the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi akiwa katika kampeni ya samia Legal Aid inayoendelea mkoani Arusha hapo jana tarehe 05/03/2025 amesema kuwa mahakama inabidi ijitafakari iwe huru na ya kutenda haki ili hata kama mkulima ataenda mahakamani kulalamika kuhusu Rais basi mahakama itende haki.
Ameeleza pia kuwa Hakimu ana haki ya kuhukumu sahihi au kwa makosa kwa kadri ya shauri lilivyo mbele yake wewe unachopaswa kufanya ni kukata rufaa kama hujaridhika.
Ameeleza pia kuwa Hakimu ana haki ya kuhukumu sahihi au kwa makosa kwa kadri ya shauri lilivyo mbele yake wewe unachopaswa kufanya ni kukata rufaa kama hujaridhika.