Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Leo wanawambia wavae suruali kesho watwambia wav..suruali,hii ni kashfa nzito sana hailingani na mabo ya ngombe,hapa tunaambiwa Watanganyika tunakwenda uchi,hivi mnatazama mambo kwa karibu,hapa akipigwa mmoja tunapigwa sote na tatizo ni baadhi yetu kulinganisha na ng'ombe,ipo wapi thamani ya ng'ombe na thamani ya Utanganyika,kila anaedharau chake basi huyo atakuwa amepotoka,siwezi kukubali kudharauliwa kwa Mtanganyika yeyote kwani dharau hiyo inanigusa na mimi moja kwa moja,nilikwenda kupigana Uganda si kwa sababu Nduli amechukua sehemu ya Kagera bali nilikwenda kupigana kwa sababu amechukua sehemu ya Tanganyika,Ngoja nitoke nje kidogo kama unayo software ya Google earth jaribu kuangalia sehemu za kusini mwa Tanzania tunapopakana na malawi utaona kuna RED Boarder ambayo imeliweka lile ziwa Nyasa au ziwa malawi kuwa au kuonekana ni sehemu ya Malawi sijui unakumbuka ile nyimbo inayosema Banda wa Malawi katuvalia ngozi ya Chui akafikiri atatustisha..hivi unaikumbuka uliza sababu ya nyimbo ile,ok nilipouliza habari ya mstari au mpaka mwekundu katika sehemu ile nikaambiwa sehemu ile ina matatizo au kuna tatizo la mpaka baina ya Tanzania na Malawi,sasa kama Mwanakijiji yupo na atasoma hii thread anifikishie hili suali kwa Waziri wa mambo ya ndani na ya inje kuulizia ni kwa nini kuna red line pale Je Tanzania ina miliki au haimiliki sehemu ya ziwa lile na kwanini hakuna mpaka unaokatiza katikati ya ziwa...damu inanichemka halafu anatokea mtu anasema anajali ubinadamu,hapa pana Utanganyika tu wanasema usicheze na mali cheza na mwenye mali,Utamaduni na mila ni mali ya kila mtanganyika kudharauliwa au kunyanyaswa mimi binafsi sitokubaliana nako hata akiwa anaebamizwa kwa utamaduni wake ni mmasai,halafu unaleta ya kuleta eti ng'ombe hivi hujawahi kuona mmasai kuuza ng'ombe,jiulize sasa kwa nini anamuuza au ndio unataka kutwambia kwamba anafanya utapeli,hizo habari za vibarazani sina nafasi nazo,kilichofanywa na serikali ya Zanzibar ni udhalilishaji wa hali ya juu kwa Mtanganyika,kama haitoshiutawasikia wakisema hii ni mipango ya serikali ya Muungano au serikali ya Bara kama wanavyoiita kuwajaza waTanganyika huko kwao visiwani,haya kama si matusi ni kitu gani jamani hebu yatazameni haya mambo kwa undani,sio mnakulupuka na jazba ya yule mfalme alietoka nje bila ya nguo mpaka mtoto mdogo akasema mfalme yupo uchiii,huku ni kutukanwa kwa watanganyika wote,bado sijaona sababu za msingi juu ya faida za Muungano labda labda kuna kundi tunalo ndani yetu kundi hili linafaidika katika mambo ya siasa inapofika wakati wa kumchagua Mgombea Uraisi wa Tanzania,hapo natumai kila mmoja anaweza kuona ndio sababu kuu lakini hakuna sababu nyengine zaidi ya hiyo,na naamini kabisa siku kundi hili kutoka Zanzibar likija kuangushwa na CUF ndio mwisho wa Muungano huu kwani sasa itakuwa waliokamata serikali kule visiwani watu wasiotaka mambo ya kuoneana haya kila kitu kitazungumzwa,tunalijua hilo kuwa hawa CUF watakuja na mambo mapya kutaka kuuzungumza Muungano katika ngazi za kimataifa ili uonekane ni muungano wa kweli na sio huu wa kulindana hata ikifikia hapo basi nitafarijika kwani itabidi tuheshimiane kikweli la wakiteleza kidogo tu tumemewawacha mkono.

maelezo yako marefu sana ,na kama ungeyatia busara nadhani yangeeleweka,sijui unamjua ni nani alovuka bahari kwenda kuomba muungano kwa mwenziwe? na kabla ya huo muungano sijui unamjua ni nani alikuwa na maendeleo kuliko mwenziwe? ni vyema tukatafuta suluhu ya huu muungano kwa maana wengi wa raia hatukubaliani nao katika namna uliokuwepo sasa. ila kumbuka kwamba jazba haiwezi kutuletea suluhu, ningekuomba upunguze ghadhabu ili tukae chini na kwa pamoja tufikirie nini cha kufanya? ikibidi ,tuishinikize serikali ili ilete kura ya maoni, na hapo ndio uje utoe jazba zako kwenye kura.
tusinyoosheaneni vidole sisi raia na kutukanana kwani waasisi wa huu muungano waliuasisi kwa kutumia vyeo vyao bila kujali demokrasia, muda upo,uwezo upo,ujasiri tunao,hoja tunazo. ni juu yetu kuamka na kuanza kudai moja kati ya mawili , ama muungano utakaoridhiwa na raia wa pande zote mbili au kama haiwezekani basi tugawane mbao.mungu atusaidie. amiin
 
Du- kaazi kweli kweli!
Inabidi tukatize maneno,maana ukiondoka kwa mwendo wa pole utaambiwa mgonjwa,hivi hii Tanganyika itakufa ,umoja wetu na utulivu wetu unatokana na muungano na hawa waZanzibar ,hawa wanaong'ang'ania watuwekee wazi jambo hili ,nchi yetu ni tulivu na ya amani tokea hatujapata uhuru na uhuru haukudaiwa kwa mapanga na kupinduana ,hayo hayapo hapa kwetu wala waliogembea na kuutafuta uhuru wa Tanganyika hawakuupata kwa kupoteza roho kama huko Zanzibar naamini sisi ni watu tofauti kabisa na wao kwa wao wameuana ndugu kwa ndugu na mpaka leo wanatoana roho wao kwa wao ,na bado wanatubebesha mzigo wa mauaji hayo sisi, huko kutoana roho bado wanasema sisi ndio wahusika wakubwa ,kama tulipeleka ndugu zetu kuwakomboa wao basi wamegeuza kibao na kusema tumekwenda kuwamaliza,mbona South Afrika tunaheshimika,mbona Msumbiji tunaheshima nasema haya kwa uhakika kabisa Mtanganyika au Mtanzania anaheshimika sana ,kama South afrika nilipokewa kama mkombozi na si kwangu waTanzania wengi wakienda huko walikuwa wanalakiwa na kufurahiwa ,wanathamini mchango wetu ambao ni roho zilizokuweko mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa nchi zao ( South Afrika,Angola,msumbiji Namibia) hizo zote zinatuthamini sana sana na wanatuona kama mashujaa na cha kutulipa hawana zaidi ya kutufariji na kutuweka katika mstari wa mbele kwa heshima zote lakini hawa ,hata sijui niwaiteje wamegeuka na kutuona ni maadui wakubwa wa nchi yao eti tunataka kuimeza ,jamani kwa jambo gani kubwa walilonalo watu hawa mbona mmekuwa wagumu wa kujibu hapa,Utanganyika hautakufa wala amani na utulivu tulio nao hautapotea ikiwa thamani yetu imekwisha leo hii wameanza kusimama na kutembea sasa wanatoa kiburi.
Mwalimu Nyerere hakukosea aliposema kama angelikuwa na uwezo angevifungasha visiwa hivi na kuenda kuvitupa au kuviweka mbaaali na Tanganyika ,maana alikwisha viona havina shukurani.
 
maelezo yako marefu sana ,na kama ungeyatia busara nadhani yangeeleweka,sijui unamjua ni nani alovuka bahari kwenda kuomba muungano kwa mwenziwe? na kabla ya huo muungano sijui unamjua ni nani alikuwa na maendeleo kuliko mwenziwe? ni vyema tukatafuta suluhu ya huu muungano kwa maana wengi wa raia hatukubaliani nao katika namna uliokuwepo sasa. ila kumbuka kwamba jazba haiwezi kutuletea suluhu, ningekuomba upunguze ghadhabu ili tukae chini na kwa pamoja tufikirie nini cha kufanya? ikibidi ,tuishinikize serikali ili ilete kura ya maoni, na hapo ndio uje utoe jazba zako kwenye kura.
tusinyoosheaneni vidole sisi raia na kutukanana kwani waasisi wa huu muungano waliuasisi kwa kutumia vyeo vyao bila kujali demokrasia, muda upo,uwezo upo,ujasiri tunao,hoja tunazo. ni juu yetu kuamka na kuanza kudai moja kati ya mawili , ama muungano utakaoridhiwa na raia wa pande zote mbili au kama haiwezekani basi tugawane mbao.mungu atusaidie. amiin

Under age,
Hivi je kila jambo linahitaji kura ya maoni? Hivi kura ya maoni ikifanyika- Zbar wakasema wnataka huwa wenyewe- wakati international water boundary is less than 200 km kati ya nchi hizi mbili je itakuwaje? Kwani fursa gani watu wa Tanzania wamekosa kutokana na huu Muungano kwa sasa ndugu yangu?
 
mimi ninafikiri kuwa muungano una faida sana kwa pande zote mbili lakini kinachokosekana ni umakini katika kuyaendeleza yale yaliyoafikiwa wakati wa kuunda huo muungano wenyewe.la msingi na la maana ni kwa viongozi waliohusika kutilia mkazo yale ambayo yana faida kwa pindi zote mbili
 
Unafikiri !!!Yaani nakushangaa sana tokea 1964,bado Mtanganyika au Mtanzania anafikiri juu ya faida za Muungano huu,unasema kuyaendeleza yale yalioafikiwa kama wewe uko na yale yalioafikiwa Wazanzibari wanasema hayo mambo sasa yako mia moja,kama haitoshi wanasema tumeyachomeka kinyemela nyemela,kwa nia ya kuwameza,jamani hivi hii lugha naifahamu mimi peke yangu mbona naona kama nazungumza na watu wageni wasionifahamu kabikabisa ,wanaziita kero lakini hakuna kero bali watanganyika tunanyanyaswa,na huna sehemu utazungumza na mtu wa Zanzibar akasema una faida zaidi utamsikia akisema mnatutawala kwa nguvu,tokea 1964 kama kungekuwepo na faida leo hii tungelikuwa na wajukuu na vitukuu yaani hata nchi nyengine zingelitamani kujiunga,lakini wanaotaka kujiunga wakisikiliza pande mbili za Muungano upande mmoja unasema unataka kumezwa,uchumi wake umeuliwa ,wabara wanapelekwa na serikali kila inapokwenda meli,waZanbar hawafikiri kabisa wala hawauoni ukubwa wa Tanganyika hata ikafika raia kukosa pa kulima au sehemu ya kujenga kijumba na kuenda au kupelekwa Zanzibar,mimi hapa sipaelewi kabisa na ndio nakataa huu muungano,hivi walitegemea Muungano uweje,andikeni hapa na kutoa faida tokea 1964 kama bado tunajenga ni mjengo gani huo wa muungano,Leo hii kuna shirikisho la ulaya,hivi ni nani asiefahamu hilo shirikisho halijafika hata miaka 30,wananchi wa shirikisho hilo wanatembea kusini na mashariki ya shirikisho lao hakuna anaeambiwa anakwenda uchi,wala husikii kama kuna upande fulani unataka kuimeza sehemu fulani,wenye shida na wenye raha huenda waendako,hapa Tanzania ndio kwanza juzi na jana wameweka kando passport na bado waZanzibar wanadai zirudishwe ukienda Zanzibar wanataka lazima hati za usafiri,hivi mnayaona na kuyasikia haya.
 
Under age,
Hivi je kila jambo linahitaji kura ya maoni? Hivi kura ya maoni ikifanyika- Zbar wakasema wnataka huwa wenyewe- wakati international water boundary is less than 200 km kati ya nchi hizi mbili je itakuwaje? Kwani fursa gani watu wa Tanzania wamekosa kutokana na huu Muungano kwa sasa ndugu yangu?
mzalendo.
tukizingatia umbali basi nadhani kila nchi itabidi iungane na nchi jirani kwani mpaka wa nchi moja ndio mwanzo wa nchi nyengine.fursa walioikosa watanzania ya kwanza ni kutokushirikishwa katika uasisi wa muungano huu na pia kuamuliwa ghafla bila kupita demokrasia halisi,pia raia tunapohoji waraka wa muungano huu hasa ule waraka asili basi tunazungushwa na hatimae wananchi tunabaki hatujui tumeungana katika vipengele gani. na ndio utaona mpaka leo wengine wanatuambia vipengele 10 wengine 12 almuradi hatuelewani.si tatizo kuwa na muungano lakini muungano wetu ni wachache sana wanaouelewa unavyopelekwa.kama kuna kura ya maoni leo basi ningechagua tuwe na serikali tatu.pia usisahau kwamba "mtafaruku wa utamaduni" unachangia katika hizi kelele za raia hivyo nadhani serikali tatu zitasuluhisha mtafaruku huu ambao yule anaejihisi mtanganyika atapata haki yake ya kutambulika kama mtanganyika na kadhalika mzanzibari (japo jambo hili ni wrong na halikubaliki lakini kwa vile lipo katika jamii lazima tulizingatie).msimamo wangu mimi sijali uzawa wangu wala kabila ila namjali yoyote muadilifu,kwani naamini siku nitakayokufa sijui atanizika nani, huenda mzanzibari mwenzangu akanisusia na mtanganyika pia na nikazikwa na mburundi.hivyo napenda kujudge individually rather than generally.
 
Hapa tatizo watu wanashindwa kuwa wazi. hili suala la muungano ukiliangalia kwa undani lina mushkeli kwa sababu ninaamini wazanzibari si wajinga kulalamika kwamba tunawameza. Siwezi kueleza kwa undani hapa lakini kuna document nyingi tu unaweza kupata ambazo zinaweza kukupa mwanga mzuri kuhusu hii ishu. This issue was done for political reasons rather than economic ones ndiyo maana wazanzibari hawalalamiki kwamba tunawameza kiuchumi bali siasa yao inakufa kwa namna moja au nyingine ukizingatia historia ya zanzibar, dini na utamaduni wake.
 
Under age,
Hivi je kila jambo linahitaji kura ya maoni? Hivi kura ya maoni ikifanyika- Zbar wakasema wnataka huwa wenyewe- wakati international water boundary is less than 200 km kati ya nchi hizi mbili je itakuwaje? Kwani fursa gani watu wa Tanzania wamekosa kutokana na huu Muungano kwa sasa ndugu yangu?
Si kila jambo linahitaji kura ya maoni lakini kila jambo linalohusu maslahi ya wananchi linahitaji uwazi. kwa nini hatuelezwi kwa uwazi ni kitu gani kinahusika na muungano na kipi hakihusiki. Jiulize?
 
wenye njozi ya kuona wazanzibari wanagawika wanaota tena sana.

waunguja na wapemba ni ndugu wadamu tokea azali. karibu kila muunguja ni mpemba na kila mpemba ni muunguja. ila wale waliotikea sehemu kuja unguja kwa mwenge.

wazanzibari wameeleza nn wanachohitaji mara nyingi tu, na ndio maana kuna kamati ya kushughulikia kero za muungano baina yetu. huku ikiongozwa na mh Shamsi na huku Mh Lowassa.

sasa wenye kuumwa na roho waendelee kuumwa. na wanalo hilo limewaganda
 
Hilo ni lao na watajiju,halafu Wazanzibar hawatosheki kabisa na kale kanchi chao,wakereketwa wa Zanzibar husikika wakisema hata Mombasa ni yao tena Kenya ilipewa ile nchi kwa Mkataba wa miaka eti pia wanao kama haitoshi utawasikia wakidai hii mikoa inayopakana na pwani ya Tanganika ni sehemu ya Zanzibar.Yaani mnaleta mabo ya zamani kabisa Mwalimu Nyerere hakukosea aliposema kama angekuwa na uwezo angelivitupa visiwa hivi mbaali saaana na Tanganyika.wanasema eti Zanzibar itambulike kama nchi,watu wana Raisi mawaziri kibao na wabungewanaowaita wawakilishi lakini hao viongozi wao kutwa wapo hapa kulalamika sasa kwa nini rais wao mawaziri wao hawahangaiki kama hawa wa Tanganyika tunamuona Muungwana kila siku hukata tiketi na kutokomea kusiko julikana kuitafutia chakula Tanganyika ila Raisi wao wa Zanzibar anakuja kudusa hapa kwetu kwa nini yeye na mawaziri wake hawaendi kujitafutia riziki kwengineko,sijawasikia kusafiri zaidi ya kufika Daresalam ,siku za kuwakumuta mikono mnapokuja kudusa Tanganyika zinakaribia.
 
Ustadhi Mwiba bwana.....iwapi ile picha yako ya Marehemu Julius ktk ujana wake akiwa na kibandiko(baraghashia)?.....huo muungano ni time bomb ambalo linaweza lisilipuke!!. Ningelikuwa mie mtawala wa Tanganyika ningewaacha Wazanzibara waelee na kutokomea zao ktk bahari ya Hindi.....hamna lolote la maana toka visiwa vile masikini zaidi ya "uswahili," uzembe na uvivu ulokithiri!!. Yes, I said it.
 
ipalilieni chuki iko siku mtajuta
 
Makubwa haya!!! Sie tulidhani unakuja kuzima moto, kumbe wewe ndio kwanza unamwaga peteroli!!!mie yangu macho!!
 
Ustadhi Mwiba bwana.....iwapi ile picha yako ya Marehemu Julius ktk ujana wake akiwa na kibandiko(baraghashia)?.....huo muungano ni time bomb ambalo linaweza lisilipuke!!. Ningelikuwa mie mtawala wa Tanganyika ningewaacha Wazanzibara waelee na kutokomea zao ktk bahari ya Hindi.....hamna lolote la maana toka visiwa vile masikini zaidi ya "uswahili," uzembe na uvivu ulokithiri!!. Yes, I said it.

Ndio umesema lakini bado ujaonyesha kwanini muungano haufai. Mpaka sasa Tanganyika imepoteza sehemu kubwa sana ya mapato yake kwa matumizi ya kijeshi kuliko matumizi ya kujiendeleza na kung'ang'ania itikadi za kipumbavu.

Mimi ni mtanganyika niliyebahatika kutembelea mikoa mingi ya Tanzania. Mikoa kama ya Kagera, Kilimanjaro, Mikoa ya Pwani ambayo walitegemea sana mazao ya kudumu kama vile mikahawa, minazi, mikorosho na mazao mengine hawana mazoea ya kufanya kazi za mitulinga.

Shule niliyosoma ilikuwa inachukua wanafunzi kutoka Kagera Mwanza,Shinyanga na Mara. Katika kazi za nje; wanafunzi 20 wa kutoka Shinyanga au Mwanza waliweza kushindana na trekta. Na wale wa Kagera ilikuwa inawachukua wiki nzima kumaliza kipande kidogo. Pamoja na juhudi kubwa za watu wa kutoka Mikoa ya Mwanza na Shinyanga vipande vyao vya kazi vilihitaji kupaliliwa mara kwa mara. Na vipande vya watu wa Kagera havikuhitaji palizi yoyote.

Tofauti hii ni kuwa watu wa Kagera wanafanya kazi katika Mashamba ya Mikahawa na Migomba. Kazi hii sio ngumu lakini inabidi ufanye kila siku na kwa uangalizi mkubwa. Watu wa Mwanza na Shinyanga wanafanya kazi kwenye mashamba ya Pamba, mahindi au mpunga au tumbaku. Kazi za mashamba haya ni za msimu na za kutumia nguvu. Na sehemu kubwa ya watanzania inatoka katika jamii inayotumia kazi za mitulinga.

Vile vile shuleni tulikuwa na makabila ya wafugaji ng'ombe ambao walipata taabu sana katika kazi za mashambani.

Wazanzibar sio wavivu kwa sababu kazi mitulinga hazihitajiki katika mazingira yao. Hali hiyo inaonekana kwa jamii zilizopo Tanganyika zenye kutegemea uchungaji au mazao ya kudumu.

Njia za kujipatia maisha ni tofauti. Na maisha ya wazanzibar hayategemei ruzuku kutoka Tanganyika.
 
1. Hizi hisia kuwa watu wa Zenj ni wavivu- sijui znatokana na nini! wanapenda kufanyabishara na kilimo- sema hawajozoea kazi za mituringa- na huu siyo uvivu! Halafu siku hizi akili kichwani- kazi za mitulinga sii mali tena.
Wapemba ndo so hard working- wanamiliki maduka makubwa Zenj na Kariakoo.
Kuna makabila mengi tu bara ya watu waswahili- wasiozea mituringa, kwa nini tusiwaongelee hawa! What is so special about Waunguja?

2. Mwanamarium I like your arguments- mara zote hakuna jazba- ingawaje kuna mengine siafikiani na wewe!
 
Ustadhi Mwiba bwana.....iwapi ile picha yako ya Marehemu Julius ktk ujana wake akiwa na kibandiko(baraghashia)?.....huo muungano ni time bomb ambalo linaweza lisilipuke!!. Ningelikuwa mie mtawala wa Tanganyika ningewaacha Wazanzibara waelee na kutokomea zao ktk bahari ya Hindi.....hamna lolote la maana toka visiwa vile masikini zaidi ya "uswahili," uzembe na uvivu ulokithiri!!. Yes, I said it.
Yuko mtu amepata kazi ya kuondoa picha ambazo naweka japo hajaniambia sababu inayokubalika zaidi ya kuwa kuna mtu tayari anatumia picha ya Mwalimu Nyerere,sioni sababu kwani picha niliyoiona inatumika ni tofauti na niliyoweka mimi na nikizidi kukandamiza picha hizi hazina hati miliki,lakini naona ni wastage of time kukaa na kubishana wakati amekamata mpini.
Mwana wamariyam usigeuze kibao,suali lilozika hapa ni kwa nini tunaendelea na huu Muungano,uliojaa matatizo kutoka upande wa pili yaani kutoka Zanzibar,maamuzi yote yanapitia Bungeni na wao ni washiriki kikamilifu kumbuka 2/3 ni wao hapo bungeni ili kufaulu kwa kupitisha muswada,sasa maamuzi yote yahusuyo Muungano yamekatiza hapo hivyo wao wamechangia ,inakuwaje leo hii wanapita vichochoroni na kusema muungano una matatizo,muungano umepandikizwa mambo kibao bila ya ridhaa yao,sasa kuhusu ile picha ya Mwalimu na kibalaghashiya kichwani ,watu hawakumfahamu bali ule ni mzigo ambao unawakilisha Zanzibar uliobebwa na Watanganyika ,sasa Mwalimu amefariki sioni sababu ya kubeba mzigo ule isipokuwa ziwepo sababu za msingi ambazo sijaziona tokea 1964 ,Watanganyika hatujafaidika na Muungano huu tusijidanganye,zaidi ya hasara na wazanzibari kutuita wauaji wamezaji wenda uchi.
 
Kama ningelikuwa Raisi wa Tanzania tayari ningelikwisha uvunja Muungano uliokuwepo wa Tanganyika na Zanzibar na kila mmoja akabeba mzigo wake mwenyewe.
Kipimo ninachokiona ni lawama kutoka kwa Wazanzibar ambao wanaona Watanganyika hutumika katika mauaji yanayotokea kila ufikapo wakati wa Uchaguzi Mkuu,na pia waZanzibar hawaeshi kulalamika kila siku kuwa wanabanwa wanamezwa,na Mawaziri wanapotembelea nchi za inje hukumbwa na masuala yanayowadhalilisha kuwa Serikali yao ni ya ukandamizaji na hpo huekewa caseti za kideo kujionea udhalilishaji na mauaji yanayofanywa na vikosi vilivyovaa nembo ya Muungano,kiasi cha mawaziri huwa hawana jibu muafaka kujibu tuhuma hizo ambazo zinaonyweshwa live mbele ya macho yao.
Nini Tanganyika itakosa ikiwa tutaachana na Muungano huu.
Naomba kuwasilisha hoja.

Haya na tuuvuje tuone mwananchi wa Nyakahaura--Biharamulo sijui atafaidika nini??? Haya na uendelee kuwepo, sijui mwananchi wa kiwira kule mbeya anafadika nini??
 
Yuko mtu amepata kazi ya kuondoa picha ambazo naweka japo hajaniambia sababu inayokubalika zaidi ya kuwa kuna mtu tayari anatumia picha ya Mwalimu Nyerere,sioni sababu kwani picha niliyoiona inatumika ni tofauti na niliyoweka mimi na nikizidi kukandamiza picha hizi hazina hati miliki,lakini naona ni wastage of time kukaa na kubishana wakati amekamata mpini.
Mwana wamariyam usigeuze kibao,suali lilozika hapa ni kwa nini tunaendelea na huu Muungano,uliojaa matatizo kutoka upande wa pili yaani kutoka Zanzibar,maamuzi yote yanapitia Bungeni na wao ni washiriki kikamilifu kumbuka 2/3 ni wao hapo bungeni ili kufaulu kwa kupitisha muswada,sasa maamuzi yote yahusuyo Muungano yamekatiza hapo hivyo wao wamechangia ,inakuwaje leo hii wanapita vichochoroni na kusema muungano una matatizo,muungano umepandikizwa mambo kibao bila ya ridhaa yao,sasa kuhusu ile picha ya Mwalimu na kibalaghashiya kichwani ,watu hawakumfahamu bali ule ni mzigo ambao unawakilisha Zanzibar uliobebwa na Watanganyika ,sasa Mwalimu amefariki sioni sababu ya kubeba mzigo ule isipokuwa ziwepo sababu za msingi ambazo sijaziona tokea 1964 ,Watanganyika hatujafaidika na Muungano huu tusijidanganye,zaidi ya hasara na wazanzibari kutuita wauaji wamezaji wenda uchi.

Hata hapa Marekani kuna watu wanataka Texas iwe nchi. Na wengine wanataka watu weusi wapewe sehemu yao na kuunda nchi. Ukienda UK, kuna watu wanaotaka Scotland iwe nchi kamili.

Nyerere, akiwa kiongozi alizikubali zawadi mbili kwa heshima kubwa fimbo na kofia. Ni mtu aliyejua Public Relatioship. Aliporudi kutoka masomoni na wazee kumtaka kuwaongoza, alikwenda mkutanoni akiwa na kaptula. Alijifunza na mikutano iliyofuatia akavaa kiheshima na watu wakampenda.

Kawaambie ndugu zako wamasai, wajaribu kujifunza na kwenda na wakati. Nguo na utamaduni wao ni muhimu wakiwa umasaaini. Nje ya umasaaini utamaduni wao hauna maana na ikiwezekana wajaribu mila na tamaduni za watu wengine.
 
mwiba, hebu jaribu kujenga picha ndani ya kichwa chako,piga picha kwamba muungano umevunjika na zanzibar ni kijisiwa kidogo chenye watu hawafiki hata milioni 2,kisiwa hiki kinapata uhuru wa kujiunga na mashirika ya misaada ya kimataifa na kinapata msaada 100% na sio 2.4,kisha pia kisiwa hicho kiwe na benki kuu yake na sarafu yake, kisiwa hicho kila mwezi kina uwezo wa kukusanya kodi isiopungua bilioni 4 ,likiwa kama ni pato la ndani tu.nadhani kwa mbaali utaona nini kitatokea. hivyo usidhani kwamba wazanzibari tutalala na njaa ukiuvunja huo muungano ,bali nadhani iko siku waingereza watakuja kuomba ukimbizi zenji(joke).zanzibar imebaniwa channel nyingi sana za kujiimarisha kutokana na huu muungano na hili jambo liko wazi.nikuulize suali. leo akitakiwa waziri wa afya tanzania kuiwakilisha tanzania katika WHO. je anaekwenda kule ni waziri wa kilimo wa zanzibar? au wa muungano ambae kwa lugha nyengine wa tanganyika ,kwani ukiangalia kijuujuu utaona tanganyika haina serikali ila ukiangalia kwa undani utaona kwamba tanganyika ina serikali iliobeba jina la serikali ya muungano.wazanzibari kulalamika kuhusu muungano huu wana haki tena kubwa hasa ukizingatia historia ya tulikotoka kiuchumi,kiutamaduni,kiuvumilivu na kadhalika.
 
Back
Top Bottom