapatikana!
 
kila uchao utasikia manung'uniko ya utendaji baina ya vyombo vya Bara na zanzibar, ZFA na TFF, Mawasiliano bara mawasiliano Zenji, wafanyakazi zanzibar wafanyakazi zenji. mara mafuta mara uekezaji mara biashara mara elimu.

hivi hasa hakuna nia ya mkato kuondoa kero hizi?

halafu kwa nn hasa hawa ndugu zetu watanganyika wanataka kuigeuza nchi yangu nilioamua kwa ridhaaa kuungana nao kuifanya kama kajimkoa na kufanya maamuzi bila ya kutushirikisha.

huu muungano mkizidi tutauvunja maana nnaona wenzetu hamtaki kuheshimu haki na sheria

ZATUC yaipinga TUCTA suala la mgomo

2007-09-26 09:08:46
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar


Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC), limesema si muafaka kwa wenzao wa Tanzania Bara kupitia Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi (TUCTA) kuitisha mgomo wa watumishi wote kama njia ya kudai maslahi bora.

Mwenyekiti wa ZATUC, Bw. Zahran Mohammed Nassor, alisema wakati akizungumzia mgogoro wa kudai maslahi uliojitokeza kati ya TUCTA na Serikali ya Muungano.

Alisema njia muafaka ya kudai maslahi ya wafanyakazi ni kutumia utaratibu wa mazungumzo baina ya pande mbili na si kuitisha mgomo nchini nzima.

Alieleza kuwa utaratibu wa mgomo unaweza kuleta athari kubwa kiuchumi na kuzorotesha jitihada za kufikia ufumbuzi wa tatizo hilo.

`Mgomo sio njia muafaka tunawasihi wenzetu wa Bara watumie mazungumzo kwa vile mgomo unaathari kubwa kwa uchumi wa taifa`, alisema.

Mwenyekiti huyo alisema pamoja na kuwa mgomo umeruhusiwa kwa mujibu wa sheria, lakini hatua inayochukuliwa na serikali kufanya mazungumzo ni muhimu na inapaswa kuzingatiwa na pande zote.

Hata hivyo alisema iwapo muafaka utashindikana na kuamua kuitishwa mgomo wa wafanyakazi na watumishi wa Serikali ya Muungano waliopo Zanzibar hawatahusika, kwa vile ZATUC haikushirikishwa tangu mwanzo katika mpango huo.

Alisema pamoja na kuwa kila upande unashirikisho lake la vyama vya wafanyakazi, suala linalojadiliwa linahusu wafanyakazi wote wa Jamhuri ya Muungano, wakiwemo wale wanaofanya kazi Zanzibar.

`Suala hili linahusu maslahi ya watumishi wote wa Jamhuri ya Muungano ndiyo maana nasema hatutaruhusu mgomo wowote kwa wafanyakazi waliopo Zanzibar kwa vile hatukushirikishwa tangu mwanzo.`

Alisema tatizo lililojitokeza Bara halina tafauti na Zanzibar kwa vile kima cha chini cha Sh. 60,000 kinacholipwa ni kidogo, ikilinganishwa na mfumko wa bei za bidhaa uliopo sasa.

Alisema serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)inapaswa kuzingatia kuwalipa mshahara wa Sh. 150,000 wafanyakazi wa kima cha chini ili waweze kumudu ugumu wa maisha .

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa TUCTA, Bw. Nestory Ngula alisema shirikisho hilo linaandaa mgomo nchini nzima kama serikali ya Muungano haitapandisha mishahara kwa watumishi wake.

Alisema kima cha chini cha Sh.80,760 kilichoongezwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2007/2008 hakilingani na mahitaji na kuwataka watumishi wote kujiandaa na mgomo utakaoitishwa na TUCTA .

Hata hivyo, Serikali ya Muungano imeunda Kamati Malum ya kushughulikia mgogoro huo ambayo itatoa ripoti na mapendekezo yake ndani ya mwezi mmoja.

TUCTA inapendekeza kima chini cha serikalini kiwe angalau Sh. 300,000 kwa mwezi.

SOURCE: Nipashe
 
Mtu wa Pwani ... mtauvunja Muungano wakati hiyo ni mojawapo ya kete kubwa sana za chama chako? Siku mkivunja Muungano ujue wazi kwamba CCM ndiyo itakuwa bye bye hapo Visiwani, utamsikia Maalim akishangilia kwa nguvu zote huku akielekea Ikulu ya Zanzibar kwa mwendo wa mikogo!
 
mie utaifa kwanza halafu ndio mengine, zanzibar ni taifa lilokubali kuingia kwenye muungano kwa ridhaaa.


sasa ni juu ya chama chochote kinachotaka kuniconvice mimi ni kuja na suluhisho lamaana.

hivi huhisi kuwa inakera kila siku kupingana kwenye mambo madogo madogo.

maalim huyu hujui kuwa yy ni CCM damu?
 
mie utaifa kwanza halafu ndio mengine, zanzibar ni taifa lilokubali kuingia kwenye muungano kwa ridhaaa.

sasa ni juu ya chama chochote kinachotaka kuniconvice mimi ni kuja na suluhisho lamaana.

hivi huhisi kuwa inakera kila siku kupingana kwenye mambo madogo madogo.

Kwenye utaifa ninakupa 5 ... lakini kumbuka kwamba Zenji ni Muungano wa Unguja na Pemba. Kasheshe hizo za mambo madogo madogo zinakuzwa hapo Unguja tu, kule Pemba wala hawana habari za hayo mambo, wao wanaongelea vitu muhimu kama polisi na siyo ZFA vs TFF au TUCTA vs ZATUC. Kumbuka matatizo ya wafanyakazi wa Unguja hayafanani na matatizo ya wafanyakazi wa bara. Kwa hiyo hawa watu naona wanatakiwa ku-differ, maana hata kima cha chini ni tofauti kati ya bara na visiwani.

Shirikisho la Vyama cha Wafanyakazi kule Jamhuri ya Pemba linaitwaje? (joke)
 
Mie naona wafanyakazi wana haki ya kuandaa mgomo,hao wazenji labda kero zao zinasikilizwa,basi wao wafanye mazungumzo na serikali,lakini huku bongo ni taabu tupu,wafanyakzi hawasikilizwi,sharti waandae mgomo ili wapate haki zao.
Mwenyekiti wa ZATUC, Bw. Zahran Mohammed Nassor,anadai mgomo unaweza kuathiri uchumi wa nchi,hii hainingii akilini,kwani mpaka sasa hajui uchumi wa tanzania ulishakufa?Bajeti yetu ni tegemezi kwa 42%,sasa ni uchumi gani tunao?

Mtu wa Pwani,kuhusu suala la muungano kuvunjika,hilo lipo karibu tu,wala usiwe na wasiwasi.
 
Maalim azuiwa Zanzibar



na Mohammed Abduralhman



ZIARA ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kutembelea wagonjwa katika hospitali za wilayani Unguja na Pemba imeingia dosari, baada ya kuzuiliwa kutembelea Hospitali ya Mkoa Kaskazini Unguja iliyopo Kivunge.
Hamad juzi alitembelea wagonjwa waliopo majumbani, lakini Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imemzuia kutembelea hospitali hiyo kwa kile kilichoelezwa sababu za kitaalamu.

Ujumbe wa Maalim Seif ulikuwa umeambatana na Mwenyekiti wa CUF, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, Bakari Makame, Katibu wa jimbo hilo, Khamis Abass na Mbunge wa Viti Maalumu wa CUF, Mwajuma pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Mawasiliano ya Umma, Salum Bimani.

Kiongozi huyo amezuiwa kutembelea katika hospitali hiyo na Daktari Dhamana wa Hospitali ya Kivunge, Mtumwa Ibrahim, ambaye alisema kutokana na sababu za kitaalamu, ujumbe huo hauruhusiwi kutembelea hospitali hiyo. Hata hivyo hakufafanua zaidi.

Alisema ni kweli uongozi wa hospitali ulipokea ombi la ujumbe huo kutaka kuruhusiwa hospitalini kuwajulia hali wagonjwa wanaopatiwa matibabu, lakini kutokana na sababu hizo haikuwezekana.

“Kutokana na sababu za kitaalamu haitawezekana kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Kivunge,” alisema daktari huyo Dhamana, katika barua yake ya Oktoba 5, mwaka huu.

Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salum Bimani, alisema CUF imesikitishwa na uamuzi huo, kwa vile umewanyima haki wagonjwa kusalimiwa na kupatiwa msaada.

Bimani, alisema ni jambo la kushangaza wakati Maalim Seif anazuiwa kuwatembelea wagonjwa, wananchi mbalimbali wanaruhusiwa kuwatembelea katika hospitali hiyo hiyo.

Alieleza kuwa tangu ziara ya Maalim Seif kuanza kuwatembelea wagonjwa hospitalini na majumbani, kumekuwa kukijitokeza matatizo mbalimbali, ikiwamo huko Micheweni ambako wafanyakazi wa hospiatli walitakiwa kujieleza ni kwanini walimruhusu katibu mkuu huyo wa CUF kutembelea hospitalini hapo.

Alisema CUF imeamua suala hilo kulikabidhi kwa kiongozi wa upinzani katika Baraza la Wawakilishi, ili kuhoiji kwanini serikali inafanya hivyo.

Tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Maalim Seif amekuwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa majumbani, hospitalini na ziara hiyo aliianzia katika mikoa miwili ya Pemba na sasa inaendelea kisiwani Unguja.

Akiwa kisiwani Pemba, katibu mkuu huyo alitembelea hospitali za Mkoani, Abdalla Mzee, Wete na Micheweni, na kutoa misaada kwa ajili ya wagonjwa, ikiwemo mashuka ya kutandikia vitanda na vyandarua.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, aliwataka viongozi wa CCM Zanzibar kuwa na utamaduni wa kutembelea wagonjwa hospitali ili kuwa karibu na wananchi.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mpendae, Makamba alisema viongozi wanapotembelea wagonjwa na kubeba zawadi kama vile matunda, kunajenga faraja kwa wahusika.

source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/10/8/habari3.php
 
Back
Top Bottom