Mvua ilivyoharibu miundombinu ya Barabara Sumbawanga - Rukwa, Waziri Bashungwa atembelea

Mvua ilivyoharibu miundombinu ya Barabara Sumbawanga - Rukwa, Waziri Bashungwa atembelea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-04-09 at 13.46.23_3de61451.jpg

WhatsApp Image 2024-04-09 at 13.46.23_3bc8425e.jpg
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inarejesha miundombinu ya barabara ya Kasansa - Muze - Mtowisa - Ilemba - Kaoze - Kilyamatundu (km 180) iliyoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo tofauti tofauti nchini.

Bashungwa ameeleza hayo Aprili 08, 2024 Mkoani Rukwa wakati akikagua barabara hiyo na kuwahakikishia Wananchi kuwa Serikali itafanya matengenezo makubwa katika maeneo korofi ya Nkwilo, Mtowisa, Zimba, Kisa, Kinambo, Ilemba na Solola ambayo yameathiriwa kwa kiasi kikubwa.

“Niwaahidi wana Rukwa, Serikali itaendelea kufanya kila jitihada kurejesha miundombinu katika maeneo yaliyoharibiwa na mvua kadri inavyowezekana ili huduma za kijamii na kiuchumi ziweze kuendelea kama kawaida,” amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amesema Wizara ya Ujenzi italeta wataalam wa miamba kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina katika Milima ya Ufipa hasa katika eneo la Nkwilo ambapo kuna changamoto ya mawe mengi yaliyoshuka kutoka Milimani ili tathimini hiyo ilete suluhisho la kudumu katika miundombinu iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa.

WhatsApp Image 2024-04-09 at 13.48.30_bdabe586.jpg

WhatsApp Image 2024-04-09 at 13.48.29_50685525.jpg

WhatsApp Image 2024-04-09 at 13.48.27_d2781b6d.jpg
Mwonekano wa miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua katika barabara ya Kasansa - Muze - Mtowisa - Ilemba - Kaoze - Kilyamatundu (km 180) katika Bonde la Ziwa Rukwa Wilaya ya Sumbawanga ambapo Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amefika na kukagua uharibifu wa miundombinu hiyo.

Kutokana na ombi la Mbunge wa Jimbo la Kwera, Deus Sangu la hitaji la kuunganishwa kwa barabara ya eneo la Muze kuelekea Sumbawanga na barabara ya Ilemba kuunganishwa na Mkoa wa Songwe, Waziri Bashungwa amesema Serikali imepokea ombi hilo ili kulifanyia kazi.

Bashungwa amempongeza Mkurugenzi wa Matengenezo kutoka TANROADS, Dkt. Christina Kayoza pamoja na Mameneja wa Mikoa wa TANROADS kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha wanarejesha miundombinu ya barabara kwa haraka pindi inapoharibiwa na mvua.

Vilevile, Bashungwa ametoa wito kwa Wananchi na waendesha vyombo vya moto kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua za El-Nino, pale wanapokuta barabara au madaraja yamejaa maji waweze kusimama na kuyasubilia yapungue ndipo wapite.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa Eng. Mgeni Mwanga ameeleza barabara zilizoathiriwa zaidi na mvua ni barabara ya Kasansa - Muze, Muze - Mtowisa, Mtowisa - Ilemba na Ilemba - Kaoze, ambapo TANROADS imerejesha mawasilino ya barabara wakati wakisubiria kufanya matengenezo makubwa.

Naye , Diwani wa Kata ya Zimba, Efraim Konta, ameishukuru Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi kwa kuweza kufika Wilayani Sumbawanga kurejesha mawasiliano hayo ya barabara hiyo ambayo ni mkombozi mkubwa kwa Wananchi kusafirisha mazao kutoka Mkoani Rukwa kwenda Mkoa wa Songwe na mikoa jirani.
WhatsApp Image 2024-04-09 at 13.46.23_432f2196.jpg

WhatsApp Image 2024-04-09 at 13.46.23_c0e5aeb0.jpg

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza na Wananchi.
 

SERIKALI YAJIPANGA KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILIYOATHIRIWA NA MVUA MKOANI RUKWA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inarejesha miundombinu ya barabara ya Kasansa - Muze - Mtowisa - Ilemba - Kaoze - Kilyamatundu (km 180) iliyoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo tofauti tofauti nchini.

Bashungwa ameeleza hayo Aprili 08, 2024 Mkoani Rukwa wakati akikagua barabara hiyo na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali itafanya matengenezo makubwa katika maeneo korofi ya Nkwilo, Mtowisa, Zimba, Kisa, Kinambo, Ilemba na Solola ambayo yameathiriwa kwa kiasi kikubwa.

“Niwaahidi wana Rukwa, Serikali itaendelea kufanya kila jitihada kurejesha miundombinu katika maeneo yaliyoharibiwa na mvua kadri inavyowezekana ili huduma za kijamii na kiuchumi ziweze kuendelea kama kawaida”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amesema Wizara ya Ujenzi italeta wataalam wa miamba kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina katika Milima ya Ufipa hasa katika eneo la Nkwilo ambapo kuna changamoto ya mawe mengi yaliyoshuka kutoka Milimani ili tathimini hiyo ilete suluhisho la kudumu katika miundombinu iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa.

Kutokana na ombi la Mbunge wa Jimbo la Kwera, Deus Sangu la hitaji la kuunganisbwa kwa barabara ya eneo la Muze kuelekea Sumbawanga na barabara ya Ilemba kuuganishwa na Mkoa wa Songwe, Waziri Bashungwa amesema Serikali inepokea ombi hilo ili kulifanyia kazi.

Bashungwa amempongeza Mkurugezi wa Matengenezo kutoka TANROADS, Dkt. Christina Kayoza pamoja na Mameneja wa Mikoa wa TANROADS kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha wanarejesha miundombinu ya barabara kwa haraka pindi inapoharibiwa na mvua.

Vilevile, Bashungwa ametoa wito kwa wananchi na waendesha vyombo vya moto kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua za El-Nino, pale wanapokuta barabara au madaraja yamejaa maji waweze kusimama na kuyasubilia yapungue ndipo wapite.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa Eng. Mgeni Mwanga ameeleza kuwa barabara zilizoathiriwa zaidi na mvua ni barabara ya Kasansa - Muze, Muze - Mtowisa, Mtowisa - Ilemba na Ilemba - Kaoze, ambapo TANROADS imerejesha mawasilino ya barabara wakati wakisubiria kufanya matengenezo makubwa.

Naye , Diwani wa Kata ya Zimba, Efraim Konta, ameishukuru Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi kwa kuweza kufika Wilayani Sumbawanga kurejesha mawasilino hayo ya barabara hiyo ambayo ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kusafirisha mazao kutoka Mkoani Rukwa kwenda Mkoa wa Songwe na mikoa jirani.
 

Attachments

  • SERIKALI YAJIPANGA KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILIYOATHIRIWA NA MVUA RUKWA.mp4
    77.1 MB
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.19.jpeg
    779.7 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.20.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.20.jpeg
    587.4 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.20(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.20(1).jpeg
    765.3 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.21(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.21(1).jpeg
    860.4 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.21.jpeg
    700.1 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.23.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.23.jpeg
    571.6 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.29.24.jpeg
    731 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.33.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.33.19.jpeg
    700.1 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.33.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.33.21.jpeg
    783.6 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.33.22(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.33.22(1).jpeg
    593.4 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.33.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.33.24.jpeg
    773.8 KB · Views: 5
Back
Top Bottom