Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Hivi karibuni kumekuwa na kauli zenye mwelekeo wa kibaguzi kutoka pande mbili za muungano wetu. Na mpaka sasa hatujasikia kauli thabiti ya serikali kuzikemea kauli hizi.
Wasiwasi wangu, kauli hizi zikiachwa zishamiri zitauingiza muungano wetu kwenye mgogoro mkubwa. Tusisahau mdharau mwiba huota tende.
Nadhani ipo hoja na haja ya kuwa na mpango endelevu wa kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu na faida za muungano kwa nchi yetu. Pengine itatusaidia kukabiliana na hisia za kibaguzi miongoni mwa wananchi yetu.
Mwisho, ni muhimu serikali zote mbili, Bara na Zanzibar zikaanza kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa ngazi za juu hususani wabunge ambao wamekuwa wakitoa kauli zenye utata kuhusu muungano. Viongozi ni kioo cha jamii, wanapotoa kauli tatanishi wanapanda mbegu mbaya kwa wananchi.
Mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe.