Mvutano wa Kisheria Waanza Kesi ya Boniface Jacob, Andiko Kuhusu Mafwele Lawekwa Kwenye Hati ya Mashtaka

Mvutano wa Kisheria Waanza Kesi ya Boniface Jacob, Andiko Kuhusu Mafwele Lawekwa Kwenye Hati ya Mashtaka

Boniface Jacob ameweza kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 19,2024,toka akamatwe hapo jana katika mgahawa wa Golden Fork, Sinza.

Hati ya Mashtaka ya kesi inayomkabili Boniface Jacob inaeleza kuwa anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, kifungu cha 16.

Katika shitaka la kwanza linaeleza kuwa Boniface Jacob mnamo Septemba 12, 2024, akiwa Dar es Salaam alichapisha taarifa za uongo zikieleza kuwa: "...Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kama mtu ambaye ameshiriki mauaji kwa moja katika kuwapoteza ndugu wa baadhi ya familia zao; kupotea kwa Mfanyabiashara Mussa mziba, Kupotea kwa Deo Mugasa, Kupotea kwa Adinani Hussein Mbezi, Kupotea kwa vijana watano wa Aggrey.." katika mtandao wa X (zamani uliojulikana kama X0 akitumia jina la Boniface Jacob@ExmayorUbungo akikusudia kuudanganya umma.

Na shitaka la pili pia linahusu kuchapisha taarifa za uongo kinyume ambapo linaeleza: Boniface Jacob mnamo Septemba 14,2024, alichapisha taarifa za uongo zilizosema;"....Mkawasifia maRCO wanaouzuia uhalifu kwa kutenda uhalifu,...Bali Ma RCO waliojua kuteka, kukamata, kupiga watuhumiwa risasi, kuwafunga tape, kuwafunga mifuko ya nailoni usoni na kisha kutupa miili ya watuhumiwa ndiyo wanaojua kazi ya upolisi..." katika mtandao wa X (zamani uliojulikana kama Twitter) akitumia jina la Boniface Jacob@ExmayorUbungo akikusudia kuudanganya umma.

Jacob aliyakana mashtaka yote mawili katika kesi hiyo anayowakilishwa na Mawakili watatu akiwemo Peter Kibatala na Hekima Mwasipu.

"Upande wa mashtaka umeleta maombi wanataka Mahakama imuamuru Boni awape maafisa wa polisi wapelelezi, wachunguzi uwezo wa kuingia kwenye simu yake na mtandao wa X. Kwa hiyo tumepinga vikali maombi hayo tumesema hayana sababu , wala msingi wowote kisheria," alieleza Wakili Kibatala akizungumzia mwenendo wa kesi hiyo.

Upande wa mashtaka pia umeiomba Mahakama isimpe Boniface Jacob dhamana kwa kueleza kuwa usalama wake upo hatarini. Jambo ambalo mawakili wake wameeleza halina msingi wowote wa kisheria.

Maamuzi kuhusu dhamana ya Boniface Jacob yanategemewa kutolewa mnamo Septemba 23, 2024, saa tano asubuhi.



View: https://youtu.be/OJBOxYR_98Y?si=LwP_XXF_niPDsoaD

hivi jina la mafwele ni la mtu mmoja, ukoo mzima mafwele ni huyo wanayemdhani tu au?
 
Swali la muhimu sana hili, pia DPP kama jamhuri (Complainant) ndio inapaswa ithibitishe uwongo wa kauli ya Boni (Accused)
Sidhani kama hili watakuwa wako tayari maana Mafwele atapaswa asimame kama shahidi wa jamhuri.
mafwele yupi, manake wapo wengi, na wengine sio mapolisi. kwani kwenye hati kuna majina yote yanayomtaja yeye tu au ni generic name ya ukoo wa mafwele? pengine yeye alimaanisha mafwele mkulima huko musoma je?
 
mafwele yupi, manake wapo wengi, na wengine sio mapolisi. kwani kwenye hati kuna majina yote yanayomtaja yeye tu au ni generic name ya ukoo wa mafwele? pengine yeye alimaanisha mafwele mkulima huko musoma je?
Mbona anatajwa kwa majina yote Faustine Mafwele, na kwa cheo chake kwenye taasisi anayohudumu
 
mafwele yupi, manake wapo wengi, na wengine sio mapolisi. kwani kwenye hati kuna majina yote yanayomtaja yeye tu au ni generic name ya ukoo wa mafwele? pengine yeye alimaanisha mafwele mkulima huko musoma je?
Ametajwa kwa majina yake yote matatu na rank yake ya kijeshi la polisi
 
Back
Top Bottom