Watanzania wenzangu nafikiri tuwe na mawanzo ya kujenga na sio kubomowa.Sikweli kama wengi mavyofikiria kuwa Zanzibar itashindwa kujiendeleza wenyewe bila kuitegema Bara. Zanzibar inaitegemea Bara kwa vile ndio inavyotakiwa iwe hivyo. Zanzibar wakati wa Abeid Karume ilikuwa mbali kimaendeleo kwa vile iliachiwa kujiendeleza haikubanwa kama sasa hivi. Hivi sasa wapo watu wasiotaka kuiona ikiendelea kama ilivyokuwa hapo mwanzo. Ni kuionea kwa maneno ya kejeli wakati haipewi nafasi inayostahiki.
Kwa wale wanaodhani kuwa Zanzibar haiwezi kuendelea na wajiulize ilikuwa vipi kabla ya kupata utegemezi wa Bara. Zanzibar itabaki kuwa sehemu ya muungano kwasababu tuliuungana cha kufanya ni kutatua kero zinzoeleweka wazi kwa nia ya ndugu mmoja juu ya ndugu mwenziwe. Tukumbuke Watanzania wenzangu hivi karibuni tu tuliungana sote kupinga shirikisho na nini zilikuwa sababu zetu?
WaTanganyika tupo huyu kidogo amejaribu ametoa joto na ukweli halisi upo katika maneno niliyoyakazia wino;-
Watanganyika tunaikandamiza bara tunauwa uchumi wao ndo wakapata sentensi hiyo.Hatutaki kuiona ikiendelea tunalitumia bunge kuweka mipaka ya kazi zao.Maamuzi yote wanayofanya inabidi yapate baraka zetu,wanasema tunawachagulia Raisi na ushahidi wanao,ukisoma kwa kina hiyo habari hapo juu utayaona yote.
Mimi sikubaliani na yote hayo aliyoyaandika kinachonipa moyo ni kuwa hawa wanataka kutubebesha hata uzembe wao,kila wanapokwama husema Bara ndio kikwazo,wanajidai kuutaka muungano ila kuna vijikero kidogo visawazishwe,hivi tuwaambie basi tufanyeni raisi mmoja kama hawajaluka !!!
Sasa someni gazeti hili ambalo nimeliweka na kulihifadhi kama baadhi ya ushahidi wa watu hawa..
0) Inawezekana kabisa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ni muungano wa pumbazo la kisiasa la kuharibu na kunyonya upande mmoja ambao ni Zanzibar
1) Zanzibar tunataka kuanzisha kampuni ya simu (ZANTEL) ambayo itatoa huduma Zanzibar bado nayo tunatiliwa ngumu eti TTCL itakosa mapato.
2)Zanzibar ni nchi yenye asilimia 99% ya Waislamu kati ya wananchi wote wa Zanzibar. Cha kushangaza serikali ya Jamhuri ya Muungano
imeizuia Zanzibar kujiunga na umoja wa nchi za Kiislamu (OIC) kwa sababu zisizoeleweka.
3)Zanzibar inashindwa kutetea nguvu za umeme wa kutumia taka kutoka Malaysia ambao ilitarajiwa kuwekeza hapa Zanzibar. Hii ni kutokana na
serikali ya Jamhuri ya Muungano kutounga mkono na shinikizo toka nje.
Zanzibar tunategemea umeme kutoka bara, hii ni kutufanya tuwe tegemezi katika nyanja muhimu ili tutawaliwe kisiasa na kiuchumi na ndivyo ilivyo. Sababu mojawapo ya kuzuia uwekezaji ule wa umeme wa taka ni kwmba eti TANESCO itakosa mapato kutoka Zanzibar
4)Kama kweli Tanzania ni muungano wa nchi mbili zenye Marais yaani Zanzibar na Tanganyika, mbona mgawanyo wa taasisi na vyuo vya elimu haupo sawa? Tanzania bara kwa mfano kuna vyuo vya biashara kama vile College of Business Education (CBE), DSA, Vyuo vya Ufundi, SIDO n.k. ambavyo vimetapakaa karibu mikoa yote ya bara na hakuna hata kimoja Zanzibar.
5)Sasa hivi tuna msuguano mwingine wa Zanzibar kuwa "Free Port" bado tunatiliwa ngumu na serikali ya Jamhuri eti serikali itakosa mapato, mapato gani hayo? Kama kweli Muungano wetu ni wa kheri kwanini tuvutane au tuwekeane ngumu kwa kuona wivu kuwa Zanzibar itanufaika.
Hitimisho lao:
Mlioliona kwa serikali ya Jamhuri kukosa mapato ni kwa Zanzibar kuwa "Free Port" tu? Vipi ndege za Kikristo zinaingia na kutoka Tanzania kwenye viwanja vyao bila kupekuliwa hamuoni kama serikali inakosa mapato? Mali inayoingizwa au kutolewa kwenye "Air Strips" za Wakristo kusiko na polisi wala Afisa "Custom" kwa ndege za Kikristo mnazijua? Ila Zanzibar tu kuwa "Free Port" huu ni udini ulio dhahiri.
Ili kujinasua na hali hii serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wazanzibari wote kwa ujumla bila kujali tofauti za kisiasa tushikamane ili tuweze kujitegemea katika njia zote kuu za uchumi na ulinzi. La sivyo, tukubali Zanzibari kuwa mkoa na siyo nchi yenye Rais.
Halafu anakuja mzanzibari hapa sijui hiki sijui kile wazandiki wakubwa,nyie mna lenu tu ,hizi ndizo faida tunazopata kwa Wazanzibar sijui wakienda nchi za nje wanazusha uzushi gani.