Binafsi ningetegemea kuwa kuna utaratibu maalum unaoeleweka wa mambo kama haya kufanyika. Kama utaratibu huo upo, na ulishajadiliwa na kukubaliwa, basi, tutafute jibu huko. Na kama bado hairidhishi, kwa maana kwamba utaratibu uliopo siyo sahihi, ufumuliwe na uwekwe wenye uwiano unaostahili.
Mkuu utaratibu upo lakini kuna hila.
Utasikia kugawana tu hakuna utaratibu wa kulipa madeni au kuchangia muungano.
Lakini kama mambo haya sasa hivi yanafanyika kama mazoea tu, kwa vile mkuu ni wa kutokea huko, basi haifai hata kidogo kuyanyamazia.
Hili linajidhihirisha kwasababu Wazanzibar waliolalamika sana hutuwasikii tena
Nadhani litakuwa ni jambo muhimu la kutumia ule utaratibu ambao mara nyingi umetumiwa na sehemu moja ya muungano, utaratibu unaoitwa 'KERO ZA MUUNGANO"..., sasa Kero zitakuwa zinaelekezwa upande wa pili (Tanganyika), badala ya kulivyozoeleka kuwa zinaelekezwa Visiwani.
Kwanza, kero za Zanzibar zimemamalizwa kwa siri sana hakuna anayejua zimemalizwaje.
Tunachojua Wazanzibar wameridhika, sasa nani amesimama kwa maslahi ya Tanganyika?
Pili, Tanganyika hawana kero, wanachotaka ni kuwajibika na kutoumizwa
Kwamba, Zanzibar iwe mshiriki wa muungano kuchangia si mshiriki wa kugawana
Kwamba, rasilimali za Tanganyika si haki ya Zanzibar ni fadhila
Kwamba, Zanzibar wapate haki kulingana na siyo kwa hadhi tu. Mfano, mgao wa mapato kwa Zanzibar ni mkubwa kuliko mkoa wa Mwanza, lakini mchango wake ni '0'
Kwamba, kuendesha muungano na taasisi ni jukumu la wote si mzigo wa Mtanganyika
Kwamba, muungano uliopo haupo , Zanzibar ina kila kitu chake
Hapa ndipo watu wanaitaka Tanganyika kila mmoja asimame na masilahi yake
Pili, hii ni hela ya mkopo, mkopo unaotolewa kwa serikali ya Tanzania, na ni hiyo hiyo itakayolipa mkopo huo. Kwa maana halisi ni kwamba sehemu kubwa sana italipwa na watu hao milioni 55 walioko sehemu moja ya Muungano, na wale milioni moja, uchangiaji wao katika kuulipa huo mkopo ni mdogo zaidi.
Zanzibar hawawezi kulipa mikopo! wanapata wapi uwezo wa kulipa mabilioni tajwa.
Tangu 'zamu yetu' mipesa ni zaidi ya bilioni 500.
Zanzibar makusanyo yake kwa mwezi ni less than 100B , deni wanalipaje?
Ni mfano ule wa Baraza la Wawakilishi lina wajumbe 50 kwasababu wanalipwa na SMZ.
Wabunge wa Zanzibar Dodoma ni zaidi ya 80 kwasababu wanalipwa na Tanganyika
Mzigo wa deni ni wa Mtanganyika si Mzanzibar. Kwanini! tumeomba tuonyeshwe formula ya kulipa deni hakuna! tuonyeshwe formula ya kuchagia! hakuna
Ni utaratibu ule ule wa Zanzibar kupewa 4.5% ya pato la Tanganyika.
Kwamba, uchumi wa Tanganyika unavyokua Wazanzibar wanavuna tu!
Wanasingizia mchango wao BoT bila kujua kuwa mchango huo si sawa na pato la nchi.
Watanganyika wanauliza, formula za kugawana zipo za kuwajibika zipo wapi?
Baada ya kuyasema haya, nami naungana nawe katika kuuona huu utaratibu wa mgawanyo kama "KERO" hasa, kwa wale walioko Bara.
Kugawana hakuwezi kuwepo bila kujua tunagawana nini.
Kugawana kuliopo ni kugawana vitu vya Tanganyika. Zanzibar ni 'ZERO' katika mchango
Kinachotakiwa sasa hivi ni kurudi kwenye rasimu, mambo 7 tu
Kwanini mambo 7 ya Rasimu ya Warioba!
Hakuna sababu ya lundo la Wabunge wa Zanzibar wakilipwa kwa kodi za Watanganyika wakijadili bei ya mafuta bara, mishahara bara, umeme bara, maji bara, kilimo bara, afya, elimu, nishati , Tamisemi, mifugo na maji. Haya hayawahusu.
Mbunge wa Zanzibar anakuwa katika kamati ya Bunge kukagua TAMISEMI kwasababu zipi? Tamisemi haiwahusu Zanzibar!
Gharama za kuwaweka Dodoma zielekezwe kujenga Hospitali na shule au mikopo ya wanafunzi. Kwanini wanajadili mambo yasiyowahusu?
Pili, wanatakiwa kuwepo kujadili mambo 7 tu tena waje kwa gharama za SMZ kwasababu wanawakilisha Zanzibar (Rasimu ya Warioba)
Tatu, hatuna sababu za kuwa na taasisi ambazo tayari Zanzibar wanazo.
Tunalipia kama Tanganyika ila Wazanzibar wao wanakuja kwa ajira na si gharama!
Nne, kila serikali itabeba mzigo wake na SMZ itakuwa na uwezo wa kukopa Trilioni 600 bila kuulizwa kwasababu watalipa, sasa hivi wanakopa tu kwasababu bili analipa Tanganyika!