Upendeleo hudanganya, uzuri ni batili..bali mwanamke amchaye bwana ndiye atakayesifiwa. In Eng bible it says Charm(the power or quality of attracting, fascinating or delighting others) and Beauty is deceptive, But the woman who fears the Lord is to be praised.
Sasa kulingana na mada hii, mvuto si kitu kinachodumu. Na Timotheo aliona hili wazi, mapema tu akatuonya gender yetu kwamba tujipambe kwa mavazi ya KUJISITIRI, adabu nzuri na moyo wa kiasi. Sio kwa kusuka nywele, dhahabu na vito vya thamani na nguo za thamani bali kwa matendo mema.
Mwanamke mwenye sifa za Mith 31, na 1Tim 2:9-10 ni mwanamke mzuri sana hata ipite miaka elfu na mia. Na zaidi ya hilo ni kwamba hata mume wake atamsifu malangoni kwa sababu uzuri wa mwanamke unaanzia ndani. Beauty starts from within then it radiates externally.
Lakin too bad weng wa wanaume unakuta walioa kwa kuangalia vgezo vya nje TU na hawakutaka kuhangaika na vgezo vya ndani. Unakuta mtu ndani ya miaka minne mmekua katika uchumba, mkaanza kwa kasi sana na matusi yakafanyika weee, ok mkaingia kwenye ndoa proudly kwamba we made it, rahisi sana uzuri wa nje kufade out kwa sabbu kuna tabia za ndani zilikua masked na great sex styles ama chura ama uzuri wa sura ama pesa.
Lakin imagine unakutana na mmama ana muonekano wa kawaida no chura no what lakin ana moyo mzuri, hekima, upendo, utu wema..iwe iweje atasifiwa tu kwamba ni mzuri na atapendwa na watoto, mume, ndugu na jamii kwa ujumla.
Uzuri katika miili yetu huwa unaexpire mapema sana. Lakini roho njema inaishi miaka mingi mno. Anayechagua achague vyema na anayechaguliwa ajitengeneze ndani ili achaguliwe na mchaguzi mzuri. Isije ikatokea mwanamke unakuwa mwema afu ukaishia kwa agent wa kuzimu. Uzuri wa nje hubatilika mapema sana. Seek God ufanywe mzuri from inside.