Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Mi naona wajitenge, halafu tuwavamie na kugeuza kua wilaya ya pemba na zanzibar kama vile waisraeli walivyo vamia palestina.
hata burundi na rwanda tunaweza kuivamia kirahisi kabisa tukawa na taifa kubwa ukiangalia nchi hizo ni ndogo ziko katika boda letu la Tanganyika...sijui hili jeshi letu linasubiri nini:tape2:
 
Mwanasheria Maarufu Zanzibar, Salum Tawfiq akitoa mada katika Kongamano la Kitaifa kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika viwanja vya Lumumba Mjini Zanzibar

Mimi naamini kabisa kwamba Muungano ni ridhaa baina ya Nchi mbili zilizoungana. Muungano wa Serikali mbili au viongozi wawili bila ya baraka za watu wa nchi hizo hauna maana yoyote. Hivyo iwapo upande mmoja katika Muungano utasita kuridhia kubaki katika Muungano, huo unakuwa si Muungano tena. Sasa leo ya nini kuunda Tume na kupoteza mabilioni ya fedha kujaribu kuutenganeza upya Muungano ambao tayari viashiria vyote vinaonesha Muungano ushapitwa na wakati. Si ungetosha tu kuwauliza Watanzania suala la msingi kwanza kabla ya kuingia katika gharama zisizo za lazima. Suala lenyewe: jee unautaka au huutaki? Kungekuwa na haja gani ya kutaka Muungano uwe madhubuti kama walio wengi hawautaki?

UTATUZI WA KUDUMU WA KERO ZA MUUNGANO

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao juzi tu ulitimiza miaka 48 umejaa kero ambazo kila upande, hasa Zanzibar, unaona zimekua karaha. Muungano huu na kero zimekuwa ni vitu vinavyokwenda pamoja – huwezi kuzungumzia Muungano bila ya kuanza kutaja mapungufu yake. Katika mada hii, nitajaribu kupendekeza namna ambavyo kero hizi tunaweza kuzitatua.

Mwalimu Nyerere akihojiwa na Gazeti la Observer la Uingereza tarehe 18 Aprili 1968 alisema:
Kama ni Rais wa Tanzania, ni jukumu langu kulinda kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano. Lakini iwapo umma wa Wazanzibari, bila ya kutumiwa na wageni, wakiwa na sababu zao binafsi, wakaona kuwa Muungano hauna maslahi kwao, sitoweza kuwalazimisha kubaki katika Muungano. Muungano utakuwa tayari umesita kuwepo endapo upande mmoja utaondoa ridhaa yake. (Tafsiri ni yangu).

Nukuu hiyo ndio chimbuko la mada yangu. Katika harakati au wasemavyo siku hizi “mchakato” wa kupitishwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011, Wazanzibari wameonesha wazi kwamba wamechoshwa na Muungano uliopo sasa. Wazanzibari walio wengi pamoja na viongozi wao, wakiwemo Mawaziri na viongozi wa dini, wamesema waziwazi kwamba Muungano huu wa miaka 48 hauna maslahi kwao. Na “Baba wa Taifa” alishaota ndoto hio; leo kero za Muungano zinaonekana zaidi kwa ndugu mdogo (Small Brother) kuliko kwa kaka mkubwa (Big Brother).
Wapo baadhi ya Watanganyika ambao nao wamekuwa wakidai Tanganyika yao lakini hawa ni katika wachache. Waliowengi, kuwepo au kutokuwepo kwa Zanzibar katika Muungano hakuathiri chochote kwao. Hawa wanaona ukubwa wa ardhi, idadi ya watu na rasilmali nyingi walonazo zinaitoa Zanzibar kama mshiriki mwenza (equal partner) katika Muungano. Hili likichanganyika na “kero ya Wazanzibari” kila siku kufanya kelele linawafanya waone Muungano hauna maana tena kwa Tanzania.

Wapo Watanganyika wengine wanaona Zanzibar “haina shukrani” kwa kuwa ati Zanzibar inategemea kila kitu – kuanzia chakula, nguvu kazi na hata fedha za kuendeshea nchi kutoka Bara. Hawa ndio wengi wanaosema Muungano unawanufaisha zaidi Wazanzibari na itakuwa ni kujitia kitanzi iwapo Zanzibar itajitowa katika Muungano.

Tabaan. Kwa wote hawa basi na warudi wenyewe kwa Mwalimu Nyerere. Sasa Zanzibar na Wazanzibari washaridhika kwamba Muungano umewachosha. Kuna haja gani ya kuunda Tume ya Katiba kukusanya maoni ya wananchi?
Sheria ya kuanzisha Tume ya Katiba imeweka hadidu za rejea au muongozo kwa Tume hiyo ambayo inategemewa kuanza rasmi kazi yake mwanzo wa mwezi wa Mei, 2012. Hadidu rejea hizi zimetajwa katika kifungu cha 8, 9 na 17 vya Sheria hiyo (Nam. 8 ya 2011). Baadhi ya majukumu yake ni:
Kukusanya maoni ya wananchi Kutoa mapendekezo kwa kila hadidu rejea
Kutayarisha na kuwasilisha ripoti kwa kuzingatia hadidu rejea
Agenda kubwa kwa Wazanzibari ambayo ni suala la kuwepo au kutokuwepo kwa Muungano si miongoni mwa hadidu rejea za Tume ya Katiba. Na wakati wa kuapishwa kwa Wajumbe wa Tume Ikulu Dar es Salaam tarehe 13 Aprili 2012, Rais Kikwete alisema wazi kwamba wanaohubiri kuvunjika kwa Muungano hawatasikilizwa! Mtu ataweza kujiuliza: nini sasa faida ya kukusanya maoni kama kiini cha matatizo hutaki kijadiliwe? Katika kulijadili hili naomba tukakisome tena kitabu cha Baraza la Katiba, Zanzibar:

Katiba Tuitakayo – Sheria ya Kuandika Katiba Mpya ya Tanzania na Suala la Muungano kwa Zanzibar, hususan Sura ya Nne (Uk.22 – 29).
Maana yake ni kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Tume, hata kama Wazanzibari asilimia 100 wakisema wamechoshwa na Muungano hawatasikilizwa! Hapa ndio udhaifu mkubwa wa Sheria ya Tume unapoonekana. Nini hasa faida ya kuunda Tume na kutumia zaidi ya bilioni 40 na kumalizia kwa kuongeza tu katika orodha ya kero za Muungano?
Napenda hapa niunganishe hili la kuundwa kwa Tume ya Katiba na kupitishwa kwa Marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar (Sheria Nam. 9/2010). Marekebisho haya yameingiza vifungu vingi ambavyo kwa maumbile yake vinaonekana vikisisitiza Utaifa (Nationhood) wa Zanzibar. Kifungu cha 1 kinasema:
Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Kifungu cha 2A nacho kimetowa mamlaka kwa Rais wa Zanzibar kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo. Pia viko vifungu vyengine vinavyoonesha dhahir kujibu kejeli ya kaka zetu wakubwa kwamba Zanzibar ni mkoa tu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunafahamu jinsi mara kadhaa wanasiasa wa Tanzania Bara na hata Mahkama ya juu kabisa ya Tanzania (Mahkama ya Rufaa) walivyosisitiza kwamba Zanzibar si Nchi. Kwa maana hiyo hata ukifanya njama ya kutaka kumuondoa Rais wa Zanzibar madarakani kwa mtutu wa bunduki, hiyo haitokuwa uhaini (treason).

Ni sawa sawa na kujaribu kuiondosha Halmashauri ya Mji wa Chake Chake, si jambo la kushtua!
Mimi naamini kabisa kitendo cha Baraza la Wawakilishi kupitisha Marekebisho hayo kimekuja katika wakati muwafaka kabisa. Unapokuwa na mwenzako ambae hafahamu lugha unayozungumza inabidi utafute lugha pekee atakayoifahamu. Kubadilisha Katiba imekuwa lugha muwafaka kuwafanya wenzetu waone nini tunataka. Marekebisho ya Katiba yameibua lawama tele kutoka kwa wanasiasa na hata miongoni mwa wanasheria mahiri wa Tanzania Bara. Wengine wamesema Muungano wa Tanzania haupo tena pale Zanzibar ilipojitangaza kuwa ni Nchi! Mie naziona hizi zote ni kelele za mlango tu.
Kwa upande mwengine naamini Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 2010 pamoja na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) ndiko kulikopelekea kaka zetu wakubwa kuleta kiini macho cha Tume ya Katiba. Kama kweli lengo la Tume ni kushughulikia kero za Muungano na kuufanya Muungano wetu kuwa madhubuti basi hilo lilipaswa kufanywa zamani sana, pale kelele za Wazanzibari na hata za makundi kama G 55 ya Tanzania Bara yalipoibuka kudai Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar.

Badala yake hali ya kisiasa ikawachwa kuwa tete. Waliokosoa Muungano wakaitwa wasaliti wasioitakia mema Tanzania. Kuunda Tume ya Katiba sasa hivi ni sawa na kujaribu kuyazuia maji ya bahari yasifike ufukweni wakati wa bamvua!
Suala la kuwepo au kutukuwepo kwa Muungano ndio suala la msingi hata kabla ya kuunda Tume. Hapa Zanzibar tunayo Sheria ya Kura ya Maoni, 2010. Bara hawana, lakini hilo haliathiri chochote. Kama alivyonukuliwa Nyerere mwanzoni mwa mada hii;

Muungano hauwezi kuwepo endapo upande mmoja utaukutaa. Cha msingi ni kulipeleka suala hili kwa wananchi wenyewe walitolee uamuzi. Kwani viongozi wanahofu ya kitu gani? Isije ikatufika hadithi ya Abunuwasi ya kuwekwa uchi halafu tukaamini hatuonekani!
Mimi naamini kabisa kwamba Muungano ni ridhaa baina ya Nchi mbili zilizoungana. Muungano wa Serikali mbili au viongozi wawili bila ya baraka za watu wa nchi hizo hauna maana yoyote. Hivyo iwapo upande mmoja katika Muungano utasita kuridhia kubaki katika Muungano, huo unakuwa si Muungano tena. Sasa leo ya nini kuunda Tume na kupoteza mabilioni ya fedha kujaribu kuutenganeza upya Muungano ambao tayari viashiria vyote vinaonesha Muungano ushapitwa na wakati. Si ungetosha tu kuwauliza Watanzania suala la msingi kwanza kabla ya kuingia katika gharama zisizo za lazima. Suala lenyewe: jee unautaka au huutaki? Kungekuwa na haja gani ya kutaka Muungano uwe madhubuti kama walio wengi hawautaki?
Kwa mawazo yangu endapo Wazanzibari watasema hawautaki Muungano, dawa iliyobaki ni moja tu nayo ni kumaliza taratibu mambo ya Muungano. Udugu wa watu wetu na mahusiano ya kidiplomasia yatandelea. Marehemu Karume aliunasibisha Muungano na koti: likikubana utalivua tu. Nadhani koti la Muungano limekuwa linawabana sana Wazanzibari na lililobaki ni kulivua tu. Tukingoja sana itabidi tulichane kwani litashindwa kuvuka!
Ahsanteni Sana
Imetayarishwa na:
Salum Toufiq, Wakili

(Mada iliyotolewa katika Kongomano lililofanyika Lumumba tarehe 01 Mei 2012)

*
 
Serikali ya zanzibar kuzui mchele usiingezwe Tanzania bara si wanamaana kwamba muungano hawahutambui, ili mimi sijalielewa.
 
Mkuu, kwani hujui kwamba kwenye muungano cha Tanganyika ni cha wote na cha zanzibar ni chao peke yao?
 
Bara michele imejaa tele, wanachokataa wao ni kusababisha KUPANDA KWA BEI ZA MCHELE, Zanzibar wapo makini na wanayoyafanya, kisa cha sukari kupanda bei ni sababu ya kutoa sukari hapa tanzania na kupelea Kenya ambapo kigunia kimoja kilikuwa kinafika mpaka LAKI, hivo kufanya sukari yote kupelekwa huko na hapa bei ikipaa kupita kiasi, wanachotaka kudhibiti wao ni bei, ikiwa wataruhusu vitu vije kuuzwa huku basi bila shaka wafanya biashara wote watavusha vitu huku na matokeao yake bei zitapaa.

Ninapenda jinsi Shein anavofanya kazi, yupo serious na kazi zake, kila siku utaona ana vikao na watu kuhusu maendeleo ya nchi yake! jamaa hataki mchezo, na ninaamini kama ataendelea hivo basi Zanzibar itapata mafanikio bila shaka.
 
@@@ mkomatembo

Pia hii ni kudhibiti pia wafanya biashara ,kwani kule zenji sukari na mchele wamepunguza ushuru ,sasa hawa wa bara wanaweza kupitisha mchele na sukari kule na kukwepa ushuru kirahisi.......
tutizame jambo kwa undani.
 
Kwahiyo unamana hizi ni nchi mbili tofauti kama kila upande una mahamuzi yake si bora muungano uvunjwe ili zanzibari wakawe na maendeleo mazuri kuliko kakaa na muungano ambao hau tusaidii.
 
Kwahiyo unamana hizi ni
nchi mbili tofauti kama kila upande una mahamuzi yake si bora muungano
uvunjwe ili zanzibari wakawe na maendeleo mazuri kuliko kakaa na
muungano ambao hau tusaidii.

mbona hilo la nchi mbili liko wazi? katiba yao mpya inasema bayana zenj ni nchi
 
Kwahiyo unamana hizi ni
nchi mbili tofauti kama kila upande una mahamuzi yake si bora muungano
uvunjwe ili zanzibari wakawe na maendeleo mazuri kuliko kakaa na
muungano ambao hau tusaidii.

mbona hilo la nchi mbili liko wazi? katiba yao mpya inasema bayana zenj ni nchi
 
Nimekuwa nasikia makelele kutoka kwa wenzetu kila siku wanasema hatuutaki muungano lakini nikiwaangalia siwaoni kama wana faida yoyote kwetu, hivi kuna mtu anayeweza nipa jibu hawa jamaa wana faida gani kwetu kwa sababu sio tunawaacha wanatukana na kutupigia kelele kila siku. mie naona tuwasikilize halafu tupige kura tanzania nzima tusikie maoni ya wote. sio kila kukicha watu kumi wanatupigia kelele zisizokwisha halafu tunakaa kimya tu
 
Jamani kati ya kitendawili kikubwa ktk Tanzania hii ni huu muungano.
1. Zanzibar ni ya wanzanzibar pekee yao lakini tanganyika ni ya wote (watanganyika na wazanzibar)
2. Tanganyika ina watu takribani 44 Mil wakati Zanzibar ina watu 1ML
3. Eneo la Zanzibar ni sawa na eneo la wilaya moja kati ya wilaya zaidi ya 130 za tanganyika
4. Ingawaje wana serikali ya huko zanzibar ambayo haina watanganyika hata mmoja, lakini wao wanataka vyeo Tanganyika kwa usawa

Zanzibar iliungana vipi? mbona 1+1=2 and not 1+1=1

Mie nadhani Karume na Nyerere walikua na lengo la kufikia serikali moja ya Tanzania, lakini in principle sasa kuna serikali mbili ambapo moja ina Jeshi lakini nyingine haina. Baada ya hawa waasisi kufa, waliowafatia, waliendelea kufanya zanzibar kuwa serikali kamili bila kufukiria muungano uliopo. as a result, misingi ya muungano miaka ya 60, 70, na 80 ni tofauti na sasa.
 

‎''WATU WANAZUNGUMZA UZANZIBARI!!!!'' ''WATU WANAJIVUNIA UZANZIBARI!!!'' ' Tunataka KIONGOZI na VIONGOZI WATAKAOELEWA HIVI, ''KUZUNGUMZA UZANZIBARI SI JAMBO LA FAHARI HATA KIDOGO, HATMA YAKE UTAVUNJA NCHI'' ''MZANZIBARI MWENYE AKILI HAWEZI ...KUUTUKUZA UZANZIBARI, KWA KUJIITA SISI WAZANZIBARI NA WAO WATANGANYIKA, ''SISI WANZANZIBARI NA WAO WATANGANYIKA'' Na AKADHANI HII INA USALAMA NDANI YAKE, HATMA YAKE ZANZIBAR ITAJITENGA, ''ZANZIBAR IKIJENGA KWA SABABU YA ULEVI TU, ''ULEVI WA MADARAKA'' ''SISI WAZANZIBAR NA WAO WATANGANYIKA'' SISI SI WAMOJA, IKITOKEA HIVYO.. ''WAKUMBUKE KWAMBA MUUNGANO NDIO UNAOWAFANYA WAJIITE SISI WAZANZIBAR NA WAO WATANGANYIKA, NJE YA MUUNGANO HAWAWEZI KUSEMA HIVYO, NJE YA MUUNGANO HAKUNA WAZANZIBARI, KUNA WAAOO WAPEMBA NA SISI WAUNGUJA, DHAMBI HIYO HAITAWAACHA..J.K Nyerere
 
hallow wana jf,
mi kijiswali kidogo2,
naombeni mnikumbushe faida za muungano we2 na zanzibar....
 
hallow wana jf,
mi nna kijiswali kidogo2,
naombeni mnikumbushe faida za muungano we2 na zanzibar....
 
Nimepitia magazeti mengi ktk kipindi cha karibuni yaliokuwa yakiripoti kilichotokea zanzibar wiki iliopita. mengi ya magazeti hayo kwa makusudi wanapotosha na kupindisha kkinachoendelea huko zanzibar. wanajaribu kutaka kuwaaminisha walimwengu kinyume na kilichopo jeee ni kwa faida ya nani ?


Si magazeti tu peke yake ambayo yameshika kani katika kummimina sumu juu ya yanayojiri huko visiwani, mablogs na forums mbali mbali kwenye mitandao ya kijamiii wanajitahidi sana kugeuza ukweli wa mambo

ila ukweli utabaki kua ukweli. HUWEZI KULIZIBA JUA KWA UNGO HATA SIKU MOJA. kinachotokea zanzibar si chengine ila WANADAI NCHI YAO. wanasema wazi wanachokitaka ni JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA. huo ndio ukweli wa yaliopo zanzibar wanaopenda kusikia na wasiopenda kusikia wanaujua ukweli huu. na sio kelele zilizoanza jana au juzi ni suali la kitambo.


mapambano yao yalianza tokea kuungana na kubaini hila za wenzetu ktk muungano mapambano yalianza kutaka kurejesha hadhi na heshima ya nchi yao ilioporwa na mwenza wake kwenye muungano. nani asiejua harakati zilizoanza tokea karume akiwa hai. hadi akasema kuwa muungano ni kama koti tukiona joto tutalivua. kwa zaidi fatilia maandishi ya muandishi wa makala za siasa Mihagwa utaona jinsi gani serikali ya karume ilivyobaini njama na wakawa wanahaha kutafuta kujinasua.

Baada ya kifo cha karume rais aliefuata alikuwa Mh Aboud Jumbe, na yeye aliendesha mapambano ya kuikwamua zanzibar kwenye muungano huu dhalimu, mwisho wake kwa ubabe wa mshirika dhalimu wakamtendea waliomtendea, Rejea "kuchafuka kwa hali ya hewa zanzibar"


Harakati za kuipagania nchi hazikukoma aliekuwa AG wa zanzibar Dourado alipaza sauti sana kiasi kilichopelekea kufungwa kwenye gereza la Tanganyika kisha wakamtenga.


Kikaja kipindi cha akina Maalim Seif na kundi lake na mwisho wakafukuzwa kwenye chama. mapambano yaliripuka na kuzimwa kwa nguvu zote kila yaliporipuka. lkn yote ilikuwa ikitoa ishara kuwa wazanzibari wanataka nchi na kutaka nchi yao si kwa kumrejeshea mkoloni au sultani kama wenzetu kwa makusudi wamejaribu na kutenda kwa makusudi kupandikiza chuki hizo.


Ilikuwa ni kosa kuuujadili muungano kipindi cha nyuma na kwa nguvu zote ukizungumzia muungano kama hauko sawa utashughulikiwa, wazanzibari walitishwa, wakagawiwa, wakapandikizwa chuki za kuangaliana asili ya huyu katoka wapi huyu kazaliwa wapi. wakati ktk katiba ya zanzibar imeeleza vizuri kuhusu nani mzanzibari

Pinda aliposema Zanzibar si nchi moto ulirindima si zanzibar peke yake bali hata bungeni, walipaza sauti na kulaani kwa nguvu zao zote juu ya udhalimu unaoendelea juu ya muungano.


Kuja suali la kuandikwa kwa katiba mpya ndio sawa kumwaga PETROLIkwenye MOTOi, wazanzibar kwa umoja wao, walionyesha nn wanachokitaka, kama utafuatilia mijadala ya zanzibar juu ya rasimu ya mswaada wa katiba mpya yaliofanyika zanzibar Bwawani na Haile sellasie utaona dhahiri juu ya hilo.


Jumuia za kisheria na kijamii kwa muda zimeendesha makongamano, mijadala na mikutano ya kujadili na kuelimishana juu ya haki zao wazanzibari na kusisitizana umuhimu wa kuungana na kutetea haki zao kwa umoja wao.



Sasa nnataka kuwaambia wenye kupotosha ukweli wa yanayojiri zanzibar wanapoteza mda, haki huwezi kuizuia unaweza kuichelewesha. kama si kizazi hiki basi kijacho watapata haki yao. wazanzibari walio wengi ni waislamu na wao ndio wataodai na wanaendelea kudai haki yao. sasa mtu mwenye kuleta udini(na hasa uislamu) ulitaka wazanzibari wakawakodi wasio wailamu nchi gani ili iwatetee juu ya nchi yao ?


Watanganyika walipodai UHURU kwa muingereza waislamu walikuwa mbele kuendesha harakati hadi miskitini, hawakuwa wadini kwa wakati ule ? ila baada ya kupata na kuona yale waliokuwa wakiyapigania wakati wa ukoloni yakiendelea na zaidi kuyasemea wamekuwa wa dini ?

Kina Sheikh takadiri, Tewa, hassan bin ameir walikuwa wakiuza hadi kadi za TANU miskitini, wakati huo walikuwa wema ila walipodai haki yao baadae wamekuwa wabaya?

WAZANZIBARI WANACHODAI NI NCHI YAO, WANATAKA IITISHWE KURA YA MAONI WAULIZWE MUUNGANO WANAUTAKA AU HAWAUTAKI
 
Hongera Mkuu, uko juu ya mstari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…