Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Haya yote kayataka baba wa Taifa, akili yake haikuwaza sawasawa
 
Duh, kwa hiyo wakati wa kulipa, Zanzibar itabidi walipe hiyo Bil 231 au nani atalipa hiyo hela, maana ni mkopo ujue.

Bila shaka, Zanzibar hairuhusiwi kukopa, mkopo ukija wa JMT nao wanapewa chao, ila kuna tatizo, formula ipi inatumika? Sbb Zanzibar ina watu wachache sana, sasa naona hela kama kubwa sana inaenda huko.
 
Kero za Wazanzibar ni kupewa tu! hakuna hata siku moja wamedai kuwajibika.
Hawajui muungano unaendeshwaje lakini wanajua kugawana
Laah!
Kipindi cha siasa za unafiki nadhani ndiyo kinaelekea mwisho wake. Tutakapoondokana na hali hiyo, hapo ndipo tutakapoanza kwenda mbele kwa uhakika.
Nafarijika kwamba hakuna tofauti kati yetu kuhusu Muungano.
 
Tukome kiherehere! Kila siku watu kama kina Kikwete wamekaa kimya. Walifikiri raisi atatoka bara milele wakati kwenye katiba wameweka kipengele lazima makamu atoke Zanzibar. Hapo acha watukamue vya kutosha labda tutaelewa vizuri. Tunajidai eti tunawachagulia rais then what? Halafu nina swali kuntu... Hivi hizi hela huwa zinakaguliwa na CAG wetu? Au tunatoa then zinapotelea kinyemela nyemela Zanzibar maana nauona mwanya mweupeeeeee usio na kiulizi. Hazitakaa zifikishwe bunge la muungano na kule Zanzibar hatutakaa tusikie maana upinzani na serikali wanakula meza moja. Zidumu fikra za mwenyekiti Nyerere! ZIDUMU
 
Tuanzishe utaratibu wa Zenj kukopa Tanganyika na warudishe kwa ribà! Tanganyika ikope kwa jina LA muungano nà badala ya kugawana na Zanzibar wao wakopeTanganyika!! Mgao ni wa kutumia tu lakini mkopo ni wa kutumia na kurejesha!! Kwa Sasa kama ambavyo sekta ya Elimu inavyopata mgao na kutumia bila kurejesha ndivyo Zanzibar inavyopata mgao na kutumia bila kurejesha!!
 

Andika katiba mpya tufuate maoni yako
 
Watanganyika Wana hoja, wasikilizwe!

Wazanzibar Wana manung'uniko, wasipuuzwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…