Muungano wa Tanzania uko katika hatua ya kwanza kuelekea kuvunjwa

Kuna mtu kakujaza ujinga kuwa Uafrika ni kuwa mweusi. Na pia umejazwa ujinga kuwa Uarabu ni kuwa mweupe.

Pole sana, huo ndio ujinga uliojazwa.

Nashukuru umekubaliana na mimi kwamba sisi watu hatukuwa wajinga kama ulivyosema. je nikuulize bara la watu weusi ni ipi duniani?
 

Averoes,Faiza Foxy na gombesugu nafyonza ilmu mujarabu.
Ahsanteni
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru umekubaliana na mimi kwamba sisi watu hatukuwa wajinga kama ulivyosema. je nikuulize bara la watu weusi ni ipi duniani?

Tafadhali acha kuwa mjinga.

Hebu pata darsa la Averoes labda utafunguka kidogo ujinga uliojazwa.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru umekubaliana na mimi kwamba sisi watu hatukuwa wajinga kama ulivyosema. je nikuulize bara la watu weusi ni ipi duniani?

magwanja,

Kuna philantropist mmoja kule USA ni Mmarekani Mweusi ametoa lecture kuwa watu weusi wenyewe ndio wabaguzi, usifanye nikakubaliana nae mimi, kwani katika kitabu gani Mungu amesema nimetenga bara hili la watu weusi?

Maana Wahindi walio wengi ni weusi na ndio wahindi original, Wa srilanka, Bangladeshi, Shirazis wa Iran (Kush) aborigines wa Australia, Khmer wa Cambodia wote hao ni weusi sasa wote hao utawaweka bara gani?

Unajuwa kuna watu weusi USA wanakwambiwa wao ni Americans tu sio Africans. Soma
 
Averoes,Faiza Foxy na gombesugu nafyonza ilmu mujarabu.
Ahsanteni

Mkuu,

Tangia jana nalikhis,yakua huyo jamaa Maganjwa hana ubavu wa hoja za kitaaluma...ndo maana nikamsihi hata Mkuu Averoes amwonee "huruma" japo kiduchu! Teeh! Teeh! Teeh!

Khalaf jamaa kama wa sampuli hiyo ati ndo wanajisifia ati "wamesoma" na kutia mbwembwe...huku wakieneza chuki na tashtit zao humu mitandanoni! Daah!

Karibu kijijini-Makete Mkuu Boko Haram...sisi bado tupo huku tunaendeleza zile "sera za ujamaa na kujitegema"...kama alivyotuamrisha yule "Baba wa Taifa"! Daah!

Ahsanta.
 
ww ni walewale, unadhani kila mtu kasoma bure kama ninyi mnavyosoma bure. Mimi baba yangu alinilipia ada, sijasoma bure, sijapendelewa shuleni ili kuleta uwiano.
Sijawahi azima akili yako, siongozwi kufikiri kama wewe ambaye huna mawazo huru, mbaguzi mkubwa wewe, huna hata haya unanivua uraia mtandaoni (kama kawaida yenu mkishindwa hoja mnavua watu uraia wao halali) unadhani utaweza
 

shida ni kwamba ukweli kuhusu sisi waafrica haujawahi kuongelewa wazi barazani ndio maana unaona kama ubaguzi wa rangi hoja yangu ni historia yetu kama watu waafrica tukiongelea sio kwamba sisi ni wabagizi.
 

Je wewe unaonaje wazungu kututangaza dunia nzima kwamba sisi waafrika hatuchangia katika ustaabu wa dunia hii ni sawa? na sisi tukianza kuwa jibu wewe unasema ubaguzi nikisema wewe umedumazwa kiakili kuona umuhimu wa kuongelea historia yako. nakuomba angalia clips hizi na fungua akili yako uelewe. Uelewa tunatofautiana sana hasa ukifundishwa uwongo ukauamini ni shida sana.
 
Last edited by a moderator:
Tafadhali acha kuwa mjinga.

Hebu pata darsa la Averoes labda utafunguka kidogo ujinga uliojazwa.

wewe si hutaki kukubali pamoja na fact niliyokuonyesha nimekuuliza swali ulitakiwa ujibu na uniconvince ili nikubaliane na wewe hujanipa hoja unawezaje kuniita mjinga.
 
Ati vile uko muungano wa kuvunjika au kuna wa kumeguka !!! Swali nipeni majibu ! sijaona lazima au faida ya huu muungano wa lazima.
Wacha kila mtu achukue zake kabla hakujaharibika zaidi.
Ikiwa Zanzibar hawaoni maslahi ya muungano kwa Tanganyika wanashikilia kuwepo kwake hiyo clearly huu muungano uko one sided.
Fikiria hiyo utakuta ndugu zetu wa kisiwani wame istukia dili.
 

Then what!!! that is how they think about us is that true according to you? what do you want to say then?

My opinion is to refuse ideas like this with evidence and teach new ideas to our people that prove the wrong ideas like this.
 

Teeh! Teeh! Teeh!

Mkuu naona hilo suala la uraia limekuumiza mno!? Daaah! Pole sana! Teeh! Teeh! Teeh!

Mimi nafahamu yakua wewe Mkuu lazima ulisomeshwa bure ile enzi yenu ya "Mwalimu",au!?...watu kama nyinyi mbona mpo wengi tu humu-JF...na hata kufikiri kwenu pia kumeathirika kwa ile elimu ya "bure" alokupeni yule Kambarage!

Ahsanta.
 
Kwelikabisa cion umuhimu wakuwabembeleza hawa wazenji kwasababu tanganyika tunawabeba sana kivyovyote wanadai wanaweza kujiongoza so tanganyika tuwabembeleze kwa kipi hapo wanakatiba yao na wimbo wao wabunge wa bara fungukeni jamani wajukuuwenu na vitukuu watakuja kuwalilia makaburini kwenu serikali tatu ndo mpango mzima hakuna chaziada hapo watanganyika tunataka wimbo wetu kama nchi ya tanganyika na bendela yatu pia nakatibayetu nawahasa wanasiasa naviongozi mbalimbali ambao sauti zenu zinaweza kuckika kilahisi tofauti na cc watanzania cc ndotunajua watanzania nn tunataka ikisjindikana serokali tatu kuvunja muungano ni muhimu pia hayo nimaoniyangutu wanasiasa tunawategemea
 


Huyu hawajui wa znz.
Wa znz hawataki kuvunja muungano . Wanachotaka ni uhuru zaidi ili nchi yao ifaidike na mahusiano na wengine bila kubanwa na masharti ya mungano.
Wawe huru katika katika mambo kiuchumi sarafu mikopo na misaada bila ya kubanwa na masharti ya muungano.
Tumeona miaka 50 namna gani uchumi wa znz ulivo poromoka kutokana na muundo wa muungano. Mfumo wa muungano ndio sababu kubwa ya kuanguka uchumi wa znz ma bila kupata msaada wa maana kutika serikali ya mungano kujikwamua.
Wakati tanganyika ikisaidiwa kujikwamua kiuchumi toka wakati wa mwinyi mkapa na sasa kikwete mazungumzo yote na mashirika ya fedha nje kama world bank IFC au IMF
Tanzania imefanya mazungumzo na mashirika haya kwa niaba ya tanganyika na wamesaidia sana kukwamua uchumi wao kwa kupewa ushauri na fedha . Katika masharti yale tanganyika ilikubali masharti magumu ili kupata kupata misaada hio kutoka mashirika ya fedha.
masharti hayo ni kubinafsisha makampuni na mashirika ya umma,
Kufungulia njia makampuni ya nje kuwekeza
Kubinafsisha ma benki
Na kubwa zaidi ambalo ulikua ni mwiba mkali ni lazima wakubali kushusha thamani ya fedha ya Tanzania.
Kutokana na hali ngumu walokua nayo serikali ya tanganyika ndani ya muungano walikubali kuumeza mwiba huo na kukubali kushusha thamani ya shilingi .
Kabla ya masharti haya USD $ 1 =Tshs 20 tu. Hii imekwenda mpaka sasa ni shs 1630.
Na hali ya uchumi na uwezo wa SMZ wakati huo haikua mbaya ulikua mzuri tu wa kujiweza.
Serikali ya mungano kwa niaba ya mambo ya tanganyika wakapokea misaada mikubwa na mikopo baada ya kukubali masharti ya IMF na World Bank.
Nini kilitokea ? Wakati tanganyika ikifaidika na misaada hio, Zanzibar ndio mwanzo wa kuanza kuporomoka uchumi wake .wao hawakupata fidia yoyote kutokana na Tanganyika kukubali kushuka kwa Shilingi.
Bajeti yake ilianza kuharibika mfumuko wa bei ukuwa juu bei ya mafuta ukawa juu . Wakati tanganyika ikipata misaada kujikwamua zanzibar ikaachwa kufa kabisa kiuchumi.
Muundo wa sasa wa muungano hauruhusu znz kuingia katika mikataba mashauriano au kupata misada kuwa na mahusiano yoyote na mashirika ya fedha au mashirika ya kimataifa kama FAo ,Unicef,UNdp,IMF au hata Comminwealth,OIC au hata mashirika ya mahusiano na umoja wa visiwa vya Indian Ocean !!
Hivyo mfumo uliopo haufai kabisa. Utakua unafaa kama kuna nia ya kuimaliza zanzibar kiuchumi na kuifanya wawe mafukara wa kutupwa.
Nadhani sote nia yetu tunapenda kuona Tanzania bara inaendelea na kusonga mbele na pia tunapenda kuona Zanzibar nao wanaendelea kiuchumi na sio tegemezi.
Kutaka serikali 3 sio kuvunja muungano ni njia nzuri ya kuumarisha kukiwa na njia njema .
Kuwa na serikali tatu sio sababu ya kuanza kuchochea chuki, sio sababu ya Tanganyika kuwabana wazanzibari na kadhalika.
Haubadili mahusiano yetu bali kuleta mfumo mzuri zaidi utaoboresha mahusiano na uchumi wetu.
Huyu mheshimiwa ametaja kuhusu ardhi na wafanyabiashara wa znz walioko walioko bara ni kweli wa znz wapo Bara na wanafanya kazi na biashara lakini wanasaidia kujenga uchumi wa bara na sio znz. Kiserikali znz haifaidiki chochote hakuna hata anaeweka akiba yake katika benki ya znz
Na pia huyu mheshimiwa ni katika watu wa kuogopwa kama ukimwi ni mbaguzi,mchochezi ndio maana maoni yake ameleta upemba na uunguja.
Hasemi kuwa Tanzania bara walotaka serikali 3 ni 66% ila yeye ameona wapemba tu. Ni Racist mkubwa.na hawa ni katika wale ambao serikali ya muungano inapoteza fedha nyingi kuwaweka madarakani ikadhaniwa kuwa wataendelea kuulinda muungano kwa porojo na propaganda.ukweli tanganyika haihitaji kupoteza fedha kuwa na mamluki kutoka znz eti waunge mkono muungano hata kama unaizika znz na kuwafanya omba omba.vibaraka hawa wanazidisha tu ari na morari ya wa znz kuuchukia muungano.
tuufanye muungano huu uwe wa wananchi na wananchi wataupenda na wataulinda , hakutakua na sababu kwa serikali ya bara kuwalinda na kuweka vubaraka kama hawa huku ikigharamika bure.hawa wanapigania matumbo yao na ndio walio influence CCM kuweka msimamo wa serikali 2 japo kwa gharama ya 66% ya watanzania bara waliotaka serikali 3.
Serikali tatu ndio suluhisho la kupata muungano wenye nguvu zaidi.
Hata wakati wa apartheid kule afrika ya kusini walikuwapo waafrika na waliojifanya wazalendo sana lakini walikubali mfumo ule wa kibaguzi .wakakubali kuwa viongozi wa zile bantustans. Na walikubali kupewa uhuru wa hizo bantustan na kupewa "urais" mimi namfananisha huyu seif khatib na buthelezi aliepewa kaji urais wa wazuli !!!
 
wewe si hutaki kukubali pamoja na fact niliyokuonyesha nimekuuliza swali ulitakiwa ujibu na uniconvince ili nikubaliane na wewe hujanipa hoja unawezaje kuniita mjinga.

Bado hujamsoma Averoes?
 
Unaonesha ni jinsi gani ulivyo na unavyojifanya huelewi, ubaguzi utakuua ww. kwa kuwa wewe umesomeshwa bure kwa hiyo unaona kila mtu kasomeshwa bure, sikusomeshwa ili kupata uwiano. Ni uwezo wangu kiakili darasani ndiyo umenifikisha hapa kielimu sio kubebwa ili kupata uwiano
 
Bado hujamsoma Averoes?

ile notes za kukaririshwa nisome nini pale angeniambia nyuma ya ukuta kuna nini sawa ila habari zile tumeshazoea na ndio ambayo hatutaki na wewe ni mojawapo kati ya waliokaririshwa mpaka unaona kitu kipya ni nilichokuonyesha kichwani mwako hautaki kukifikria hata kidogo nakuomba kaa chini kidogo uiangalie kwa umakini utagungua vitu vipya kabisa.
 
Kwani kabla ya muungano zanzibar ilikua wanaishi vp? ata ukivunjika leo washindwe kujiendesha. Mimi naona znz watafaidika zaidi wakiwa nje yamuungan.angalieni miaka 20 yanyuma znz ilivokua na anagalieni tanganyika ilivokua ikisha mtapata jibu kwann wazanzibari wanalalamika. Kiufupi muungano umeuwa uchumi wa zanzibar kwaiyo wanataka nchi yao. Kama znz ni mzigo kwann tumewang'ang'ania? Tuwawache wapumue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…