Mvua ya mawe kubwa kuwahi kutokea duniani

Mvua ya mawe kubwa kuwahi kutokea duniani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwaka 2017, Shirika la hali ya hewa duniani (WMO) lilitangaza mvua kubwa ya mawe kuwahi kutokea duniani.

Baada ya uchunguzi wa kina, ilionekana mvua iliyowahi kutokea Uttar Pradesh, India, tarehe 30 April 1888 ndio mvua kubwa kuwahi kutokea duniani, na ikaingia kwenye rekodi ya dunia ya guiness.

Mvua hiyo ilikuwa na vimbuka na radi zenye nguvu, mawe ya mvua hiyo yalikuwa na ukubwa wa yai la bata mzinga au mpira wa cricket.

Taarifa hiyo ilisema mvua hiyo iliua watu 246, hiyo ndio mvua kubwa ya mawe iliyowahi kutokea duniani.
 
Acha mvua ya mawe! Niliwahi kushuhudia mvua ya samaki huko Kiomboi miaka ya 1980's.
Na ajabu samaki wengine walidondoka wakiwa hai kabisa na kutapatapa.
 
Acha utani ww
Sikumalizia story nikivizia wadadisi kama wewe. Nilishangaa sana kuona mvua imenyesha na samaki wamedondoka toka juu.
Baada ya udadisi wa maajabu hayo ndio nikagundua kuwa mvua ile ilikuja na kimbunga (wanaita chamchela, kile kinatembea kwa kuzunguka kwa kasi), hivyo mvua ikinyesha eneo la ziwa samaki wanatoka chini na kucheza juu ya maji wakidhani matone ya mvua ni chakula.
Kikipita hicho kimbunga kinachota hadi samaki na kuwatupa mbali na ziwa kinapoisha nguvu. Hivyo huu sio utani
 
Juzi tu mwaka jana Arusha ilichapa mvua ya mawe ya maana kiasi kwamba Yale mabarafu ungeweza kusafirishia samaki wabichi hadi Dubai. TCRA mpoo?
 
Acha utani ww
Sikumalizia story nikivizia wadadisi kama wewe. Nilishangaa sana kuona mvua imenyesha na samaki wamedondoka toka juu.
Baada ya udadisi wa maajabu hayo ndio nikagundua kuwa mvua ile ilikuja na kimbunga (wanaita chamchela, kile kinatembea kwa kuzunguka kwa kasi), hivyo mvua ikinyesha eneo la ziwa samaki wanatoka chini na kucheza juu ya maji wakidhani matone ya mvua ni chakula.
Kikipita hicho kimbunga kinachota hadi samaki na kuwatupa mbali na ziwa kinapoisha nguvu. Hivyo huu sio utani
 
Waongo hao kuna ile mvua ilinyesha huko sijui shinyanga jiwe moja la barafu linatoboa bati vunja chochote inachokutana nacho mbuzi ng'ombe walikufa huyo anasema nini

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa inawezekana ilikuwa hivyo, je kuna aliheripoti hilo tukio? Hivyo vyombo vya kimataifa vilikuwa na representatives wao katika hayo maeneo kuripoti tukio moja kwa moja?
Inawezekana wewe ulioziona athari zake, je ziliripotiwa? Kwahiyo tusijadiri sana athalkzitukumbazo hapa nchini kama hakuna wa kuifahamisha dunia...
 
Achana na hiyo tarehe 3/9/1995 siku ya jumapili saa3 asubuh ilitokea bonge la mvua ambayo mvua hiyo ndan yake ilikua na vimvua vidogo vidogo vingi yaan kama mti unavyokua na matawi yake madogo madogo
 
Back
Top Bottom