Mvutano wa madaraka umeanza kuipasua Iran. Baadhi ya viongozi Iran wamekubali sitisho la wiki 2 huku wengine wakiendeleza mashambulizi

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Mvutano wa madaraka umeanza kuipasua Iran, viongozi wakigawanyika wazi kati ya wanaounga mkono makubaliano ya kusitisha mashambulizi na wale wanaosisitiza kuendeleza vita. Hali hii inaashiria mabadiliko makubwa katika muundo wa uongozi wa nchi hiyo, ambapo tofauti za kimkakati zinaanza kujitokeza hadharani badala ya kushughulikiwa ndani kwa ndani kama ilivyokuwa hapo awali.

Mara baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Iran kutangaza makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki mbili na kutoa nafasi ya makubaliano zaidi, viongozi wengine wa Iran waliamuru mashambulizi yaendelee wakilenga nchi kama Israel, UAE, Qatar, Saudi Arabia. hii inaonesha Waliotoa tamko la Iran kukubali kusitisha vita na walioendeleza mashambulizi wanaonekana kuwa ni pande mbili zinazovutana ndani ya uongozi wa nchi.

wanaoendeleza mashambulizi ni wale wafuasi kindaki ndaki wa Ayatollah Khamenei, hawataki kabisa makubaliano, bado wana hasira sana iweje Israel na Marekani wameua viongozi wao kibao akiwemo Ayatollah Khamenei halafu kuna upande ndani ya nchi wameanza kukaa meza moja na kina Netanyahu na Trump, kwao ni kama usaliti.

Kwa miaka iliyopita, viongozi waliokuwepo walionyesha mshikamano mkubwa katika maamuzi ya kijeshi na kisiasa. Umoja huo uliipa Iran uwezo wa kuendesha sera zake za kikanda kwa uthabiti na bila migongano ya wazi. Lakini baada ya kuondoka au kuondolewa kwa baadhi ya viongozi hao, pengo la uongozi linaonekana kuchangia hali ya sintofahamu inayoonekana sasa.

Mgawanyiko huu wa ndani unaweza kuwa na athari pana zaidi, si tu kwa Iran bali pia kwa usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati. Wakati upande mmoja ukiona diplomasia kama njia ya kupunguza shinikizo la kimataifa, upande mwingine unaona kuendelea kwa mashambulizi kama njia ya kudumisha ushawishi na kuonyesha nguvu.

Kwa mtazamo wa geopolitics, hali hii inaweka Iran katika nafasi nyeti, ambapo maamuzi ya ndani yanaweza kuathiri mizania ya nguvu ya kikanda. Swali kubwa linalobaki ni kama uongozi wa sasa utaweza kurejesha ule umoja uliokuwepo awali, au kama mgawanyiko huu utaendelea na kuifanya nchi hiyo kuwa dhaifu zaidi mbele ya changamoto za kimataifa.
 
Wacha story za kikanisa wewe Iran kaipiga Israel sababu Israel kashambulia Lebanon wakati Hezbullah aliwacha kushambulia Israel sababu ya ceasefire ndio ikabidi Iran apige base ya America na UAE na Israel na kwa tarifa yako America hakujibu kipigo cha Iran hapa ni wazi USA anataka amuachie Israel opokee kichapo ili asisubutu kuvunja sheria ya ceasefire


Kule Israel magazeti yameandika hivi israel is no longer roaring lion but a crying cat 🐈 😻
 
πŸ˜€ Last para
 
Mkuu jaribu kuepuka kuleta uzushi na taharuki.

Israeli kwa hasira (kwa kuona kuna ceasefire) bado waendelea kuwashambulia Hezbollah kule Lebanon jambo ambalo Iran nao hawawezi kulifumbia macho.
 
Waliotoa tamko la Iran kukubali kusitisha vita na walioendeleza mashambulizi wanaonekana kuwa ni pande mbili zinazovutana ndani ya uongozi wa nchi.

wanaoendeleza mashambulizi ni Pro Ayatollah Khamenei hawataki kabisa makubaliano, bado wana hasira sana iweje Israel na Marekani wameua viongozi wao kibao akiwemo Ayatollah Khamenei halafu kuna upande ndani ya nchi wameanza kukaa meza moja na kina Netanyahu na Trump, kwao ni kama usaliti.

Kumbuka Ayatollah aliuawa kwa rekodi ya operesheni iliyofanyika kwa sekunde 40 tu, sio rahisi kusahau kwa baadhi ya wafuasi wake kindaki ndaki waliobaki
 
Mkuu jaribu kuepuka kuleta uzushi na taharuki.

Israeli kwa hasira (kwa kuona kuna ceasefire) bado waendelea kuwashambulia Hezbollah kule Lebanon jambo ambalo Iran nao hawawezi kulifumbia macho.
Waliotoa tamko la Iran kukubali kusitisha vita na walioendeleza mashambulizi wanaonekana kuwa ni pande mbili zinazovutana ndani ya uongozi wa nchi.

wanaoendeleza mashambulizi ni Pro Ayatollah Khamenei hawataki kabisa makubaliano, bado wana hasira sana iweje Israel na Marekani wameua viongozi wao kibao akiwemo Ayatollah Khamenei halafu kuna upande ndani ya nchi wameanza kukaa meza moja na kina Netanyahu na Trump, kwao ni kama usaliti.

Kumbuka Ayatollah aliuawa kwa rekodi ya operesheni iliyofanyika kwa sekunde 40 tu, sio rahisi kusahau kwa baadhi ya wafuasi wake kindaki ndaki waliobaki
 
Hii habari haijaripotiwa kokote na vyombo vya habari vya ulimwengu na hata wewe huna chanzo chochote, tulichoshuhudia na kuona baada ya ceasefire ni sherehe na nderemo kwa wa Iran wote kutokana na ushindi mkubwa walioupata., sambamba na faida kedekede kwa Iran, Mlango wa bahari utakuwa chini ya Iran, Nchi za Saudia Arabia na aila zao wote walipokea vichapo kutoka Iran na hakuna aliyejaribu kumjibu mnyama Iran ambaye alipambana na anayejiita superpower ulimwengu US mpaka alipoomba poo.

Iran imeandika historia ya ulimwengu kwamba ni Taifa pekee liloweza kuimudu USA na Israel kwa mashambulizi makali na yasiyotegemewa na taifa lolote mpaka trump alipokiri "tumeshangazwa na nguvu za Iran" huyo ndo muajemi.
 
Waliotoa tamko la Iran kukubali kusitisha vita na walioendeleza mashambulizi ni pande mbili zinazovutana, wanaoendeleza mashambulizi ni Pro Ayatollah Khamenei hawataki kabisa makubaliano.

Mpasuko upo
Si kweli Iran haipo kabisa kwenye matatizo ni Israel ndio alie vuruga ceasefire lakini Iran kamwambia Hezbullah msimjibu niachieni mimi kampelekea mvua za Missiles nadhani kashika adabu zake sidhani kama ataendelea tena kuvunja ceasefire sababu America kakaa kando hakuingilia na kumbuka base yao imepigwa na Iran leo yeye na UAE
 
Mkuu, ni Pakistan ndo walopendekeza Ceasefire baada ya kuzungumza na China.

Issue iko complex na nafahamu utauliza China imeingiaje hapo, lakini nyuma ya pazia China wapo busy kuhakikisha Marekani hatekelezi anayoyapanga.

China pia imetishia kufuta ziara ya Trump China baada mwezi huu endapo angeshambulia miundombinu ya kiraia ya Iran. Na pia utakua umemsikia Trump kasema nchi itayoendelea kuipa silaha Iran itawekewa tozo ya ushuru wa asimilia 50 hapo awaambia China.
 
Katika kitu nawalaumu iran basi kusitisha vita, kumuamini mmarekani ipo siku atajutia.
America hawezi kugusa Iran tena strategy aliyo pigana vita na America hakuna njia ingine ya kumshinda.

Lazima ufahamu Kuna point America kaikubali ya kulipa gharama zote za vita mbili na Iran awe na Nuclear ya peaceful tena kuna nchi nyingi zimeshirikishwa ziwe mashahidi.
 
Hata Gaza huwa washangilia kushinda vita hivyo siwezi kushangaa Iran inayoifadhili Hamas wakishangilia kushinda baada ya ya Israel na Marekani kumtwanga Ayatollah kwa sekunde 40, kuwatwanga mamia ya viongozi, kuzamisha meli karibia zote za jeshi la Iran, kuharibu airforce ya Iran, kuharibu radar, kuokoa rubani wake aliekuwa anawindwa na nchi nzima, n.k ndo ushindi huo ?

Na hio ndio sababu kuna viongozi wamekataa hayo makubaliano wanaendelea na mashambulizi, bado hawajalipiza kisasi walichoapa cha kumuua Netanyahu halafu kuna viongozi wanenda kukaa meza moja na waliomuua Ayatollah Khamenei kwa Sekunde 40 tu,
 
Kama lilikuwa ni suala la Israel basi Iran wangemalizana na Israel peke yake kama ilivyokuwa vita ya mwaka jana ya siku 12, lakini badala yake wamesambulia Saudi Arabia, UAE, Qatar ambao wapo upande wa Marekani.

wanaoendeleza mashambulizi ni Pro Ayatollah Khamenei hawataki kabisa makubaliano, bado wana hasira sana iweje Israel na Marekani wameua viongozi wao kibao akiwemo Ayatollah Khamenei halafu kuna upande ndani ya nchi wameanza kukaa meza moja na kina Netanyahu na Trump, kwao ni kama usaliti.
 
Hakuna meli ya Iran iliyozamishwa ilikuwa ni propaganda zenu tu huko gongolamboto, kilichofanyika kilionekana hadharani na vyombo vya habari vyote vya ulimwengu Iran iliangusha ndege za US ambazo walisema ni ndege za kisasa zisizoonekana na rada wala mifumo yoyote ile ya ulinzi

Meli ya Abrahama Lincolin ya marekani ilingongwa mapema sana na ikaonyweshwa na vyombo vyote vya habari ulimwenguni ikiburutwa na mwenzake kurudi mbali zaidi ili kwa matengenezo, kumbuka hii ni meli iliyokuwa na historia kubwa zaidi kwa US na ilivyoishia, Ndege za US zilizokuwa nchi za kiarabu zilipigwa na kuhamishiwa Syprus, pigo ni kubwa walilokutana nalo US na huko uyahudini ndio mana Trump aliomba msaada wiki ya kwanza tu ya vita, wenzake wa ulaya wakamtema.

Marekani walipata hasara sana, na ukisoma hizo points 10 za Iran utaona Iran ndio italipwa gharama za vita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…