Muziki kama Pesa: Iga Akili ya Diamond, Usiige ubongo wa 20%

Muziki kama Pesa: Iga Akili ya Diamond, Usiige ubongo wa 20%

unachekesha sana unashindwa kujituma unasingizia chama cha siri! kaa hivyo hivyo na mawazo mgando watu wanapiga pesa na mwisho wa siku mnakaa vijiweni kuwasema ni freemasons

Mkuu,Unajua maana ya 'tetesi'
^^
 
Hope mafanikio ya diamond si kwenye muziki tu na media bali mpk katika maisha yake binafsi na future yake kwa ujumla
 
ujumbe Mzuri Ila Ulipomtaja King Wangu Kiba
Lihabari Lako Nimelichukia Vibaya Sana
ahsante Jigo

hapa ndipo unapokosea binamu, asipotajwa atajulikana vipi jamani??? kwani kamtaja kwa ubaya???
 
Huyu mwandishi hunivutia sana,, aina hii ya wandishi wamebaki wachache sana,, asante sana luqman hata sis wahamiaji haramu huku Congo tuna liona hili. kwa DRC, msanii wanaemjua toka Tanzania ni Diamond Platnumz, huyu kijana wa mama Nasibu alianza kwa kuvuma mashariki ya Congo yote,, South and North Kivu, baadae akapanda mpaka mbali zaidi. Mwezi wa 11 nilikua kinshasa wenyewe wanaita KIN,,, nimekuta diamond nyimbo zake zinapigwa club. Labda niseme ukweli DR Congo kupata fursa ya kupenya na mziki wako upigwe club hasa Kinshasa na kwenye club maalrufu kama Chez ntemba. si mchezo kwa waliofika KIN wanajua nisemacho... Huyu kijana kajitangaza sana tuache ushabiki maadazi huwezi mlinganisha na na mwanamuziki yeyote east Afrika kwa sasa. Mwingine ambaye mpaka leo japo ni marehemu ni Kanumba ,, mpaka leo DR Congo hasa mashariki analiliwa,, wakati sisi msiba tukiwa tumeusahau wacongo bado wana mlilia Kanumba. ni hayo tu vijana wangu

Mkuu ulipotaja Kivu aiseee kuna sehemu ninafanya kazi wamejaa raia wa kicongo hatari nimeona kama umenigusa flani hivi aiseee...ingawa sijawahi fika DRC ila hawa wabembe wa huko kivu wenyewe wanaita Sud Kivu aiseee wananisimuliaga sehemu za huko mpaka nimezikariri kuanzia huko sebele, Nemba, Ruchuru, ebana tafkiri na mimi ni mkongomani aiseee...daaahh...
 
MR. CONFIDENT shikamoo umecompare na kukontrast mpaka X ikawa = 2, team kiba na mondi wakipita hapa wote ule ujinga wetu wa kutoleana mapovu kule kwenye special thread zetu utakuwa umepata panadol.
 
Last edited by a moderator:
Si mlishawashindanisha kwenye fiesta ? Na jibu mkalipata !

20% media zinambania kiukweli anatoa nyimbo nzuri mpka kesho ila nazckia TBC tu
inawezekana anabaniwa ila nyimbo ikiwa nzuri utapigwa tu na hata wamachinga kwenye toroli,ile albam ya 20 iliyopita mi nilianza kuisikia kwa wamachinga,ila ukweli sasaivi 20 amefuria toka agombane na man water
 
Mkuu ulipotaja Kivu aiseee kuna sehemu ninafanya kazi wamejaa raia wa kicongo hatari nimeona kama umenigusa flani hivi aiseee...ingawa sijawahi fika DRC ila hawa wabembe wa huko kivu wenyewe wanaita Sud Kivu aiseee wananisimuliaga sehemu za huko mpaka nimezikariri kuanzia huko sebele, Nemba, Ruchuru, ebana tafkiri na mimi ni mkongomani aiseee...daaahh...

Karibu sana niko Goma ila kwa leo nimekuja huku Beni,,, hahahah vipi Butembo, Bunia, Masisi, Kirumba, mambasa, walikale, ndo mambo ya huku......
 
Hivi hawa wasanii wetu wanauza nyimbo itunes, maana huko ndo watu wanapiga hela, waweza kukaa hata mwaka bila show na ukawa bilionea wa ajabu, mfano rihanna alipotoa wimbo wa diamonds aliuza copy zaidi ya mil.3,ukifanya copy 1 sawa na dola 1 utapata dola mil.3, hapo ni nyimbo moja tu, mimi naona hawa wasanii wetu wangejipenyeza huku kuliko kuishia shoo za ajabu ajabu
 
Ila usela mav ni tabu sana, raia tulijipinda kumpigia kura akaondoka na tuzo 5 fadhila alizokuja kutulipa mashabiki ni kupuliza mibangi hadharani, 20% please just go to hell, bahati haiji mara2. Nakumbuka miezi michache baada ya kutwaa tuzo 5 wasanii walikuja Mbeya kwenye fiesta akiwepo na 20%. Kwavile wasanii walikuwa wengi na mda ulikuwa umeenda B12 alikuwa anawacontrol wasanii wasiimbe zaidi ya nyimbo 3, but alipoingia 20% akawa anataka kuimba nyimbo zake zote sijui maana alikuwa anaimba nyingine ambazo hata hatuzijui, B12 akamstua 'time' amalizie awape nafasi wasanii wengine cha ajabu jamaa akazira akaweka mic chini akasepa bila hata kuaga mashabiki. Yaani mashabiki tukabaki tunashangaa tu alichokifanya jamaa. Kuanzia sikuile sitaki hata kumsikia
 
Umeharibu kuanza kusema Diamond anavuna alichostahili Ali Kiba na pia Ali Kiba ana kipaji kuliko Diamond.Huo ni mtazamo wako. Kipaji umekijudge kwa ku-consider nini. Kumbuka kipaji sio kuwa na sauti nzuri pekee. Kuandika mashairi kiustadi pia ni kipaji, kucheza pia na kwenyewe ni kipaji..Hivyo Diamond anastahili kuwepo alipo kutokana na kipaji na juhudi zake. Ali Kiba nae hivyo hivyo kwa nafasi yake. Kwahyo usitushawishi wote tuamini kwamba Ali Kiba ana Kipaji zaidi ya Diamond.Ungesema ni mtazamo wako ungekuwa sahihi zaidi.
 
Back
Top Bottom