Mwabukusi alaani unyanyasaji waumini kanisa la Gwajima

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Wakili na mtetezi wa haki za binadamu, Boniface Mwabukusi, ametoa tamko kali akilaani hatua ya Serikali dhidi ya Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Dkt. Josephat Gwajima, akisema ni shambulio la wazi dhidi ya uhuru wa imani na haki ya kuabudu.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa Juni 29, 2025, Mwabukusi ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi amesema kitendo hicho hakijafanywa kwa nia ya kuleta amani, bali kinadhihirisha mkakati wa kuwadhibiti wale wanaoikosoa Serikali kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo utekaji na upoteaji wa watu.

“Ni dhahiri kuwa kwa kutumia mamlaka ya kiserikali, hatua imechukuliwa si kwa nia ya kulinda amani bali kuwadhibiti wale wanaosema ukweli kuhusu utekaji, upotezaji wa watu, na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini”, amesema Mwabukusi.

Amesisitiza kuwa atachagua daima kuendelea kumtii Yesu Kristo kuliko mamlaka ya kibinadamu, akisema kuwa imani yake haipaswi kuzuiwa kwa kisingizio cha sheria au amani ya kupangwa.

Wakili huyo amesema kufungiwa kwa Kanisa la Gwajima kumevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hasa ibara ya 19 inayolinda uhuru wa imani, na ibara ya 13(6)(a) inayomtaka mtu kusikilizwa kabla ya kuchukuliwa hatua ya kisheria au kiutawala. Vilevile, amesema hatua hiyo inakiuka mikataba ya kimataifa kama Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR).

Aidha, ametoa wito kwa jamii ya Wakristo nchini kusimama kwa uthabiti na kusema kwa sauti kuwa hawatakubali kunyamazishwa.

“Hili ni jaribio la kulinyamazisha Kanisa na kulivua mamlaka yake ya kinabii… Hatunyamazishwi. Hatubabaishwi. Hatutaukana Msalaba,” amesema, akinukuu maandiko matakatifu ya Matendo 5:29 na Mathayo 5:10 kama msingi wa msimamo wake.

Mwabukusi amehitimisha taarifa yake kwa kusema kuwa yuko tayari kuhesabiwa pamoja na Kristo, kulipa gharama yoyote kwa ajili ya kuutetea ukweli, uhuru wa imani na haki ya kuabudu.
1751265083251.png
 
  • Thanks
Reactions: K11
Ni vile tu binadamu tunakuwa na kiburi cha uzima, ila tungejua yatupasayo kutenda hata tusingefanyiana ubaya
 
View attachment 3388992
NO REFORMS NO ELECTION, Watanzania wanajua vyama vingine nje ya CHADEMA ni Mali ya CCM hivyo uchaguzi bila CHADEMA tafsiri yake ni kwamba CCM inasimama peke yake kwenye uchaguzi na kujipigia kura.NO REFORMS NO ELECTION Hesabu zetu tunazifungia hapo.
 
Back
Top Bottom