Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Zanzibar iwe mikoa/mkoa! i think it is more better to live them alone.
 
Kama sijakosea, Ndugu Shamhuna alishawahi kukaririwa na vyombo vya habari mwaka jana akisema suala la mafuta si la muungano, hadi wanasisiemu wenzake wakamshangaa. Kama haitoshi, naye Nahodha akapigilia msumari wa moto katika jeraha hili kwa kusema suala la mafuta Zanzibar ni nyeti, na sirikali ya muungano isiliingilie.
Sasa nasikia hili la madini tena, kwamba wanataka mrahaba toka bara! Yaani nachanganyikiwa kabisa.
 
mimi sitaki tanganyika watusaidie lolote kwani tulipokuwa hatujaungana na tanganyika ,kumbukumbu iko wazi namna tulivyokuwa. hata kipofu au kiziwi anajua kwamba zanzibar imeuliwa na muungano. all i need ni fair union ya serikali tatu.tanganyika kivyao na zenji kivyao na serikali ya muungano kwa vipengele tutakavyokubaliana.ni very simple lakini sijui kwanini watanganyika hawalitaki hili. unapoona mtu anakataa kuwa na serikali yake basi BE AWARE kuna kitu kimejificha. lakini the day will come
 
Labda ungefafanua kuwa ni kitu gani unahisi kimefichika hapa, kwani hapa JF huwa tunajadili mambo waziwazi.
Be there man!
 
Zanzibar ifidiwe na Tanzania na EAC kwa hasara za kiuchumi
Na Ally Saleh

Matukio mawili wiki hii yamenishitua sana kiasi cha kujenga mtizamo mpya katika suala zima la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuanzia sasa nimeamua fikra hiyo kuipigia debe.

Kama nitasikilizwa au nitapuuzwa, kama nitapata waungaji mkono au watu watakaoniona nimepotoka mimi sitajali kwa sababu imani yangu ni kuwa napaswa kuchukua hatua hiyo kutoa angalau wakia moja katika mchango wa kuiinua mizani ya Zanzibar, ambayo uzito wa upande wa pili umeielemea sana.

Kilichonifanya nije na mtizamo huu ambao ni mkali kidogo ni warsha ya siku moja niliyohudhuria ambapo wataalamu wa Afrika Mashariki kupitia Baraza la Biashara la Afrika Mashariki walikuja kuelezea jumuia ya wafanyabiashara juu ya mpango mpya ambao Tanzania imeingia chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mpango huo ni ule uuitwao Economic Partnership Agreement (EPA), mpango ambao unachukua nafasi ya utaratibu wa zamani uliokuwa umeleta pamoja nchi za Carribean, Pacific na Afrika kwa ajili ya kufanya biashara na Ulaya katika kile kinachoitwa Lome Convention.

Sababu ya pili iliyonichochea kuandika makala hii ni matamshi ya Waziri wa Mambo ya Muungano, Dk Hussein Mwinyi wakati akitoa majumuisho ya mambo ambayo yameshapatiwa ufumbuzi katika zile zinazoitwa kuwa ni kero za Muungano.

Wengi wetu tunajua kuwa moja ya kero kubwa, au kero ya msingi na suala zima linalohusu uchumi wan chi moja hii ndani ya mbili lakini pia mgawanyo wa fedha au misaada inayoletwa nchini kupitia utaratibu wa wafadhili iwe ni kwa kuunga mkono bajeti ( budget support) au hata kwa minajili mingineyo yoyote ile.

Kwa muda sasa mgawano wa fedha za wafadhili umekuwa kwa asilimia 4.5 kupelekwa Zanzibar ingawa utaratibu huo umeanza kutekelezwa kwa dhati miaka ya hivi karibuni tu, lakini niliumia pale nilipomsikia Dk Mwinyi akisema, " Suala hilo bado linajadiliwa maana wako wanaosema asilimia hiyo iongezwe na wako wanaosema ipunguzwe..."

Afanaleik Dk. Mwinyi! Suala la kusemwa kuwa asilimia hiyo ipunguzwe nalo pia ni hoja? Hoja kwa vipi ndugu yetu? Lakini kwa sasa tuachie hapo na nakuahidi msomaji wangu tutarudi tena katika hoja dhaifu ya Dk. Mwinyi, maana kwa mawazo yangu hiyo ni hoja yake mwenyewe, kwa kuwa siamini kama inaweza kutolewa na mtu mwingine.

Sasa hoja yangu ya leo ni kuwa wakati umefika kwa Zanzibar kudai fidia ya kupata hasara za kiuchumi au uchumi wake kudumaa kutokana na Tanzania kuingia katika mikataba ya kibiashara ambayo inaitia Zanzibar katika dhiki ya kiuchumi.

Na kwa hivyo wadaiwa wa fidia watakuwa ni Serikali ya Tanzania kwa hasara yote kabla ya kuundwa EAC na baada ya kuundwa EAC kwa kuingia makubaliano ya EPA.

Kama vile EAC inavyotakiwa kujua kuwa Zanzibar ina uchumi wake, bali pia tunajua kuwa nchi mbili hizi zina chumi mbili, mmoja mdogo lakini unaotarajiwa kusimama kwa miguu yake, lakini mwingine mkubwa ambao pamoja na ukubwa wake lakini bado unataka kumegewa kutoka upande wa uchumi mdogo.

Tunajua kuwa upande mmoja tu katika Muungano ndio unaopanga sera za fedha na matumizi (monetary and fiscal policies) na uchumi wa upande mmoja kulazimika kujibana ndani ya sera ambazo hauna sauti nazo na pengine ni miaka ya karibuni tu ndipo kumekuwa na mawasiliano kipindi cha kabla ya bajeti.

Wakati mmoja katika mwaka 1985, wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi na Waziri Kiongozi Seif Shariff Hamad bajeti nzima ya Zanzibar iliharibiwa kwa mambo yaliyopitishwa kwenye bajeti ya Serikali ya Muungano na palizuka kasheshe kubwa kwa Zanzibar kudai kufidiwa.

Tanzania imeingia katika soko la pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukubali sera ya Kodi Sifuri (Zero Tariff) katika wakati muafaka lakini wakati huo huo imeingia katika mpango wa EPA ambao unalenga kuwa na Kodi Sifuri pia kwa bidhaa zitokazo nje na kuingia Zanzibar.

Ingawa hilo litakuja kukamilika baada ya kipindi cha miaka, lakini wataalamu waliokuwapo katika kongomano la uhamasishaji walisema kuwa hilo halitaepukika kabisa na ni bora tu Wazanzibari wakajitayarisha kukosa kodi zitokanazo na bidhaa zinazoingia ndani.

Sasa suala kubwa linalokuja hapo ni vipi Zanzibar itaweza kupona bila ya kupata kodi zitokanazo na bidhaa ziingiazo kupitia bandari yake? Hapo ndipo, paliponichafua maana kulikuwa na jawabu nyingi za mkato mkato, si kutoka kwa washirika wetu kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini hata Watanzania wenzetu.

Mtu hapo atajiuliza kwa vipi Wakenya na Waganda wanahusika katika hili? Kuhusika kwao kunatokana na kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamezungumza kwa pamoja kama kundi la uchumi na kutia saini mkataba kwa pamoja chini ya huo mpango wa EPA ambao unatekeleza utandawazi katika uhalisi wake.Basi walipoulizwa vipi Zanzibar utapoiondoshea kodi za bandari na wakati haina ardhi, haina viwanda wala haina maliasili za kujivunia, jawabu iliyotoka ni kuwa lazima wapanie kujibadilisha ili wawe na viwanda vitavyoshindana kutoa bidhaa, wakuze eneo la kutoa huduma na waingie katika sekta ya intellectual property kwa nguvu zaidi.

Sasa hapo jamani ndio kimesemwa nini? Yaani Zanzibar ijitahidi kujenga viwanda ambavyo vitaweza kuingiza bidhaa Ulaya, iingie katika sekta ya huduma hadi makampuni yake kushindana Ulaya na ichukulie mfano wa karafuu na zao hili lisajiliwe kuwa la asili ya Zanzibar na kama litaongezwa thamani (any value adding) iwe ni mamlaka ya Zanzibar ndiyo ichukue uamuzi huo.

Kisha wataalamu wetu wakatutolea mifano wa nchi masikini za magharibi hapo nyuma kidogo Ureno, Uhispania na Uturuki zilivyoweza kujigeuza na mifano ya Ulaya ya Mashariki akina Romania, Czech na nyinginezo. Jamani wataalamu wetu, nchi hizo mnazifananishaje na Zanzibar , kwa lipi au kwa kipi? Kwa ardhi, kwa viwanda, kwa elimu au kwa taaluma? Hivi wataalamu wetu hawajui au hawataki kusema kuwa misaada na mipango mikubwa ilitekelezwa ili kupelekea mabadiliko katika nchi hizo, ambazo zilikuwa tayari zimelengwa kukaribishwa uanachama wa EU pana zaidi?

Hivi wataalamu wetu wanashindwa vipi kushauri kuwa uchumi wa Zanzibar lazima upate msukumo maalum? Kwamba Zanzibar isiwachwe kupigania rasilimali zile zile na kwa wafadhili wale wale ambao Tanzania inajipeleka mbele hata kwa mambo yasiyo ya Muungano lakini inavaa koti la Muungano?

Je, wataalamu wetu hawangeweza kushauri kuwa Bodi ya Mapato ya Tanzania (TRA) isikusanye kodi Zanzibar kwa miaka 10 ijayo ili fedha zinazoingia kupitia kodi ziunde mfuko maalum wa ujenzi wa Zanzibar ( Special Fund for Zanzibar Reconstruction) na fedha hizo zikawa ni sehemu ya fidia?
Au wataalamu wetu kuishauri Serikali ya Tanzania na halikadhalika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikawa na wazo kuu la kuifanya Zanzibar kuwa ni sehemu maalum na ya uchumi maalum (Special Economic Zone) kama vile China ilivyofanya kwa baadhi ya maeneo yake?
Professa Issa Shivji aliwahi kusema kuwa kama Tanzania ingetaka in'gare kiuchumi basi haikuwa na njia zaidi ya kuimarisha uchumi wa Zanzibar uwe ni dirisha lake la kuonyeshea mafanikio. Lakini hilo halikufanywa na hakuna nia ya kulifanya.
Serikali ya Muungano haijawahi kuwa na nia, wanaojua vyenginevyo wanisamehe, kuifanya Zanzibar kwa vitendo kuwa ni dirisha la kuonyesha mafanikio. Sio vitu vya kushitukiza na kimoja kukitekeleza leo na kingine mtondogoo.
Ndipo nikasema nimekereka sana na maneno ya Dk Mwinyi aliyesema ati, kuna hoja ya kutaka kuijadili asilimia 4.5 ambayo inapata Zanzibar kama gawio la misaada na hisa za Benki Kuu. Itakuwa vipi hoja iwe kiwango hicho kipunguzwe? Ikiwa hoja ni kuwa hiyo 4.5% Zanzibar haistahili kupata, kwani kuna lipi lilobadilika na je Zanzibar imekuwa ndogo zaidi na imekuwa na mahitaji madogo zaidi?

Hoja yangu kwa leo ni kuwa Serikali ya Muungano inafanya maamuzi kwa niaba ya Zanzibar na maamuzi mengine ambayo yanaathari kubwa ya kiuchumi kwa Zanzibar. Na Zanzibar hiyo hiyo inatarajiwa ishindane kiuchumi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Fikra zangu ni kuwa Zanzibar ifidiwe na Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki au kwa maneno mengine taasisi hizo mbili ziwe na mipango maalumu ya kuisaidia Zanzibar.

Kama nchi za visiwa zitazama kwa kuongezeka joto duniani na kina cha maji kuongezeka, basi Zanzibar itazama mapema kwa kitanzi cha kiuchumi, ikiwa mfumo wa ?Kodi Sifuri? utatekelezwa bila ya Zanzibar kutayarishwa.

+255 777 4300 22

www.eternaltourszanzibar.net

jumbamaro.blogspot.com
 
Wa pwani mwenzangu kwanza chukua zako tano kwa kutuwekea hii kitu, then kama ni kumkoma nyani basi huyu kakomaliwa hadharini, kweupeeeeeeeee.
Nawaachia wenye meno watafune kwanza, yangu mabovu.
A day will come
 
Mtu wa Pwani,
Nakupongeza kwa kuongea kwa uwazi ndugu yangu. Your comments are relevant.
1. Kwenye fidia- pesa itoka Bara au Kenya? May be tukihsakuwa na shirikisho- hata Burundi na Rwanda watasema wafidiwe kwa kuwa uchumi wao ni mdogo kama ilivyokuwa Ireland na Ureno.

2. Wapinzani akina Mbowe wanaongelea Majimbo- Kenya Raila akiwa raisi nao wanaelekea huko2- hata kwa bara kuna mikoa iko nyuma- kama Lindi, Kigoma, Pwani na Mtwara inabidi nayo ifidiwe. Swala ambalo nami linanipa shida- ni ipi nafasi ya Zbar ktk Majimbo?

3. Over 4.5%. Misaada. Mimi nina mtizamo tofauti- sijawahi ona nchi iliyoendelea kwa kutegemea misaada. Kitu kinachorudisha nyuma kifkra ni hili la kutegetemea ufadhili. O.k kama ni msaada then we must have a time frame- say 10 or 15 years! We just can not be dependent on msaada foever- iwe Bara, Zbar, Uganda n.k. Kenya sasa hawana budget support- je sii wanaende mbele?
 
Mzalendohalisi aliandika:
2. Wapinzani akina Mbowe wanaongelea Majimbo- Kenya Raila akiwa raisi nao wanaelekea huko2- hata kwa bara kuna mikoa iko nyuma- kama Lindi, Kigoma, Pwani na Mtwara inabidi nayo ifidiwe. Swala ambalo nami linanipa shida- ni ipi nafasi ya Zbar ktk Majimbo
Nakubaliana nawe ya kuwa majimbo ni sera ya CHAMA. Majimbo yatakuwepo Zanzibar ikiwa Chama chenye sera hiyo kitashinda uchaguzi wa Zanzibar na kuungwa mkono hoja hiyo na BARAZA LA WAWAKILISHI.
Majimbo hayatakuwepo Zanzibar ikiwa CHAMA chenye sera hiyo kitashinda uchaguzi wa MUUNGANO pekee.
Serikali ya Muungano haina mamlaka yoyote kupeleka MAJIMBO Zanzibar. Ikumbukwe ya kuwa Zanzibar ni nchi ndani ya Muungano, yenye mamlaka yake kiutawala.
Muungano au msuguano!
 
Zanzibar ifidiwe na Tanzania na EAC kwa hasara za kiuchumi
Na Ally Saleh

Matukio mawili wiki hii yamenishitua sana kiasi cha kujenga mtizamo mpya katika suala zima la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuanzia sasa nimeamua fikra hiyo kuipigia debe.

Kama nitasikilizwa au nitapuuzwa, kama nitapata waungaji mkono au watu watakaoniona nimepotoka mimi sitajali kwa sababu imani yangu ni kuwa napaswa kuchukua hatua hiyo kutoa angalau wakia moja katika mchango wa kuiinua mizani ya Zanzibar, ambayo uzito wa upande wa pili umeielemea sana.

Kilichonifanya nije na mtizamo huu ambao ni mkali kidogo ni warsha ya siku moja niliyohudhuria ambapo wataalamu wa Afrika Mashariki kupitia Baraza la Biashara la Afrika Mashariki walikuja kuelezea jumuia ya wafanyabiashara juu ya mpango mpya ambao Tanzania imeingia chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mpango huo ni ule uuitwao Economic Partnership Agreement (EPA), mpango ambao unachukua nafasi ya utaratibu wa zamani uliokuwa umeleta pamoja nchi za Carribean, Pacific na Afrika kwa ajili ya kufanya biashara na Ulaya katika kile kinachoitwa Lome Convention.

Sababu ya pili iliyonichochea kuandika makala hii ni matamshi ya Waziri wa Mambo ya Muungano, Dk Hussein Mwinyi wakati akitoa majumuisho ya mambo ambayo yameshapatiwa ufumbuzi katika zile zinazoitwa kuwa ni kero za Muungano.

Wengi wetu tunajua kuwa moja ya kero kubwa, au kero ya msingi na suala zima linalohusu uchumi wan chi moja hii ndani ya mbili lakini pia mgawanyo wa fedha au misaada inayoletwa nchini kupitia utaratibu wa wafadhili iwe ni kwa kuunga mkono bajeti ( budget support) au hata kwa minajili mingineyo yoyote ile.

Kwa muda sasa mgawano wa fedha za wafadhili umekuwa kwa asilimia 4.5 kupelekwa Zanzibar ingawa utaratibu huo umeanza kutekelezwa kwa dhati miaka ya hivi karibuni tu, lakini niliumia pale nilipomsikia Dk Mwinyi akisema, " Suala hilo bado linajadiliwa maana wako wanaosema asilimia hiyo iongezwe na wako wanaosema ipunguzwe..."

Afanaleik Dk. Mwinyi! Suala la kusemwa kuwa asilimia hiyo ipunguzwe nalo pia ni hoja? Hoja kwa vipi ndugu yetu? Lakini kwa sasa tuachie hapo na nakuahidi msomaji wangu tutarudi tena katika hoja dhaifu ya Dk. Mwinyi, maana kwa mawazo yangu hiyo ni hoja yake mwenyewe, kwa kuwa siamini kama inaweza kutolewa na mtu mwingine.

Sasa hoja yangu ya leo ni kuwa wakati umefika kwa Zanzibar kudai fidia ya kupata hasara za kiuchumi au uchumi wake kudumaa kutokana na Tanzania kuingia katika mikataba ya kibiashara ambayo inaitia Zanzibar katika dhiki ya kiuchumi.

Na kwa hivyo wadaiwa wa fidia watakuwa ni Serikali ya Tanzania kwa hasara yote kabla ya kuundwa EAC na baada ya kuundwa EAC kwa kuingia makubaliano ya EPA.

Kama vile EAC inavyotakiwa kujua kuwa Zanzibar ina uchumi wake, bali pia tunajua kuwa nchi mbili hizi zina chumi mbili, mmoja mdogo lakini unaotarajiwa kusimama kwa miguu yake, lakini mwingine mkubwa ambao pamoja na ukubwa wake lakini bado unataka kumegewa kutoka upande wa uchumi mdogo.

Tunajua kuwa upande mmoja tu katika Muungano ndio unaopanga sera za fedha na matumizi (monetary and fiscal policies) na uchumi wa upande mmoja kulazimika kujibana ndani ya sera ambazo hauna sauti nazo na pengine ni miaka ya karibuni tu ndipo kumekuwa na mawasiliano kipindi cha kabla ya bajeti.

Wakati mmoja katika mwaka 1985, wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi na Waziri Kiongozi Seif Shariff Hamad bajeti nzima ya Zanzibar iliharibiwa kwa mambo yaliyopitishwa kwenye bajeti ya Serikali ya Muungano na palizuka kasheshe kubwa kwa Zanzibar kudai kufidiwa.

Tanzania imeingia katika soko la pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukubali sera ya Kodi Sifuri (Zero Tariff) katika wakati muafaka lakini wakati huo huo imeingia katika mpango wa EPA ambao unalenga kuwa na Kodi Sifuri pia kwa bidhaa zitokazo nje na kuingia Zanzibar.

Ingawa hilo litakuja kukamilika baada ya kipindi cha miaka, lakini wataalamu waliokuwapo katika kongomano la uhamasishaji walisema kuwa hilo halitaepukika kabisa na ni bora tu Wazanzibari wakajitayarisha kukosa kodi zitokanazo na bidhaa zinazoingia ndani.

Sasa suala kubwa linalokuja hapo ni vipi Zanzibar itaweza kupona bila ya kupata kodi zitokanazo na bidhaa ziingiazo kupitia bandari yake? Hapo ndipo, paliponichafua maana kulikuwa na jawabu nyingi za mkato mkato, si kutoka kwa washirika wetu kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini hata Watanzania wenzetu.

Mtu hapo atajiuliza kwa vipi Wakenya na Waganda wanahusika katika hili? Kuhusika kwao kunatokana na kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamezungumza kwa pamoja kama kundi la uchumi na kutia saini mkataba kwa pamoja chini ya huo mpango wa EPA ambao unatekeleza utandawazi katika uhalisi wake.Basi walipoulizwa vipi Zanzibar utapoiondoshea kodi za bandari na wakati haina ardhi, haina viwanda wala haina maliasili za kujivunia, jawabu iliyotoka ni kuwa lazima wapanie kujibadilisha ili wawe na viwanda vitavyoshindana kutoa bidhaa, wakuze eneo la kutoa huduma na waingie katika sekta ya intellectual property kwa nguvu zaidi.

Sasa hapo jamani ndio kimesemwa nini? Yaani Zanzibar ijitahidi kujenga viwanda ambavyo vitaweza kuingiza bidhaa Ulaya, iingie katika sekta ya huduma hadi makampuni yake kushindana Ulaya na ichukulie mfano wa karafuu na zao hili lisajiliwe kuwa la asili ya Zanzibar na kama litaongezwa thamani (any value adding) iwe ni mamlaka ya Zanzibar ndiyo ichukue uamuzi huo.

Kisha wataalamu wetu wakatutolea mifano wa nchi masikini za magharibi hapo nyuma kidogo Ureno, Uhispania na Uturuki zilivyoweza kujigeuza na mifano ya Ulaya ya Mashariki akina Romania, Czech na nyinginezo. Jamani wataalamu wetu, nchi hizo mnazifananishaje na Zanzibar , kwa lipi au kwa kipi? Kwa ardhi, kwa viwanda, kwa elimu au kwa taaluma? Hivi wataalamu wetu hawajui au hawataki kusema kuwa misaada na mipango mikubwa ilitekelezwa ili kupelekea mabadiliko katika nchi hizo, ambazo zilikuwa tayari zimelengwa kukaribishwa uanachama wa EU pana zaidi?

Hivi wataalamu wetu wanashindwa vipi kushauri kuwa uchumi wa Zanzibar lazima upate msukumo maalum? Kwamba Zanzibar isiwachwe kupigania rasilimali zile zile na kwa wafadhili wale wale ambao Tanzania inajipeleka mbele hata kwa mambo yasiyo ya Muungano lakini inavaa koti la Muungano?

Je, wataalamu wetu hawangeweza kushauri kuwa Bodi ya Mapato ya Tanzania (TRA) isikusanye kodi Zanzibar kwa miaka 10 ijayo ili fedha zinazoingia kupitia kodi ziunde mfuko maalum wa ujenzi wa Zanzibar ( Special Fund for Zanzibar Reconstruction) na fedha hizo zikawa ni sehemu ya fidia?
Au wataalamu wetu kuishauri Serikali ya Tanzania na halikadhalika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikawa na wazo kuu la kuifanya Zanzibar kuwa ni sehemu maalum na ya uchumi maalum (Special Economic Zone) kama vile China ilivyofanya kwa baadhi ya maeneo yake?
Professa Issa Shivji aliwahi kusema kuwa kama Tanzania ingetaka in'gare kiuchumi basi haikuwa na njia zaidi ya kuimarisha uchumi wa Zanzibar uwe ni dirisha lake la kuonyeshea mafanikio. Lakini hilo halikufanywa na hakuna nia ya kulifanya.
Serikali ya Muungano haijawahi kuwa na nia, wanaojua vyenginevyo wanisamehe, kuifanya Zanzibar kwa vitendo kuwa ni dirisha la kuonyesha mafanikio. Sio vitu vya kushitukiza na kimoja kukitekeleza leo na kingine mtondogoo.
Ndipo nikasema nimekereka sana na maneno ya Dk Mwinyi aliyesema ati, kuna hoja ya kutaka kuijadili asilimia 4.5 ambayo inapata Zanzibar kama gawio la misaada na hisa za Benki Kuu. Itakuwa vipi hoja iwe kiwango hicho kipunguzwe? Ikiwa hoja ni kuwa hiyo 4.5% Zanzibar haistahili kupata, kwani kuna lipi lilobadilika na je Zanzibar imekuwa ndogo zaidi na imekuwa na mahitaji madogo zaidi?

Hoja yangu kwa leo ni kuwa Serikali ya Muungano inafanya maamuzi kwa niaba ya Zanzibar na maamuzi mengine ambayo yanaathari kubwa ya kiuchumi kwa Zanzibar. Na Zanzibar hiyo hiyo inatarajiwa ishindane kiuchumi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Fikra zangu ni kuwa Zanzibar ifidiwe na Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki au kwa maneno mengine taasisi hizo mbili ziwe na mipango maalumu ya kuisaidia Zanzibar.

Kama nchi za visiwa zitazama kwa kuongezeka joto duniani na kina cha maji kuongezeka, basi Zanzibar itazama mapema kwa kitanzi cha kiuchumi, ikiwa mfumo wa ?Kodi Sifuri? utatekelezwa bila ya Zanzibar kutayarishwa.

+255 777 4300 22

www.eternaltourszanzibar.net

jumbamaro.blogspot.com

tutasikia mapya kila siku, na kila linalokuja linaizamisha zanzibar,kina mtu wa pwani, side ,engineer na wazanzibari wengine, nadhani pamoja na kwamba tunaandika hapa lakini kuandika kutupu hakutoshi, ni vyema tungeamua kujitolea kwa njia moja au nyengine kuwaamsha wazanzibari kwa vitendo ili waungane na wawe kitu kimoja(tuwasiliane nao na tuwadarisishe umuhimu wa kuungana kwetu). cuf na ccm watangulize uzalendo mbele kabla ya sera za vyama. mara nyingi hii ccm kumuona cuf adui au cuf kumuona ccm adui ndiyo inayowapa mwanya hawa wasioipendea mema zanzibar kutoa maamuzi kama haya. na pia wale watanzania bara wanaopendelea kuiona zanzibar inaendelea basi tutashukuru sana mkaungana nasi katika huu mchakato.
naamini tutashinda .its just a matter of time.
 
naam ndugu zangu nyote nnakutakieni eid njema.

siku mbili hizi nilikuwa niko ktk pirika pirika za eid nikawa nnapita na kusoma mbio mbio bila ya utulivu, ila sasa alhamdulillahi nimeanza kutulia kidogo maana shughuli za kifamilia kwa ajili ya eid zimeenda vyema.

tukija kwenye mjadala wetu tumeona sehemu moja ikieleza kuwa uwanja wa ndege wa zanzibar ni miongoni mwa worsest airport in the world.

hili ni kweli na halipingiki na wala halihitaji tochi.

lkn hili pia liko wazi ni nani anaesababisha hili. ndugu zetu wako makini ktk kukusanya kodi(TRA) lkn bila ya kuvijali vyanzo hivyo.

serikali ya zanzibar uchumi wake umedumazwa na muungano kiasi ambacho kulipia mishahara tu haitoshi seuze kuweka miundo mbinu ya kiuchumi.

wenzetu bado wanabeba zima hiyo kama tulivyoainisha hapo nyuma.

ss tulitegemea mungano uwe ni njia njema ya kuendelea na kushirikiana kisiasa na kiuchumi. bali wenzetu wameweka zaidi siasa na kutuuuwa basi.

leo wakisikia CUF wanasema serikali hawaitambui au uchaguzi tutaletewa majeshi na mapolisi na hata magari ya pili pili.

lkn kwenye masuala ya maendeleo hamna msaada wowote wa maana.

jamani huu ni aina gani ya muungano?

kuna swahiba yangu mmoja mtu wa bara ananiambia nyny wazenji mnajiona ndio tunataka kukuonesheni, yaani anasema mbon go hata akimpata mzenji anavyoserebuka nae kwa uson go yaani kumkomoa kiroho mbaya
 
Mtu wa Pwani,

Baraza la Wawakilishi na Wabunge ni mzigo mkubwa sana kwa wananchi wa Zanzibar.

Hivi mkipunguza nusu ya hao mtakuwa mme-save kiasi gani?

Uchumi mnao ila mnaukalia.

Suala lingine ni vizuri mkaanzisha viwanda. Hii import export haitawasaidia in a long run.
 
mawazo yako ni mazuri sana

ila haya hayatatekelezeka ikiwa muundo wa muungano hujawekwa sawa.

kwanza sioni umuhimu wa wabunge wetu kuwepo huko hata kwa mambo yasio ya muungano.

jengine kuhusu viwanda ukiangalia utaona kama jepesi ila tukisajili viwanda na viwanda vikitaka kuleta bidhaa zake bara bara wanaviwekea mikwala kwamba havijaregister na muungano mfano zantel walizuiliwa kuwa na coverage bara kwa kuwa wameregister zanzibar ila ukiregister bara unaingia zanzibar bila ya hodi ati ni sehemu ya jamhuri.

tukiweka sawa muundo wa muungano na wenzetu hawa kwa nia njema waishauri serikali ya SMZ wapunguze ukubwa serikali yake na wapunguze vikosi vya ulinzi na mengineo ili waekeze nguvu kwenye uchumi huku wakitusaidia kutuondolea vikwazo wallahi tutasonga mbele.

muungano unajua kuchangia mambo ya fitna tu kule kwetu.

ss tunaamini ndugu zetu mkitaka kutusaidia tutafika mbali, ila mna roho ya kwa nn.
 
Mtu wa Pwani,

Baraza la Wawakilishi na Wabunge ni mzigo mkubwa sana kwa wananchi wa Zanzibar.

Hivi mkipunguza nusu ya hao mtakuwa mme-save kiasi gani?

Uchumi mnao ila mnaukalia.

Suala lingine ni vizuri mkaanzisha viwanda. Hii import export haitawasaidia in a long run.

Joka mimi naamini hao wawakilishi sio mzigo kabisa kwa Zanzibar, mimi nina imani kubwa WABUNGE na MUUNGANO ndio gunia la misumari kwa Zanzibar.
Wawakilishi wote ni 81 na wanatunga sheria za Zanzibar, tuna Wabunge kama 70 kwenye Bunge ila wao wanaimaliza Zanzibar.
KWA MFANO Rais wa Zanzibar alipoondelewa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Muungano, walijua kuwa hilo ni bomu ila mbona walikaa kimya! walipitisha.
Sasa kama Muungano wa NCHI MBILI, Najiuliza huyu kiongozi wa Zanzibar ana nafasi gani kwenye Muungano huu? Hawashi hazimi, just yupoyupo tu.

Kuhusu uchumi na viwanda, Mtu wa Pwani kamaliza mchezo.
A day will come
 
tutasikia mapya kila siku, na kila linalokuja linaizamisha zanzibar,kina mtu wa pwani, side ,engineer na wazanzibari wengine, nadhani pamoja na kwamba tunaandika hapa lakini kuandika kutupu hakutoshi, ni vyema tungeamua kujitolea kwa njia moja au nyengine kuwaamsha wazanzibari kwa vitendo ili waungane na wawe kitu kimoja(tuwasiliane nao na tuwadarisishe umuhimu wa kuungana kwetu). cuf na ccm watangulize uzalendo mbele kabla ya sera za vyama. mara nyingi hii ccm kumuona cuf adui au cuf kumuona ccm adui ndiyo inayowapa mwanya hawa wasioipendea mema zanzibar kutoa maamuzi kama haya. na pia wale watanzania bara wanaopendelea kuiona zanzibar inaendelea basi tutashukuru sana mkaungana nasi katika huu mchakato.
naamini tutashinda .its just a matter of time.

CCM ZNZ hawana uzalendo wala hawaupati huo uzalendo maisha, hawa ni watu wamekaa pale wale then warisishe watoto hadi tunapata MKOA wetu.
Hawa jamaa CCM ZNZ hawana mamlaka wala maamuzi yoyote kwenye CHAMA chao wala SERIKALI yao, Ngoma inapigwa Dodoma wao wanacheza tu.
Naibu Waziri wa Elimu miaka hiyo Sultan Mugheir alisema kwenye baraza kama hivi: Cuf nyinyi semeni kuhusu Muungano hadi mchoke haiwi kitu, ila sisi Ccm hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu tunaogopa kukatwa vichwa. Hii yaonesha kuwa wanayajua maovu ya MUUNGANO ila maslahi kwanza.
Hata kwenye kura za maoni kutafuta mgombea Urais ZNZ 2000, Utaratibu ni kuwa majina matatu ya mwanzo kutoka KAMATI MAALUM CCM ZNZ yanapelekwa Dodoma, kwa kuwa Amani hakuwemo humo kwenye watatu wakaambiwa wapeleke majina yote Dodoma.
Hapa uzalendo utatokea wapi!
 
SiDE,

ktk chaguzi zile za kabla ya Mapinduzi ya 1964 viti vya Bunge la Zenj vilikuwa havifiki 30. Sasa kulikoni leo hii kuwe na wawakilishi, na juu yake wabunge zaidi ya 100?

Halafu hao wawakilishi na wabunge wanalipwa mshahara,posho,na marupurupu kiasi gani? hiyo ni gharama kubwa mno kwa nchi ndogo kama Zenj. huo ndiyo "MZIGO" ninaozungumzia.

suala lingine ni vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali ya Mapinduzi. what is KMKM and JKU for? tayari ktk Muungano kuna JWTZ na Polisi.

Ukipunguza viti vya wabunge na wawakilishi, na hivyo vyombo vya ulinzi, SMZ itabakiwa na fedha za ziada kusaidia maendeleo ya wananchi.

Waswahili wanasema, KUPANGA NI KUCHAGUA.
 
JK tatizo sio wawakilishi au vingenevyo, tatizo ni ubinafsi wa viongozi na watawala wetu. There is enough for every body in Tanzania ila wachache wanazidi kuhodhi kwa manufaa yao.

Nasema tena, mpaka wananchi tutakapozinduka na kuona uzandiki wa watawala wa CCM tutazidi kuumia. na kwa kuwa tumeamua kuikumbatia CCM basi hatuna budi kulipa gharama inayostahili AMBAYO NDO HUU UMASKINI TUNAOLIA NAO KILA SIKU. Kwa hiyo tusilalamike. Kuhusu Zanzibar mimi siwahurumii hawa jamaa kwa sababu na wao ni wanafiki wanaikumbatia CCM na sera zake kwa sababu wachache wananufaika! Nchi ya watu million moja inakosa hata aspirin, harafu unaniambia hiyo ni akili au ni tope? Let them suffer, wakizinduka-as all Tanzanians, then we shall move forward. For now we are enjoying the consequences of our choices!

Noel Njema!
 
Jokakuu,
Hata Tanganyika kila siku majimbo mapya- miaka 40 tulikuwa na wabunge less than 200- leo hii Wabunge ni over 300!

Je hii inatofautiane na Z'bar? Kwa nini bara nao wasipunguze wabunge??
 
JK tatizo sio wawakilishi au vingenevyo, tatizo ni ubinafsi wa viongozi na watawala wetu. There is enough for every body in Tanzania ila wachache wanazidi kuhodhi kwa manufaa yao.

Nasema tena, mpaka wananchi tutakapozinduka na kuona uzandiki wa watawala wa CCM tutazidi kuumia. na kwa kuwa tumeamua kuikumbatia CCM basi hatuna budi kulipa gharama inayostahili AMBAYO NDO HUU UMASKINI TUNAOLIA NAO KILA SIKU. Kwa hiyo tusilalamike. Kuhusu Zanzibar mimi siwahurumii hawa jamaa kwa sababu na wao ni wanafiki wanaikumbatia CCM na sera zake kwa sababu wachache wananufaika! Nchi ya watu million moja inakosa hata aspirin, harafu unaniambia hiyo ni akili au ni tope? Let them suffer, wakizinduka-as all Tanzanians, then we shall move forward. For now we are enjoying the consequences of our choices!

Noel Njema!
napenda watu kama wewe unaeonesha true colour yako kwani kuna wengine hasa wanasiasa, wanaojifanya wanaipendelea mema zanzibar kumbe mioyo imejaa unafiki.na kama kuikumbatia ccm ni unafiki basi nadhani tanganyika ndio mama wa wanafiki ,maana ccm hushinda bila upinzani katika chaguzi za rais.angalau huku zanzibar wanaoikumbatia na wasioikumbatia wako karibu idadi sawa.
 
SiDE,

ktk chaguzi zile za kabla ya Mapinduzi ya 1964 viti vya Bunge la Zenj vilikuwa havifiki 30. Sasa kulikoni leo hii kuwe na wawakilishi, na juu yake wabunge zaidi ya 100?

Halafu hao wawakilishi na wabunge wanalipwa mshahara,posho,na marupurupu kiasi gani? hiyo ni gharama kubwa mno kwa nchi ndogo kama Zenj. huo ndiyo "MZIGO" ninaozungumzia.

suala lingine ni vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali ya Mapinduzi. what is KMKM and JKU for? tayari ktk Muungano kuna JWTZ na Polisi.

Ukipunguza viti vya wabunge na wawakilishi, na hivyo vyombo vya ulinzi, SMZ itabakiwa na fedha za ziada kusaidia maendeleo ya wananchi.

Waswahili wanasema, KUPANGA NI KUCHAGUA.
ni mawazo mazuri kwa serikali inayokubali kupokea mawazo.thankz bigisnake (jokakuu)
 
Under age ndugu yangu mimi na wewe tumechoshwa na huu unafiki wa viongozi wetu. Ndo maana tunafika sehemu tunasema labda tukiumia tutapata akili. Kama Karume au wenzake wasingekuwa wanaangalia vitumbua vyao, unafikiri hali isingebadilika? Tatizo ni uongozi unaojali matumbo yao. Wadanganyika na wazanzibari we share common heritage na mahitaji yetu ni yale yale, sema tuu basi tunaangushwa na wale tuliowapa dhamana.

Uzanzibari na utanganyika mimi simo, hizo ni kauli za walioishiwa mawazo, as long as we can forge a common future together, Then our Union will be relevant thousands of years to come as it was fifty years ago when the idea was put on the table.
 
Back
Top Bottom