Mwabukusi asipotumia taaluma yake vyema, hekima na busara kuongoza TLS atavurunda zaidi ya ilivyokuwa kwa Tundu Lissu na Fatma Karume

Mwabukusi asipotumia taaluma yake vyema, hekima na busara kuongoza TLS atavurunda zaidi ya ilivyokuwa kwa Tundu Lissu na Fatma Karume

Sifahamu kama kuna mtu anakumbuka au kufahamu kilifanyika wakati wa uongozi TLS chini ya Lissu na huyu mwanamama mwingine Fatma Karume, zaidi ya malumbano, mipasho na mambambano dhidi ya Serikali zilizokuako wakati huo, ambapo matokeo yake sasa, hapakuwezekana kufanyika chochote TLS kwa maslahi na manufaa mapana ya waTanzania.

Na kwahivyo basi,
Ni muhimu sana kwa Rais wa TLS wa sasa kutumia taaluma yake kuiongoza TLS, na kwa hekima na busara, kwa niaba ya waTanzania kutumia njia muafaka za kisheria kuwatetea waTanzania na kufikia hitimisho lenye manufaa kwa ustawi bora wa haki, uhuru na usawa miongoni mwa waTanzania.

Hakuna haja ya kutumia kiburi, majivuno, jeuri, huruma au hisia kwenye mambo muhimu tena ya kisheria kwenye vyombo vya kutolea haki, huko ni kufanya mzaha na harakati binafsi za siasa kwenye haki za wananchi.

Na kwa kufanya hivyo wengi watakosa haki zao za msingi na TLS inaweza kua sababu ya waTanzania wengi kupoteza haki zao, jambo ambalo ni aibu na fedheha kubwa sana kwa jumuiya na familia muhimu sana nzima ya wanasheria Tanzania.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
cyo ccm wa uvccm macho yote kodoo kwa TLS ya Msomi Mwabukusi,tulieni wasomi wafanye kazi yao kwa mujibu wa katiba na misingi yake acheni kurukaruka maana kwa sasa mkigeuka huku moto kule fire
 
Tuko upande wa HAKI...Taifa lipo nyuma sana Keki kwa wachache umaskini uliotukuka
Umaskini wa kujitakia. Mbona sisi huku tuna masters lakini tunaendesha bodaboda na kwa siku tunapata elfu 50. Zinduka we kijana kamata boda moja njoo borabarani acha kulialia. Umaskini chini ya samia haupo tena
 
mimi kama mbobevu ni wajibu wangu kutoa ushauri mujarabu tena hadhara tofauti na hao washauri wake wa kificho gentleman 🐒

hofu ni hulka ambayo kila binadamu anayo, kuna wanaume wanaogopa hadi panya sembuse uongozi gentleman 🐒
Ha ha ba ha 😄😄 anamwambia mkewe embu panya huyo, mke anamwambia mme wangu tandu njoo umpige, utasikia mke wangu chukua kiatu mpige, hapo ndipo wanawake wanakuwa majasiri 😄😄😄
 
Kipindi cha Lisu na Fatma sifa za kijinga zilikua zaidi ya hizi gentleman 🐒

Na hakuna kuchoka kusema na kueleza ukweli.

Na mpaka leo hao watu hawajulikani hata walifanya nini mpaka wa leo, ule wa sifa na kiburi, ujuaji mwingi kumbe mbele kiza uliwaponza 🐒

Ushauri mwanana wa maana sana nimeutoa kitaamu na kwahivyo nimetekeleza wajibu wangu vyema na sidaiwi tena ikiwa mambo yatakwenda kombo huko tuendako 🐒
Twambie aliyemtangulia Mwabukusi amefanya nini kama kumbukumbu? Chawa mnamatatizo mengi.
 
Back
Top Bottom