Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Wengi hamjui Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 1977 inasemaje kuhusu Mambo ya Muungano. Haya tuambie juu ya Ibara yoyote inayosema kuwa "Shughuli za Maendeleo" ni jambo la Muungano! Ndio maana JK hajaona umuhimu wa kujibu maswali ya mzee wenu Warioba kwa kuwa hiyo Katiba ya sasa inampiga chenga huyo mzee Warioba!

Aisee! Ivi unajua maendeleo ni nini?
Ivi raisi(Kikwete) na waziri mkuu (pinda pinda) wa Tz (Zanzibar and Tanganyika) hawajawahi kuingia upande wa pili kwa issue ya maendeleo halafu wewe unataka upewe kifungu cha katiba kinachosema hivyo?
Ivi unaakili kweli?
Embu wewe taja ibara ya katiba ya jamuhuri ya Tz ya 1977 iliyotaja kuhusu maendeleo ya Tanganyika!
...
Watu wanaongea pumba lakini hiyo ya kwako ni zaidi ya pumba! Sjui niite pumbu!
 
Hapo mwanzo babu zetu kwa kila upande walidai uhuru wa TANGANYIKA na ZANZIBAR. Katika kudai uhuru, TANGANYIKA ndiye alizaliwa kwanza (Kifungua Mimba) Tarehe 9/12/1961, na kisha kufuatiwa na ZANZIBAR tarehe 12/01/1963. Hata hivyo TANGANYIKA kutokana na NJAA yake ya KISIASA alikubali kuuza Haki ya Mzaliwa wa Kwanza (BIRTH RIGHT) kwa ZANZIBAR hapo Tarehe 26/04/1964 kama ambavyo ESAU aliuza haki yake ya uzaliwa wa kwanza kwa YAKOBO.

Katika ulimwengu wa roho, ukeshauza au kuikana haki yako ya uzaliwa kwanza, unafutika kabisa katika ulimwengu wa roho na mwili (ni mojawapo ya laana). Maana yake, huwezi kurithi baraka zinazoendana na jina lako wala haki yako ya uzaliwa wa kwanza. Ndicho kilichotokea kwa ESAU, na ndicho kilichotokea kwa TANGANYIKA hadi leo hii. Leo hii Zanzibar yupo, lakini Tanganyika yupo wapi?

Kwa wasomaji wa Biblia mtakumbuka kuwa hadi leo hii YAKOBO yupo na anashamiri (Taifa la Israeli) lakini je, yu wapi ESAU au taifa lake duniani? Hapa chini napachika tukio hilo kama linavyosomeka katika BIBLIA:

(MWANZO 25:29-34)
29 Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana.
30 Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu (Edomu maana yake ni Mwekundu).
31 Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.
32 Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi?
33 Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
34 Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

===
Kazi kwako Mwananchi, TAFAKARI na Oanisha jambo hili na TANGANYIKA===
 
Tanganyika ni Eneo kubwa sna
ukilinganixia na Z'bar,
kinachonixhanga za, kwanini
Watanganyika Tunaukana
utanganyika na na Kuulilia
Utanzania ?
Ushirikiano si kitu kibaya lakini
ikishafikia hatua km hii ya
kuvutana kwa vitu visvyoeleweka
Haina haja tena.
Kisehemu kidogo km Z'bar ndo
kinakupigisheni kelele.
Tanganyika kuna madini, mbuga,
maziwa n.k, Tukitumia fursa hzi
Lazma tutoke tu, au hatuwezi kufikia Millenium Goalx bila Z'bar ??
via Mtazamo
 
1. Muungano ni baina ya nchi mbili huru-Jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar. Lengo likiwa nni kusshirikiana kwa faida ya wote na sio mmoja kumtawala mwingine. Zanzibar imekuwa ikilalamika kwamba inachukuliwa kama koloni la Tanzania kutokana na maamuzi yake ya siri ambayo mara nyingi hukataliwa na JMT kwa kuwa ni kinyume na makubaliano ya Muungano. Mfano suala la OIC

2. Zanzibar sio nchi wala wilaya wala jimbo la Tanzania bali ni nchi. Hii iinatokana na historia yake. Ktk hili Zanzibar imekuwa ikidai mambo yaliyo kinyume na mkataba wa muungano unaoonesha kwamba nchi hizi zitaungana kwa jima moja lla Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia kwamba kila moja amepewa madaraka ya juu ya mambo mengine yasiyo kwenye idadi ya mambo ya muungano.

3. Msingi wa Katiba za nchi hizi mbili ni hati ya muungano.

4. Serikali imepewa mamlaka ya juu ya mambo ambayo kimsingi ndiyo yanayoleta mantiki ya muungano.

5. Haijaletwa hoja ya msingi sana ya kuuvunja muungano. Kinachoonekana hapa ni utamaduni wa upande mmoja kubaguana ama influence ya mtu au kikundi kimoja chenye maslahi na muundo wa serikali tatu.
 
Hakuna mabadiliko yaliyowahi kufanywa bila Wazanzibari kuridhia! Hayo mengine ni blah blah tu!
 
Kwann mnakuwa wagumu wa kukubali utanganyika wenu na hawa wazanzibar munaukana utanganyika wenu leo hii tatizo nn hasa tukubali Matokeo tu wazanzibar wanadai nchi yao na nyinyi mubaki kama watanganyika halafu tuangalie muungano
 
Sam,

Inasikitisha sana kusoma huo mswada unaotegemewa kufanywa sheria katika siku za usoni , swali langu mimi ni moja tuu Watanzania ni nani aliyetuloga ? Kwa nini atufikirii kabla ya kufanya maamuzi ?

Kweli , kuna haja ya kuwa rocket scientist kujua ya kuwa huo mswada ni ujinga na ni kuwatukana wazalendo ? Yaani mapato ya madini yagawanywe katika uwiano wa 60% bara na 40 % zanzibar ....Ni vigezo gani wametumia kupata hizi figure ? kwanza zanzibar ina population ya watu wangapi .

Sam , naona utakuwa unaumiza kichwa tuu . Hawa viongozi awajali watu wa kawaida wanachodai ni masilahi yao binafsi ! siasa za bongo ni upotevu wa muda kwani wananchi wako so dormant na mara nyingi wanaishia kulalamika tuu .kikifika kipindi cha uchaguzi wanapitishiwa mswada wa kuwapa pilau " wanahongwa pilau " then wanawachagua kwa asilimia 80%.

Yaani hata mimim ninashindwa kuelewa sijui sisi watanzania tunalaana ya aina gani ya kutenda bila kufikiria ni moja wapo .Kwa takwimu walizozitoa wao ni balaa huwezi sema watu 4mil ni sawa na 42mil pia huwezi linganisha usawa wa eneo Tanzania bara ni 945,203kmsq while Zanzibar ina 2650kmsq hapo haina usawa habisaaa
 
Kwanini usivunjike kwani ukivunjika tutakufa au wao watakufa? maisha si yataendelea kama kawaida? mimi napendekeza serikali moja tu sio tatu wala mbili....zanzibar iwe ni mkoa wa unguja na pemba ndani ya tanzania.

Yaani nawashangaa watu wanaokurupuka na serikali Tatu! Ujue muungano ni saw a na ndoa, Zanzibar haikupaswa kuwa na serikali so as Tanganyika Kama kweli ziliungana! Kwani ndoa si Mke na mume kila mmoja anaacha wazazi wake anaungana na mwenzie wanakuwa mwili mmoja? In short hakuna na hakukuwahi kuwepo muungano! Muungano utakuwa na mantik iwapo tutakuwa na serikali Moja chini ya raisi mmoja tofauti na hapo hakuna muungano ila CCM wanatufanyia viini macho tu
 
muumgano hakuna Kuna uvamizi ulopewa jina muungano. January 64 Nyerere aliivamia Zanzibar na kuwakamata viongozi wake ma kuwaweka katika jela za Tanganyika kabla ya huo aliouita muungano April 26 -1964. Kina jofanyika nikuhalalissha uvamizi kwa njia ya katiba
 
Sam,

Inasikitisha sana kusoma huo mswada unaotegemewa kufanywa sheria katika siku za usoni , swali langu mimi ni moja tuu Watanzania ni nani aliyetuloga ? Kwa nini atufikirii kabla ya kufanya maamuzi ?

Kweli , kuna haja ya kuwa rocket scientist kujua ya kuwa huo mswada ni ujinga na ni kuwatukana wazalendo ? Yaani mapato ya madini yagawanywe katika uwiano wa 60% bara na 40 % zanzibar ....Ni vigezo gani wametumia kupata hizi figure ? kwanza zanzibar ina population ya watu wangapi .

Sam , naona utakuwa unaumiza kichwa tuu . Hawa viongozi awajali watu wa kawaida wanachodai ni masilahi yao binafsi ! siasa za bongo ni upotevu wa muda kwani wananchi wako so dormant na mara nyingi wanaishia kulalamika tuu .kikifika kipindi cha uchaguzi wanapitishiwa mswada wa kuwapa pilau " wanahongwa pilau " then wanawachagua kwa asilimia 80%.
Maprofessor wa kuchumia tumbo. Vigezo ni kufikria tumbo lako unapta hizo 60% na 40%.
 
tanganyika ni eneo kubwa sna
ukilinganixia na z'bar,
kinachonixhanga za, kwanini
watanganyika tunaukana
utanganyika na na kuulilia
utanzania ?
Ushirikiano si kitu kibaya lakini
ikishafikia hatua km hii ya
kuvutana kwa vitu visvyoeleweka
haina haja tena.
Kisehemu kidogo km z'bar ndo
kinakupigisheni kelele.
Tanganyika kuna madini, mbuga,
maziwa n.k, tukitumia fursa hzi
lazma tutoke tu, au hatuwezi kufikia millenium goalx bila z'bar ??
Via mtazamo
congratulations. It can be a nice peom for the ears.
 
Uvunjwe coz kama kweli ni muungano? Why are we asked for passport when travelling to Zanzibar? Why Zanzibar has her national anthem and flag?
 
Machafuko ni moja ya sifa ya nchi za kiafrika. Na hatua moja kwa nyingine husababishwa na weredi na ufanisi wa wanasiasa uchwala wasio jali uhai na haki za wananchi wao. Hufikisha mataifa yao katika machafuko ya umwagaji damu kwa midomo yao na ndimi zao kwa maslai ya vyama vyao na mabwana zao wanao waabudu na kuwahusudu. Tusidanganyane waheshimiwa wa bunge la katiba kwa kutaka kuiweka AMANI yetu rehani kwa maslai yenu binafsi. Kuna vitu zaidi ya 1000 vya kujadili kwa mustakabali wa taifa letu. Muundo wa serikali nisehemu dogo sana ya matakwa ya wananchi wenu ila ni sehemu kubwa sana ya matakwa ya vyama vyenu na maslai yenu. Kwa kipindi hicho chote mpka sasa ni siku 60 zimefika hatua hata moja na uelekoo wa kupata katiba mpya yenye weredi wa kuipatia tz maendeleo binafsi hakuna zaidi mnataka kuifanya iwe ombaomba milele kweli kwenye miti hakuna wajenzi. Hivi hatima ya maendeleo ya watz ipo kwenye serikali 3 au 2 au 10??? kina mama wajawazito wanafariki mahospitali chozo ni serikali 2 au ni uhaba wa rasilimali katika mahospitali??? wabunge kwa siku 60 wanakula 18 Million bila kodi kwa kupiga kelele na vijembe mchanganyiko na matusi hiyo ndio nafuu kwa wananchi. Hii dhambi itawarudia wenyewe msio kuwa na uchungu na damu za wananchi mnazotaka kuweka rehani ya mafanikio yenu kisiasa na vyama vyenu. Hatua ya maendeleo ktk ubora ina sifa 1 tu ambayo ni: kutoka chini kwenda juu kwa maana hii ukiwa wa kwanza kwenye mitihani yako basi ww ni bora zaidi ya walio kuwa wa pili na watatu.
KAMA KWELI NYINYI NI WAUMINI WAZURI SANA WA MUUNGANO BASI UGANISHENI TAIFA LIWE MOJA LENYE SERIKALI MOJA YA URT. ila sehemu mbili za muungano zipewe mamlaka ya kuwa majimbo huru katika usimamizi wa maendeleo hebu tujifunze katika taifa lililoendelea la USA Obama ni mmoja ila kuna majimbo takriba 52 yenye uhuru wa kusimamia maswala baadhi ya maendeleo ya ndani ya jimbo. TAFAKURI.
Ni mtanzamo wangu.
#CC .
#Bunge_La_Katiba
#Zomeazomea
 
Kaka umenena,lakini wenzetu wamekula za wazungu hasa Chadema ,na waliberali wa CUF tufanyeje?
 
Yesu alimwaga damu kwa lengo la kupata ukombazi na leo ni siku kubwa!!
Sasa nchi hii tupo chini ya utumwa , watawala wetu wamekumbatia uchawi na kumuasi Mungu.
Roho zote ni mali ya Mungu
 
Back
Top Bottom