Mvutano wa madaraka umeanza kuipasua Iran, viongozi wakigawanyika wazi kati ya wanaounga mkono makubaliano ya kusitisha mashambulizi na wale wanaosisitiza kuendeleza vita. Hali hii inaashiria mabadiliko makubwa katika muundo wa uongozi wa nchi hiyo, ambapo tofauti za kimkakati zinaanza kujitokeza hadharani badala ya kushughulikiwa ndani kwa ndani kama ilivyokuwa hapo awali.
Mara baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Iran kutangaza makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki mbili na kutoa nafasi ya makubaliano zaidi, viongozi wengine wa Iran waliamuru mashambulizi yaendelee wakilenga nchi kama Israel, UAE, Qatar, Saudi Arabia. hii inaonesha Waliotoa tamko la Iran kukubali kusitisha vita na walioendeleza mashambulizi wanaonekana kuwa ni pande mbili zinazovutana ndani ya uongozi wa nchi.
wanaoendeleza mashambulizi ni wale wafuasi kindaki ndaki wa Ayatollah Khamenei, hawataki kabisa makubaliano, bado wana hasira sana iweje Israel na Marekani wameua viongozi wao kibao akiwemo Ayatollah Khamenei halafu kuna upande ndani ya nchi wameanza kukaa meza moja na kina Netanyahu na Trump, kwao ni kama usaliti.
Kwa miaka iliyopita, viongozi waliokuwepo walionyesha mshikamano mkubwa katika maamuzi ya kijeshi na kisiasa. Umoja huo uliipa Iran uwezo wa kuendesha sera zake za kikanda kwa uthabiti na bila migongano ya wazi. Lakini baada ya kuondoka au kuondolewa kwa baadhi ya viongozi hao, pengo la uongozi linaonekana kuchangia hali ya sintofahamu inayoonekana sasa.
Mgawanyiko huu wa ndani unaweza kuwa na athari pana zaidi, si tu kwa Iran bali pia kwa usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati. Wakati upande mmoja ukiona diplomasia kama njia ya kupunguza shinikizo la kimataifa, upande mwingine unaona kuendelea kwa mashambulizi kama njia ya kudumisha ushawishi na kuonyesha nguvu.
Kwa mtazamo wa geopolitics, hali hii inaweka Iran katika nafasi nyeti, ambapo maamuzi ya ndani yanaweza kuathiri mizania ya nguvu ya kikanda. Swali kubwa linalobaki ni kama uongozi wa sasa utaweza kurejesha ule umoja uliokuwepo awali, au kama mgawanyiko huu utaendelea na kuifanya nchi hiyo kuwa dhaifu zaidi mbele ya changamoto za kimataifa.