TANZIA Mvumbuzi wa kanda za kaseti Mholanzi, Lou Ottens afariki dunia

TANZIA Mvumbuzi wa kanda za kaseti Mholanzi, Lou Ottens afariki dunia

na zinanunuliwa kweli? ila uko town nashangaaga kuna shop niliona wanauza tochi za tiger, pipi za tiffany sijui, duh nikabaki nashangaa, mtu unachukua fremu unauza ivo vitu town?
😳😳😳
 
R.I.P engineer
Ila kaseti bana zilikuwa na ladha yake hususani kuishi muda mrefu bila kuharibika.
Vifaa vya kidigital ni vizuri ila kudumu sasa ndio tatizo lingine.
Hasa hasa vya kichina
 
Habari,

Mvumbuzi wa kanda za kaseti Mholanzi, Lou Ottens amefariki wiki hii akiwa na umri wa miaka 94.

Screen-Shot-2021-03-12-at-10.25.17.png


Mabilioni ya kaseti zimeuzwa duniani tangu zilipobuniwa miaka ya 1960

Mtoto wa kike wa mvumbuzi huyo, Arine Ottens alikiambia chombo cha habari cha WTOP News juu ya kifo hicho ”Tunasikitika sana kukuarifu kuwa Lou amefariki Dunia siku ya Jumamosi Machi 6, 2021.”

Ottens alianza kazi katika kampuni ya electronic ya Royal Philips mwanzo mwa miaka 20. Inakadiriwa kuwa kaseti bilioni 100 zimeuzwa duniani tangu zilipobuniwa miaka ya 1960. Uvumbuzi wa Ottens ulibadilisha jinsi watu walivyo sikiliza muziki, na katika miaka ya hivi karibuni kaseti zimeanza kutumika tena.

Injinia huyo amefariki nyumbani kwake Duizel wikendi iliyopita, familia yake ilitangaza Jumanne Jumanne ya wiki hii.

Ottens alikuwa mkuu wa kitengo cha utengenezaji bidhaa katika shirika la Philips miaka ya 1960, ambapo yeye na timu yake walitengeza kaseti.

Mwaka 1963, iliwasilishwa katika maonyesho ya bidhaa za kielektroniki ya Redio ya Berlin na muda mfupi baadae ikapata umaarufu duniani.

Ottens pia ilihusika katika utengenezaji wa CD, na zaidi ya diski bilioni 200 ziliiuzwa duniani hadi leo.
Huyu sasa ndiyo Injinia! Siyo hawa wa kwetu!! Mbwembwe nyiingi halafu hakuna kitu! Wanapenda tu kujiita Mainjinia huku wakiwa hawajawahi kuvumbua chochote!

Utawasikia tu Injinia Mfugale, Injinia Manyanya, Injinia Msukuma! Injinia Kibajaji! Injinia Jah People!! Bure kabisa!!
 
Huyu sasa ndiyo Injinia! Siyo hawa wa kwetu!! Mbwembwe nyiingi halafu hakuna kitu! Wanapenda tu kujiita Mainjinia huku wakiwa hawajawahi kuvumbua chochote!

Utawasikia tu Injinia Mfugale, Injinia Manyanya, Injinia Msukuma! Injinia Kibajaji! Injinia Jah People!! Bure kabisa!!
😂 😂 Injinia soma hiyo
 
Back
Top Bottom