Mvua yakata mawasiliano Dar na Mikoa ya Kusini

Mvua yakata mawasiliano Dar na Mikoa ya Kusini

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Daraja la Mto Matandu likiwa limekatika tena leo, Jumatatu Aprili 7, 2025, baada ya mwaka jana kukatika kufuatia mvua za El Nino zilizoambatana na kimbunga Hidaya. Pia, daraja la Somanga Mtama limekatika na kukata mawasiliano kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini.

SOURCE: Mwananchi Digital

Tazama: Daraja la Somanga lilivyokatika mwaka 2024
 
Nakumbuka waliweka mawe mengi tuu tena kwa mbwembwe na Engineers wote wa Tanroads wakiafiki Ujenzi huo. Hawakuendeleza kujenga kitaalaam au waliacha ujenzi wa Kisiasa.🙆 Mvua zikiwa nyingi kama za mwaka jana itakuweje?
 
Daraja la Mto Matandu likiwa limekatika tena leo, Jumatatu Aprili 7, 2025, baada ya mwaka jana kukatika kufuatia mvua za El Nino zilizoambatana na kimbunga Hidaya. Pia, daraja la Somanga Mtama limekatika na kukata mawasiliano kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini.

View attachment 3295822

SOURCE:Hapa ndo utagundua uwezo wa viongozi na watendaji walio nao kutatua kero za wananchi.
We tangu mvua za mwaka jana mpaka Leo mvua nyingine Yamuna kilichofanyika.
Taifa linapata hasara kwa uzembe tu wala hotosikia yao Takukuru wala usalama wa Taifa kuchunguza uzembe huu.

Hakika hapa Kuna kiongozi anahujumiwa
 
Huku kusini kumetelekezwa:

Kutoka maktaba :

24 March 2024

Mi mwenyewe safari yangu ya kwanza kama sikosei 2001/2002 nilitumia meli ilikuwa inaitwa Santorini, sijui iliendaga wapi baadae.
Santorini ilitokea ugiriki ilikuwa inafanya biashara na serikali Kwa njia ya uwekezaji ila biashara iliwashinda kutokana na gharama kubwa za uendeshaji.
Ile meli ilikuwa kubwa Sana na abiria walikuwa wachache hata mizigo iliyokuwa inasafirishwa ilikuwa machache, Ile meli ilikuwa kubwa mno
 
Ilikuwa kubwa mno
 
Back
Top Bottom