Mvutano Kwenye Mtandao: Mzungu Agoma Kulea Mimba Aliyosingiziwa

Mvutano Kwenye Mtandao: Mzungu Agoma Kulea Mimba Aliyosingiziwa

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312

Hivi karibuni, kanda ya video imeibuka mtandaoni na kusambaa kwa kasi ikimuonesha mzee mmoja wa kizungu akiwa na ghadhabu akieleza masaibu yaliyomfika baada ya kudaiwa kupewa ujauzito na msichana mdogo.

Kulingana na mzee huyo, baada ya miezi minne kupita tangu awasiliane na msichana huyo, alipokea ujumbe na barua kutoka kwake ikidai kuwa ana mimba. Hata hivyo, mzee huyo alikataa vikali kuhusika na ujauzito huo akisema:

"Kulea mtoto sio wangu, mimi sitakubali hata chembe! Sitaki, mtoto sio wangu. Niko na haki, nimeweka uso sababu ni ukweli."

Aidha, mzee huyo alionekana kukasirishwa na mfumo wa sheria na uendeshaji wa masuala ya kifamilia, akidai kuwa mambo yanapofika kwenye masuala ya sheria za familia, haki haitendeki ipasavyo na kwamba mara nyingi wanaume ndio wanaoonekana kubeba lawama au gharama za kila kitu bila haki yao kusikilizwa. Alisema kuwa angependa kuona haki inatendeka bila upendeleo, iwe ni barani Afrika au Ulaya, akisisitiza kuwa rushwa na mifumo mibovu inatakiwa kupigwa vita.
  1. Je, ni mara ngapi tumeshuhudia wanaume wakisingiziwa mimba au kuhukumiwa bila ushahidi wa kutosha?
  2. Mfumo wetu wa sheria za familia unawalinda vipi wazazi wote wawili dhidi ya ulaghai wa namna hii?

Weka maoni yako hapa chini tuweze kujadiliana

Chanzo : Zonedigital
 
Back
Top Bottom