KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Wasalamu
Kama ilivyo ada, ninapenda kuchukua nafasi na muda huu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na Uhai. Pia ,ninawapongeza viongozi wa serikali wakiongozwa na Rais Samia kwa juhudi na jitihada mbalimbali wanazoonesha katika kuongoza nchi yetu kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.
Moja ya maslahi ya Taifa yanayozingatiwa na viongozi wetu ni kudumisha Muungano. Ninawapongeza wale wote wenye mtazamo wa kudumisha Muungano bila kujalisha changamoto zilizopo.
Binafsi, ninatambua Muungano wetu unafaida nyingi na kuendelea kudumishwa ni faida kubwa. Nchi nyingi zinatamani kuungana kulinda maslahi yatokanayo na Muungano lakini nashangaa baadhi ya watu kuukejeli, kuubeza na kuubagaza Muungano wetu kwa hoja nyepesi na kufikia hatua kudai uvunjwe.
Changamoto za muungano zimezungumzwa sana na ni za kipindi kirefu lakini hoja za kuvunja Muungano ni dhaifu mno. Bado Muungano ni imara hauna matatizo.
Siku za karibu nimeona suala la teuzi wa wakuu wa wilaya kwamba kuna wazanzibar wameteuliwa ukuu wa wilaya Tanzania bara huku Zanzibar hakuna wakuu wa wilaya kutoka Tanganyika na watu kupelekea kuujadili Muungano na wengine kuubeza na kusema uvunjwe hauna faida kwa Tanzania bara.
Hoja hii ni dhaifu sana kuwaza kuvunja Muungano. Hoja hii ilitakiwa iwe ni mjadala na baadala ya kujadiliwa uamuzi utolewe. Changamoto za muungano zinajadilika na kutamani uvunjike ni kukubali uwezo wako wa kutatua changamoto ni mdogo.
Kwa manufaa na mustakabli wa Muungano, Serikali ianzishe jukwaa maalumu la kuujadili na kujadili changamoto zake ili udumu zaidi kwa maslahi mapana yaliyopo.
Kwa mara nyingine ninaipongeza Serikali kutatua mara kwa mara za Muungano na kuufanya ni moja ya Muungano iliyoendelea kuwepo mpaka leo.
MUUNGANO HAUNA MATATIZO ILA UNA CHANGAMOTO zinazojadilika na kutatulika ,hoja yoyote ya kuuvunja Muungano haina mashiko wala haioneshi uelewa wa faida, umuhimu na fursa za muungano kwa wote wenye hoja hiyo.