Muziki wa bongo fleva ni haramu katika dini ya Kiislamu?

Muziki wa bongo fleva ni haramu katika dini ya Kiislamu?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Bila shaka kila mtu atakubali kwamba wanamuziki wanaofanya vizuri zaidi katika muziki wa bongo fleva na taarabu ni wanaotoka Pwani na hasa kutoka jamii ya Kiislamu, wanaofanya vizuri katika muziki wa injili (muziki wa mungu) ni kutoka bara, mkoani Mbeya.

Ambacho huwa huwa sielewei vizuri ni hii habari ya masheikh kadhaa kuwasikia wakisema muziki ni dhambi ila sina uhakika kama ni mtazamo wao tu au hii ni kwa mujibu wa mafundisho ya dini kutoka kwenye Quran na Hadithi za mtume.
 
Quran haijataja bongo fleva, ni kiherehere chenu tu
 
Mnataka muongezee aina ya dhambi ambazo mtume hazijui
 
Music ni haraam katika Uislam. Wanajitoa ufahamu tu.
 
Bila shaka kila mtu atakubali kwamba wanamuziki wanaofanya vizuri zaidi katika muziki wa bongo fleva na taarabu ni wanaotoka Pwani na hasa kutoka jamii ya Kiislamu, wanaofanya vizuri katika muziki wa injili (muziki wa mungu) ni kutoka bara, mkoani Mbeya.

Ambacho huwa huwa sielewei vizuri ni hii habari ya masheikh kadhaa kuwasikia wakisema muziki ni dhambi ila sina uhakika kama ni mtazamo wao tu au hii ni kwa mujibu wa mafundisho ya dini kutoka kwenye Quran na Hadithi za mtume.
muziki ni haramu hata aimbe nani
 
Muziki,qaswida na izo nashid zote ni haramu kwenye Uislamu yani kila sehemu yenye Ala ya muziki ni haramu kwenye Uislamu
 
Muziki,qaswida na izo nashid zote ni haramu kwenye Uislamu yani kila sehemu yenye Ala ya muziki ni haramu kwenye Uislamu
weka vizuri kwasida wanapiga wanawake na zina ala ambazo ni dufu ni ruksa sheria haijakata, fafanua ili usikosee.
 
Kina diamond, zuchu, jux, harmonize hawa ni waislam wa kuchovya hawalijui hilo
 
Kama bongo feva wanaimba na kucheza wale tu na kitimoto hawatadhurika
 
Hakuna kitu haramu kwa kobazi zaidi ya kuwa mkiristo
Vingine vyote halal
 
weka vizuri kwasida wanapiga wanawake na zina ala ambazo ni dufu ni ruksa sheria haijakata, fafanua ili usikosee.
Dufu lina ala za muziki? Ukiona sehemu yeyote ile wameweka Ala za muziki basi ujue uharamu umeshaingia
Dufu linaruhusiwa kwenye Uislamu ila sio hili la siku hizi changanyikeni kama kigodoro
 
Dufu lina ala za muziki? Ukiona sehemu yeyote ile wameweka Ala za muziki basi ujue uharamu umeshaingia
Dufu linaruhusiwa kwenye Uislamu ila sio hili la siku hizi changanyikeni kama kigodoro
dufu yenyewe ni ala
 
halafu uliza nani "alianzisha" na kuleta hata ku-promote ushenzi na hata ushetani kwenye real music tuliokuwa nao? ni wao wenyewe, wakati ya Nyerere tulikuwa na real music kama moro jazz, tabora jazz, kulikuwa na vipaji kama Remi ongala, vijana jazz etc kulikuwa na real musicians wapiga gitaa au wapuliza saxophone mahili kabisa, muziki wa heshima tuilikuwa nao tulikuwa tunaweza kwenda kucheza dance kwa heshima kabisa ila "muziki" wa kufoka foka faka aka rap music ulianzia awamu ya pili ya raisi Mwinyi pia wakati wa Nyerere na B:Mkapa tulikuwa na filamu real na nzuri kama kaole iliyotoa vipaji vizuri tu hakukuwa na aina ya ushenzi wa muziki na filamu zilizopo leo hii, hii bongo bs ya sasa hivi imeanzia awamu ya 2,4 na sasa hivi ...
 
Back
Top Bottom