Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mimi sitaki tanganyika watusaidie lolote kwani tulipokuwa hatujaungana na tanganyika ,kumbukumbu iko wazi namna tulivyokuwa. hata kipofu au kiziwi anajua kwamba zanzibar imeuliwa na muungano. all i need ni fair union ya serikali tatu.tanganyika kivyao na zenji kivyao na serikali ya muungano kwa vipengele tutakavyokubaliana.ni very simple lakini sijui kwanini watanganyika hawalitaki hili. unapoona mtu anakataa kuwa na serikali yake basi BE AWARE kuna kitu kimejificha. lakini the day will come
Zanzibar ifidiwe na Tanzania na EAC kwa hasara za kiuchumi
Na Ally Saleh
Matukio mawili wiki hii yamenishitua sana kiasi cha kujenga mtizamo mpya katika suala zima la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuanzia sasa nimeamua fikra hiyo kuipigia debe.
Kama nitasikilizwa au nitapuuzwa, kama nitapata waungaji mkono au watu watakaoniona nimepotoka mimi sitajali kwa sababu imani yangu ni kuwa napaswa kuchukua hatua hiyo kutoa angalau wakia moja katika mchango wa kuiinua mizani ya Zanzibar, ambayo uzito wa upande wa pili umeielemea sana.
Kilichonifanya nije na mtizamo huu ambao ni mkali kidogo ni warsha ya siku moja niliyohudhuria ambapo wataalamu wa Afrika Mashariki kupitia Baraza la Biashara la Afrika Mashariki walikuja kuelezea jumuia ya wafanyabiashara juu ya mpango mpya ambao Tanzania imeingia chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mpango huo ni ule uuitwao Economic Partnership Agreement (EPA), mpango ambao unachukua nafasi ya utaratibu wa zamani uliokuwa umeleta pamoja nchi za Carribean, Pacific na Afrika kwa ajili ya kufanya biashara na Ulaya katika kile kinachoitwa Lome Convention.
Sababu ya pili iliyonichochea kuandika makala hii ni matamshi ya Waziri wa Mambo ya Muungano, Dk Hussein Mwinyi wakati akitoa majumuisho ya mambo ambayo yameshapatiwa ufumbuzi katika zile zinazoitwa kuwa ni kero za Muungano.
Wengi wetu tunajua kuwa moja ya kero kubwa, au kero ya msingi na suala zima linalohusu uchumi wan chi moja hii ndani ya mbili lakini pia mgawanyo wa fedha au misaada inayoletwa nchini kupitia utaratibu wa wafadhili iwe ni kwa kuunga mkono bajeti ( budget support) au hata kwa minajili mingineyo yoyote ile.
Kwa muda sasa mgawano wa fedha za wafadhili umekuwa kwa asilimia 4.5 kupelekwa Zanzibar ingawa utaratibu huo umeanza kutekelezwa kwa dhati miaka ya hivi karibuni tu, lakini niliumia pale nilipomsikia Dk Mwinyi akisema, " Suala hilo bado linajadiliwa maana wako wanaosema asilimia hiyo iongezwe na wako wanaosema ipunguzwe..."
Afanaleik Dk. Mwinyi! Suala la kusemwa kuwa asilimia hiyo ipunguzwe nalo pia ni hoja? Hoja kwa vipi ndugu yetu? Lakini kwa sasa tuachie hapo na nakuahidi msomaji wangu tutarudi tena katika hoja dhaifu ya Dk. Mwinyi, maana kwa mawazo yangu hiyo ni hoja yake mwenyewe, kwa kuwa siamini kama inaweza kutolewa na mtu mwingine.
Sasa hoja yangu ya leo ni kuwa wakati umefika kwa Zanzibar kudai fidia ya kupata hasara za kiuchumi au uchumi wake kudumaa kutokana na Tanzania kuingia katika mikataba ya kibiashara ambayo inaitia Zanzibar katika dhiki ya kiuchumi.
Na kwa hivyo wadaiwa wa fidia watakuwa ni Serikali ya Tanzania kwa hasara yote kabla ya kuundwa EAC na baada ya kuundwa EAC kwa kuingia makubaliano ya EPA.
Kama vile EAC inavyotakiwa kujua kuwa Zanzibar ina uchumi wake, bali pia tunajua kuwa nchi mbili hizi zina chumi mbili, mmoja mdogo lakini unaotarajiwa kusimama kwa miguu yake, lakini mwingine mkubwa ambao pamoja na ukubwa wake lakini bado unataka kumegewa kutoka upande wa uchumi mdogo.
Tunajua kuwa upande mmoja tu katika Muungano ndio unaopanga sera za fedha na matumizi (monetary and fiscal policies) na uchumi wa upande mmoja kulazimika kujibana ndani ya sera ambazo hauna sauti nazo na pengine ni miaka ya karibuni tu ndipo kumekuwa na mawasiliano kipindi cha kabla ya bajeti.
Wakati mmoja katika mwaka 1985, wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi na Waziri Kiongozi Seif Shariff Hamad bajeti nzima ya Zanzibar iliharibiwa kwa mambo yaliyopitishwa kwenye bajeti ya Serikali ya Muungano na palizuka kasheshe kubwa kwa Zanzibar kudai kufidiwa.
Tanzania imeingia katika soko la pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukubali sera ya Kodi Sifuri (Zero Tariff) katika wakati muafaka lakini wakati huo huo imeingia katika mpango wa EPA ambao unalenga kuwa na Kodi Sifuri pia kwa bidhaa zitokazo nje na kuingia Zanzibar.
Ingawa hilo litakuja kukamilika baada ya kipindi cha miaka, lakini wataalamu waliokuwapo katika kongomano la uhamasishaji walisema kuwa hilo halitaepukika kabisa na ni bora tu Wazanzibari wakajitayarisha kukosa kodi zitokanazo na bidhaa zinazoingia ndani.
Sasa suala kubwa linalokuja hapo ni vipi Zanzibar itaweza kupona bila ya kupata kodi zitokanazo na bidhaa ziingiazo kupitia bandari yake? Hapo ndipo, paliponichafua maana kulikuwa na jawabu nyingi za mkato mkato, si kutoka kwa washirika wetu kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini hata Watanzania wenzetu.
Mtu hapo atajiuliza kwa vipi Wakenya na Waganda wanahusika katika hili? Kuhusika kwao kunatokana na kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamezungumza kwa pamoja kama kundi la uchumi na kutia saini mkataba kwa pamoja chini ya huo mpango wa EPA ambao unatekeleza utandawazi katika uhalisi wake.Basi walipoulizwa vipi Zanzibar utapoiondoshea kodi za bandari na wakati haina ardhi, haina viwanda wala haina maliasili za kujivunia, jawabu iliyotoka ni kuwa lazima wapanie kujibadilisha ili wawe na viwanda vitavyoshindana kutoa bidhaa, wakuze eneo la kutoa huduma na waingie katika sekta ya intellectual property kwa nguvu zaidi.
Sasa hapo jamani ndio kimesemwa nini? Yaani Zanzibar ijitahidi kujenga viwanda ambavyo vitaweza kuingiza bidhaa Ulaya, iingie katika sekta ya huduma hadi makampuni yake kushindana Ulaya na ichukulie mfano wa karafuu na zao hili lisajiliwe kuwa la asili ya Zanzibar na kama litaongezwa thamani (any value adding) iwe ni mamlaka ya Zanzibar ndiyo ichukue uamuzi huo.
Kisha wataalamu wetu wakatutolea mifano wa nchi masikini za magharibi hapo nyuma kidogo Ureno, Uhispania na Uturuki zilivyoweza kujigeuza na mifano ya Ulaya ya Mashariki akina Romania, Czech na nyinginezo. Jamani wataalamu wetu, nchi hizo mnazifananishaje na Zanzibar , kwa lipi au kwa kipi? Kwa ardhi, kwa viwanda, kwa elimu au kwa taaluma? Hivi wataalamu wetu hawajui au hawataki kusema kuwa misaada na mipango mikubwa ilitekelezwa ili kupelekea mabadiliko katika nchi hizo, ambazo zilikuwa tayari zimelengwa kukaribishwa uanachama wa EU pana zaidi?
Hivi wataalamu wetu wanashindwa vipi kushauri kuwa uchumi wa Zanzibar lazima upate msukumo maalum? Kwamba Zanzibar isiwachwe kupigania rasilimali zile zile na kwa wafadhili wale wale ambao Tanzania inajipeleka mbele hata kwa mambo yasiyo ya Muungano lakini inavaa koti la Muungano?
Je, wataalamu wetu hawangeweza kushauri kuwa Bodi ya Mapato ya Tanzania (TRA) isikusanye kodi Zanzibar kwa miaka 10 ijayo ili fedha zinazoingia kupitia kodi ziunde mfuko maalum wa ujenzi wa Zanzibar ( Special Fund for Zanzibar Reconstruction) na fedha hizo zikawa ni sehemu ya fidia?
Au wataalamu wetu kuishauri Serikali ya Tanzania na halikadhalika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikawa na wazo kuu la kuifanya Zanzibar kuwa ni sehemu maalum na ya uchumi maalum (Special Economic Zone) kama vile China ilivyofanya kwa baadhi ya maeneo yake?
Professa Issa Shivji aliwahi kusema kuwa kama Tanzania ingetaka in'gare kiuchumi basi haikuwa na njia zaidi ya kuimarisha uchumi wa Zanzibar uwe ni dirisha lake la kuonyeshea mafanikio. Lakini hilo halikufanywa na hakuna nia ya kulifanya.
Serikali ya Muungano haijawahi kuwa na nia, wanaojua vyenginevyo wanisamehe, kuifanya Zanzibar kwa vitendo kuwa ni dirisha la kuonyesha mafanikio. Sio vitu vya kushitukiza na kimoja kukitekeleza leo na kingine mtondogoo.
Ndipo nikasema nimekereka sana na maneno ya Dk Mwinyi aliyesema ati, kuna hoja ya kutaka kuijadili asilimia 4.5 ambayo inapata Zanzibar kama gawio la misaada na hisa za Benki Kuu. Itakuwa vipi hoja iwe kiwango hicho kipunguzwe? Ikiwa hoja ni kuwa hiyo 4.5% Zanzibar haistahili kupata, kwani kuna lipi lilobadilika na je Zanzibar imekuwa ndogo zaidi na imekuwa na mahitaji madogo zaidi?
Hoja yangu kwa leo ni kuwa Serikali ya Muungano inafanya maamuzi kwa niaba ya Zanzibar na maamuzi mengine ambayo yanaathari kubwa ya kiuchumi kwa Zanzibar. Na Zanzibar hiyo hiyo inatarajiwa ishindane kiuchumi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Fikra zangu ni kuwa Zanzibar ifidiwe na Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki au kwa maneno mengine taasisi hizo mbili ziwe na mipango maalumu ya kuisaidia Zanzibar.
Kama nchi za visiwa zitazama kwa kuongezeka joto duniani na kina cha maji kuongezeka, basi Zanzibar itazama mapema kwa kitanzi cha kiuchumi, ikiwa mfumo wa ?Kodi Sifuri? utatekelezwa bila ya Zanzibar kutayarishwa.
+255 777 4300 22
www.eternaltourszanzibar.net
jumbamaro.blogspot.com
Mtu wa Pwani,
Baraza la Wawakilishi na Wabunge ni mzigo mkubwa sana kwa wananchi wa Zanzibar.
Hivi mkipunguza nusu ya hao mtakuwa mme-save kiasi gani?
Uchumi mnao ila mnaukalia.
Suala lingine ni vizuri mkaanzisha viwanda. Hii import export haitawasaidia in a long run.
Mtu wa Pwani,
Baraza la Wawakilishi na Wabunge ni mzigo mkubwa sana kwa wananchi wa Zanzibar.
Hivi mkipunguza nusu ya hao mtakuwa mme-save kiasi gani?
Uchumi mnao ila mnaukalia.
Suala lingine ni vizuri mkaanzisha viwanda. Hii import export haitawasaidia in a long run.
tutasikia mapya kila siku, na kila linalokuja linaizamisha zanzibar,kina mtu wa pwani, side ,engineer na wazanzibari wengine, nadhani pamoja na kwamba tunaandika hapa lakini kuandika kutupu hakutoshi, ni vyema tungeamua kujitolea kwa njia moja au nyengine kuwaamsha wazanzibari kwa vitendo ili waungane na wawe kitu kimoja(tuwasiliane nao na tuwadarisishe umuhimu wa kuungana kwetu). cuf na ccm watangulize uzalendo mbele kabla ya sera za vyama. mara nyingi hii ccm kumuona cuf adui au cuf kumuona ccm adui ndiyo inayowapa mwanya hawa wasioipendea mema zanzibar kutoa maamuzi kama haya. na pia wale watanzania bara wanaopendelea kuiona zanzibar inaendelea basi tutashukuru sana mkaungana nasi katika huu mchakato.
naamini tutashinda .its just a matter of time.
SiDE,
ktk chaguzi zile za kabla ya Mapinduzi ya 1964 viti vya Bunge la Zenj vilikuwa havifiki 30. Sasa kulikoni leo hii kuwe na wawakilishi, na juu yake wabunge zaidi ya 100?
Halafu hao wawakilishi na wabunge wanalipwa mshahara,posho,na marupurupu kiasi gani? hiyo ni gharama kubwa mno kwa nchi ndogo kama Zenj. huo ndiyo "MZIGO" ninaozungumzia.
suala lingine ni vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali ya Mapinduzi. what is KMKM and JKU for? tayari ktk Muungano kuna JWTZ na Polisi.
Ukipunguza viti vya wabunge na wawakilishi, na hivyo vyombo vya ulinzi, SMZ itabakiwa na fedha za ziada kusaidia maendeleo ya wananchi.
Waswahili wanasema, KUPANGA NI KUCHAGUA.
napenda watu kama wewe unaeonesha true colour yako kwani kuna wengine hasa wanasiasa, wanaojifanya wanaipendelea mema zanzibar kumbe mioyo imejaa unafiki.na kama kuikumbatia ccm ni unafiki basi nadhani tanganyika ndio mama wa wanafiki ,maana ccm hushinda bila upinzani katika chaguzi za rais.angalau huku zanzibar wanaoikumbatia na wasioikumbatia wako karibu idadi sawa.JK tatizo sio wawakilishi au vingenevyo, tatizo ni ubinafsi wa viongozi na watawala wetu. There is enough for every body in Tanzania ila wachache wanazidi kuhodhi kwa manufaa yao.
Nasema tena, mpaka wananchi tutakapozinduka na kuona uzandiki wa watawala wa CCM tutazidi kuumia. na kwa kuwa tumeamua kuikumbatia CCM basi hatuna budi kulipa gharama inayostahili AMBAYO NDO HUU UMASKINI TUNAOLIA NAO KILA SIKU. Kwa hiyo tusilalamike. Kuhusu Zanzibar mimi siwahurumii hawa jamaa kwa sababu na wao ni wanafiki wanaikumbatia CCM na sera zake kwa sababu wachache wananufaika! Nchi ya watu million moja inakosa hata aspirin, harafu unaniambia hiyo ni akili au ni tope? Let them suffer, wakizinduka-as all Tanzanians, then we shall move forward. For now we are enjoying the consequences of our choices!
Noel Njema!
ni mawazo mazuri kwa serikali inayokubali kupokea mawazo.thankz bigisnake (jokakuu)SiDE,
ktk chaguzi zile za kabla ya Mapinduzi ya 1964 viti vya Bunge la Zenj vilikuwa havifiki 30. Sasa kulikoni leo hii kuwe na wawakilishi, na juu yake wabunge zaidi ya 100?
Halafu hao wawakilishi na wabunge wanalipwa mshahara,posho,na marupurupu kiasi gani? hiyo ni gharama kubwa mno kwa nchi ndogo kama Zenj. huo ndiyo "MZIGO" ninaozungumzia.
suala lingine ni vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali ya Mapinduzi. what is KMKM and JKU for? tayari ktk Muungano kuna JWTZ na Polisi.
Ukipunguza viti vya wabunge na wawakilishi, na hivyo vyombo vya ulinzi, SMZ itabakiwa na fedha za ziada kusaidia maendeleo ya wananchi.
Waswahili wanasema, KUPANGA NI KUCHAGUA.