Watanganyika nawashauri hili suali la ardhi mlisahau maana liko complicated sana. Huku wenyewe zanzibar tuna issue kubwa uhusu ardhi, ndugu zetu kutoka pemba wanakuja unguja na wanatafuta ardhi na kununua na wanauziwa bila tatizo, lakini sisi tukitoka unguja kwenda pemba kununua ardhi hatuuziwe ng'o! Hakuna sheria inayokataza hilo ila ndugu zetu hawako tayari hata siku moja kumuachi muunguja amiliki ardhi pemba. Ni narda sana kuona muunguja anamiliki ardhi au nyumba pemba. Ndugu zetu wa kisiwa cha pemba wana unwritten code kama watu wenye asili ya kihindi ya kulinda na kutunza sehemu ambazo jamii yao kubwa wanaishi na wanahakikisha asokuwa wao hauziwi ardhi sehemu zao.