Mvutano wa madaraka umeanza kuipasua Iran. Baadhi ya viongozi Iran wamekubali sitisho la wiki 2 huku wengine wakiendeleza mashambulizi

Mvutano wa madaraka umeanza kuipasua Iran, viongozi wakigawanyika wazi kati ya wanaounga mkono makubaliano ya kusitisha mashambulizi na wale wanaosisitiza kuendeleza vita. Hali hii inaashiria mabadiliko makubwa katika muundo wa uongozi wa nchi hiyo, ambapo tofauti za kimkakati zinaanza kujitokeza hadharani badala ya kushughulikiwa ndani kwa ndani kama ilivyokuwa hapo awali.

Mara baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Iran kutangaza makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki mbili na kutoa nafasi ya makubaliano zaidi, viongozi wengine wa Iran waliamuru mashambulizi yaendelee wakilenga nchi kama Israel, UAE, Qatar, Saudi Arabia. hii inaonesha Waliotoa tamko la Iran kukubali kusitisha vita na walioendeleza mashambulizi wanaonekana kuwa ni pande mbili zinazovutana ndani ya uongozi wa nchi.

wanaoendeleza mashambulizi ni wale wafuasi kindaki ndaki wa Ayatollah Khamenei, hawataki kabisa makubaliano, bado wana hasira sana iweje Israel na Marekani wameua viongozi wao kibao akiwemo Ayatollah Khamenei halafu kuna upande ndani ya nchi wameanza kukaa meza moja na kina Netanyahu na Trump, kwao ni kama usaliti.

Kwa miaka iliyopita, viongozi waliokuwepo walionyesha mshikamano mkubwa katika maamuzi ya kijeshi na kisiasa. Umoja huo uliipa Iran uwezo wa kuendesha sera zake za kikanda kwa uthabiti na bila migongano ya wazi. Lakini baada ya kuondoka au kuondolewa kwa baadhi ya viongozi hao, pengo la uongozi linaonekana kuchangia hali ya sintofahamu inayoonekana sasa.

Mgawanyiko huu wa ndani unaweza kuwa na athari pana zaidi, si tu kwa Iran bali pia kwa usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati. Wakati upande mmoja ukiona diplomasia kama njia ya kupunguza shinikizo la kimataifa, upande mwingine unaona kuendelea kwa mashambulizi kama njia ya kudumisha ushawishi na kuonyesha nguvu.

Kwa mtazamo wa geopolitics, hali hii inaweka Iran katika nafasi nyeti, ambapo maamuzi ya ndani yanaweza kuathiri mizania ya nguvu ya kikanda. Swali kubwa linalobaki ni kama uongozi wa sasa utaweza kurejesha ule umoja uliokuwepo awali, au kama mgawanyiko huu utaendelea na kuifanya nchi hiyo kuwa dhaifu zaidi mbele ya changamoto za kimataifa.
Mkuu hayo unayaongea kutokana hisia za matamanio yako tu.
Vip kuhusu Israel ambao pamoja na kusitisha mapigano lakini bado anaendelea kuishambulia lebanon na penyewe wamegawanyika.
 
Walio toa pendekezo hilo ni hao wanao rutubisha uranium ili iive vizuri.

Hakuna kitu iran itafany bora asile ni kuivisha mzigo uive mapema dunia ijue kuwa anao.

Kila siku tuna sema aliye kuwa anazuia hayo madude ni Aliyepita huyu IRGC damu damu ni chap tu.
 
Hakuna meli ya Iran iliyozamishwa ilikuwa ni propaganda zenu tu huko gongolamboto, kilichofanyika kilionekana hadharani na vyombo vya habari vyote vya ulimwengu Iran iliangusha ndege za US ambazo walisema ni ndege za kisasa zisizoonekana na rada wala mifumo yoyote ile ya ulinzi

Meli ya Abrahama Lincolin ya marekani ilingongwa mapema sana na ikaonyweshwa na vyombo vyote vya habari ulimwenguni ikiburutwa na mwenzake kurudi mbali zaidi ili kwa matengenezo, kumbuka hii ni meli iliyokuwa na historia kubwa zaidi kwa US na ilivyoishia, Ndege za US zilizokuwa nchi za kiarabu zilipigwa na kuhamishiwa Syprus, pigo ni kubwa walilokutana nalo US na huko uyahudini ndio mana Trump aliomba msaada wiki ya kwanza tu ya vita, wenzake wa ulaya wakamtema.

Marekani walipata hasara sana, na ukisoma hizo points 10 za Iran utaona Iran ndio italipwa gharama za vita
Hakuna meli uliyoandika inayoitwa Abrahama Lincolin labda ni boti, punguza kufatilia habari kwenye vyanzo vilivyokudanganya kwa video za AI kwamba Netanyahu ana vidole 6 na kauawa.

Meli kubwa inayojulikana inaitwa ABRAHAM LINCOLN na bado inayoendelea na operesheni zake hadi sasa
 
Mvutano wa madaraka umeanza kuipasua Iran, viongozi wakigawanyika wazi kati ya wanaounga mkono makubaliano ya kusitisha mashambulizi na wale wanaosisitiza kuendeleza vita. Hali hii inaashiria mabadiliko makubwa katika muundo wa uongozi wa nchi hiyo, ambapo tofauti za kimkakati zinaanza kujitokeza hadharani badala ya kushughulikiwa ndani kwa ndani kama ilivyokuwa hapo awali.

Mara baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Iran kutangaza makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki mbili na kutoa nafasi ya makubaliano zaidi, viongozi wengine wa Iran waliamuru mashambulizi yaendelee wakilenga nchi kama Israel, UAE, Qatar, Saudi Arabia. hii inaonesha Waliotoa tamko la Iran kukubali kusitisha vita na walioendeleza mashambulizi wanaonekana kuwa ni pande mbili zinazovutana ndani ya uongozi wa nchi.

wanaoendeleza mashambulizi ni wale wafuasi kindaki ndaki wa Ayatollah Khamenei, hawataki kabisa makubaliano, bado wana hasira sana iweje Israel na Marekani wameua viongozi wao kibao akiwemo Ayatollah Khamenei halafu kuna upande ndani ya nchi wameanza kukaa meza moja na kina Netanyahu na Trump, kwao ni kama usaliti.

Kwa miaka iliyopita, viongozi waliokuwepo walionyesha mshikamano mkubwa katika maamuzi ya kijeshi na kisiasa. Umoja huo uliipa Iran uwezo wa kuendesha sera zake za kikanda kwa uthabiti na bila migongano ya wazi. Lakini baada ya kuondoka au kuondolewa kwa baadhi ya viongozi hao, pengo la uongozi linaonekana kuchangia hali ya sintofahamu inayoonekana sasa.

Mgawanyiko huu wa ndani unaweza kuwa na athari pana zaidi, si tu kwa Iran bali pia kwa usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati. Wakati upande mmoja ukiona diplomasia kama njia ya kupunguza shinikizo la kimataifa, upande mwingine unaona kuendelea kwa mashambulizi kama njia ya kudumisha ushawishi na kuonyesha nguvu.

Kwa mtazamo wa geopolitics, hali hii inaweka Iran katika nafasi nyeti, ambapo maamuzi ya ndani yanaweza kuathiri mizania ya nguvu ya kikanda. Swali kubwa linalobaki ni kama uongozi wa sasa utaweza kurejesha ule umoja uliokuwepo awali, au kama mgawanyiko huu utaendelea na kuifanya nchi hiyo kuwa dhaifu zaidi mbele ya changamoto za kimataifa.
Tupe kwanza source ya habari yako
 
Kama lilikuwa ni suala la Israel basi Iran wangemalizana na Israel peke yake kama ilivyokuwa vita ya mwaka jana ya siku 12, lakini badala yake wamesambulia Saudi Arabia, UAE, Qatar ambao wapo upande wa Marekani.

wanaoendeleza mashambulizi ni Pro Ayatollah Khamenei hawataki kabisa makubaliano, bado wana hasira sana iweje Israel na Marekani wameua viongozi wao kibao akiwemo Ayatollah Khamenei halafu kuna upande ndani ya nchi wameanza kukaa meza moja na kina Netanyahu na Trump, kwao ni kama usaliti.
Mossad la buselesele.
 
Hakuna meli ya Iran iliyozamishwa ilikuwa ni propaganda zenu tu huko gongolamboto, kilichofanyika kilionekana hadharani na vyombo vya habari vyote vya ulimwengu Iran iliangusha ndege za US ambazo walisema ni ndege za kisasa zisizoonekana na rada wala mifumo yoyote ile ya ulinzi

Meli ya Abrahama Lincolin ya marekani ilingongwa mapema sana na ikaonyweshwa na vyombo vyote vya habari ulimwenguni ikiburutwa na mwenzake kurudi mbali zaidi ili kwa matengenezo, kumbuka hii ni meli iliyokuwa na historia kubwa zaidi kwa US na ilivyoishia, Ndege za US zilizokuwa nchi za kiarabu zilipigwa na kuhamishiwa Syprus, pigo ni kubwa walilokutana nalo US na huko uyahudini ndio mana Trump aliomba msaada wiki ya kwanza tu ya vita, wenzake wa ulaya wakamtema.

Marekani walipata hasara sana, na ukisoma hizo points 10 za Iran utaona Iran ndio italipwa gharama za vita
Nyie jamaa mnapenda kujifariji mno
 
Israel haijapenda terms za kusitisha vita kwa hiyo inaendelea kuleta chokochoko, na Iran imesema kuwa vidole vyao viko kwenye trigger, kama adui asipositisha mashambulizi dhidi yake basi nao wanaendeleza mkong'oto.

Kitakachotokea sasa Iran huenda akasitisha kupiga maslahi ya Marekani ktk nchi za Gulf ila ka nchi ka wazayuni kakiendelea kuleta ngenga basi Iran itaendelea kukatwanga tu. Na tunajua vizuri kuwa bila Marekani hako ka entity hakuna kitu
 
Wacha story za kikanisa wewe Iran kaipiga Israel sababu Israel kashambulia Lebanon wakati Hezbullah aliwacha kushambulia Israel sababu ya ceasefire ndio ikabidi Iran apige base ya America na UAE na Israel na kwa tarifa yako America hakujibu kipigo cha Iran hapa ni wazi USA anataka amuachie Israel opokee kichapo ili asisubutu kuvunja sheria ya ceasefire

Kule Israel magazeti yameandika hivi israel is no longer roaring lion but a crying cat 🐈 😻
Haya kata hilo uunoo Iran kaipiga Israel
 
America hawezi kugusa Iran tena strategy aliyo pigana vita na America hakuna njia ingine ya kumshinda.

Lazima ufahamu Kuna point America kaikubali ya kulipa gharama zote za vita mbili na Iran awe na Nuclear ya peaceful tena kuna nchi nyingi zimeshirikishwa ziwe mashahidi.
Haya ngoja tuone, america ni kigeugeu, hapo kaona maji yamezidi unga anatafuta mlango wa kutokea, nakuahdi atarudi kivingine
 
Back
Top Bottom