Muziki wa zilipendwa na vijana wa kisasa

Muziki wa zilipendwa na vijana wa kisasa

Cytochrome p450

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Posts
5,638
Reaction score
15,044
Habari viongozi,

Jana nimetoka kumsikia mtoto aliyezaliwa kwenye miaka ya 2004 (15) akiimba wimbo wa Kilimanjaro Band uitwao Boko.

Sasa najiuliza hawa vijana, wanawezaje kuimba nyimbo ambazo kipindi zinatamba wao hawakuwepo?

Au hizi nyimbo zinarithishwa kama zinavyorithishwa genetic information kutoka kwa wazazi wao?

Naomba mawazo yenu wakuu.
 
Nyimbo za zamani zilitungwa na kuimbwa kwa ufasaha mkubwa zikiakisi yaliyopo na ya yajayo ! Huoni hata vijana wa Leo wanaimba na kusakata Georgina wimbo wa Marijani Rajabu ! Miziki ya Leo ni sawa na moto wa mabuwa, ile ya zamani ni makaa ya mawe 🙂

Wimbo wa sasa: hapo vipi, hapo sawa hapo vipi, hapo sawa 🎵🎶📣

Wimbo wa zamani: Nawashukuru wazazi wangu wakati wowote, ushauri wao umeniletea mafanikio mema tantararaa 🎵🎼🎷🎸🎺🥁🔊

Kuna tofauti kubwa sana !
 
Wkt nakuwa nilikuwa nikisikia milindimo na vionjo vya miziki hiyo zilipendwa! Nimekuwa muhanga mkubwa wa nyimbo hizo kiasi kujidhania ile dhana ya kuwa ukifa unazaliwa tena ni kweli!! Ni Kama vile nilikuwepo miaka hiyo nimezaliwa Tena! Napenda sana miziki ya zamani
 
Umekuja kuzipigia promo nyimbo zenu za kizamani.

Mbona kuna wazee wa miaka themanini wanaimba nyimbo za Alikiba. Alikiba wala hajigambi maana hapendi Show off.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi ni mmoja wa wapenzi pia wa nyimbo za kale ingawa sikuwepo. Kinachotokea ni kuwa wakati nakuwa nimezisikia kwa watu wazima wakizisikiliza n.k. kumbuka pia hazijaacha kupigwa redioni.
 
Havipewi pesa ya kwenda kujirusha, vinakuta vinasikiliza ile miziki ambayo mzee anasikiliza hapo sebuleni, ukibadili stesheni tu umechezea kichapo..
 
Mimi huwa najikuta nakunywa bia kwenye bar wanazopiga copy za live band za mziki wa zamani ingawa si wa kizazi hicho. Hizi ngoma zina utamu wake aisee.
Zamani walikua wanatumia vyombo live kutengeneza muziki..

Sasa hivi teknolojia imekua sana,, inatumika computer kutengeneza mziki..

So, livebands wanalazimika kupiga nyimbo za zamani kwa sababu ni rahisi uki"compare na hizi nyimbo za sasa..

All and all,, muziki wote ni bora inategemea tu na umeusikiliza upi kwa kipindi gani, na unakukumbusha nin...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani mazingira na wazazi huchangia,mfano mimi sometimes nasikiliza Fela kuti,Jimi Hendrix,Dk Remmy,Peter tosh,Bob Marley,oliver Mutukuzi etc kwa kuwa ndiyo muziki uliokuwa unapigwa na mshua nikiwa kinda.
 
Back
Top Bottom