Mvua zasababisha abiria wa Dar, Arusha na Kilimanjaro kukwama njiani zaidi ya saa 20

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611

Mamia ya Wananchi (abiria) waliokuwa wanasafiri kutoka Arusha, Kilimanjaro na nchi jirani na waliotoka Dar es Salaam kuelekea mikoa mbalimbali wamekwama tangu jana mchana wilayani Korogwe na Handeni Mkoa wa Tanga sababu zikielezwa ni kutokana na maji kupita juu ya daraja la Mandera na kulisomba daraja la Handeni mkoani humo.

Wakizungumza na leo, Jane Mathias na Juma Kombo wamesema tangu jana saa 5 asubuhi wamekwama katika daraja hilo kutokana na wingi wa maji uliotokana na mvua inayoendelea kunyesha mkoani Tanga

"Tumefika hapa jana saa 5 asubuhi hadi muda huu (leo saa1 asubuhi) hatuoni uwezekano wa kuvuka," amesema Mathias.

Kombo ameiomba Serikali kuondoa adha hiyo kwa sababu kwa wiki mbili sasa daraja la Mandera limekuwa likijaa maji.

"Ni aibu barabara muhimu kama hii watu kukwama kutokana na daraja kujaa maji, kila siku wanajenga vivuko hawaimarishi barabara," amesema Mathias.
 
.
View attachment 1245087
 
Hapo wapige mbizi tu..

Poleni sana,najua hapo kuna watu wanasafirisha marehemu wao,wagonjwa,kuna watu wanadharura.. polen sana
 
Pole yao sana...

Hivi hatuwezi kupeleka wanajeshi wakajenge kwa dharula haraka haraka...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom