Mwabukusi: Jeshi la polisi lichunguzwe kwa uhalifu wa wazi na uvunjaji wa sheria .
JESHI LA POLISI LICHUNGUZWE KWA UHALIFU NA UVUNJAJI WA KATIBA.
kwa barua hii sasa ni uthibitisho kwamba kuna hitajika uchunguzi maalum kwa Jeshi la Polisi.
Huu ni Uharamia na Uvunjwaji wa Sheria .Sheria inataka unapo mkamata mtu moja ya haki ni kuwasiliana na Ndugu zake au mwanasheria wake au la Umfikishe Mahakamani .
Haiwezekani ukae na mtu siku tano halafu baada ya kitisho cha Maandamano ndiyo uje na kipeperushi hiki.Huu ni Uhalifu.This is a 5 days enforced disappearance.
Barua hii imethibitisha kuwa Jeshi la Polisi linatekeleza wajibu wake Kihalifu na kuvunja Katiba.
BAK MWABUKUSI