Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Akili za vutu ,kuwaza kujamba tuu.
Muungano ki serikli, unawafaidisha zaidi Watanganyika kuliko wazanzibari.
Kiuwananchi ,wote tuna faidika, maana wako wabongo kibao wasaka tonge huku zenji, aidha wako wazenji kibao wasaka tonge kule Mrima.

Ama kwa kuowana ,tuna peana kimtindo .Mimi nina wandugu wawili wameolewa Bongo.

Uraisi ni hakiyetu ya Msingi tuliyozuiliwa toke a Mzee Mwinyi alipomaliza muhula wake.
Yafaa Kupeana kwa zamu uraisi wa Muungano.

Huenda Wabongo wakaondosha matabakayao kwa kupata Raisi Mzenji asiyeegemea ukanda wowote kule bara. Ila inafaa pia kuwekwa % ya viongozo kutoka bara na % ya kutoka Zenji wanaounda serikali ya Muungano. Kinyume chake Hakuna Haki na Muungano hauna Mantiki.
 
Tarehe 26 mwezi huu tunaadhimisha miaka 57 ya muungano. Miaka 57 ni umri wa mtu anayekwenda kustaafu, kama ni mtumishi.

Naomba wanaofahamu manufaa yaliyopatikana kwa Tanganyika, ambayo pengine bila kuungana yasingepatikana wanijulishe na mimi niweze kuyafahamu.
 
Nilichokigundua katika umri wangu huu ni kwamba epuka Miungano ya Kiafrika kwa gharama zote.

Miungano ya kiafrika huwa ni vurugu tupu na ukiamua kuondoka kwenye Muungano inakuwa ni Vita na mauaji makubwa.

Mfano mzuri Muungano huu wa hapa ni kumezana na kufanyana Makoloni badala ya Muungano wa haki.

Angalia Muungano wa Senegambia tena wale Wagambia walikuwa na bahati walishtuka mapema.

Angalia Muungano wa Somalia mpaka damu imemwagika mno ndio wakaachana.

Hizi jumuiya ziishie kuwa jumuiya laa sivyo tukisema tuungane Kenya itatumeza na kutufanya koloni la wavuta bange

Mimi huwa nasema kila mtu akae na kwake turuhusu muingiliano wa Waafrika ikibidi tuunganishe hadi fedha ila kila mmoja abaki na jeshi lake.

Fedha moja,Paspoti Moja,Forodha Moja hapo sawa ila sio zaidi

Muungano wa Kibiashara kufugua Masoko ila Sio Muungano wa Kisiasa

Mkitaka kujuta na kusaga meno Unganeni Kiafrika
 
Moja na kubwa kuliko yote ni uhakika wa amani hasa kipindi kile cha cold war ya Warsaw na Nato. Tukawa na siasa zisizo fungamana na upande wote wote na tukafaidisha wote Warsaw kwa uwazi na Nato kwa kinafiki. Kwa dunia ya sasa hilo halina mashiko kihivyo.

Tanganyika ni kama inalazimishia huu Muungano wa Zanzibari wanajidai hawautaki. Wakati wa mchakato wa Katiba mpya wakapawe vidonge vyao na Watanganyika akili zikaelekea kuona umuhimu wa Muungano kwa mbali.

Mgao wa kipato hapo ndio kizungu mkuti kilipo. Itafutwe formula ya sasa hiyo ya kipindi cha vita baridi Tanganyika ndio itaumia kutoa fedha kuipa Zanzibari ili muongano uwepo sioni kama inatija. Utaratibu ule wa maendeleo ya mafuta uchukuliwe kwa kila jambo lihusulo Muungano.
 
Nilichokigundua katika umri wangu huu ni kwamba epuka Miungano ya Kiafrika kwa gharama zote.

Miungano ya kiafrika huwa ni vurugu tupu na ukiamua kuondoka kwenye Muungano inakuwa ni Vita na mauaji makubwa.
Hivi watanganyika wakiona muungano hauna faida kwao wakaamua kuuvunja watapigwa na kuuliwa na wazanzibari?!
 
Mi sijui kwakweli faida kubwa mbali ya hiyo kusafiri free kwenye hizi nchi mbili.

Ila niliuliza nikapewa eti sababu za kiusalama zaidi, kwamba bara inaweza kuingiliwa na maadui kupitia Zanzibar kama zikitengana sijui maadui gani sasa wenye shida na sisi.
 
Swali hili lilitakiwa kuulizwa na kujibiwa kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar/Pemba mwaka 1964, kuliuliza sasa sidhani kama utapata majibu zaidi ya yale unayoyajua leo, vinginevyo utawekwa kwenye kundi la watu watukutu wenye nia ovu ya kuvunja Muungano na hasa kupinga mapinduzi matukufu, muundo ulioasisiwa na viongozi wetu wakuu enzi hizo.

Kama kuna watu wenye uthubutu wa kulijadili hili, kwa maoni yangu wangeanza kwa kuzichambua faida zilizopatikana kwa kuvunja tawala za machifu zilizokuwepo kabla ya ukoloni na mahali pake kuunda nchi moja Tanganyika.🤔🥱🤫
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…