Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Hivi ni mkoa gani ambao ni mzigo wa mkoa mwingine? Unaweza kutupatia takwimu hapa ili tulinganishe maneno yako kama ni kweli au umeamua tu kuzusha kama mwanzilishi wa topic hii. Mzee Ruksa alikuwa rais wa Zanzibar na baadaye Tanzania hakuona sababu ya kuvunja muungano, BWM na sasa JK hakuna anayetaka kuvunja muungano.

Dodoma ni mmoja wapo.
 
1. Dodoma ni tajiri sema watu wake wameamua huwa omba omba tu-na viongozi toka mkoa huo kama akina Malecela hawakuchukua hatua za makusudi kuwabadilisha- ni hulka tu ya watu!

2. Zbar ni nchi kweli- kelele ni nyingi kwa vile ni nchi ndogo ya watu milioni moja against 37 m bara. Mimi nadhani wote wanavumuliana tu bara na visiwani- ndo maana 40 years sasa muungano umedumu!

3. Over Wapemba- hii dhambi itatupeleka pabaya! Kwa nini tusiulize kwa nini Wachagga wamesambaa nchi nzima na biashara zao? Watz wako huru kufanya shughuli yoyote na kokote Jamhuri ili hali tu walipe kodi!

4. Mimi ningependa Chuo Kikuu kinafunguliwa Pemba kama ilivyo Dodoma, Dar, na Moro! Hii ingeimarisha zaidi Muungano!
 
Majibu kama 'mtandao' umekufa ndani ya CCM baada ya uchanguzi yaanza kupatikana. Walau kwa upande wa Zanzibar...

Waziri Kiongozi mstaafu Z'bar asema CCM sasa ni moja

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Kiongozi mstaafu Dk Gharib Bilal ameeleza kuwa, baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa CCM, chama hicho kwa upande wa Zanzibar ni kimoja na hakuna makundi ndani yake.

Bilal aliliambia gazeti hili jana kuwa, kuna watu waliokuwa wakitangaza taarifa za kuwepo makundi kwa lengo la kuwaumiza wenzao na akafafanua kuwa wakati wa uchaguzi makundi ni jambo la kawaida na tena historia ya CCM Zanzibar inaonyesha kufa kwa makundi chaguzi zikiisha.

"Tuna kazi moja tu ya kukijenga chama chetu. Tulikuwa na kipindi kirefu cha kampeni na kisha uchaguzi. Katika kipindi hiki kulikuwa na mengi na sasa tumemaliza;" alisema Bilal na kuongeza;

"Kauli ya Mwenyekiti wetu Kikwete aliyoitoa Dodoma kuhusu kutosemeana mambo yasiyo ya kweli ni ya muhimu na nadhani tutazidi kuihubiri kwa wanachama ili kukibakiza chama chetu katika mshikamano na umoja."

Dk Bilal alieleza pia kuwa, kazi iliyopo mbele ya wana CCM wote ni kutazama namna wanavyoweza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao wa mwaka 2010 na akafafanua kuwa, lengo la maandalizi ya mapema ni kujihakikishia ushindi kwa CCM katka uchaguzi huo.

"Uchaguzi ni suala gumu, linahitaji maandalizi ya pamoja kama chama. Naamini kazi iliyopo mbele yetu ni kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao huku tukiwa wamoja zaidi," alisema.

Source link: Mwananchi.

SteveD.
 
Hivi ni mkoa gani ambao ni mzigo wa mkoa mwingine? Unaweza kutupatia takwimu hapa ili tulinganishe maneno yako kama ni kweli au umeamua tu kuzusha kama mwanzilishi wa topic hii. Mzee Ruksa alikuwa rais wa Zanzibar na baadaye Tanzania hakuona sababu ya kuvunja muungano, BWM na sasa JK hakuna anayetaka kuvunja muungano.
Na hilo pia hawako radhi nalo wanasema Mzee Ruksa ni mzaramo wa Kisarawe na ukiwahoji sana watakwambia uwatajie sehemu alipozaliwa huko Zanzbar, kama baba yao wa Taifa Karume faza wanasema ni Mmalawi,huna la kuwaambia wanasema toka wapate Uhuru hawajapata raisi mzanziba,na hao waliowapata wamewekwa na sisi Watanganyika utawasikia tunawachagulia Raisi kutoka Dodoma ,hawa ni watu hawachukuliki hata kidogo.
 
Sio upemba kwani wapemba ni watu wazuri tu,tena ni watu wenye imani sana tofauti na Wazanzibari wengine wenye asili ya Unguja ambao inasemekana ni wavivu sana.Bora kuwepo Wapemba hapa Bongo kuliko hawa wa kutoka Unguja ambao mara nyingi inaonekana ni mizigo kama walivyo huko Bungeni,wapemba walioko bungeni wanapigania maslahi ya Tanzania nzima na wanahoji kila kitu wanachokiona kina maslahi na Taifa na ni bora tukaungana na Wapemba kuliko waunguja,weka mbali hilo.
Ninachokisema ni hizi serikali ya Zanzibar ambayoinaonekana ni mzigo usio tulika hapa kwetu Bongo,wanatudhalilisha vibaya sana leo gazetini wamewapiga marufuku wanao toa mihadhara kuhutubia huko Zanzibar ,kama mtakumbuka yuko shehe ajulikanae kwa jina la shehe Kurwa huyu alitimuliwa Zanzibar chini ya mtutu au chini ya ulinzi mkali na walisema anarudishwa kwao Tanganyika eti anajihusiha na uchochezi hiyo ni chini ya utawala wa Salimini,hivi huku ndio kuungana kama si unyanyasaji wa mtu ndani ya Nchi yake ni kitu gani ? Na hili si kwa mashehe tu hata dini zingine hazina uhuru wa kueneza neno lao,wanaogopa.
Wapemba wana mabiashara hapa na wameajiri vijana wengi wa Tanganyika kuliko kutoka kwao naweza kusema ni waekezaji wazuri tu wanaokubalika na jamii yetu,sifa yao nasikia ni ya kuhama hama na kuenea kibiashara kama walivyo wa jamii ya kichaga na huweza kujituma bila ya kuchagua kazi kama walivyo jamii ya kisambaa,hivyo kuwepo kwao sio mzigo bali ni lubricate kwa vijana wetu.

Samahani Mwiba,
Nilivyoona mimi kuwa umefanya haraka sana kuingia kwenye mjadala na kuanza kwenda nje ya mada ambayo wewe umeianzisha tena kwa kuegemea kwenye mambo yasiyo na msingi, ya kuwagawa hata Wazanzibari.
 
1. Dodoma ni tajiri sema watu wake wameamua huwa omba omba tu-na viongozi toka mkoa huo kama akina Malecela hawakuchukua hatua za makusudi kuwabadilisha- ni hulka tu ya watu!

2. Zbar ni nchi kweli- kelele ni nyingi kwa vile ni nchi ndogo ya watu milioni moja against 37 m bara. Mimi nadhani wote wanavumuliana tu bara na visiwani- ndo maana 40 years sasa muungano umedumu!

3. Over Wapemba- hii dhambi itatupeleka pabaya! Kwa nini tusiulize kwa nini Wachagga wamesambaa nchi nzima na biashara zao? Watz wako huru kufanya shughuli yoyote na kokote Jamhuri ili hali tu walipe kodi!

4. Mimi ningependa Chuo Kikuu kinafunguliwa Pemba kama ilivyo Dodoma, Dar, na Moro! Hii ingeimarisha zaidi Muungano!

Hata sisi Tanganyika tunavumiliana. Pesa zinazotumika kujenga mji mkuu hazitoki Dodoma na kama Dodoma haindelei kwa kutumia kisingizio cha makao makuu sioni Malecela anachoweza kubadilisha.

Unafikiri watu wa Kigoma sio wavumilivu kuwa Tanganyika. Toka mjerumani aachie ngazi bado inatumika reli hilehile.

Bila kuruhusu meli binafsi serikali ya Tanganyika ilishindwa kununua mtumbwi wa kupeleka watu mikoa ya kusini.

Kagera pamoja na kuzalisha sana Kahawa barabara zote zilikuwa za mavumbi.

Kuhusu vyuo vikuu naona bado unashindwa kuita mapera mapera na ukwaju ukwaju.

Hawaii ina idadi ya watu kama 1.2 Milioni na shughuli nyingi wanaziendesha wenyewe ikiwamo vyuo vikuu bila kutegemea serikali kuu. Na kama vyuo vikuu vinaimarisha muungano basi Jamuhuri za Kisoshalisti za Kisovieti zingedumu kwani wao walijenga mavyuo kila sehemu.

Muungano ni mambo ya katiba na sheria. Serikali kuu inatakiwa ishughulikie mambo yake ya kikatiba. Mambo mengine yakiwemo ya vyuo vikuu yaachiwe serikali za majimbo au mikoa kushughulikia.
 
Hapana ndugu,katika hili ni tofauti na kufananisha mkoa,hizi ni Inchi mbili zilizoungana,leo Wazanzibar wakikusikia unawaita mkoa basi kidole machoni,kuna ule wakati waliambiwa hawajalipa umeme,wakasikika wakisema umeme ukikatwa Muungano ndio mwisho,sasa wakilipa wasilipe ni hiari yao,hapo hawakulipa kitu na umeme hatukuona kukatwa inamaanisha sisi ndio tunawahitaji bila ya wao hatuwezi kujiongoza,hatuwezi kujiamulia imekuwa kama wanatuburuza na hata hivyo bado wanasema hatuwatendei haki,haki gani hiyo watumie umeme bure na mapato waweke ndani,lile deni hawajalilipa mpaka kesho.
Kuhusu mikoa iliyokuwa haizalishi hii ni yetu na hailalamiki kama inatengwa ,na haiwezi kulalamika kwani wanajijua kwamba hawazalishi kitu hivyo ni tegemezi lakini kwa upande wa Zanzibar wanajiona wao ni matajiri sijui mila zao ni kubwa na za ajabu ambazo sisi huku tunaonekana wahuni tu,tukienda huko tunaenda kuwaharibia na kuwaenezea magonjwa na kuharibu mila zao,sijui wana mila gani ambazo ni bora kuliko zetu ,mimi sijaona utamaduni wao wala siujui na kuambiwa huu ni utamaduni wa wazanziba.Imetoka amri jamii ya wamasai wavae suruali na shati hivi huu kama si udhalilishaji ni kitu gani,ni ubabe tu tunaofanyiwa na watu hawa.
Kuna rafiki yangu wa Arusha ambae yuko katika cheo ndani ya chama CCM nilimuuliza kuna faida gani kuendelea na watu hawa ambao wanatuona waTanganyika ni wakandamizaji akanijibu ,unajua hawa tukiwaacha kutawalana watauana halafu lawama zitaturudia sisi,nikamjibu si bora waachiwe wauane wenyewe kwa wenyewe kuliko sisi ndio tunaonekana ndio tunaopeleka majeshi na kuwaua kila unapofika uchaguzi mkuu,na lawama zinazotufika ni kubwa kiasi cha kutukosesha maslahi na kuturudisha nyuma,kila tunapopagusa pako moto kwa hali ya huko Zanzibar tunaambiwa tunahusika wakati hatupati faida yeyote kuwepo kwa huu muungano angalau tuna cha kusema tukivunja Muungano basi Inchi yetu itaporomoka kwa sababu huko Zanzibar tunategemea kitu hiki na kile,hivi jamani ni vitu gani hivyo tusivyovijuwa sisi wingine??

Mkia wa Mbuzi ni mfupi sana, lakini ukitaka kujua faida zake, basi uukate na uondoe kabisa.
Kwa maoni yangu mimi, matatizo yaliyopo katika muungano wetu, ni mambo yanayoweza kupatiwa ufumbuzi. Na nina imani kuwa serikali ya awamu ya nne iko makini kuendeleza jitihada zilizoanza huko nyuma katika kuhakikisha kuwa 'kero' za muungano zinapunguzwa kama sio kuondolewa kabisa. Na hatua tumeona zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwepo Waziri Maalum anayeshughulikia masuala ya Muungano katika Ofisi ya Makamu wa Rais.
Muungano wetu ni lazima tuungalie kwa jinsi gani wananchi wa kawaida kabisa wanaweza kupata nafasi kuishi maisha yaliyo bora. Kwa mfano, ukiangalia historia ya Zanzibar (Unguja na Pemba), huwezi ukadharau kuwepo kwa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar. Ilikuwa ni muhimu kwa wazanzibar wapate fursa ya kushirikiana na Tanganyika ili kuweza kuleta uwiano sawa ndani ya wakazi wa visiwa hivyo (kumbuka historia kabla ya mwaka 1964). Mimi binafsi nafarijika kuona kuwa kuna namba ya wazanzibar ambao bara ndiyo nyumbani kwao kama walivyo watanzania wengine. Nafarijika kuona kuwa tangu mwaka 1964 hadi leo wazanzibar wengi tu wamepata fursa ya kusoma bara katika fani mbalimbali na sasa hivi wanafanya kazi bara wakiitumikia nchi yao ya Tanzania bila ya kupata hisia tofauti kwamba wao ni wa upande fulani wa jamhuri. Nafarijika kuona jamii zetu zimeingiliana sana kwamba kunavizazi ambavyo ni mchanganyiko kati ya wabara na wa zanzibar.
Sababu kubwa ambayo ninajivunia pia ni kwa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kunakuwepo hali nzuri ya kisiasa huko Zanzibar kwa kipindi chote tangu mwaka 1964 ( hili siyo jambo la kubeza hata kidogo). Leo hii tabaka la watu wa hali ya chini Zanzibar linaweza kushiriki katika maamuzi mbalimbali kinyume na hapo zamani. Vilevile ni heshima kubwa kwa nchi yetu ya Tanzania kuweza kuwa na Muungano huu na kuweza kuundeleza kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka 40.
Kwa kifupi watanzania wote ni ndugu sasa hivi, tofauti zilizopo za muungano ni ndogo sana ulilinganisha na undugu wetu tulionao.
 
Kama unafarijika na muungano huu kwanini mnakataa Muungano na nchi zingine za Afrika Mashariki?
 
Kama unafarijika na muungano huu kwanini mnakataa Muungano na nchi zingine za Afrika Mashariki?

Muungano wa Afrika Mashariki haujakataliwa, na huenda usiepukike, lakini wakati mufaka haujafika.

Kwa Zanzibar na Tanganyika Muungano ulikuwa ni muhimu hasa ukizingatia historia na mazingira yaliyokuwepo kabla na baada ya mwaka 1964.
 
Samahani Mwiba,
Nilivyoona mimi kuwa umefanya haraka sana kuingia kwenye mjadala na kuanza kwenda nje ya mada ambayo wewe umeianzisha tena kwa kuegemea kwenye mambo yasiyo na msingi, ya kuwagawa hata Wazanzibari.
Sijawagawa ila alichosema mmoja ni ikiwa muungano utavunjika basi watu wa visiwa warudishwe makwao,hapa ndio nikasema kama kurudishwa basi wapemba wasiwemo kwani ni wachapa kazi kuliko waunguja,kama utakumbuka Mugabe aliwatimua wachapa kazi wazungu,kilichotokea ni kuzorota kwa mashamba na mengine kufa kabisa,si watu wote wanapendelea ulimaji hasa wakisasa ambao unahitaji mtu mwenye ari ya kulima kitaalamu,wazungu waliliweza hilo na wakifuata utaratibu wote wa kutayarisha mashamba kuanzia udongo mpaka mbegu,wezangu mimi hilo hatuliwezi kwani si sawa na kuokota mahembe asubuhi.Na nilivyoona ni wapemba ni watafutaji na wanaweza kuendeleza kuliko kusema tunawaondoa kwani pirika zao hatuziwezi.
Ila hoja bado sijaiona kujibiwa ni kitu gani tunafaidika nacho kuendelea na Muungano huu usiokwisha malumbano tokea tulipoungana 1964 mpaka leo,maana natumai kama pangelikuwepo na faida basi neno Muungano leo lisingekuwepo lingebaki ni historia tu inayoandikwa vitabuni,au ianzishwe hoja ya kuwa nchi moja Raisi mmoja na Katiba moja neno Muungano liondolewe kabisa,kitu serikali ya mapinduzi baraza la mapinduzi katiba ya zanzibar hivi vyote viondolewe na kuchomwa moto kwani ndivyo vinavyoleta kisirani na jeuri ya watu hawa.
 
karibuni wana wa mtikila,mnaopenda kuutukuza utengano ili khali utengano ni uzaifu,
mie nisingependa muungano ufe bali ufanyiwe marekebisho kidogo
 
karibuni wana wa mtikila,mnaopenda kuutukuza utengano ili khali utengano ni uzaifu,
mie nisingependa muungano ufe bali ufanyiwe marekebisho kidogo
Kuna wakati ukifikia gari inakuwa haitengenezeki na kila ukijaribu kuitengeneza ndio unapojizidishia hasara ,kwa nionavyo tulipofikia panatosha na sikioni hicho cha kurekebishwa kama kipo kitajeni hapa tuone maoni ya wengi,tumeanzisha TRA na kupanga nao kila kitu pamoja ,leo si wazanzibariCCM si wa wazanzibari CUF wanapiga makelele kama ndio tumewaulia uchumi wao na hawana kitu bandari zao ambazo ni mbovu tokea hio zamani wameipatia sababu kwamba TRA ndio imeziua bandari zao na waliokua wanaagiza mitumba kupitia bandari za Zanzibar niseme ya zanzibar maana ndio hiyo hiyo moja tu wameirithi toka kwa mkoloni muarabu) wote wamehamia bandari za Tanga na Daresalamu wakati feza walizopewa za msaada kutengenezea bandari zao wamezitafuna,wajamani huku si ndio kunako kero.
Yaani chao ni chao lakini chetu ni vyetu,hawa hawahitaji marekebisho nihuu Muungano kupigwa kumbo tu na kupelekwa kwenye vyuma chakavu,labda baadae watakuja kujuta na kuona mbadala wa Muungano ni kuwa Inchi moja tu.
 
1. Wakati TRA hawako Zenj bidhaa nyingi zilikuja kwa magendo Bara kutumia upenyo wa bandari ya Zenj- is this fair?

2. Muungano umedumu kwa miaka 40 sasa- jawabu ni kuuvunja? Kwa sababu zipi? Tatizo ni Uchumi tu- na hii haipo tu Zenj- ipo hata Lindi, Ddma n.k. Jawabu ni hardwork! Muungano has been too much politicized- tugawane kipi- tufanye kwanza kazi tuzalishe!

3. Mawazo ya kuvunja Muungano hayataijenga Tanzania-Wazenj wapo Dar, na Wachaga wapo Zenj! Ni kazi tu.. to tape opportunities- Tanzania ni kubwa na kuna opportunities nyingi! Ni kama mtu unafamilia ukapata matatizo ya kiuchumi- badala ya kutafuta mbinu za kuyatatua unamlaumu mke wako na unataka kumfukuza!
 
Siku U.S.A itakapo sambaratika na kila state kuwa kivyake ndo siku U.R.T (United Republic Of Tanzania), nayo itasambaratika... Maana nasikia huu muungano uliwekwa na wao kwa kuogopa ukomonisti na uislam. Ukomonist umesambaratika kwa asilimia fulani, bado Uislam ambao pia wanauogopa, That why nchi yoyote inayojitangazia kuwa the real Islamic state U.S.A hawakubaliani nayo... Na hii ilionekana Zanzibar... Aidha ingeangukia mikononi mwa makomredi au Muslims...
 
1. Wakati TRA hawako Zenj bidhaa nyingi zilikuja kwa magendo Bara kutumia upenyo wa bandari ya Zenj- is this fair?

2. Muungano umedumu kwa miaka 40 sasa- jawabu ni kuuvunja? Kwa sababu zipi? Tatizo ni Uchumi tu- na hii haipo tu Zenj- ipo hata Lindi, Ddma n.k. Jawabu ni hardwork! Muungano has been too much politicized- tugawane kipi- tufanye kwanza kazi tuzalishe!

3. Mawazo ya kuvunja Muungano hayataijenga Tanzania-Wazenj wapo Dar, na Wachaga wapo Zenj! Ni kazi tu.. to tape opportunities- Tanzania ni kubwa na kuna opportunities nyingi! Ni kama mtu unafamilia ukapata matatizo ya kiuchumi- badala ya kutafuta mbinu za kuyatatua unamlaumu mke wako na unataka kumfukuza!
Vipi unaweza kuhoji kuwa ni magendo wakati wao wanasema kuja kwa TRA kumeua Uchumi wa Zanzibar na bandari zao,hilo ndugu ulifahamu ni tatizo ,hapa bora wasipasikie maana kama ni magendo itakuwa si kwa upande wao,ni sheria zilizopo ndizo zinazofanya kiingiacho kutoka kwao kionekane ni magendo wakati wao wanasema walikuwa na bei poa ya kuwavutia wafanya biashara,wanachodai eti TRA wameweka kiwango kikubwa Zanzibar na kuweka kiwango kidogo Tanga na Dar na tatizo ambalo niliambiwa ni kuwa ukishusha mzigo Zanzibar na kutaka kuupeleka bara itakubidi ulipie tena,yaani kuna kutofahamiana zaidi wanaposema kinachopatikana kwenye TRA kwa upande wa Zanzibar hakiingii katika serikali hivyo serikali inapoteza mapato na serikali ya Muungano kupitia TRA inawaibia wateja na feza za kodi,serikali kwa kweli hazifahamiani,ni mvutano wa mmoja kuachia mmoja apate,hapo pana tatizo,kama tungelikuwa Nchi moja Tanzania basi lisingekuwepo.
Ni juzi tu nimesikia ukiwa na gari hutoruhisiwa kuliendesha likiwa na namba za upande wa pili,za huku haziruhusiwi kuendeshwa huku na za huku haziruhusiwi kuendeshwa huku,ndugu huo si muungano ni nchi zisizokuwa na uhusiano wa aina yeyote ,huu si muungano bali ni matatizo ya kijinga ,hivi muungano gani uliodumu kwa miaka zaidi ya arubaini uliokuwa na kitu kama hiki,hebu fikiria ulete jibu la uhakika,hawa wanatufanya sisi kama tuna shida sana sana,tukitembea kwao huwa wanatutazama kwa jicho baya yaani kama ni wageni kutoka nchi nyengine kabisa,hebu nendeni mkatembee Zanzibar muone,wana jeuri kabisa na kutuona sisi ni masikini tunaokimbia makwetu,na kuivamia nchi yao utawasikia wakisema tunajazana wakati ni kisiwa kidogo tu,waliwahi kuniambia ninakimbia kodi wakati nilienda kikazi.
sababu za kuuvunja ni kwamba sijaona faida na sababu za kuuendeleza,nimesema nitajiwe sababu wewe unauliza suali kinyumenyume niseme sababu za kuuvunja,sasa sijui husomi au huelewi,nasema hakuna faida zaidi ya majungu tu na kutudhalilisha mimi mmasai unaniambia nivae suruali na shati wakati najihisi nipo ndani ya Nchi yangu Tanzania na kuvaa nguo zangu za asili sijavunja sheria ya Inchi hii,hivi ngugu unajua unachokieleza.
Hata wazungu wapo Tanganyika na hatujaungana kuna sheria itabidi zifuatwe kama inchi mbili zinazoheshimiana lakini sio zilizoungana hapo ipo tofauti ya kuishi na anaetaka atabadili uraia sio tatizo,wao watakuwa na sheria zao na sisi na zetu,kuna nchi unaishi mpaka unazeeka lakini hupati uraia na kuna nchi ukimaliza miaka mitano unapewa uraia,waachwe wakafie mbele ya safari umeshatuchokesha sasa eti wanasema Dhahabu na almasi ziwe zetu sote ,mbona walipoambiwa waende kuanika karafuu dodoma waliruka.
 
Wewe kama raia wa Bara yenye watu mil 37,
Kama Muungano ukivunvika leo hii- wewe binafsi utafaidika nini?

Muungano huu utadumu tu- mafaifa huungana sii tu kwa sababu za kiuchumi tu. Wengi wa Watu wa Zenj asili yao ni bara- tu watu wamoja tu!
 
yalaiti !yalaiti! natamani ! natamani ! moja ni kiswahili,kiingereza ni one, kiarabu ni waahed, kihindi ni ek.naomba muwe na subira, msiwe na jazba vijana.moja ikikaa na mbili huitwa kumi na mbili na haiitwi moja mbili.damu inanichemka ili niropokwe kwa maneno makali nilioyaona kwenye hii thread lakini najua hawa waliosema wana lao .acha ninywe maji nikate jazba .naamini iko siku tutafika tunapokwenda, langu jicho.atakaenithamini nitamthamini bila kujali mipaka ya kijiografia, elewa kitu kimoja kutoka kwangu, usidhani kwakuwa ni mtanzania mwenzangu ndio nitakujali hata kama unanikejeli , no and never, nitamthamini mburundi alie mbali kuliko mtanganyika anaemkashifu mzanzibari. sijali kuhusu jina la nchi yangu najali anaenithamini.niliongea siku za nyuma na narudia tena . identity yangu sio utanzania wala uzanzibari bali ni ubinadamu.
ni mimi mheshimiwa msaliti.
 
1. Wakati TRA hawako Zenj bidhaa nyingi zilikuja kwa magendo Bara kutumia upenyo wa bandari ya Zenj- is this fair?

2. Muungano umedumu kwa miaka 40 sasa- jawabu ni kuuvunja? Kwa sababu zipi? Tatizo ni Uchumi tu- na hii haipo tu Zenj- ipo hata Lindi, Ddma n.k. Jawabu ni hardwork! Muungano has been too much politicized- tugawane kipi- tufanye kwanza kazi tuzalishe!

3. Mawazo ya kuvunja Muungano hayataijenga Tanzania-Wazenj wapo Dar, na Wachaga wapo Zenj! Ni kazi tu.. to tape opportunities- Tanzania ni kubwa na kuna opportunities nyingi! Ni kama mtu unafamilia ukapata matatizo ya kiuchumi- badala ya kutafuta mbinu za kuyatatua unamlaumu mke wako na unataka kumfukuza!

MzalendoHalisi:

Akhsante kwa kuipa mada hii uzito. Mpaka sasa sijaona mtu yoyote anatoa point sababu za kuvunja muungano.

Wanachukua point moja na kuzunguka nayo. Na point zenyewe sio za mambo ya katiba na sheria ambavyo ni kiini cha muungano.

Mtu anasema tuvunje muungano kwa sababu wamasai wameambiwa wavae suruali. Damn right, wamasai wavae suruali. Je kuna mtanganyika gani anayepokelewa na jamii ya kimasai ? Wamasai wanaamini kuwa ni kabila lao pekee ndilo lenye haki ya kumiliki ng'ombe na makabila mengine ni washenzi tu.

Wakati jimbo la Quebec linataka kujitenga kutoka Canada, mfanyabiashara aliulizwa kuhusu hali matatizo ya kiuchumi yatayoweza kujitokeza. Mfanyabiashara huyo akajibu pesa haifuti bendera. Hivyo ushuru ukiwa mkubwa Zanzibar, wafanyabiashara watatumia Tanzania bara kupitisha mizigo na kuipeleka kimagendo Zanzibar. Ushuru ukiwa mdogo Kenya watapitisha mizigo Kenya na baadaye kuileta Tanganyika.

Na Tanganyika inaathirika sana katika masuala ya magendo kwa sababu ushuru ni mkubwa kiasi cha kudidimiza uzalishaji. Na hili sio suala la muungano bali ukiritimba.
 
Leo wanawambia wavae suruali kesho watwambia wav..suruali,hii ni kashfa nzito sana hailingani na mabo ya ngombe,hapa tunaambiwa Watanganyika tunakwenda uchi,hivi mnatazama mambo kwa karibu,hapa akipigwa mmoja tunapigwa sote na tatizo ni baadhi yetu kulinganisha na ng'ombe,ipo wapi thamani ya ng'ombe na thamani ya Utanganyika,kila anaedharau chake basi huyo atakuwa amepotoka,siwezi kukubali kudharauliwa kwa Mtanganyika yeyote kwani dharau hiyo inanigusa na mimi moja kwa moja,nilikwenda kupigana Uganda si kwa sababu Nduli amechukua sehemu ya Kagera bali nilikwenda kupigana kwa sababu amechukua sehemu ya Tanganyika,Ngoja nitoke nje kidogo kama unayo software ya Google earth jaribu kuangalia sehemu za kusini mwa Tanzania tunapopakana na malawi utaona kuna RED Boarder ambayo imeliweka lile ziwa Nyasa au ziwa malawi kuwa au kuonekana ni sehemu ya Malawi sijui unakumbuka ile nyimbo inayosema Banda wa Malawi katuvalia ngozi ya Chui akafikiri atatustisha..hivi unaikumbuka uliza sababu ya nyimbo ile,ok nilipouliza habari ya mstari au mpaka mwekundu katika sehemu ile nikaambiwa sehemu ile ina matatizo au kuna tatizo la mpaka baina ya Tanzania na Malawi,sasa kama Mwanakijiji yupo na atasoma hii thread anifikishie hili suali kwa Waziri wa mambo ya ndani na ya inje kuulizia ni kwa nini kuna red line pale Je Tanzania ina miliki au haimiliki sehemu ya ziwa lile na kwanini hakuna mpaka unaokatiza katikati ya ziwa...damu inanichemka halafu anatokea mtu anasema anajali ubinadamu,hapa pana Utanganyika tu wanasema usicheze na mali cheza na mwenye mali,Utamaduni na mila ni mali ya kila mtanganyika kudharauliwa au kunyanyaswa mimi binafsi sitokubaliana nako hata akiwa anaebamizwa kwa utamaduni wake ni mmasai,halafu unaleta ya kuleta eti ng'ombe hivi hujawahi kuona mmasai kuuza ng'ombe,jiulize sasa kwa nini anamuuza au ndio unataka kutwambia kwamba anafanya utapeli,hizo habari za vibarazani sina nafasi nazo,kilichofanywa na serikali ya Zanzibar ni udhalilishaji wa hali ya juu kwa Mtanganyika,kama haitoshiutawasikia wakisema hii ni mipango ya serikali ya Muungano au serikali ya Bara kama wanavyoiita kuwajaza waTanganyika huko kwao visiwani,haya kama si matusi ni kitu gani jamani hebu yatazameni haya mambo kwa undani,sio mnakulupuka na jazba ya yule mfalme alietoka nje bila ya nguo mpaka mtoto mdogo akasema mfalme yupo uchiii,huku ni kutukanwa kwa watanganyika wote,bado sijaona sababu za msingi juu ya faida za Muungano labda labda kuna kundi tunalo ndani yetu kundi hili linafaidika katika mambo ya siasa inapofika wakati wa kumchagua Mgombea Uraisi wa Tanzania,hapo natumai kila mmoja anaweza kuona ndio sababu kuu lakini hakuna sababu nyengine zaidi ya hiyo,na naamini kabisa siku kundi hili kutoka Zanzibar likija kuangushwa na CUF ndio mwisho wa Muungano huu kwani sasa itakuwa waliokamata serikali kule visiwani watu wasiotaka mambo ya kuoneana haya kila kitu kitazungumzwa,tunalijua hilo kuwa hawa CUF watakuja na mambo mapya kutaka kuuzungumza Muungano katika ngazi za kimataifa ili uonekane ni muungano wa kweli na sio huu wa kulindana hata ikifikia hapo basi nitafarijika kwani itabidi tuheshimiane kikweli la wakiteleza kidogo tu tumemewawacha mkono.
 
Du- kaazi kweli kweli!
 
Back
Top Bottom