Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

 
Mbona unajichanganya! Kwa maana hiyo njia mnayotumia kudai nchi yenu ya kuchoma makanisa na vitisho kwa wakristo na wabara ni sahihi? Acheni ujinga bana!
 
WAZANZIBARI WANACHODAI NI NCHI YAO, WANATAKA IITISHWE KURA YA MAONI WAULIZWE MUUNGANO WANAUTAKA AU HAWAUTAKI

Sasa kinawazuia nini kuitisha hiyo kura ya maoni waulizane wao kwa wao? MBona wameweza kuandika Katiba yao mpya na kuitangaza Zanzibar ni "nchi" kitu ambacho kinavunja hoja ya kudai nchi tena!

Kama kweli wanachodai ni nchi "yao" ambayo tayari wanayo kwa mujibu wa katiba yao kwanini wasiamue kupitisha sheria kwenye baraza la wawakilishi ili waulizwe hilo swali?

Au wanataka nani awaulize? Lakini kama kweli umeshajua wanachotaka ni ''nchi yao" kwanini hamuwaambia viongozi wenu walioko kwenye Muungano wajiuzulu na Wazanzibari wote wanaofanya kazi kwenye taasisi za Muungano kujiuzulu na kurudi Zanzibar ambako watapewa kazi nyingine?
 

usitake kutuzungusha weye unayeumwa na mwenye choyo kwa wazanzibari, mwenye kujaribu kutumia kalamu yako kufitini na kugeuza ukweli kwa choyo na husda zako


mwanzo mliataka kuaminisha watu kuwa kule mapambano ni juu ya watu wenye asili ya bara kutengwa. mkaona haitoshi mkataka kupandikiza kuwa ati kinachotokea ni waislam kuuchukia UKRISTO, mkaona haitoshi mkaleta hoja kuwa wanachochewa na mfalme ili arudi mkaona haitoshi mkaja waaarabu ndio wanaendesha mchakato. mara alqaeeda mara imekuja jeuri kwa sababu ya uchoyo, wamesikia zanzibar kuna mafuta wanataka kuwatenga ndugu zao kwa sababu ya mafuta

sasa ndio nikasema kupotosha huku kuna faida gani wakati ukifatilia historia utagundua wazanzibar wamepambana kudai haki yao kuanzia wanamapinduzi na waliopinduliwa na hata wengineo, waislam na wakristo walio wazanzibar.

kabla hata alama ya mafuta haijaanza kuongelewa. ukweli usemwe WAZANZIBARI WANATAKA NCHI YAO

na kuhusu kura ya maoni wazanzibar wanaishinikiza serikali yao iwape hio fursa na wala sio tanganyika na wao wanashangazwa na kigugumizi cha viongozi wao. na hapo wanaona jinsi wanasiasa wanavyoogopa nguvu ya muungano, hatujui na wao weshatishwa kama alivyotishwa karume? historia itakuja kuweka wazi


ILA WAZANZIBAR BILA KUJALI SIASA WATAENDELEZA KWA AMANI NA BUSARA KUDAI HAKI YAO HADI KIELEWEKE
 
Mbona unajichanganya! Kwa maana hiyo njia mnayotumia kudai nchi yenu ya kuchoma makanisa na vitisho kwa wakristo na wabara ni sahihi? Acheni ujinga bana!

hizi ndio baadhi ya njama za makusudi za kupotosha hoja. angalia huo mpambano ulianza lini na makanisa yalichomwa lini? kwa nn minor issue igeuzwe ndio issue na kupewa airtime kuliko habari
 
Hivi hawa wazanzibar wasiotaka muungano inakuwaje wakati wa kura wanawapigia kura rais wa muungano na wabunge wa bunge la j. ya muungano kutoka zanzibar?! Kwa nini wasigome kupiga kura ili kusiwepo na wabunge wa kuwawakilisha huko Tanganyika!?!
 
Zanzibar yasiyotakiwa ni Makanisa tu, ndio maana magari kibao ya Wachungaji yalichomwa moto! Wazanzibari ni wanafiki kupita maelezo maana watakuletea story nzuri nzuri kuwa hawautaki Muungano lakini cha ajabu wamejazana Tanzania Bara huku wakiwatimua Watz Bara huko Zanzibar. Wapo hata katika taasisi zisizo za Muungano, Sasa Muungano upi usiotakiwa? Hivyo vibaraghshia vimefunika bongo zenu na kuwapumbaza akili?
 

tulia sasa ueleweshe na usirukie post ya mtu kama huna jibu lake.. hapa hatupo kwenye mihadhara au mabishano ya yesu ni mungu ama sio mungu ...'
hapa umeulizwa kwa nini viongozi wenu waliopo bara msiwashinikize waachie ngazi zote warudi huko visiwani muwape kazi zingine? charity beggin at home ...waambieni na wabunge wote na wote walipo kwenye nafasi yoyote huku bara wasusie na kuachia ngazi ...sio mnajifanya hamtaki huku mmekishikilia
 

Mkuu kuwaelewa Wazanzibari unatakiwa kufanya kazi ya ziada!
 
zanzibar kuwaelewa rahisi sana, na si watafunaji maneno, wameshasema sana ila kwa ubabe na vitisho hubinywa kutepewa haki zao. na kupotoshwa madai yao, kuhofishwa na kugawanywa. kuna mmoja anasema kwa nn wasiamue tu serikali kuwapa wanachokitaka. wazanzibar wanajua viongozi wao wanatishwa na kwa hofu yao wanashindwa kuamua kwa ajili ya wananchi nakwa sasa wananchi wameamua mpaka kieleweke. na ndio ukaona uamsho wanafanya kazi ya kuamsha umma na kwa kwei umma umeamka.
 

usiwe mtumwa wa fikra, ukakubali kirahisi kuingizwa kwenye mtego wa kutawaliwa kifikra. nimekuonyesha hapo juu mapambano haya yalipoanzia. sasa utahusishaje na kutotakiwa makanisa mawili tu ambayo yamechomwa na wahuni kwa lengo la kupindisha ajenda iliopo mezani

soma historia hata huo ukristo uliletwa huko Tanganyika kutokea Zanzibar, makanisa yaliruhusiwa kujengwa tokea zamani na huyo mnaemchukia sultani ndie alieruhusu na kuwapa ardhi wajenge.

tuache hizi fitna na uzushi, ajenda sio makanisa. bali watu wanataka nchi yao
 
Hiyo picha ya mwisho hiyooooooooo! Mzee wa mkasi wameungana na Baba ritz? Faida yake nini, nani Boflo hapo?
 
Jamani kumbe fauida za muungano nyingi hivi....kwanini watu wanataka uvunjwe sasa?
 
Tusaidiane wadau

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…