Mvua zinanyesha lakini Maji hayatoki

Mvua zinanyesha lakini Maji hayatoki

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Mwanzo nilidhani Maji kutokutoka yawezekana ilikuwa ni upungufu wa maji kama tulivyokuwa tukiambiwa na Viongozi tuliowapa dhamana kumbe haikuwa hivyo zilikuwa ni porojo za wendawazimu.

Kila mahali kwa sasa mvua zinanyesha na mto Ruvu umejaa maji tele lakini jambo la kuiskitisha ni kwamba maji hayatoki,hapa nilipo leo ni wiki sasa hakuna maji.Hivi Tatizo huwa ni ukosefu wa Maji kweli au huwa mna agenda za siri?

Aisee hii nchi ngumu sana.

Kuna muda huwa nawaza sababu zinazofanya maji yasitoke au kukatwa kwa maji nabaki nakosa majibu naishia kuongea mwenyewe kama chizi.

Hebu DAWASA niambieni sababu za msingi za kutokutoka kwa maji.
 
Mwanzo nilidhani Maji kutokutoka yawezekana ilikuwa ni upungufu wa maji kama tulivyokuwa tukiambiwa na Viongozi tuliowapa dhamana kumbe haikuwa hivyo zilikuwa ni porojo za wendawazimu.

Kila mahali kwa sasa mvua zinanyesha na mto Ruvu umejaa maji tele lakini jambo la kuiskitisha ni kwamba maji hayatoki,hapa nilipo leo ni wiki sasa hakuna maji.Hivi Tatizo huwa ni ukosefu wa Maji kweli au huwa mna agenda za siri?

Aisee hii nchi ngumu sana.

Kuna muda huwa nawaza sababu zinazofanya maji yasitoke au kukatwa kwa maji nabaki nakosa majibu naishia kuongea mwenyewe kama chizi.

Hebu DAWASA niambieni sababu za msingi za kutokutoka kwa maji.
Watakuja!
 
Wewe subiria kuletewa bill ya upepo Huku
maji uyaoni........ni chizi Pekee anayejua haya mambo
 
Nchi hii mkuu mtoa hoja ina safari ndefu sana, na umbali huu umesababishwa zaidi na nchi kuwa na middle class walio waoga ,uzuzu mwingi, sio risk takers ila ni mahodari wa kulalama kwenye key boards, jiji la Dar baada ya miaka zaidi ya 50 ya kutawaliwa na chama dola bado linategemea mto Ruvu kwa mahitaji yake makubwa ya maji, haya ni makosa makubwa, ilitakiwa kufahamu kuwa kiwango cha mvua inayonyesha ni kikubwa, tujenge mabwawa makubwa kama 4 ya kuhifadhi haya maji, na maji haya yatasaidia sana hasa kipindi ambacho mto Ruvu kina chake kinapopungua,ningependa wataalamu wa maji wa jiji letu wafanye ziara pale kwenye majiji ya GABS, CAPETOWN, JHB na nchi ya Lesotho wakajionee jinsi wanavyotumia mbinu za ukusanyaji wa maji ,tuelewe vita kuu kama itatokea itatokana na MAJI, it's craze nchi imezungukwa na 3 big fresh water lakes hadi leo tunashida ya maji
 
Tulichojifunza ni kwamba serikali ya tanzania haina uwezo wa kuhudumia wananchi wake, sio hilo tu mkuu, ni mengi mno ambayo serikali yako haina uwezo wa kutoa huduma.

Ndio maana ukipita kila nyumba utakuta matanki ya maji, utaona mshimo ya vyoo, utaona watu wamefunga solar, kujenga shule bora, hospitali, haya yote ni ishara kuwa serikali inashindwa kuhudumia watu wake.

Fanya tu namna ununue tank uhifadhi maji, huko mbelez huwezi kuta matanki kila nyumba, au mashimo ya vyoo, serikali zao zipo na uwezo wa kujenga miundombinu kwa ajili ya jamii.
 
Ni kweli tu nilijua pengine kwangu tu kuna shida maana sijayaona maji wiki sasa kesho Mungu akipenda nitawapigia sim niwaulize kulikoni nisikie longolongo zao.
 
Kipindi hiki cha mvua mabomba mengi yamekatika na hakuna na namna ya kujua, hadi mvua zikate ndio utajua wapi bomba lina hitilafu. Halafu mvua inanyesha kwanini usivune ya mvua kwa kipindi hiki?
 
Hata huku kwetu maji yalitoka siku moja tu nayalikuwa Ni tope sana.Baada ya hapo hayakutoka tena hadi Leo japo mvua inanyesha kubwa sana.Sababu zilizotolewa Ni kwamba siku maji yalipotoka,watu weka hawakufungua mabomba hivyo kutokana na pressure kubwa mabomba mengi yalipasuka na kupelekea kufunga hayo maji.
 
Tanzania eeh nchi angu eeeh Tanzania nakupenda sana ila viongozi wangu wanafanya uonekane ni mbaya nakupenda sana Tanzania siwapendi hata kidogo Viongozi wangu wanaojali matumbo yao na sio mustakabali wa nchi
 
Mvua zinaponyesha kwa kiasi kikubwa huharibu miundombinu sasa unakuta kuna maeneo uharibifu unapotokea wanabid wafunge kuepusha upotevu, sina uhakika ila hayo ni mawazo yangu
 
Back
Top Bottom