DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Rais wa Chama cha Wanasheria nchini Tanzania (TLS), Boniface Mwabukusi, ametoa tamko kali akilaani kitendo cha polisi kuwashambulia raia na Wakili Mahinyila ndani ya viunga vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Amesema, “Shambulio lolote dhidi ya wanasheria ndani ya eneo la Mahakama ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya haki.”
Mwabukusi amesema tukio hilo ni la kihalifu na haliwezi kutetewa kwa namna yoyote.
TLS imeagiza afisa wake maalum kufuatilia tukio hilo na kukusanya taarifa kamili.
Kulingana na Mwabukusi, baraza Kuu la TLS litakutana haraka kujadili suala hilo na kutoa mwelekeo rasmi.
Amesisitiza kuwa haki, uwajibikaji, na ulinzi wa wanasheria na raia ni misingi isiyoyumbishwa ambayo TLS itasimamia kwa uthabiti.