Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Mvua imenyesha na hakika ardhi imepokea maji hadi imetota.
Wakazi wa mijini tumeshuhudia adha kubwa inayotokana na ubovu wa miundombinu ya kutiririsha maji.
MTWARA
Nyumba zaidi ya 17 zimezingirwa na maji (kwa mujibu wa taarifa ya habari ITV) na wananchi wanalalamikia ufunyu wa mitaro iliyojengwa kutiririsha maji ya mvua
DAR
Ni mafuriko kila kona.
Wakazi wa Mwananyamala wanalalamikia mwekezaji kufunga njia za maji na kusababisha maji kuelekea makazi yao
Maeneo ya Kisiwani wananchi watalala nje siku kadhaa ili maji yapungue majumbani kwao
Picha inayofuata inaonesha eneo la mjini kati chuo cha biashara CBE likiwa ipo ndani ya maji. Na bado tulivyo na akili za usahaulifu watu watapanga foleni kuipigia kura CCM.
Hali ya kukosa mipango sahihi yenye tija kwa ncbi ni utamaduni uliosimikwa na serikali ya CCM ambapo wanapambana kushikilia dola kwa gharama yeyote ile huku wakifanya mambo ya hovyo kwenye kuisimamia serikali.
Pale eneo la soko la samaki ferry ambapo ni hatua chache kuelekea baharini, mvua ikinyesha hata ya dakika tano inajaza maji ambayo yanakosa muelekeo na kutuama barabarani ambapo ujenzi wa barabara na kituo cha mwendokasi havikuzingatia matoleo ya maji kuelekea baharini. kumbuka hapo ndipo ilipo Ikulu yetu. Aibu hii inatufanya tuonekane kituko duniani.
Mkuu wa Mkoa yupo bize kupambana na wamachinga badala ya kusimamia tija ya miradi ya serikali mkoani kwake.
Bungeni ni drama za kupmbea kura 2025 zinaendelea wskijifanya wana uchungu na nchi huku wakijua wazo kwsmba hatima yao ipo mikononi mwa kamafi za chama na siyo wananchi.
Tufike mahala tuwaache wateuane na watenguane lakini wakija kwetu tuwachuje na kuwakataa kuanzia Rais hadi mwenyekiti wa kitongoji