Heshima kwako Rev Kishoka,
Muungano una fadia zaid kwa Wazanzibar kuliko Watanzania bara.
Zanzibar waliungana na Tanzania bara kwaajili ya usalama wao kipindi cha vita baridi.Mazingira ya wakati huu siasa za vita baridi hazipo tena na pengine ndiyo maana tunashuhudia wazanzibar wakitaka sauti zaidi kwa kutambua kitisho cha miaka ya sitini na sabini hakipo tena.
Muungano wa Tanzania bara yenye idadi ya watu 44 milioni na eneo lenye ukubwa wa 945,087 sq km dhidi ya Zanzibar yenye watu 1 milioni na ukubwa wa eneo 2,461 sq km tu ni baadhi ya chamgamoto kubwa zinazosumbua muungano.Ukizingatia ukubwa wa Tanzania bara na idadi ya watu wake ukilinganisha na ukubwa wa Zanzibar na idadi ya watu wake tayari mgongano wa kimaslahi [kisiasa,kiuchumi na kijamii] ni sababu tosha za kuyumbisha muungano.
Muundo wa muungano wa serekali mbili uliandaliwa na Mwl J Nyerere kwaajili ya kuaccomaodate kanchi kadogo sana "Zanzibar" [hakana ukubwa wa mkoa wa Tanga au Mbeya] ndani ya muungano wa nchi mbili moja kubwa "Tanzania bara".Kinachotokea sasa ni nchi moja ndogo kutaka usawa na nchi moja kubwa sana kugawana madaraka ya kisiasa na kiuchumi.Zanzibar ina wabunge zaidi ya sabini [70] ndani ya bunge la JMT, mkoa wa Dar es Salaam hakuna zaidi ya wabunge kumi [10] lakini ina idadi ya watu zaidi ya 3 milioni amabayo ni idadi ya watu mara tau zaidi ya Zanzibar.Mkuu hiki nikipengele kimoja tu, ukijaribu kuangalia vipengele vingine utabaki kinywa wazi ni kwanini tulazimishe muungano.
Mkuu wazanzibar wanatumia fursa kubwa za kiuchumi zinazopatikana Tanzania bara.Ushahidi uko wazi kabisa siku ikatokea wapemba wakaambiwa wafungashe warejee kwao hakika wangewalaumu sana wapinga muungano.Zanzibar haina rasilimali nyingi kama Tanzania bara bado wanaota mafuta amabyo mpaka sasa hakuna dalili za kuwepo mafuta ya kutosha kwaajili ya biashara.
Zanzibar haichagii uendeshaji wa serekali ya JMT,Mahakama ya rufaa na Bunge la JMT.Utashangaa wazanzibar wanadai nyongeza ya mgao wa mapato ya misaada lakini wanasahau hawachangii senti tano ya uendeshaji wa serekali ya JMT.
Ipo hasara moja kubwa sana iwapo Tanzania itaamua kuvunja muungano leo hii au siku za usoni,Ni rahisi sana magaidi kujipenyeza Zanzibar isoyopenda kufanya kazi ya kuwakomboa wananchi wake kiuchumi na badala yake inajikita kuota uwepo wa mafuta kwenye pwani yake.Tanzania itajikuta ikipokea wakimbizi wa kizanzibar maelfu kwa malaki kama ilivyotokea Burundi na Rwanda.Zanzibar wakijitenga leo tujiandae kukaa na Somalia nyingine kilometa chache kutoka Dar es Salaam na Tanga.